
SEHEMU YA SELATHINI NA NNE
ILIPOISHIA SEHEMU YA SELATHINI NA TATU : sasa ilikuwa ni sauti ya boss wake, hapo Denis akapata picha kwamba yupo nyumbani kwake na hao ni wakina Mahadhi, akajaribu kufumbua macho, yaka fumbuka, akajikkuta yupo ndani ya chumba chake nyumbani kwake kibamba njia panda ya shule, ameamka jamani, wakwanza kumwona alikuwa Mahadhi, “we mshenz… umefikaje huku bila kuniambia nawakati nilikucha ofisi, au… unampango na mke wangu” aliongea Denis kwa sauti ya uchovu, huku akijaribu kuinuka toka kitandani, kumfwata Mahadhi, ambae akutaka kumwonyesha kabisa mpenzi, ENDELEA …….
Wote mle ndani walicheka sana, kasolo Denis mwenyewe ambae aliduwaa akiwatazama wenzie wakimcheka, “Denis siwezi kufanya kitu kamahicho rafiki yangu, kuwa na amani” alongea Mahadhi wakati huo Jackline alikuwa amemuwai Denis asiinuka, akamshika na kumrudisha kitandani, “tulia mume wangu, bado auna nguvu” aliongea Jackline, ambae mda huu wote alionekana mwenye tabasamu la furaha, kwa sauti ya upole na unyenyekevu, kiasi cha kuwasisimua wakina Mahadhi, “hivi ilikuwaje kuwaje, maana nakumbuka nilikuwa naongea na dada mmoja hivi….. yuleeee tulie mpa lifti juzi, mala… nikazidiwa na pombe” aliongea Denis, kwa sauti ya kichovu, huku anajaribu kuvuta kumbu kumbu, “mimi mwenyewe na shangaa umekuja na gari ukasimama hapo nje kisha uka lala humo humo, na siyo leo ni juzi” aliongea Jackline, na kumfanya Denis ashikwe na mshangao mkubwa kama ameonanyoka mwenye miguu, “toka juzi, inamaana leo lini?” aliuliza Denis akitazama dirishani, akaona mwanga mkali wa jua, ikionyesha ni kama saa tano za asubuhi, akakumbuka alipo kuwa pale bar ilisha timia saa kumi na mbili na dakika zake, akajuwa kuwa inawezekana akawa kweli amezima gari kwa siku tatu, “punguza pombe Denis, utaibiwa mke” aliongea Mahadhi, ambae toka alipo mwona mke wa rafiki yake, alikilikuwa kimya cha rafiki yake kilikuwa na maana kubwa sana, “nita kunywa supu ya mtu siku nikijuwa naibiwa” aliongea Denis ambae bado alikuwa kitandani akionyesha kuwa akuwa na nguvu za kutosha, Jackline akatoka kwenye kile chumba chawageni alicho lazwa Denis, na kuelekea jikoni ambako dakika chache akaja na uji wenye mchanganyiko wa nafaka mbali mbali, kama karanga ulezi ngano soya, mahindi na vitu vingine vingi sana, ukiwa uanfuka moshi kwenye bakuri kubwa sana, “kunywa kwanza huu uji, kiisha nikuletee, supu ya kuku, aliongea Jackline akiweka mezani, lile bakuli la supu na kumsaidia mume wake kukaa pale kitandani, ilianywe uji, “ungekuwa ujapata mke, sijuwi kama tusingekukuta umsha kauka” aliongea boss wao wakina Mahadhi, ambae alioneka na kuwa ni mcheshi sana, wote mle ndani wakacheka,kasolo Denis ambae alikosa nguvu yakucheka, “lakini boss mwambie Mahadhi ni malufuku kuja kwangu kama mimi mwenyewe sipo nyumbani” aliongea Denis wote wakacheka tena, kasolo Denis mwenyewe, ambae alikuwa ana nyweshwa uji na Jackline mpenzi wake, baaa ya kushindwa kukimiliki kijiko kutokana na mkono wake kutetemeka sana baada kujaribu kukamata kijiko, wakina Mahadhi walikuwawepo pale kwa mda mrefu, waliongea sana mpaka saa kumi za jioni, walipo amua kuondoka, wakimtaka Jackline aendelee kumtazama Denis, nakwamba akiwa anaitaji msaada wowote awajulishe mala moja, ka kutumia simu ya mumewake, yalishapita masaa saba, toka Denis azinduke toka kwenye usingizi wa siku tatu kasolo, “samahani Jack, nime kutesa sana mpenzi wangu” aliongea Denis ambae alisha anza kulejewa na nguvu zake, na sasa walikuwa wame kaa sebuleni wakitazama Tv, “wala ujanikosea, ni bahati mbaya tu inatokea, ila usinywe tena pombe kwenye bar ukiwa peke yako, au na mtu usie mfahamu vizuri” alijibu Jackline akimlaza Denis kwenye mapaja yake, licha ya kuwa ni mapenzi makubwa aliyo nayo kwa mwanaume huyu, lakini pia Jackline alifanya hivyo, kwaajili ya kumzuwia Deinis asitazame picha zilizo kuwa zikionyeshwa kwenye Tv, zinazo husu habari iliyo kuwa inaendelea, “watu hao wanao tajwa kuwa ni mume na mke waliowai kufanya matukio kadhaa ya utapeli, wakutwa wame uwawa kwenye poli la hifadhi la kisopwa, sikuchache zilizo pitwa, kisi cha miili yao kuliwa na wanyama wa polini, “kama ni matapeli wacha tu wauwawe” alisema Denis pasipo kutazama kwenye Tv, “alafu yule mwanamke sijuwi aliniwekea nini kwenye pombe yangu?” aliuliza Denis huku akivuta kumbu kumbu flani, “yani kama unamachale hivi, umenitumia ile sms, kwamba nisinywe tena pombe, ndio yakanikuta majanga” aliongea Denis akionekana kujilahumu sana, “ila mimi ni noma yani nimeendesha gari bila kujitambua mpaka hapa, duuh!” ilo lilimshangaza ata Denis mwenyewe, ambae alimfanya Jackline aangue kicheko, “ila yule mwanamke nita mtafuta nijuwe alikuwa na maana gani, si amesema anauza duka la simu pale Kamanga,” aliongea Denis safari hii akionyesha kupania, “wala aina haja, mume wangu kana alikuwa nania mbaya anaweza kukudhuru” aliongea Jackline akijifanya kuwa na wasiwasi, “weeee! aniwezi, mimi mwenyewe mtoto wa mjini” alijitapa Denis na kumfanya Jackline acheke tena, “vipi mtoto anasemaje alinimissi” aliongea Denis akiwa analipapasa tumbo la Jackline, wote wakacheka kidogo, ** ilikuwa hivi, Jackline akiwa bado amekaa pale kwenye meza na yule jamaa, akaona kama kuna mawasilano yanaendelea kati yake na mtu mwingine aliopo maeneo ya karibu, na yeye akazidi kuwa makini, asa alipohisi kuwa, yule jamaa karibu yake anawasiliana na mwanamke alie kaa na Denis, hapo akaona kuwa hilo siyo fumanizi tena, kinachofwata ni kumwokoa mpenzi wake, ambae alisha jaribu kumpima kwa kumtumia ujumbe kuwa yupo wapi, ili aone kama atamdanganya au atamweleza ukweli, Denis nae akiwa na mapenzi ya kweli kwa Jackline akamweleza ukweli, hapo ndipo Jackline akajuwa kuwa hapakuwa na usaliti, lakini kuna jambo linataka kutokea, wakati akiwa amesha choka kusubili, na amesha mwona mpenzi wake amekunywa pombe nyingi, akataka kwenda kumchukuwa na kuondoka nae, lakini akamwona anainuka nakuelekea chooni, akajuwa kuwa akitoka ndio utakuwa wakati mzuri wa kuondoka nae, lakini akasngaa kuona yule mwanamke aliekuwa amekaa na Denis akiinuka na kuja pale alipo kaa yeye na yule mwanaume, alicho fanya yeye nikujiziba vizui na ile nguo aliyo iba kaliakoo, akiofia kugunduliwa na yule mwanamke, ambae walishawai kukutana nae, siku tatu zilizopita walivyo mpatia lifti pale kibamba, kweli akamwona yule mwanamke akija mpaka kwenyeile meza yao na kuongea na yule mwanaume, akimwambia kuwa anawasi wasi ya kushindwa kufanikisha mpango wao, sababu Denis anaonekana bado ajalewa, ndipo yule jamaa alipo mpa kile kichupa cha dawa, akisisitiza kumwinua mala tu baada ya Denis kunywa pombe yenye dawa hiyo, kwanza kabisa Jackline alitaka kuanza kazi pale pale, lakini akajuwa itakuwa ni hatari sana kwake sababu Denis ata usishwa kwenye tukio na kusababisha yeye kupatikana kilahisi,akatulia huku akichekecha kitu cha kufanya, wakati huo alimwona yule mwanamke akichanganya ile dawa aliyopewa kwenye bia ya Denis, ambayo aliambiwa kuwa ni ya usingizi, hapo Jackline akapata wazo la kumwai Denis kule chooni, akachukuwa begi lake jeusi chini ya miguu yake kisha akainuka na kuanza kuifwata njia ya kuelekea chooni, lakini akuwai kwani Denis alisha toka na kuelekea kwenyemeza yake ndipo yeye alipo ghaili kuelekea chooni na kuelekea nje, huku akiandika ujumbe na kuutuma kwa Denis “usinywe hiyo bia” licha ya kumwona Denis akiitoa simu yake toka mfukoni, lakini akashangaa kumwona akianza kuimalizia bia yake kisha akausoma ule ujumbe, “amechelewa” alijisemea Jackline huku aki tembesa haraka na kwenda kusimama kwenye maegesho ya magari, yapale coner bar, Jacklne Michael Nyati akiwa amesimama ubavuni mwa gari la pili, toka kwenye gari la Denis, aliwaona yule mwanamke na mwanaume wakimkokota Denis wakija usawa wa gari la Denis, ambae alionekana kuzidwa na ulevi, akuna mtu alie wajari, maana mambo ya klewa mpaka kuzima garo, uwa yanatokea sana kwenye mabar mengi, Jackline aliwaona wale watu wawili wakimfikisha Denis kwenye gari lake, alafu yule mwanamke anaingiza mkono mfukoni mwa Denis na kutoa funguo ya gari kisha akafungua mlango mkubwa nyuma wa lile gari, alafu wote kwapamoja waanza kusaidiana kumwingiza Denis ndani ya gari, mpaka walipo fanikiwa, wakaufunga ule mlango wa nyuma na wote wakaamia seat za mbele wakipitia ndani kwa ndani, yule mwanamke akampatia funguo yule mwanaume ambae alikuwa amekaa kwenye seat ya dereva, mala moja bila kuchelewa yule jamaa akaliwasha gari, “yes linamafuta yakutosha” alisikika yule jamaa akiongea huku akiingiza gia tayari kuondoa gari, ndipo kwa haraka sana Jacklin Michael Nyati alio chomoka toka mafichoni na kuwai mlango wa wa nyuma wa gari na kuufungua kisha akaingia ndani ya gari kwa haraka sana na kuufunga mlango, “nani wewe”aliuliza yule jamaa kwa sauti ya uoga na mstuko, “islael mtoa roho” alijibu Jackline kwa sauti kavu yakike, na kitendo bila kuchelewa, yule jamaa akahisi kitu kizito kikitua shingoni mwake karibu na kisogo, na kumlegeza pale pale, “he! wifi nanii dada, nili kuwa nanii, shemeji amelewa sana…” alisema yule mwanamke huku akijaribu kufungua mlango ambao ulikuwa bado kwenye lock, lakini alistukia nay eye akipigwa kama yule mwanaume wake na kulegea pale pale kisha kutulia, hapokamamwizi Jackline aka laza seat zote za mbele walizo kalia wale mtu na mke wake ambao walikuwa wamezimia,akawa vutia kwenye seat za nyuma, kisha akakaa kwenye seat ya dereva, kitu ambacho Denis alikuwa akijuwi ni kuwa mke wake anajuwa kuendesha gari, tena amejifunzia kwenye gari ngumu sana land lover one ten, manu transmision gear, na nyumbani kwao songea anamiliki gari, toyota harrier, ambayo alinunuliwa sikuchache kabla ya kuja dar es salaam kwa kazi maalumu, hivyo kwa hili toyota noah kwa ke aikumpa shida, dakika chache nusu saa baadae alikuwa ndani ya msitu wa kisopwa, akiwa shusha abilia wake ambao baada ya kuwashusha, aliwa sachi mifukoni akiwakuta na visu, simu ile chupa ya dawa camera ndogo na kamba nyembamba kama ya kuvulia samaki, alicho kifanya aliwa vutia kwenye kichaka na kuwa wakata shingo zao kwa kutumia kile kisu alicho wakuta nacho, maana chakwake akuweza kutembea nacho siku hiyo, kutokana na nguo alizo vaa, Jackline akuweza kuwaacha watu awa kutokana na kuwa yule mwanamke alisha mtambua kuwa yeye ninani, hivyo ingekuwa lahisi wao kumtaja endapo polisi wange tangaza juu ya kutafutwa kwa mwanamke muuwaji, alipo akikisha ame maliza kuwa kata shingo zao pasipo kuzitenganisha na kiwili wili, Jackline Michael Nyati aliingia kwenye gari na kuelekeanyumbani kwao kibamba njiapanda ya shule, ambako ali mshusha mume wake, kisha akaoga na kuzisafisha nguo zake alizo fanyia kazi mwisho akaelekeasebuleni akawasha tivi na kusikilizia matukio aliyo yafanya kaliakoo, huku akiendelea na mapishi, akiamini mume wake ataamka asubuhi baada ya pombe na dawa aliyowekewa kuisha nguvu, *wakati huo insp Johnson alikuwa amekutana na PC Busungu, kumweleza kuwa anaitaji amfwatilie mzee Masinde yani baba yake huku akimficha kuwa ni baba yake, “akikisha unakuwa nae makini sana kufwatilia nyendo zake, maana naishi uwenda na yeye ni mmoja kati ya watu wanao takiwa kuuwawa, kwa hiyo jitaidi, sana kuwa nae karibu, na akikisha apatwi na jambo lolote baya, sababu ni shahidi muhimu katika kesi hii” huo ndio ujanja alio utumia Johnson kumlinda baba yake, alipo toa maelezo hayo, wakaagana na kuelekea nyumbani kwake mbezi beach,ambako alipokelewa na mke wake, ambae kwakipindi hiki alijawa na wasi wasi mwingi juuya kazi za hatari za mume wake, ** usiku waleo bwana Masinde Alex na Kaijage akuna alie weza kwenda kwenye msiba, kila mmoja akiofia kuuwawa, maana waliona kuna kila dalili ya adui yao kuwa shinda nguvu, walibaki wakitumiana meseji, wakijadiliana juu ya mabo yanayo tokea, ‘kama vipi twendeni songea tuka mtafute Nyati’ lilikuwa wazo la Alex, ‘alafu tukifika tutamwambia atuelewe?” aliuliza mzee Masinde, “akun swala jingine zaidi ya kuomba samaha, na kumpatia kiasi cha pesa’alishauri tena Alex, ‘nazani tukifanya hivyo,atuta pata atanafasi ya kuwekewa matanga, atatuuwa kimya kimya nakutufukia huko huko’ lilikuwa wazo la Kaijage’ mzee Masinde akaunga mkono, wakidai kuwa huyu jamaa lazima atakuwa na hasira kali sana juu yao, ‘kwahiyo hapa tusubili zamu yetu?’ lilikuwa swali toka kwa Alex, ambae aliamini kuwa suluhisho ni kumfwata Michael Nyati na kumwomba msamaha, huku wakimpatia kiasi kikubwa cha fedha, ‘mimi naona tuame mji’ alishauri Kaijage, ‘unazani nisehemu gani hapa tanzania, atashindwa kutufikia?’alihoji mzee Masinde, kwakweli mjadala huu ulikosa mwafaka, * siku yapili Jackline aliamka saakumi nambili nanusu, akamtazama mume wake akamwona bado amelala, akajaribu kumwamsha, lakini hakustuka kabisa, akatoka kitandani na kuelekea sebuleni, na kuanza kufanya mazoezi, alitumia lisaa lizima kisha akafanya kazi zake za kila siku, mpaka alipo stuliwa na simu, ya Denis ambayo ilikuwa ina ita, akaifwata na kuitazama, mpigaji alikuwa ni Mahadhi, akaipokea, “hallow, habari” alisalimia Jackline, “hooo! shemeji hongera sana” aliongea Mahadhi kwa sauti ya uchangamfu utazani wamesha wai kuonana, “hongera ya nini?” aliuliza Jackline kwa sauti ambayo aikuwa ya uchanga mfu wala ya hasira, huku akionyesha kushangaa, “au Denis ametudanganya, amesema una ujauzito” hapo Jackline akajikuta akitabasamu na kumtazama Denis pale kitandani, “nikweli shemeji, asante” alijibu Jackline, “tuta kuletea zawadi zako, ok! huyu bwana vipi, mbona ajaja kazini?” aliuliza Mahadhi, “anajisikia vibaya kidogo bado amelala” alijibu Jackline ambae aliamini kuwa, mda wowote Denis anaamka, “ok! kumbe unajuwa tulipatwa na wasi wasi, maana jana alinitoroka mchana, nashangaa mpaka leo kimya, nasi utatujulisha anavyo endelea” waliagana na kukata simu, Jackline akamtazama tena Denis, “amka mume wangu, tayari wabaya wako wamesha pata malipo yao” alinong’ona Jackline, kiisha akarudi jikoni kuendelea na kazi zake, mpaka saa nne ina ingia bado Denis alikuwa amelala ajitambui,ndipo Jackline akaamua kumpigia baba yake, iliapate ushauri, bahati nzuri akapokea mama yake, “hongera mwanagu, naona umebakiza watatu, ndani ya miezi mitatu” alisema mama yake baada ya kumaliza kusalimiana, Jackline alimweleza mama yake kilichotokea jana juu ya Denis, hapo mama yake akamwambia, asubiri baada ya mda mfupi atapewa maelezo kwanjia ya sms, na kweli baada ya mda mfupi akapokea sms, iliyo mwelekeza kitu cha kufanya, akashauliwa aende kwenye duka la dawa za hasiri (wengine wanaita dawa za kisuni) huku wakiholozesha dawa za kwenda kununua, kisha awapigie wampe maelekezo hapo mala moja Jackline aka jiandaa na kuanza safari ya kuelekea barabarani madukani, akiwa amevalia nguo za kiheshima ya kimama, licha ya kuvaa gauni lakini alijiziba kwa vitenge mwili mzima akiachia uso peke yake, lakini uvaaji huu aukuzuwia bahadhi ya vitu kuonekana, asa msambwanda, pale kibamba apakuwa na duka la dawa za hasiri, alielekezwa aende mbezi, ilikuwa bahati yake, maana baada ya mda fupi kufika mbezi alipata kila kitu alicho kiitaji, akaingia kwenye dala dala na kuanza kurudi kibamba, *** pc Kessy ni askari polisi wa kituo kikuu, waliopo chini ya insp Jonhson, ni mmoja kati ya askari walio kuwepo kwenye tukio la kumkimbiza Jackline, kule buguruni, miezi mitatu iliyo pita kwenye jengo la baraka shopers, leo akwenda kazinin baada ya kupatwa na udhuru, akiwapigia simu kazini kwake kuwa anakwenda kumwona mgonjwa, tumbi hosptali, huko kibaha, kaini ilikuwa ni mbinu ya kwenda kula starehe nanyumba ndogo yake inayo kaa kiluvya kwa komba, PC Kessy akiwa amevalia mavazi nadhifu ya kiraia, alipanda magari yaendayo mbezi mwisho, akitokea nyumbani kwake magomeni kagera na kushilia mbezi mwisho, kisha akapanda gari la mkata kwa minajili ya kushukia kiluvya kwa komba, lakini akiwa ndani ya daladala linalo subiri habilia wajae, mala akamwona mwanamke mmoja alie jitanda vitenge akiingia kwenye gari hilo na kukaa siti moja karibu kabisa na mlango, licha ya PC Kessy kuvutiwa na uzuri wa huyu mwanamke pia alijaribu kuvuta kumbu kumbu kwamba aliwai kumwona wapi, maana sula yake aikuwa ngeni kwake, licha ya kujaribu kuvuta sana kumbukumbu lakini akufanikiwa, akawa ana mtazama kwa umakini uzuri wa yule mwanamke, ambae alikuwa amekaa mbele yake, baada ya mda gari likaondoka, huku kondakta mwenye mbwewe akianza kukusanya nauli, akianza na yule mwanamke aliekuwa amekaa karibu na mlangoni, akamwona akitoa shilingi miambili amsini, “kwani ukusikia wakati tuna tangaza” aliongea yule kondakta akikataa kupokea ile ela toka kwa yule mwanamke mzuri wakutamanisha, “kwani nauli ya kibamba ni ngapi?” aliuliza yule dada kwa mshangao, “kwani umeambiwa ili gari ni la kibamba? lipia mia sita nauli ya maili moja” aliongea yule konda, huku akichukuwa nauli kwa mtu mwingine, “kama ni uzuri kwa mume wako, sisi tume tumwa elea mjini” PC Kessy alimwona yule dada akifungua pochi yake na kutoa noti ya elfu kumi, akamkabidhi yule konda, “hivi we demu mbona una nyege hivyo, yani mia sita nikate kwenye huu msimbazi” yule Kondakta alisema hayo huku akiipokea hile fedha, Kessy alimeona yule dada akiwa anamtazama yule kondakta huku amekunja hasira, “angekuwa na uwezo amnge mmeza mzima mzima” aliwaza Kessy, huku akiwatazama kondakta na yule mwanamke, wakati huo bahazi ya watu walionekana kushundwa kuvumilia maneno ya yule kondakta, nakumwonya aache kauli zake chafu, lakini ndio kwanza yule kondakta akazidisha, weunazani nitatoa wapi, chenj ya buku kumi, ela zenywe mna ongwa, alafu unakuja kutusumbua tu!, sasa utashukia nitakapo pata chenji” abiria wote mle ndani walizani kuwa maneno ya konda ni ya hasira tu! ange mshusha yule dada kibamba, “nishushe kibamba” lakini wakaamini baada ya kuona gari lina pita kibamba kwa speed kali, licha ya mschana huyu kupiga kelele za kuomba kuwa ashushwe, hapo kila mmoja akiwa anamtazama kwa huruma yule dada mkimya, walimsikia kondakta akiendelea kuongea, maneno yake ya hajabu, “siku nyingine utakuwa umejifunza, utamwambia mteja wako awe anakupa buku buku, ilikuondoa usumbufu, simama hapo gogoni tumwache huyu changu” aliongea yule Kondakta huku akisogea mlangoni na kugonga ubavu wa gari kwanguvu, pc Kessy akiwa kama mtu wa usalama wa raia alikuwa ametulia kimya akitazama yule mwanamke anazalilishwa, garilikapunguza mwendo na kusimama, hapo kikatokea kitu mambacho hakuna aliamini macho yake, kitu ambacho kilimfanya pc Kessy amkumbuke huyu mwanamke, maana baada ya gari kusimama yule kondakta akatangulia kushuka chini akampatia yule dada noti yake ya elfu kumi kama ilivyo, “naoba ela ya texi” ilisikika sauti ya yule dada, ikionyesha akuwa na utani, “mwe malaya una kichaa nini, ela yanini wakati ela yako sija…” mpaka hapo watu wote awakusikia manemno ya mwisho ya yule kondakta, zaidi walishuhudia kipokea ngumi nzito ya mdomo, iliyo sababisha damu nyngi ziruke toka kwenye mdomo wa konda, zikiambatana na meno matatu, “mama nakufaaaaa!” alipiga kelele yule kondakita huku akipepesuka nakwenda kujibamiza kwenye ubavu wa gari, na kuanguka chini, na kuziachia fedha alizokuwa nazo mkononi, hapo yule mwanamke akaziokota, na kuhesabu ambazo zinge tosha kupandia taxi, wakati huo yule kondakta alikuwa anajiinua toka alipo anguka na kumfwata yule dada, kwa nia ya kupambana, maana akuamini kama amepigwa na mwanamke kama yule, konda akarushangumi ambayo ilidakwa na huyu mwanamke, kisha akaonekana kiuminya kwanguvu sana, “sijisikii kuuwa naomba usinifwate” alonong’ona yule mwanamke, kisha akampatia yule konda fedha zilizo bakia, dereva kuona kuwa mwenzie amezidiwa na mwanamke akaona labda mwenzie alizidisha dose ya ulevi anao tumia, bola akamsaidie kumwadabisa yule mwanamke, wakati huo abilia wote walikuwa wana shangilia, wakimtazama dereva akijiingiza kwenye mikono hatari,hapo sasa kilicho fwata kilimfanya pc Kess ashuke haraka kwenye gari, itaendelea …………….
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU