BINTI MDUNGUAJI (31)

SEHEMU YA SELATHINI NA MOJA

ILIPOISHIA SEHEMU YA SELASINI : kijana mmoja kati ya wale watatu alimwona Jackline, akajaribu kuvuta kumbu kumbu ya kuwa amemwona wapi huyu mwanamke mrembo, lakini kijana huyu, kwa kuwa alikuwa kazini, akapotezea akijiambia kuwa ule aukuwa mda wakutamani wanawake, japo aliendelea kumtazama mpaka alipo ingia kwenye jengo la MH Production, endelea …….
Ndani ya ofisi ya mkuu wa kitengo cha upelelezi, insp Johnson David Masinde, alikuwa amesimama mbele ya meza kubwa yenye vikolombwezo vingi sana, ukiachilia ma file mengi yaliyo pangwa vizuri, pia ulikuwa na vibendela vidogo viwili kimoja cha taifa na kingine cha jeshi, diary peni za kla rangi, vitabu vya sharia na simu tatu za mkononi, bla kusahau simu ya mezani, huku mbele kabisa ya meza hiyo kikionekana kibao kidogo, chenye maadishi, cssc J J Kishiko “jambo afande” alisalimia insp Johnson, kwa kupiga saruti, “jambo inspector, kuna swala moja nyeti nime kuitia,” aliongea afande Kishiko, “ndo afande nakusikiliza,” alijibu Johnson ambae alikuwa amesimama imara mbele ya mkubwa wake, “imegundulika kuwa gari la bwana Mathayo, lili ripotiwa kuibiwa siku tano kabala ya tukio, hivyo bwana Mathayo ausiki na mauwaji ya wale watu wawili waliotoroshwa” hapo Kishiko alitulia kidogo na kutoa lost riport na kumwonyesha Johnson, ambae wakati huo alisha anza kuhisi kuna jambo lime tendeka, juu ya swala hilo, “lakini afande, huyu mzee ni mtu muhimu sana katika kesi ninayo ifwatilia” aliongea Johnson baada ya kuiangalia ile lost riport, “ok! utafwatilia baada ya yeye kuondoka hapa kituoni, maana juu ya swala la mbezi lipo kwenye kitengo changu, kwahiyo leo usi mhoji lolote” alongea bwana Kishiko, na Johnson alipotaka kuongea jambo, mzee Kishio alimdaka juu kwa juu, “hiyo ni amri, unaweza kwenda sasa” hapo Johnson hakuwa na neno, akapiga saruti na kuondoka zake, akiwa amejawa na hofu kubwa sana juu ya kesi hii, ambayo kuto kuifanikisha ni sawa na kuruhusu kifo cha baba yake, wakati anatoka nje, ndipo alipo mwona baba yake, akiwa ameongo zana na mzee Mathayo, wanatoka nje ya jengo la ofisi za kituo hicho, “samahani nyie wazee wawili” mzee Masinde na Mathayo, ambao walikuwa wamesha fika mlangoni, wakageuka na kumwona Johnson, akija usawa wao, wakasimama kumsubiri, huku wameachia tabasamu kwenye nyuso zao, “hooo! insp habari za asubuhi?” aliongea mzee Masinde, “safi mzee wangu, shikamoni” aliwa salimia kwa pamoja, nao wakaitikia kwa pamoja, “hongereni kwa ushindi wa kupapatua kesi hii” aliongea Johnson na yeye akionyesha tabasamu, “kama wewe unashindwa kuni saidia mimi rafiki wa baba yako, unazani tuta fanyaje?” alijibu mzee Mathayo, kwa sauti ya chini sana, akimlahumu mtoto wa rafiki yake, Johnson akawasogelea zaidi wa zee awa wawili na kuwanog’oneza “baba ilimlilolifanya siyo kwamba mnatatua tatizo, ila mna zidisha tatizo” hapo wazee awa waliachia kicheko huku wakipeana ishara ya kuondoka zao, ** Jackline Michael Nyati, alikuwa juu kabisa ya jengo la MH Production, lenye gholofa sita tayari amesha iseti silaha yake aina ya mugnum siper rifle, aliyo ielekeza kwenye jengo la kituo kikuu chapolisi ambacho kilikuwepo umbari wa mita kama mia tatu toka alipo kuwa yeye, jicho lake la kulia lilkuwa kwenye kilengeo, ambacho kilikuwa kina uwezo mkubwa wa kuona mbali bila matatizo yoyote, Jackline alikagua jengo la kituo kile kwa kupitia madirishani, lakini hakuona kitu, alikagua sana bila mafanikio, lengo lake likiwa ni kumwona mzee Mathayo na kumtandika risasi, mwisho Jackline akategeshakileneo kwenye diridha la chumba cha mahojiano, akiwa na uakika kwa siku hiyo ya jumatatu, lazima mzee Mathayo ahojiwe hivyo lazima amuwai kabla ya kurudi mahabusu, alikuwa tayari kushinda utwa nzima, akimsubilia mzee Mathayo aingie kwenye chumba hicho ili aseme nae, japo kuna wakati alitembeza silaha yake kuangalia maeneo mengine ya jengo lile, sasa basi, wakati anapitisha kwenye mlango ndipo alipo mwona mzee Mathayo akiwa na mzee Masinde, wakitoa ndani yay a kituo hicho na kuelekea kwenye mahegesho ya magari, “yes! nime wapata washenzi, kumbe mpo wote wawili” alijisemea Jacklini huku akikoki silaha yake na kuingiza risasi kwenye chemba, hapo sasa Jackline akawa ana lenga kwa umakini, akitafuta uswa wa watu wale wawili ili atumie risasi moja kuwa maliza wote wawili, wadunguaji wanaita moja kwa mbili, ** insp Johnson David Masinde alisimama mlangoni akiwa tazama baba yake na rafiki yake wakitembea taratibu huku wakiongea na kucheka kwa furaha, kiukweli insp Johnson aliumia sana kwa swala la kuachiwa kwa mzee Mathayo, kwani ange msaidia sana kumaliza swala hili, “sasa wao wana jifanya wajanja, awajuwi kuwa kifo kina wawinda” alosema Johnson, huku akitikisa kichwa kwa masikitiko, wakati anafanya hivyo mala akahisi ame mlikwa na mwanga wa kioo, toka kwenye jengo moja refu, lililopo umbali wa mita mia tatu toka pale kituoni, akatazama tena vizuri, safari hii alikiona vizuri kitu kinachong’aa kilicho tazama upande wa kituoni, hapo akijiuliza mala mbili insp Johnso alitoka mbio kumwafwata wale wawee wawili, huku akipiga kelele, “lala chiniiiiiiiii” kamailivyo kawaida ya waswahili ndio kwanza wakamsangaa kamanda hyu wapolisi, ambae ali powafikia waina mzee Masinde ali mrukia baba yake na kumpiga kikumbo, kilicho wapeleka chini wote wawili, huku wakirukikwa na damu nyingi sana zilizo changanyika na uji uji mweupe, kisha wakamtazama mzee Mathayo aliekuwa bado amesimama, kama anasubiri bendera ipandishwe, kisha sekunde chache akaanguka ‘chini puu!’ huku kichwa chake kikionekana kimevurugika kwa kupasuliwa upande mmoja, na mwengine ikionekana arama ndogo tu! kama kama alie jichoma na msumari, “lala chiniiiiiiii” aliongea Insp Johnson, huku akiwa bado ame mzuwia baba yake pale chini, “baba najuwa bado uja saau mambo ya kivita, jitaidi utambae mpaka kwenye yale magari,” Johnson alimwambia mwambia baba yake, ambae alikuwa anatetemeka kwa uoga, “sawa usiniache mwanangu” aliongea mzee Masinde kwa sauti ya uoga ulio pitiliza, tupo pamoja baba, usogope” aliongea Johnson nakuanza kutambaa, kuelekea kwenye gari lakalribu yao, huku akimvuta baba yake ambae nae alijitaidi kujivuta, sambamba na mwanae, ** huku nako wale vijana watu walishuhudia tukio la mmoja wa bosi wao akipigwa risasi, “yule demu” aliongea mmoja kati ya wale vijana, wa aliekuja pale kwaajili ya ulinzi wa mzee Masinde na Mathayo ambae kwa sasa tayari yupo chini, “demu gani wewe” aliuliza kijana mwingine ambae alikuwa akitazama jinsi mtafaruku ulivyo kuwa mkubwa pale kituo cha polisi, ambapo, olisi wote walikuwa wame lala chin kwenye maficho ya kichwa, (wapiganaji wanaita, over head cover), na wanchi wakiwa wana kimbia huku na huku, “alipita hapa, ameelekea kwenye jengo lileeee” aliongea tena yule kijana huku anafungua mlango wa gari na kuchukuwa bastora ambayo ilikuwa imeifadhiwa chini ya seat, “jamani tunachelewa, tumuwai” aliongea yule jamaa kwa msisitizo, hapo nikitendo cha haraka sana, wale wenzake waka chukuwa bastora zao kama alivyo fanya mwenzo, kisha wakaanza kukimbilia kwenye jengo lile alilo onyesha wenzao, jenge la MH Production, wakiwa waeficha vizuri bastora zao, ** “baba tulia hapa hapa” baada ya kumfikisha baba yake kwenye maficho, ambayo aliamini yanaweza kuwa salama kwa baba yake, kisha akatoka mbio kuelekea ndani jaengo nakueleea moja kwa moja kwenye ghala la silaha, akiamrisha askari ambao walikuwa wame jificha mlendani wachukuwe silaha na kuelekea kwenye kwenye gholofa la MH Productin, dakika chache baadae askari kumi na tatu, walikuwa na wakiwa na silaha aina ya smg mikononi mwao walikuwa wakielekea kweye jengo la MH Production, ** Jackline Michael Nyati, alifungua silaha yake, akitenganisha kifaha kimoja baada ya kingine, na kuweka kwenye begi lake, kilikuwa ni kitendo cha haraka sana, alipo maliza akaliweka begi lake begani, nakuanza kushuka ngazi kwa haraka sana, lakini hakufika mbali akawaona vijana watatu wakipandisha ngazi mbio mbio, akajuwa kuwa ni wageni wake, hapo akajuwa uwa anatakiwa kufanya jambo kabla awaja mchelewesha, maana alsha juwa kuwa kuna polisi alishaona uwepo wake kule gholofani itaendelea ….

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata