
BINTI MDUNGUAJI (48)

SEHEMU YA AROBAINI NA NANE
ILIPOISHIA SEHEMU YA AROBAINI NA SABA: Jackline wakati anashuka ngazi kwa tahadhari, lile basotra yake aliyo iviligishia shuka ikiwa mkononi, alitazama mlango wa kutokea nje na kuwaona wale watu wawili, yani yule doctor na yule mwanamke wakianza kutembea kuelekea nje kabisa, “washenzi nyie mme kwisha” aliongea Jackline kwa suti ya chini kidogo, endelea …..
hapo Jackline akapandisha tena juu, mpaka kwenye meza ya yule Nesi, ambae sasa alikuwa amesha tulia, kakata roho, aka chukuwa lile file, ambalo alielekezwa aweke ashihi yake, akaliweka kwenye ile nguo aliyo jifunga ndani ** kwa upande wa Doctor fake na mzazi wake wauongo, baada ya kupiga simu kwa nesi ale wasaidia kupaa mtoto wa kutolea kafara, kwa kisi cha million tano, bila kupokelewa simu hiyo, wakaendelea kutembea kuelekea kwenye maegesho ya magari, wakizani labda simu ilijipiga yenyewe, ukweli ni kwamba huyu kijana Anson na na mwana dada Nuru, ni watu wanao jusisha na shuguli za uchimbaji wa madini huko tunduru mpakani na Msumbuji, na baada yakuona kuwa diri zao aziendi sawa, ndipo walipo enda kwa mganga wao kutafuta suluhisho, na mganga akawaambia kuwa wapeleke mtoto mchanga, kwa ajili ya kusafishia nyota zao, na shaliti kubwa nikwamba, mtoto huyo lazima awe mzima, na sio aliekufa, hapo wawili hao wakamtafuta nesi huyu wanae mfahamu toka siku nyingi, na alisha wai kuwasaidia mala moja, lakini ilikuwa ni kupata mtoto mfu, lakini safari hii waliambiwa wapeleke mtoto mzima ili akauwawe kule kule, kwa mganga, na walifanikiwa kuiba mtoto na sasa wakiwa na uakika, walikuwa wanaelekea kwenye gari lao aina ya Toyota stalet, walipo lifikia wakaingia ndani ya gari lao na kuliwasha, kisha wakaanza kutoka nje akilifwata geti kubwa la kutokea nje, bahati nzuri kwenye gate lakutokea hapakuwa na na upekuzi mkubwa, walirudisha card ya maegesho ya gari, na wakaruhusiwa kupita, “yew, tumefanikiwa” alishangilia Nuru kwa sauti kubwa, baada yakuliacha gate kwa atuwa kadhaa, iliyo mstua mtoto France, ambae alistuka na kuanza kulia, lakini ghafla wakashngaa kumwona mschana mmoja akiwa amesimama kati kati ya barabara, Amson akakanyaga breck kwanguvu sana na kusimama, wote wakamtazama yule mwanamke ambae alikuwa ameshika kitu kilicho viligiwa na kipande cha nguo nyeupe, huku mwonekano wake kama mtu hasie na akili timamu, utokana na nywele zake kuwa timu timu, na miguuni hakuwa na viatu, licha ya kunusulika kugongwa lakini chakushangaza yule mwanamke alikuwa ame achia tabasamu ambalo utazani, ni tabasamu la mjumbe wa kuzimu, hapo Anson akashuka toka kwenye gari kwa hasira kali sana, “we mbwa koko, ebu pisha hapo kabla sija kupasua pasua” aliongea Amson, akimsogelea kwa kasi yule mwanamke, ambae bado alikuwa amesimama mbele ya gari, lakini tabasamu likiwa limesha yeyuka usoni mwake, “nimechoka kuuwa, naomba uni patie mwanangu” alisema mwanamke huyu kwa sauti kari ya chini chini, hapo Amsoni akamkumbuka, huyu dada kuwa ndie yule walie mwibia mtoto, Nuru nae aliekuwa amekaa siti ya nyuma, alisha mtambua mwanamke huyu, hapo Amsoni akaona kimesha nuka, swala ni kuingia kwenye gari na kumgongelea mbali, kisha waondoke zao, hapo Amson akageuka na kurudi kwenye gari, lakini hakuwai kuufikia mlango wa gari hilo, akastuka amesha shikwa bega, na yule mwanamke, kisha kwa itendo cha haraka sana yule mwana mke aka mvuta nyuma Amsoni, aliejibwaga chini, hapo yule mwanamke aka zima gari na kuchomoa funguo ya gari hilo, Amsoni akajiinua haraka na kumfwata Jackline Michael Nyati, kwa lengo la kumtandika ngumi, lakini kwa wepesi wa haraka sana, Jackline alimkwepa na kusababisha Amson, ajibamize kwenye gari lake, wakati wote ilisikika sauti ya mtoto France akilia, “sikia kaka, mpaka sasa kifo chako kitakuwa cha maumivu makali sana” aliongea Jackline kwa suti ambayo kama ungesikia ungezani anatania, lakini Amsoni kama asie amini maneno aliyo ongea Jackline, alijaribu kurusha tena ngumi, lakini sarari hii Jackline akumkwepa kama mwanzo, akatumia mkono hule hule alioshikia funguo na kuupeleka usoni kwa Amsoni, na kutuwa kwenye usawa wa jicho lake la kushoto, ambapo Amsoni alihisi kitu kwenye mcha butu kikipenya kwenye jicho lake, na kusababisha maumivu makali, na ghafla jicho ilo lika tandwa na giza, “mama na kufaaaa” alipiga yowe Amson, huku akiinama na kuziba jicho lake, lililo tobolewa na funguo ya gari, “nime kwambia leo utakufa kwa machungu” aliongea Jackline huku aki mwinua Amson aliekuwa ameinama kashikilia jicho lake la kushoto, na kumvutia mlango wa nyuma wagari, kisha akaufungua, “dada samahani na omba usini uwe mtoto wako huyu hapa, aliongea Nuru, kwa sauti ya uoga iliyo tawaliwa na kilio cha uoga, “lakini Jackline kama vile hakusikia ali mnyooshe mkono wake wakulia ulio kamatia bastora iliyo viligiwa kipande cha shuka, akamwelekea mdomoni na kuizamisha kwenye mdomo wa mwanamke huyu, “tafadhari dada yangu tusamehe, usi mwu..” Ansoni hakumalizia maneno yake, alishuhudia mwanamke wake akifumuliwa kichwa na ubongo uki tokea kisogoni, na kutapakaa wenye kioo cha nyuma cha gari hilo, “sijawai kukutana na mwanamke katiri kama wewe” aliongea Amson, akijaribu kufurukuta, ili akimbie, lakini mkono imara wa Jackline ulikuwa umemkamata vyema, “sidhani kama dunia itaniesabia kuwa mimi ni katili, kwa kuwauwa nyie wakatili kuliko mimi” aliongea Jackline akimwinamisha Amson, kwa kumkandamiza chini, kisha akaiweka bastora yake kwenye mgongo wa kijana huyu karibu na iuno kisha akafyetua risasi moja iliyopenya kwenye sehemu hiyo ya mwili wa kijana huyu, “mama nakufaaa” alipiga yowe la uchungu kijana Amson, ambae alijuwa kuwa ameingia coo cha kike, “wamaume uwaga analia kimya kimya” aliongea Jackline huku aki mwongezea Amson risasi ya pega, nakumfanya Amsoni alie nakuongea kama mtoto anae adhibiwa kwa kukuwa ana iba mboga, “nisamehe mama yangu, nishetani tu! alinipitia, aikuwa hakili yangu” kelele za Amsoni zili wafikia walizi wa geti la kutokea muhimbili Hospital, ambao walipiga simu kituo simu kituo cha polisi kilichopo mle ndani ya Hospitali hii kubwa ya taifa, Jackline akaendelea na kazi yake, akamwongeza risasi ya kwenye goti, “haaaa tafadhari nimalizie we mwanamke shetani” aliongea Amson kwasauti iliyo jaa uchungu mkubwa, akisahau ushetani wake, akiuona wa Jackline, “usiJali nita kuuwa tu! lakini nataka ufe taratibu” alionga Jackline huku akimshika yule kijana mwizi wa mtoto, nakumwinua, kisha akaushindilia ule funguo ya gari shingoni mwake, na kuizamisha yote wenye koo, ikigota kwenye kishikio, nakusababisha damu ziruke kama kuna bomba lenye kasi kubwa ya maji limetoboka, “krooo kroooh kwoooh!” ali lalamika kwa mikoromo ya hajabu, iliyo ashilia kuwa jamaa anaelekea kukata roho, Jackline Nyati akamchukuwa mwane, kisha akaanza kutembea kuelekea upande wa diamond jubilee, akiliacha gari na wenye gari pale pale huku funguo ya gari, ikiwa shingoni kwa Amson, baada ya kuakikisha amesha fika mbali, Jackiline akachumoa simu yake sehemu alipo iweka, ikiwa ni kwenye nguo aliyo jiviligishia ndani, bahadhi ya makabila wanaita chikwinda, akapiga simu kwa baba yake, na kumsimulia kilichotokea, nakumwomba msaada wa kuja kumchukuwa, baada ya kutembea atuwa chake Jackline, aliinua gauni lake na kuifadhi simu yake huku akichomoa lile file alilo lichukuwa mezani kwa yule nesi, mwizi wa watoto, ** wakati huo Denis alikuwa sebuleni kwake, akinywa bia nyingi sana, akionekana ni mwenye furaha kubwa sana usiku ule, huku akimpigia simu rafiki yake mahadhi, ambae leo alikuwa amewai nyumbani kwake mapema sana, ni baada ya kukasirishwa, na kitendo cha jana kuzinguliwa na Janeth, Denis akamwelezea Mahadhi juu ya wake, kujifungua mtoto wa kiume, wakapanga wataenda pamoja saa sita mchana, kumtazama, wakati huo Denis akipanga kuwai saa kumi nambili za asubuhi, lakini wakati anaendelea kunywa pombe, akaona simu ya mke wake kiliita, “wewe bado ujalala tu?” aliuliza Denis baada ya kupokea simu ya mke wake, “nili taka niakikishe kaa hupo nyumbani au bar” alitania Jackline alie onyesha kuwa, yupo sehemu tulivu sana, “haaah! sina ujanja huo nipo tu nyumbani, vipi anaendeleaje mtoto, au kamelala” aliongea Denis, huku huku akicheka cheka, ni wazi alijawa na furaha kubwa sana, “kamelala, ila amesema hacha kunywa pombe sasa ulale” aliongea Jackline, akimtania mume wake, waliongea mengi, Jackline akimweleza Denis kuwa, yeye ameomba uamishiwa hosptali ya Matumaini, ya Doctor stellah, kutokana na huduma ya kule kutokuwa nzuri, kwake na kwa mtoto, “sasa usiku huu luksa amekupa nani usiku huu?” aliuliza Denis kwa mshangao, “wame niachia tu wakaniambia niseme nilizalia nyumbani” hapo Jackline, akamsisitiza Denis kuwa kesho akija aseme hivyo, kuwa alizalia nyumbani, *** siku ya pili magazeti mendi na maredio bila kusahau television, zote zilitangaza kuhusu mauwaji yaliyotokea cosovo Hotel, watu walionekana wakiwa wamesimama vikundi vikundi, wakijadiri swala hilo, ata waliopo maofisini, viwandani maskoni ata wanafunzi mashuleni walikuwa wakizungumzia swala hilo, saa mbili asubuhi, insp Johnson akiwa ofisini kwake, anajiandaa kwenda kupokea taalifa ya uchunguzi, wa mauwaji ya mzee Alex na walinzi wake watatu, alipokea talifa ya mauwaji yaliyotokea jana usiku Hospital ya mwimbili ndani ya hodi ya wazazi, na nje ya hospital hiyo, hapo Insp akona nibora awai huko hospital, kupata maelezo yakina, juu ya mauwaji hayo, nusu saa baadae insp Johnson akiwa na askari wake saba, alifika hospital ya muhimbili na kukutana na askari wa zamu, aliekuwepo jana usiku, mwenye cheo cha koplo, maelezo yake yalikuwa ni mafupi tu! kuwa jana akiwa amekaa pale kituoni na wenzake wawili, wakapokea simu toka kwenye gate kuu la kutokea magari, kuwa kuna gari lime simama, ila inasikika sauti ya mtu ana piga kelele na kuomba msamaha, samba mba na sauti ya mtoto mchanga, ndipo wao walipoenda na kukuta vijana wawili wakike na wakiume wakiwa wame uwawa, “tukapiga simu kituo cha polisi salendar bridge, wakaja polisi wa doria, na kuukagua mwili wa marehemu wote wawili, kisha wakaingiza ndani miili, nakwenda kuifadhiwa sehemu usika” aliendelea kusimulia yule Coplo wa polisi, akisema kuwa saa nane usiku walipokea taalifa nyingine, toka chumba cha wazazi, kwamba kunanesi amekutwa ameuwawa, kwenye sehemu ya ofisi ya ward hiyo ya wazazi, walicho fanya wao ni kumhoji nesi mwenzie, ambae alikuwa jengo la chini, upande wa mapokezi, alicho eleza mwenzie, ni kwamba, mala ya mwisho aimwona mwenzie akiongea na watu watatu waliokuwa wame mleta mwanamke kujifungua, kisha yule nesi akaanza kuongea na mtu mwingine ambae ni doctor, lakini alikili kuwa yule doctor akuwai kumwona pale kwenye jengo la wazazi, baadae akawaona wale watu watau wakitoka na kuondoka zao, wakiwa na magari mawili tofauti, “nusu saa baadae nikiwa nasinzia nikasikia mlio wasimu, nikachungulia nikamwona yule kaka aliekuwa amevaa koti la doctor, akiwa amesha livua, yupo na mwanamke mmoja hivi wame beba mtoto mkoni, yule kaka akaongea na simu, akisema ‘ndio tuna toka kwenye jengo ili, vipi kuna ishu?” alisimulia nesi yule, akielezea tukio alivyo liona yeye, akaendela kusimulia kuwa baada yahapo akuwajali tena, maana aliowaona waktoka nje ya jengo hilo, la wazazi kisha wakapotelea kwenye magari, na dakika mbili baadae akawaona wakito, nesi yule alieleza kuwa saa saba usiku alipandisha ghlofa ya pili ili amstue mwenzie awapatie wagonjwa dawa, ndipo alipo mkuta ame sha uwawa, kitu cha kushangaza apakuwa na report yoyote ya kuonekana fedha, pia yule polisi akaeleza kuwa, tukio jingine ambalo hakuweza kulitambua vizuri, kuna mwanamke mmoja amekimbia na kuacha maiti ya mwanae kitandani, na mbaya zaidi hakuna kumbu kumbu yoyote, iliyo andikwa juu ya mwanake kulazwa chumba hicho ch VIP, pia yule koplo alimkabidhi insp Johnson simu tatu za maremu wote, “ok! naomba vipimo na harama za vidole katika miili ya maehemu” aliongea insp Johnson, ambae alionekana kuchanganyikiwa na tukio hilo ambalo mpaka hapo ni tukio moja, itaendelea ………..

