
SEHEMU YA KUMI NA NANE
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI SABA : Saa mbili na dakika tano, mzee Masinde alikuwa ametulia nyumbani kwake akamsubiri mwanae ambae alimwambia aje hapo nyumbani mida hii ilionyesha alikuwa ana kitu muhimu anataka waongee, mala mlango uka gongwa “fungua tu! hupo wazi” mlango ukafunguliwa akaingia Insp Johnson akiwa amevalia mavazi ya kiraia, tofauti na aliivyokuwa mchana, endelea …….
“karibu mwanangu, karibu sana” alikaribisha mzee David Masinde “asante baba , daaah! nyumba imepoa sana inamaana mama alisafiri na dada wakazi?” aliongea Johnson huku ana kaa kwenye kochi, karibu na baba yake, “yaaa! amesafiri naye, si unajuwa mama yako anavyopenda u’boss, nimeona bora asafiri na mfanyakazi asije akawasumbua kule kijijini” aliongea mzee Masinde ambae ndie baba wa kijana Insp Johnson David, baada ya porojo za hapa na pale wakaanza maongezi, Johnson akimtaka baba yake, amweleze ukweli juu ya Michael Nyati, ukweli ni kwamba, Johnson alistushwa sana na ile picha aliyoiona kwa mzee Soud, inayo wahusu wanajeshi walioenda nchini Congo, na baba yake akiwemo, pamoja na Michael Nyati, na wale wachungaji wawili walio uwawa, mzee Kileo na Chilumba, lakini mzee Masinde alikuwa mjanja sana, akacheza na hakili ya mwanae, kamsimulia Mwanae Johnson kama ilivyo andikwa kwenye report, aliyoitoa mwaka 1988 akiwa commander officer, Johnson akuona kama kuna tofauti ya simulizi, alizo sikia kutoka kwa watu wawili tofauti leo hii, “lakini baba unazani mtu alie wauwa wenzako ni huyu Michael Nyati?, kwamba inawezekana bado yupo ahi” aliuliza Johnson, akimtazama baba yake usoni, “mh! sizani sababu kwa umri atakao kuwa nao sasa, na aina ya mauwaji yaliyotokea jana, sizani kama ni yeye, isitoshe atukuwai kukosea mpaka afanye mauwaji kama haya” aliongea mzee Masinde akijaribu kupotosha kile ambacho yeye anakijuwa, “najuwa yeye hawezi, lakini anaweza akawa amemtuma huyu mwanamke ambae anafanya haya mauwaji” alistuka sana, mzee Masinde, baadda ya kusikia kuwa muuwaji ni mwanamke, “mwanamke?, ina maana Kileo ame uwawa na mwanamke?” hapo Johnson aligunduwa kosa lake “baba naomba maongezi yetu yaishie hapa hapa, lakini kumbuka kuwa polisi inaweza kukuitaji muda wowote, wewe na wenzako, kwa mahojiano zaidi ya kipolisi, pia kama kuna lolote utakalo likumbuka, naomba unijulishe mimi na siyo mtu mwingine” Huyu anaitwa Johnsonn David Masinde, ni mtoto wa kwanza, kati ya watoto wanne wa mzee masinde ** Saa tatu kasoro za usiku, Jackline akiwa ndani ya nyumba, pasipo mweji wake kurudi, “mbona leo amechelewa kurudi” Jackline aliwaza akienda kuchungulia dirishani, akaona kimya akuna dalili ya gari, “huyu mlevi, atakuwa sawa sawa na wale nilio wachinja kule manzese, kazi yake kuvizia wanawake kwenye bar” alijisemea Jackline kwa hasira, huku akirudi na kukaa kwenye kochi, sasa alikuwa amevaa, kile kigauni kifupi cha kulalia alicho leta Denis, pasipo kujuwa ameletewa nani, huku ndani akivalia kipensi cha jinsi, na zana zake za kazi ziki ning’inia kama kawaida, lakini kitu cha hajabu leo, Jackline alijikuta anatamani sana kuwa karibu na Denis, maana alimkumbuka vituko vya mwenyeji wake huyo, asa anapo kuwa amelewa, alikumbuka sana jana usiku alipo kodoa macho kushangaa paja lake, Jackline akachukua simu yake na kutazama muda, bado ni saa tatu kasoro, “mh! kumbe mida yake bado” alijishangaa Jackline, wakati huo huo akasikia muungurumo wa gari, akakaa vizuri kwenye kochi, akipandisha kigauni chake juu na kuyahachia mapaja yake wazi, lakini akificha zana zake za kazi zisionekane, hapo Jackline alijiandaa kumwona jinsi mwenyeji wake atakavyo mshangaa mapaja, kama jana alivyo mshangaa mapaja, kiukweli Jackline alianza kumzowea Denis na vituko vyake, Jackline akasikia gari likizimwa, Jack akajiandaa kupokea vifuko vya chips, lakiniukapita muda kidogo pasipo mlango kufunguliwa zikapita dakika kumi nyingine, pasipo Jackline kumwona Denis akiingia ndani, hapo Jackline akainuka na kutokanje, akaenda mpaka kwenye gari akajaribu kufungua mlango, akakutana na muungurumo kama wa simba, “gruuuuu! gruuuuuuu!” alikuwa ni mwenyeji wake Denis cha pombe, alikuwa amelala kwenye gari, “jackline aliuma meno kwa hasira akainua mkono wake wakulia na kushusha kofi languvu, kichwani kwa mwenyeji wake, likalia ‘paaa!’ Denis akastuka na kutaka kukimbia, akajigonga kwenye kingo ya mlango wa gari, akapepesa macho huku na huku, akmwona dada mama ntilie, ambae bado alikuwa amjuwi jina, “daah! nime…nime..nime rudi zamani hen?” aliuliza Denis kilevi levi “hapana ndo unarudi sasa hivi” Denis akajikokota kushuka kwenye gari huku akijishika kichwani, pale alipo jigonga, akamkabidhi Jack funguo za gari, “ebu! kuna mizigo hapo kwenye seat ya pembeni, hiyo..hiyo ya huko nyuma nita shusha kesho” aliongea Denis akielekea ndani, akamwacha Jackline akifunga mlango wa dereva, na kuzungukia mlango wa abilia wa mbele, akaufungua na kuanza kukusanya vitu vyote vya pale kwenye seat, na pale chini ya seat, bila kujuwa anachukuwa nini, alichokignduwa kwa haraka ni mifuko ya chips kuku na carton za bia, akafunga mlango wagari, nakuingia ndani ya nyumba, na mizigo yake, akamkuta Denis akisinzia juu ya kochi, akachambua vifuko na kuvitenganisha, kulikuwa na mfuko kuku walio tengenezwa tayari kwa kuwa kaanga, au kuwa chemsha, jackline akawaweka kwenye friji pamoja nasoda, pia akakuta vifuko vya chips akaweka pembeni, kisha akafungua mfuko wa mwisho ambao ulikuwa tofauti na mingine, ata kwa rangi na aina ya mfuko, akaingiza mkono ndani ya mfuko hule, na kutowa kilichopo ndani yake, Jackline aliduwaa baada ya kuuona mdori mweupe, na mzuri sana, akaugeuza geuza mpaka alipo yaona maandishi yaliyopo kifuani kwa yule mdori “only you can show me what love is … ” Jackline akiwa amesha elewa maana ya maneno yale, alijikuta akijawa na hasira kari sana, hapo hapo akageuka ghafla, akiwa amesha iandaa ngumi nzito, na kuielekeza usoni kwa mweji wake, lakini ikaishia hewani, kwani Jackline alisita, kishusha ngumi hiyo usoni kwa mwenyeji wake, ambae tayari aliukuwa amesha pitiwa na usingizi, kutokana na kuzidiwa na pombe, akiwa amekunja sura kwa hasira, Jackline akamtazama mwenyeji wake, ambae alikuwa amesha anza kukoroma tena, Jackline akajikuta baada ya kukasirika akacheka kidogo, japo alikuwa amesha kula, Jack akachukuwa vimifuko vya chakula na kuanza kula, huku akitazama kile kimdori allichokuja nacho Denis, wakati mwingine akimtazama Denis pale alipo lala anakoroma, wakati Jackline anaendelea kula na kuwaza ili na lile juu ya kile kimdori, ghafla akamwona mweji wake akistuka, toka usingizini, “unaona bwana, ndiyo ikawa hivyo” aliongea Denis baada ya kustuka toka usingizini, Jackline akimshangaa, akimkazia macho Denis, ambae alitazama huku na huko, kisha akatulia sekunde kadhaa, kama anakumbuka kitu flani, kisha akamtazama Jackline “hivi… ume niongelesha?” hapo Jackline alishindwa kujizuwia, alihachia kicheko kikubwa sana, kilicho mfanya Denis ashangae “haaaah! Sasa kichekesho nini hapo?” Denis aliuliza, lakini hakujibiwa, maana Jackline alikuwa anaendelea kucheka, Denis naye akashikwa na kichekesho, na yeye akaanza kucheka, pasipo kujuwa anacho cheka mgeni wake, kitendo kilicho zidisha kicheko kwa Jackline, ambae alicheka kiasi cha kujishika sehemu za mbavu, walitumia kama dakika tano adi walipo tulia, wakitazamana huku Jackline akihema kwanguvu, akijitaidi kujizuwia kuendelea kucheka, akamwona mwenyeji wake, akichukuwa kopo la bia na kulifungua, kisha anamwona akipiga funda kadhaa kabla ya kuweka weka mezani, Jackline akaendelea kumtazama mwenyeji wake, sasa alikuwa anajikuna kichwani, huku akijisonya sonya kama anajilahumu jambo flani, Jackline akachukulia kama niulevi, kiukweli Denis alikuwa anawaza namna ya kuanza kumchombweza mgeni wake, ili aweze kumtamkia ya moyoni, “kaka kuna tatizo?” Jackline aliulia na kumfanya Denis azinduke toka kwenye mipango yake “mh! umesema kuna tatizo, lipi tena? Mbona huja niambia”, ni kauli iliyo mfanya Jackline aanze upya kuangua kicheko, Denis akashangaa tena, safari hii akucheka aliishia kutabasamu, akainuka na kuibeba bia yake na kuingia chumbani, akimwacha Jackline peke yake sebuleni akiendelea kucheka, ** baada ya kuachana na mwanae Johnson, mzee Masinde alitoka na kuelekea msibani kwa mchungaji kileo, maeneo ya Tabata Bima, ambako aliwa tumia sms wenzake wakutane hapo, aliwakuta wote wanne wakiwa pale msibani wakimsubiri, wote wanne waliingia ndani yagari, la Alex, na kuanza kikao chao, mzee Masinde aliwaeleza aliyoyasikia kwa mwanae insp Johnson, pia akawaambia alichoongea yeye, akawaambia kuwa, kuna uwezekano wa wao, kuitwa na kuojiwa na polisi, wote kwa pamoja wakapanga kukataa kuliushisha tukio la kuuwawa kwa wakina kileo, na tukio lao la Congo, la mwaka 1988 , japo walishangaa kusikia kuwa ni mwenamke ndie anaye wamaliza, baada ya kumaliza simulizi hiyo, mzee Masinde akatowa pendekezo lake, “unajuwa lazima tutumie mbinu za kijeshi, lazima tumpate adui kabla ajatufikia” kwa hiyo mzee Masinde alishauri waanze kumsaka Michael Nyati mapema na kumtowa roho, hoja iliungwa mkono kwa asilimia mia na wote, huku luten Kaijage aliahidi kutowa vijana saba wenye uwezo wa kimapigano na silaha, kusaidia kumsaka Michael, na huyo mwanamke anaye wawinda, luten Kaijage sasa alikuwa nimfanya biashara, alikuwa anamiliki magari makubwa ya kusafirisha mizigo toka ndani na nje ya nchi, biashara aliyotumia kama kimvuri cha matukio ya usafirishaji wa pembe za ndovu, na ngozi za chui, pamoja na nyala nyingine za serikali, pia alikuwa na kundi lake kubwa la vijana ishirini na tano, hatari sana kwa mapambano ya mikono na silaha, ambao aliwatumia kufanya shuguli zkeo za uharifu, Mwingine alie ahidi mchango ni Sajent taji msataafu Mathayo, aliahidi kutowa gari tatu, na madereva na mafuta, kwaajiri ya matumizi ya vijana hao, yeye Mathayo alijiusisha na uuzaji wa magari ya liyotumika, (used car) tofauti na yale tanayotka nje ya nchi, alicho kifanya yeye, ni kufungua garage kubwa sana, kisha kuwaajili mafundi wenye uwezo mkubwa na madereva wazuri wenye uwezo mkubwa pia, kisha akaanza kununua magari mabovu kabisa, na wakati mwingine, ufanya dili za wizi wa magari, kisha kulibadilisha gari na kwenda kulibadiri usajiri, kisha kuliuza tena, akisaidiwa na vijana wake kumi, ambao ni hodari kwa wizi wa magari, Wawili waliobaki Masinde na Alex, waliahidi kuchangia fedha kwa ajili ya chakula, maladhi, na malipo ya vijana hao, huku Masinde akiongezea na vijana wanne, aliowaita kuwa ni wazuri, kwenye kazi za hatari, wawili hawa kila mmoja alikuwa na dili zake, Alex alikuwa anajiusisha na biashara za kuagiza dawa za binadamu toka nchini India, akizileta na kuziuza, kwenye hospital za nchini, huku akisaidia kwenye taasisi za kujitolea kama za watoto yatima na wazee wasio jiweza, kumbe alikuwa anajiusisha na biashara za madawa ya kulevya, kila alipotowa mzigo India, alipitia Pakstan na kuunganisha na dawa za kulevya, na kuingia nazo nchi, bila kikwazo, kwa kigezo cha kusaidia jamii, Wakati mzee Masinde alijiusisha na uvuvi, alikuwa anamiliki meli kubwa ya uvuvi, aliwaajiri vijana kumi na nane, ambao waliweza kupotelea baharini ata mwezi mzima, wakivua samaki, walipo rudi walirudi na samaki wachache, tofauti na muda walio kaa baharini, kitu ambacho wengi walikuwa awakijuwi, ni kwamba, ndani ya meli ya mzee Masinde kulikuwa na silaha kumi aina ya smg, na boti ndogo nne zenye speed kali sana, ambazo utumika kuteka na kupora meli kubwa zitokazo nje ya nchi, pia meli kubwa ya mzee Masinde ilitumika kuingiza na kutoa mali za magendo, wakati mwngine alishirikiana na luten kaijage, kuvusha pembe za ndovu, na kwenda kupakiza kwenye meli kubwa ambazo zilikuwa zina wasubiri , kwenye bahari kuu, au kuingiza madawa ya kulevya ya Alex, mwisho wasiku, mpango wao ulikaa vizuri, walipanga utekelezaji uanze mala moja, ****huku nako Jackline pale sebuleni, alikaa kwa muda mrefu sana, akimsubiri mwenyeji wake, lakini Denis akutoka chumbani, sasa lilipita lisaa limoja, akainuka na kwenda kumtazama kule chumbani alikoelekea mwenyeji wake, mlango ulikuwa wazi, aikumpa shida kuingia, kwa sababu alishaanza kukizowea chumba hiki, ata leo alioga na kubadiri nguo ndani ya chumba hiki, mle chumbani alimkuta mwenyeji wake amelala kama alivyo, nguo na viatu vikiwa mwilini, kopo labia likiwa pembeni yake tupu, akakunja sura kwa hasira “inamaana leo mwenyeji chumbani, mgeni sebuleni?” aliwaza kwa hasira huku akitoka, akakagua madirisha na milango, allipo akikisha imefungwa akaingia store ya vifaa vya ujenzi na kuifadhi kisu na bastora kwenye beg lake jeusi, akazima taa zote za ndani, na kurudi chumbani, akajilaza kwenye kitanda, pembeni ya mwenyeji wake mlevi, akiacha taa yenye mwanga afifu ya blue ikiwaka mle chumbani, kwa sababu kitanda kilikuwa ni sita kwa sita haikuwa shida kwake, ilimchukuwa muda sana kupata usingizi, kutokana na Denis kukoroma sana, ilifikia kipindi Jackline alikuwa akipiga kofi dogo, na Denis alihacha kukoroma, na baada ya dakika mbili angeanza tena kukoroma, adi saa sita usiku alipo pitiwa na usingizi, Jackline alilala adi saa tisa usiku, ndipo usingizi wake ulipo katika ghafla, Jackline akabaki pale kitandani amejilaza chali akisikilizia mikoromo ya mwenyeji wake, akiwa bado amejilaza chali, Jackline alihisi Denis ameamka, akafumbua macho taratibu na kuangalia upande wa Denis, kweli mwenyeji wake alikuwa amekaa kitandani, akimshangaa yeye, macho ya mwenyeji wake yalikuwa yametulia kwenye usawa wa mapaja yake, jackline akatulia ili aone mwisho wa mwenyeji wake, akiwa amejifanya amelala, Jackline alimwona Denis akiwa anamtazama, asa maeneo ya mapajani, pia Denis alitumia sekunde kadhaa, akimtazama, sehemu moja baada ya nyingine ya Jackline, Jackine akiwa anaendeea kumtazama Denis, akamwona mwenyeji wake huyu, akishuka toka kitandan na kusimama chini, kwakutumia mwanga afifu wa taa ya blue, Jackline aliweza kuona dudu ya mwenyeji wake, ikionekana jinsi ilivyo vimba kwenye suluwali, kwa kusimama, ilionekana kutamani kitumbua chake, sasa Jackline aka mwona mwenyeji wake chapombe, akianza kulegeza mkanda wa suruali, huku macho yake ame yakodoa kitandani alipo lala yeye, hapo Jackline Michael Nyati, taratibu alikunja ngumi, tayari kumtandika mwenyeji wake, endapo atafanya ujinga wowote, haya mdau umeshaona kuwa inspector Johnson, ni mtoto wa mzee Masinde ja Devid atafanya nini?, itaendelea……..
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU