
BINTI MDUNGUAJI (41)

SEHEMU YA AROBAINI NA MOJA
ILIPOISHIA SEHEMU YA AROBAINI : kutangaza taflija ile ambayo ilikuwa imebakiza week moja kufanyika, akuna redio au Tv ambayo inge pitisha siku pasipo kutangaza uwepo wa taflija hiyo, huku magazeti yakiongoza kwa kutangaza taflija hiyo, wakitoa na picha ya mzee Alex Mwasaga, wakimwelezea kama mfanya biashara mkubwa, sana ambae anania ya dhati ya kusaidia wasio jiweza, akiwa amelishika gazeti, mzee Nyati akatabasamu kidogo, “miezi tisa kasoro sijuwi kama ataweza” aliwaza mze Nyati, ENDELEA ………
Aliwaza mzee Michael Nyati, kisha akamwita mke wake akimwagiza aje na ile pad anayotumia kumfwatilia mwanae Jackline, sekunde chache mama Jackline aliingia sebuleni akiwa na pad mkononi, “ina bidi tuitafute Cosovor Hotel na mazingira yake, naona mmja amesha jilengesha” aliogea mzee Nyati, huku ana bofya bofya ile pad na kuiweka wazi ramani ya jiji la Dar, akiikuza sehemu a mwenge, kwakutumia ramani ya internet, “lakini sidhani kama jambazi wako ataweza kufanya kazi, maana mimba yake inakaribia miezi tisa” aliongea mama Jackiline huku anakaa pembeni ya mume wake, “hapo ndipo napo changanyikiwa, maana tukishindwa kuuwa kipindi hiki, itakuwa vigumu kwa baadae,” aliongea mzee Nyati, huku akiendelea kulikagua eneo lote la cosovor hotel, lililopo maeneo ya mwenge barabara ya morocco, “kwanini ishindikane?” aliuliza mama Jackline, “unajuwa Alex ana hakili nyingi sana, lengo la kugawa misaada hii, ni kuteka hakili za wakuu wa serikari, ili ahesabike kama ni mmoja kati ya watu wenye mchango mkubwa sana katika jamii, hivyo nilahii kupewa ulinzi wa vyombo vya ulinzi na usalama mda wowote atakao itaji, na akipewa ulinzi itakuwa vigumu sana kwa sisi kumpata,” aliongea mzee Nyati, akiendelea kukagua eneo lile, ambalo licha ya kuwepo ile Hoteli kubwa, yenye ukumbi mkubwa wamikutano, naofisi mbali mbali, ndaniyeke, pamoja na vyumba visivyo pungua hamsini, pia kulikuwa na bar kubwa pembeni yake, ijulikanayo kwa jina la mwenge pub, ambayo uwa inakesha usiku kucha, “mh! kwa hakili za Jack, sizani kama ni vigumu kwake kumpoteza Alex, atakama atakuwa na kikosi kizima cha jeshi,”aliongea mama Jackline kwakujiamini, “kuna kitu ujaelewa mama Jack, endapo mtu huyu atakuwa karibu na na viongozi wa serikali, ni lahisi yeye kuwashawishi viongozi ilikunikamata, nakunipoteza gerezani kwa kosa lolote, pasipo kujitetea” aliongea mzee Nyati akiendelea kukagua kagua lile eneo, “kweli mume wangu mtu huyu anapaswa kupotezwa mala moja, ** mzee Soud Hassan ni mmoja kati ya watu walioweza kulisikia tangazo la Taflija iliyo andaliwa na mzee Alex, ya kukutana na watu wenye ulemavu, “mh! unja mwingi mbele kiza,” aliwaza mze Soud, huku ana chukuwa simu yake ya mkononi toka kwenye meza na kubofya namba kadhaa, kisha akaweka sikioni, sekunde chache baadae mzee Soud akaanza kuongea, “malahaba kijana wangu,…. jitaidi tuonane mala moja ….. ndio kuna jambo muhimu sana … ok! fanya hivyo …… jitahidi nakusubiri” kisha akakata simu, ** siku hiyo pia ili wakuta Denis na Jakline wakiwa sebuleni wana leteana michezo ya kiutani, “hivi kwanni autaki nikuletee mchana wakukusaidia?” aliuliza Denis huku akilipapasa tumbo la mke wake, “mh! anisaidie mimi, au akusaidie wewe?” aliuliza Jackline akonyesha dalili ya wivu, na denis akangua kicheko, wakati wanaendelea ma maongezi yao ya utani mala wakasikia simu ya Denis ikiita, akaitazama ilikuwa simu toka kwa baba yake Jackline, “baba mkwe huyo” alisema Denis huku anapokea simu, “hllow mzee shikamoo…. ndiyo mzee tunaendelea vizuri, sijuwi nyie baba kuna lolote huko kijijini? ….. tuna shukuru kama mnaendelea viziru… ndio huyu hapa…” aliongea Denis kisha akampatia Jackline simu, ambae alipokea simu na kuiweka sikioni huku akimwonyesha ishara mume wake ya kuomba maji yakunywa “shikamoo baba ……” ndiomana mneno pekee yaliyo sikika kisha kisha ikawa “ndio … ndio… ndio… sawa baba” nahapo maongezi yakwa yameisha, Jackline akakata simu, na kumtazama Denis ambae alikuwa anakuja na grass ya maji mkononi, “vipi amesha kata simu?” aliuliza Denis, huku anamkabidhi grass ya maji Jackline, “amekata, siuna juwatena anabania vocha” aliongea Jackline akimkabidhi Denis simu yake na kuanza kunywa yale maji, “ila baba yako sauti yake utazani bado kijana” aliongea Denis nakuanza kulichezea tumbo la mke wake, ** msaa mawili baadae insp Johnson alikuwa amesha fika kwa mzee Soud Hassan huko mji mwema kigamboni, akimsikiliza mzee Soud, kwa umakini sana kile alicho mwitia, “kwa kifupi kijana taflija hii aitamsaidia bwana Alex wala wakina Masinde, zaidi itaamsha yaliyo lala, maana Alex amtenge neza mtego wa panya, utakao waingiza wote kwenye tundu moja” aliongea mzee Soud kwa umakini sana, huku Johnson akimsikiliza mzee huyu, ambae aliamini anachoongea kinaweza kuwa na manufaa kwake, “unajuwa atujuwi kwanini mauwaji yalisimama kwa miezi sita sasa, pia kumbuka kuwa, kila linapotokea tukio moja ndipo linapozaliwa tukio lingine, kwa hiyo inaonyesha kuwa muuwaji alisha wapoteza watu wake, na anawapata kutokana na matukio kama haya” aliongoea mzee Soud, na mpaka hapo insp Johnson alisha pata mwanga, “kwa hiyo mzee Soud uanataka kusema, kwa jinsi mzee Aex alivyo jitangaza, muuwaji atakuwa amesha mtambua na kuanza kumuwinda?” aliuliza insp Johnson akitaka kupata uakika, “aswaaaaaa! na kikomo chake ni siku ya taflija” alisawazisha mzee Soud Hassan, hapo Johnson alikooa kidogo kwa kusafisha koo, kisha akamwuliza mzee Soud, “kwahiyo mzee wangu una nishauri nifanye nini?” hapo mzee Soud alitabasamu kidogo, “wewe ni afisa mpelelezi wa jeshi la polisi, akika utakuwa unajuwa nini cha kufanya” alijibu mzee Soud, akimwacha Johnson njia panda, “mzee Soud, wewe ni mwelewa sana, na unauzoefu mkubwa wa haya mambo, pengine unaweza kujuwa njia ya kuaribu shambulizi hili” hapo mzee Soud alitabasamu kidogo, “ok! Johnson, inabidi utumie akili zako zote, zakipolisi na kibinadamu” aliongea mzee Soud huku lile tabasamu likiwa limeyeyuka usoni, nakuwa katika hali ya umakini sana, “nitawezaje mzee wangu, maana muuwaji anaonekana kuwa makini sana” hapo insp Johnson alitumia sauti iliyo jaa dalili za kukata tamaa, “upaswi kuwa hivyo isnp, kumbuka jeshi linakutegemea,” aliongea mzee Soud kisha akatulia kidogo, kama anevuta kumbu kumbu, baada ya sekunde chache akainua usowake na kumtazama insp, “ok! fanya kitu kimoja, lichunguze eneo lote linalo zunguka Cosovor hotel, watakayo fanyia taflija, akikisha una yachunguza majengo yote marefu yaliyopo kuanzia umbali wa mita ziro, mpaka mita elfu moja na miatano, na uakikishe umeweka ulizi wakutosha wapolisi waliovalia nguo za kiraia, wawe na silaha pia vesti la kuzuwia risasi, wawenaso kwa siri, asijuwe mtu yeyote ata bwana Alex mwenye asijuwe kama watuwako wapo eneo lile, na jambo jingine muwe na mwasiliano wakati wowote wa taflija, na mwisho jitaidi baba yako asiwepo eneo la tukio, nikama nilivyo kuambia, huu ni mtego wa panya” mzee Soud alitulia kidogo, “hoooo! nimekumbuka jambo,” insp Johnson ambae alionyesha kuyaelewa vizuri maneno ya mzee Soud, akazidi kutulia na kusikiliza maujuzi hayo, “kumbuka licha ya muuwaji kutumia, silaha yenye uwezo wa kupiga mbari, lakini amesha fanya matukio ya papo kwa papo, kwakutumia mikono yake” insp Johnson aliitkia kwa kichwa, akikubaliana na mzee Soud, ambae aliendelea kuongea, “na kama nikweli Nyati ndie anausika na matukio haya, inabidi uwe plani zaidi ya tatu, maana mipango yake aitabiriki ata siku moja” ** wakati insp Johnson David Masinde anapewa maelekezo na mkongwe Brg Gen mastaafu Soud Hassan, huku nako wazee watatu, ambao ni kati ya wale walioshiriki mapigano nchini congo (kipindi hicho Zaire) waka 1988, walikuwa wame kaa kwenye bar moja, mitaa ya Kimara mwisho, ijulikanayo kama Tukutane Pub, wakiendeleza majidiliano makali, ambayo yalionekana kuungwa mkono na kila mmoja wao, huku wakipata vinywaji taratibu, nyuma yao vijana sita walikuwa wame tulia kwenye meza tofauti tofauti, nawao wakipata vinywaji vyao, lakini lengo lao ni kutoa ulinzi kwa wazee hao, “katika vitu ambavyo umewai kuvi plani, hili la safari hii ndiyo kiboko” aliongea mzee Masinde, huku akiiweka gras yenye bia nusu mezani, “lakini umetumia ghalama kubwa” aliongea mzee Kaijage, “hahahahahaha wewe unazungumzia ghalama, kwanza kunamzigo hupo njiani unakuja, kwakuwa nitakuwa VIP, serikalini, moja kwamoja mzigo utaingia kilaini, kwakutumia meli ya bwana Masinde, pili kwa ulinzi tukao upata, nizaidi ya fedha ninayo itumia” hapo wote wakacheka na kugonga gras zao, wakiunga mkono hoja ya Alex “ila mimi nilikuwa na wazo jingine” aliongea mzee Masinde, “wazo gani hilo?” Alex na Kaijage waliuliza kwa pamoja, “ni hivi, baada ya kuishawishi serikali na kukuamini, kwanini usimshawishi mkuu wa kitengo cha upelelezi wakamkate huyu panya kwa kosa lolote tu, ata la kumsingizia?” hapo wote waka cheka kwa furaha, na kugonga mikono yao ikiwa ni ishara ya ushindi, “hapo bwana masinde, umeongea point, yani ikipita taflija tu! tuakikishe huyu mshenzi anae jiita Nyati, anakuwa sungura” ** wazee awa wali panga ya kwao pasipo kujuwa kuwa mzee Nyati na yeye, alikuwa katika mpango mzito wa kutengeneza tukio la mauwaji kwa njia nyepesi sana, aliyafanya hayo huku akiwasiliana na mwanae Jackline, mala kwamala, akimpatia maelekezo, ambayo Jackline aliyafanyia kazi, kama alivyo elekezwa, kutokana na tukio ili kupangwa wakati Jackline ni mjamzito, wa miezi tisa kazoo siku chache, kwa lugha ya uzazi tuna sema yupo kwenye siku za matazamio, ili mlazimu mzee Michael Nyati, kupanga safiri mwenyewe na mke wake kwenda dar, ili kutoa saport kwa mwanae ** siku zilienda huku Insp Johnson akizidi kutengeza mpango wa ulinzi, wa eneo lile la Cosovor Hotel, na maeneo yote kuzunguka hotel hile, licha ya kuongeza askari wengine ishilini, lakini kazi ile ilkuwa ni ya siri sana, kwa askari wengine, akifwata maelekzo ya mzee Soud, insp Johnson alikagua majengo yote mnne makubwa na marefu, kisha kuwapangia askari watano kila jengo akiwaelekeza sehemu za kukaa, ambazo aliamini kuwa muuwaji ni lahisi kukaa na silaha yake, nakulenga kwenye ukumbi wa mikutani wa pale Cosovor, ambao hupo kwenye gholofa ya pili ya hotel hiyo, ** siku zilisogea atimae siku moja kabla ya tukio, ilikuwa ijumaa, saa nane mchana, Denis akiwa na Mahadhi wanarudi toka kwenye mgahawa wa mama Bupe, kupata chakula cha mchana, ile wanaingia tu! ofisini kwao, mala Denis akasikia mlio wa simu yake ukiita, akaitoa simu na kutazama mpigaji, alikuwa ni Jackline, “ananini huyu mwanamke” alijiuliza Denis huku akitabasamu, akaipokea ile simu, “vipi mke wangu nimechelewa kurudi?” aliuliza Denis kwa sauti iliyo jaa utani, “fanya haraka Denis njoo nyumbani yani mtoto nacheza cheza sana” aliongea Jackline kwa sauti ya kulalamika, na kukata simu, kitendo hicho kilimstua sana Denis, hapo akamtazama Mahadhi, na kuganda kwa sekunde kadhaa, kisha akaongea kama alietoka usingizini, “tayari huko!” hapo Mahadhi alimwona Denis akikurupuka na kutoka nje ya ofisi, “wewe unashangaa nini twende tukamsaidie, mke wake anataka kujifungua” alisema Janeth akimwambia Mahadhi, huku akikurupuka toka kwenye kiti na kuingia kwaboss wao, ambae alimweleza kwakifupi nae akawaluhusu, waende kumsaidia Denis, kisha wamjulishe kitakacho endelea, ile Janeth anatoka kwaboss, akakuta mahadhi amesha toka nje ya ofisi, nayeye akaliunga kuwawai, ile anafika kwenye kilido anawaona wanapotelea kwenye ngazi, yeye akapanda lift, ** licha ya kupanga mipango yake vizuri na kuwapangaia askari wake majukumu ya kesho, siku ya taflija, na mpango wa kumzuwia baba yake asiudhulie taflija, lakini insp Johnson, bado alikuwa anaumiza kichwa, endapo kama muuwaji atatumia ujanja mwingine, nasiyo silaha ya kudungulia atafanyaje, baada ya uwaza sana akapanga kuwa yeye mwenyewe akae ndani yaukumbi kwenye taflija, pamoja na askari sita, ili kuangalia kama kuna dalili ya kutokea kwa kutukio lolote la hatari, *** Denis alie onekana kujawa na hofu, ya mke wake kwenda kujifungua, akiwa pamoja na rafike yake Mahadhi, pamoja na msaidizi wa boss wao, walitumia lisaa limoja tu! kufika nyumbani kwa Denis kibamba njiapanda ya shule, huku wakiwa wame vunja sharia nyingi sana za barabara, kwa mwendo wa kasi sana ambao ulikuwa hatari sana kwao, atimae waliingia nyumbani kwa Denis na kusimamisha gari nje ya nyumba kubwa ya baba kijacho, ambapo kwa Janeth ilikuwa ndiyo mala yake yakwanza, kufika nyumbani hapo, wakati Janeth anaendelea kushangaa, wakina mahadhi na Denis walishuka kwenye gari mala moja, na kukimbilia ndani haraka sana, wakitegemea kumkuta Jackline akiwa katika hali mbaya sana, yakukaribia kujifungua, lakini awakukuta mtu pale sebuleni, Denis akakimbilia chumbani, akimwacha Mahadhi amesimama na Janth alikuwa anaingia humo ndani huku anaendelea kuishangaa nyumba ya kijana huyu mlevi, kule chumbani Denis alitumia mda mfupi, akatoka akiwa anatikisa kichwa kwa masikitiko, huku amejishika mikono kiunoni, ikionyesha ni ishara ya kuchoshwa na jambo flani, akawatazama usoni wakina Mahadhi na Janeth, ambao walishindwa kumwelewa mwenzao, kuwa ametabasamu au anataka kulia.
HUU NDIO MWISHO WA SEASON TWO

