BINTI MDUNGUAJI (46)

SEHEMU YA AROBAINI NA SITA

ILIPOISHIA SEHEMU YA AROBAINI NA TANO: ila amenifurahisha sana alikoifadhi simu na zile risasi” aliongea mama Jackline wote wakacheka, na mda huo huo wakaliona gari la Denis lina ingia kwa fujo, nakusimama mbele ya jengo lile walilo kuwepo wao, wakamwona akishuka na kusogea walipo kuwepo wao, huku anatoa simu yake n kupiga, mala mama Jack akaona simu ya Jackline, iliyo kuwa mikononi mwa mama Jackline, ikianza kuita, Denis akaonekana kuutambua mlio wa simu ya mke wake, akamtazama mama Jack, endelea ………
Akamtazama mama Jackline, akijaribu kukumbuka kuwa alisha wai kumwona wapi mama huyu, kisha akamtazama mzee Nyati, nae sura yake aikuwa ngeni sana, “samahani jamani, nyie ndio mlio msaidia mke wangu?” aliuliza Denis pasipo kusalimia, wazee awa wakatazamana, kisha mama Jackline akamtazama Denis, “wewe ndie mume wayule dada mjamzito?” aliuliza mzee Nyati, “ndio ni mimi aliniaga anakwenda kununua dawa, nikashangaa mnanipigia simu mnaniambia mpo huku” aliongea Denis ambae pombe ilisha pungua kichwani mwake, basi kijana wacha sisi tukuache hapa, umsubiri mkeo, ilaombi moja kijana” aliongea mzee Nyati, akimtazama Denis, “aina tatizo mzee wangu, kiasi gani nikulipe?” aliongea Denis, akitoa pochi yake toka mfukoni, “hapa kijana, sina maana ya fedha, ninaombi moja tu!” aliongea mze Nyati, huku akitabasamu kidogo na kumtazama mke wake, “ok! aina tatizo mzee wangu nakusikiliza” aliongea Denis, pasipo kujuwa kuwa waliopo mbele yao ni wakwe zake, “asante kwa kunipa nafasi ya kunisikiliza” alisema mzee Nyati, akajikooza kidogo, kisha akaendelea, “mimi na mke wangu tumefurahi sana kukutana na familia yako, mkeo ametueleza kuwa, huyu anaezaliwa ndie mtoto wenu wa kwanza, kama aouto jari naomba jambo moja, kamatazaliwa mtoto wakiume mwite Fransis, na kamani wakike mwite Rufina” alimaliza kuongea mzee Nyati, nakuttulia akimtazama mkwe wake, “haaa! usijari mzee wangu, tena mke wangu atafurahi sana, sababu babu yake mzaa baba anaitwa Fransis, ila ilo la rufina sija juwa” aliongea Denis kwa uchangamfu sana, wote kwa pamoja wakionekana wenye furaha wakendelea na maongezi, huku wakina mzee Nyati wakisahau kama walisha aga, ** akiwa nyumbani kwake Kinyelezi, mzee Masinde aliegahili kabisa ata kwenda kwe taflija, baada ya wale polisi wawili kumchelewesha, kwa maswali ya kipuuzi, alikuwa sebuleni kwake akinywa pombe kali kwa fujo, huku mda wote akitukana matusi ya nguoni, kiasi cha kumshangaza ata mke wake, ambae alishindwa kuhoji kitu, kutokana na maelewano mabaya ya mda mrefu yaliyo ikosesha amani familia hii, wakati akiedelea kunung’unika na kutukana ovyo, mala mzee Masinde akasikia simu yake inaita, akaichukuwa toka mezani na kutazama mpigaji, “watakuwa wamesha maliza” alijisemea mzee Masinde huku anapokea simu na kuiweka sikioni, “nimbie bwana Mwijage, Taflija imeendaje?” aliongea Mzee Masinde, ambae alitambua kuwa mzee mwenzake tayari amesha toka kwenye Taflija kutokana na kusikia utulivu, wa eneo alilokuwepo Mwijage kuwa tulivu ikiashilia kuwa yupo kwenye gari, “kaka sijuwi unabahati gani? maana kilicho tokea hapa cosovo, nizaidi ya matukio yote ya liyo wapata wenzetu” aliongea Mwijage, akiwa katika hali flani ya taaluki, “unataka kusema nini Mwijage,?” aliuliza mzee Masinde katika hali ya wasi wasi, hapo mwijage akamsimulia mzee Masinde jinsi ilivyo kuwa, akimweleza tokea walipo mwona mzee Nyati, akija mbele kuchangia shilingi million moja, pia akmweleza jinsi walivyo pokea taalifa ya kuuwawa kwa Alex alie kuwa amee nda chooni, pamoja na walinzi wake watatu, hivyo akamweleza kuwa yeye binafsi anamshukuru sana mwane, insp Johnson, kwa kumpatia ulinzi na kumpakiza kwenye gari, kisha yeye pamoja na mlinzi mmoja alienae, kuelekea nyumbani, “kwahiyo umemwona Nyati live?” aliuliza Masinde kwa mshangao, uliotawaliwa na wasi wasi, tena anaonekana yupo vizuri, siyo wa wasiwasi, ni mtu mwenye fedha zake” aliongea Mwijage, ambae alionekana kukata tamaha, ya kukwepa mtego huu wa Nyati, “kwa hiyo Michael Nyati yupo hapa dar es salaam?” aliuliza Masinde kwa sauti ya uoga zaidi, “yani dah! kama mzim vile sijuwi kwanini ukumtandika risasi ya kichwa yule mshenzi?” aliongea Mwijage, “ok! mwijage tume baki wawili, ebu tukae chini tujuwe lakufanya, chamsingi tutulie majumbani ketu, huku tuna panga jambo la kufanya” aliongea mzee Masinde, na wawilihao wakakubaliana kisha wakakata simu, “sina ujanja, ina bidi nimshirikishe mwanangu katika jambo hili” aliwaza mzee Masinde, huku akiinua grass iliyo jaa pome kali, “pumzika kwa amani shujaa” kisha akagugumia hiyo grass iliyo jaa pombe kali, na kuishusha ikiwa ainakitu, huku amekunja sura yake kwa uchungu wa pombe hiyo, hapo mzee Masinde akaonekana uwaza jambo flani kwadakika kadhaa, kisha akatabasamu, huku anajisemea peke yake, “Johnson ana akili nyingi sana” **saa saba usiku, ndio wakati ambao Johnson mwenyewe, alikuwa anaingia nyumbani kwake mbezi beach, akitokea Cosovo Hotel, akiwa amesha angaika kukagua watu wote waliokuwepo pale hotelini, pasipo kujali ni mlemavu au mtazamaji, pia wapangaji wa mle hotelini akikagua chumba kimoja adi kingine, pasipo mafanikio, “huyu mzee anambinu nyingi kali sana, kuna kila sababu ya kumsaidia baba, ata kwa kukiuka miiko ya jeshi, vinginevyo nita mpoteza” aliwaza Johnson, wakati anavua nguo ili kuingia bafuni, kiukweli licha ya kuwa baba yake alikuwa na tabia zinazo ashilia uvunjaji wa sharia za nchi, lakini baba yake huyo alisha mfanyia mambo mengi sana ya kimaisha, ukiachilia kumsomesha na kumsaidia kupata kazi aliyo kuwa anaipenda ya polisi, pia kumjengea hii nyumba anayo ishi sasa huku mbezi bichi, ae mnunulia gari zuri aina ya Nissan patrol isitoshe mzee Masinde akujali kama mwanae anakazi, yeye alimpatia kisi kikubwa cha fedha mala kwa mala, “nazani mzee Soud atanielekeza namna ya kumpata mzee Nyati” ** Denis akiwa mekaa pale nje na wakina mzee Nyati, mala wakamwona nesi mmoja akitoka nje na kuwa uliza, “nyie ndio mlie mleta, dada mzazi usiku huu?” “ndio ndio ndio sisi, mimi ni mume wake” wakwanza kuitikia alikuwa Denis huku anainuka toka kwenye benchi, alilokuwa amekaa pamoja na wakina mzee Nyati na mke wake, “hongera sana kaka,mkeo kajifungua salama, mtoto wa kiume, japo ailuhusiwi kwa usiku huu, lakini nawapeni mda mfupi mka mtazame” hapo Denis na wakina mzee Nyati wali ruka kwa furaha kubwa sana, wakaongozana na yule nesi mpaka kwenye hodi ya wazazi, chumba cha VIP, “mnaenda wapi nyie, kwani huu ndio mda wakutazama wagonjwa?” ilikuwa ni sauti kavu ya kike, toka kwa mwanamke alie valia kama yule nesi mwingine, huku amekunja sura, iliyo mfanya azidi kuwa mbaya wa sura, japo kwa matazamo ni mwanamke mwenye miaka selathini na tatu, ambae sasa alikuwa ameziba mlango akiwazuwia wasiingie, watu awa watatu wakabaki wame simama wakimtazama Jackline, ambae alikuwa busy anamkagua mtoto alie lazwa kitandani, *** ndani ya chumba kutembelea mahabusu, wa kituo kikuu cha polisi, Jackline ambae alikuwa ameilaza mikono yake iliyo fungwa kwa pingu za minyololo mapajani kwa Denis, akiendela kumwelezea kuwa yeye ni muuwaji na kwanini alifanya hivyo, alitulia kidogo na kumtazama Denis usoni, maana alimwona kama alikuwa anajambo alilotaka kuuliza, “ndio maana huyu mzee alilipia hile ward ya VIP, nayule ness ambae tulisikia amekutwa bafuni amekufa, je ulimuuwa pia?” aliuliza Denis, ambae mpaka hapo alisha anza kumwogopa mke wake, itaendelea ……….

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!