BINTI MDUNGUAJI (50)

SEHEMU YA HAMSINI

ILIPOISHIA SEHEMU YA AROBAINI NA TISA: kumbe lengo lake likiwa ni kumvamia na kundi kubwa la askari kisha wammiminie risasi na kumpoteza kabisa, wakidai alijaribu kupambana na polii akiamini ndio utakuwa mwisho wa mauwaji na kwamba baba yake anakuwa ameepuka kifo, wakati anapanga hayo insp Johnson alijuwa fika kuwa lazima atumie hakili nyingi sana kuzungumza na mzee Soud ili akubari kumwelekeza nyumbani kwa mzee Nyati, na kisingizio kikubwa ni kuwa anaenda kuongea nae kutafuta suruhu, endelea ………
Nusu saa baadae insp Johnson alikuwa nyumbani kwa mzee Soud akiongea nae juu ya wazo lake la kukutana na mzee Nyati, “sikia Johnson, swala lako ni zuri sana na lina faa kumaliza huu mgogoro, lakini je una uakika kuwa, unania ya kuongea na bwana Nyati?” aliuliza mzee Soud huku akitabasamu, kisi cha insp kujistukia juu ya ule mpango wake wa kwenda kuvamia kwa mzee Nyati, “yesi mzee mpango wangu niuo, sababu ata wewe uliwai kusema kuwa, ndio njia pekee ya kumaliza tatizo hili, ila ikitokea kuwa tukishindwa kuelewana, nitatumia plan B” aliongea insp na hapo mze Soud alicheka kidogo, “vipi mzee mbona unacheka kuna tatizo, mbona unacheka?” aliuliza insp huku akionyesha mshangao kidogo, “sijajuwa hiyo plan B, lakini usi jali” aliongea mzee Soud huku akisimama na kueleka kwenye kabati, akachukuwa kalamu ya wino, na karatasi, akarudi mezani, na kuanza kuandika, kwenye lile karatasi, “hii ni namba ya simu ya mtu atakae kuwa mwenyeji wako” aliongea mzee Soud huku akiendelea kuandika, na hapo anime andika jina la mtaa, ambao ata mimi nilipoenda Songea, nilikutana na mtu huyo, na akanielekeza kwa bwana Nyati” aliendelea kuongea mzee Soud huku akimkabidhi ile karatasi insp Johnson, ambae alilipokea na kulitazama kidogo, kisha akaliweka mfukoni, kisha akamtazama mzee Soud, “kuna lolote unataka unieleza au naweza kuondoka?” aliuliza insp Johnson, “tatizo lipo, nakuomba usije kujaribu kufanya jambo lingine lakipuuzi, maana ukijaribu kufanya kitu kingine chochote cha kipuuzi, utasababisha damu nyingi sana kumwagika, na mmoja wawatu watakao mwaga damu utakuwa wewe” aliongea mzee Soud hapo alikuwa akionea kwa umakini sana, akionyesha jambo analo ongea ni muhimu kulizingatia, “inamaana anauwezo wa kupambana na kombania ya polisi wa kutuliza ghasia?” swali hilo la Johnson lilimfanya mzee Soud acheke kidogo, usifikilie kumzibiti Nyati, kwa nguvu hiyo ndogo ya kijeshi” aliongea mzee Soud huku akiendelea ucheka, “nazani mzee Soud umeanza kusahau muhundo wa kivita, sija sema section, nimezungumzia kombania, na maanisha watu zaidi ya themanini” aliongea insp Johnson, akiwa na uakika mzee Soud akumwelewa mwanzo, “inawezekana wewe ndie ujanielewa vizuri, na inawezekana pia uja mfahamu vizuri mtu ane itwa Michael Francis Nyati” maneno hayo ya mzee Soud yalimstua kidogo insp Johnson, “inawezikanaje?” aliuliza insp kionyesha kuto kumwamini mzee Soud, “achilia kombania ya polisi, aliwai kuwaokoa watu sita wakiwepo baba yako na hao marehemu, katika kambi kubwa la jeshi, lenye silaha nzito, alitumia saa moja tu!” mpaka hapo insp Johnson alijikuta akisisimkwa na mwili wake, akatulia kidogo na kupitisha mawazo kichwani mwake, “mh! inawezekanaje, askari mmoja, kambi zima, hapana huyu mzee anajaribu kunitisha, ili nisiende kumkamata huyu mshenzi” aliwaza insp akisahau kuwa toka mwanzo wa upelelezi wake amekuwa akisaidiwa sana na mzee huyu, insp Johnson akukaa sana akaaga na kuondoka zake, akimwakikishia mzee Soud, kuwa lengo lake ni kufanya mazugumzo na sio kupambana na mzee Nyati, safari ya bwana Johnson ili kuwa ni ofisini kwake, kituo kikuu, kwenda kuonana na mkuu wakitengo cha upelelezi wa makosa ya jinai, leo week end alikuwa ofisini kutokana na matukio ya mauwaji mfurulizo yaliyotokea usiku, ** saa nane mchana Denis alikuwa anamchukuwa mke wake kutoka hospital ya Matumaini kwa Dr Stellah, shangazi yake Jayden, (#shangazi anataka) na kuelekea nyumbani tayari kuandaa safari ambayo mwisho wasiku, walipanga waende wote wawili kwamba Denis mwenye ndie ampeleke, japo ilikuwa ni ngumu sana kwa Jackline kukubaliana na Denis swala hilo, lakini Denis alikuwa king’ang’anizi akitoa sababu za msingi ambazo Jackline alishindwa kutoa sababu za kukataa, kupelekwa na mume wake, ambae alisema kuwa kutokana na mtoto kuwa na umri mchanga sana, si vyema kusafiri nae kwenye basi, “lakini mume wangu aita kuwa vyema kwa wew kufika nyumbani kwetu, sababu bado uja peleka barua na kujitambulisha kuwa ni mchumba wangu, yani kwetu tuna sharia kali sana kwetu” aliongea Jackline, kwa sauti ya upole na upendo wa hali ya juu, “dah! sijuwi itakuwaje lakii siyo lazima nifike nyumbani kwenu, naweza kuishia ata sehemu nyingine kisha tukaomba mtu akupeleke” alitoa ushauri Denis, “ebu subir niongee na baba kisha nita kupa jibu, kama ata kurhusu ufike nyumbani au uishie sehemu nyingine” aliongea Jackline ambae alikuwa anafahamu kuwa wazazi wake walitegemea wasafari nae kesho yake, ** insp Johnso ambae alionekana na pilika nyingi sana, alienda ofisini kwa mkuu wa upelelezi, licha ya kumpa report ya vifo vya mzee Alex na wale wa Muhimbili, pia alimweleza mpango wake wa kwenda Songea, alimweleza kuwa anaenda kumkatama mzee mmoja anaeitwa Michael Nyati, kuwa anamshuku mtu huyo, kuusika na mauwaji yaliyotokea jana usiku Cosovo Hoel, akisema kuwa sababu huyu mzee licha ya kutoweka baada ya tukio, pia ni asakari aliekuwa ana tafutwa na jeshi la ulinzi, baada ya kutoroka akiwa na silaha za kijeshi, insp aliomba apatiwe silaha na askari ili aweze kumkamata mshukiwa huyu, wa mauji yaliyotokea Cosovo, baada ya kueleza mpango wake, mkuu wa upelelezi alikubari mpango huo, na alimsisitiza insp kuwa mpango huo uwe wasiri, akamweleza kuwa wataanza maandalizi jumatatu, waliagana huku mzee huyu akionyesha kulizika na mpango wa insp Johnson, na aliombea ufanikiwe maana muuwaji huyu, alikuwa analizalilisha jeshi la polisi, na serikali kwa umla, hapo insp Johnson akaondoka zake, kuelekea nyumbani kwake akipanga kesho mapema kukutana na baba yake, akimwacha mkuu wa upelelezi akiwa ofisini kwake akipitisha mawazo kichwani mwake, mkuu huyu wa pelelezi alijaribu kuvuta kumbukumbu za mauwaji, yaliyofanywa na muuwaji huyu, ambae baadhi ya matukio yanaomyesha kuwa ni mwanamke, lakini anae tajwa ni mwanaume, “lakini huyu mtu anaonyesha kuwa anauwa waalifu” hapo mzee huyu mwenye nyota nyingi mabegani, aliwaza hayo huku akikumbuka mauwaji ya mchungaji chilumba, ambae aliuwawa guest House pale Kmamnga Plaza, “mchungaji na guest wapi na wapi?” aliendelea kukumbuka mauwaji ya vijana watatu, wenye visu, ndani ya chumba kilicho pangwa na mwanamke, “haya sasa na awa nao sijuwi walikuwa wana iba mtoto wa nini?, lakini kwanini yeye afanye kazi hiyo ya kuuwa waarifu?” ilo ndio lilikuwa swali la msingi, mwasho wa siku afande huyu akamaliza kwa kusema kwa sauti yachini na kusimama, “muuwaji wa wauliwa wote waalifu” mkuu wa upelelezi, akatoka nje na kuondoka zake, ** tayari Jackline alisha mpigia simu baba yake, na kumweleza ung’ang’anizi wa mume wake, kuwa anataka ampeleke mwenye Songea, hapo mzee Nyati kwakutumia hakili akajuwa kuwa endapo wata endelea kuzuwia Denis asiende Songea, watamfanya amtilie mashaka mtoto wao na kuanza kumfwatilia kwa ukaribu, kwania ya kupafahamu kwao na wazazi wao, pengine waliofia Denis anaweza kuzani Jackline anampango wa kuto kumtambulisha kwao, na kuachana nae katika siku za mbele, hivyo walikubari kuwa kijana huyu aende Songea, ila mzee Nyati akapanga ya kwake, ili Denis asifahamu ukweli juu ya familia yao, ** siku ya pili safari ilianza mapema sana, gari aina ya Toyota noah lili sheheni mizigo, ambayo mingi ilikuwa ni zawadi kwa baba na mama, Jackline akiwa ameacha zana zake amesha zihifadhi vizuri, sababu pale nyumbani walimwacha kijana mmoja ndugu wa boss wake Denis, alinde nyumba, safri aikuwa na tatizo lolote, japo ilikuwa ni a mwendo wa taratibu sana, kiasi chakuwa fanya wachelewe kufika Songea, ambapo waliingia saa saba usiku, wakapitiliza na kuelekea kijijini kwa kina Jackline, ambako ni pembeni ya mji, huko walipokelewa na mzee mmoja wa makamo, alie jitambulisha kuwa ni baba yake Jackline, pamoja na kijana mmoja, usiku ule Denis akuweza kuona mazingila ya kijiji kile, ila asubuhi siku ya pili Denis alijikuta akiamka toka kwenye nyumba ya udongo, yenye ukubwa wa wastani, iliyo zungukwa na migomba ya ndizi, na mazao mengine ya msimu kama mboga mboga mboga na nafaka, jilani hapakuwa na nyumba nyingine zaidi aliweza kuona kitu kama mtaa mdogo, ulio zungusiwa uzio mkubwa sana katikati ya msitu, alipo uliza akaambiwa kuwa ile ni nyumba ya tajiri mmoja wapale mkoani, asubuhi ile pale nyumbani, zaidi ya Jackline na yeye mwenyewe palikuwa na binti mmoja mdogo kidogo, alie valia kama wakazi wengine wa vijijini hapa Tanzania, tunavyo zowea kuwaona wakivaa, kwa kipindi kile) “baba na mama wapo wapi?, alafu na yule kijana alie tupokea jana usiku, pia simwoni” aliuliza Denis, “waliondoka jana usiku, awa ruhusiwi kukaa pamoja na wewe, mpaka utakapo jitambulisha, hivyo awata rudi mpaka uondoke” aliongea Jackline wakati huo walikuwa wana kunywa uji na na viazi vitamu, “aina tatizo wacha niende nikafanye utaratibu wa kuwajulisha ndugu zangu ili waje walete barua, maana sasa itakuwa kasheshe, unajuwa nimeshindwa kuwa kabidhi zawadi zao” wawili awa waliongea mengi sana, wakijadiliana swala hilo, japo upande wa Jackline alisisitiza kuwa, Denis asifanye lolote, mpaka yeye atakapo rudi Dar, ** siku hiyo ya jumapili, Insp Johnson aliamka mapema sana akiwa na mke wake, wakaenda kanisani, na baada ya kumaliza ibada, wakaenda nyumbani, kwa wazazi wa insp Johnson, huko kinyelezi mwisho, bahati ilikuwa upande wa Johnson, maana walimkuta mzee Masinde ndio kwanza anapata supu, aliyoandaliwana mke wake, ni baada ya mzee huyu leo hii kuamka akiwa amekosa nguvu za mwili, maana siku iliyopita akuweza kupata muda na hamu ya kula, kutokana na kunywa pombe kali nyingi sana, baada ya kusalimiana, mke wa insp Johnson akaenda upande wa jikoni, akikaa na mama mkwe wake, na Johnson akabakia na baba yake, ambae kumtazamo, alionekana kukata tamaa, pale sebuleni, insp alimweleza baba, kuwa ame pewa uamisho wa muda kwenda Songea, kumchunguza Michael Nyati, “mwanangu sikiliza unachotaka kukifanyani kitu cha hatari sana, nakuomba kataa hiyo safari” aliongea mzee Masinde kwa msisitizo, “kwa nini baba, lazima huyu mtu akatwe na ikiwezekana amalizwe kabisa, maana ni hatari sana kwako,” hapo yakaanza majadiliano, huku mzee Masinde akisisitiza kuwa Nyati siyo mtu mzuri, ata kidogo, endapo atagunduwa kuwa anafwatiliwa, ni wazi kuwa atapoteza maisha ya Johnson, baada ya majadiliano ya mda mrefu wakakubariana kuwa, litakapo kuja jukumu la kumkamata mzee Nyati, basi Johnson akae mbali na eneo la tukio, ** mpaka juwa linazama jumapili ile, Jackline na Denis, walisha kubariana kuwa siku inayo fwata Denis arudi Dar, ilikuwapa nafasi wazee waje wamwone mjukuu wao, na kweli siku ya pili ambayo ni jumatatu Denis aiondoka mapema sana, toka Songea, akiwa meshindwa kukaa na kuongea na wazazi wa Jackline, kutokana taratibu za kimila za wakina Jackline, ** huku nako siku saa mbili na nusu mkuu wa kitengo cha upelelezi alikuwa ofisini kwa General of Polisi (GOP) akimweleza juu ya mpango wa kwenda zingila na kumkamata Michael Nyati, huku mkuu wakitengo cha upelelezi akimweleza GOP jinsi wanavyo muusisha mzee huyo na matukio ya mauwaji, yanayo endelea ndani ya jiji la dar, mkuu wa jeshi la polisi hakuwa na kipinga mizi juu ya jambo hilo, aka mpa kibari cha kuandaa askari na silaha, kwaajili ya zoezi hilo la kumtianguvuni mzee huyo hatari sana, *** kazi ya maandalizi ilitumia siku saba, wakichuliwa askari polisi stini, toka mikoa mitatu, Mbeya Lindi na Mtwara, wakichaguliwa skari wenye uwezo mkubwa sana kimapigano, taalifa ilitumwa kwa kamanda wapolisi mkoa wa Ruvuma, akielezwa kuwa kuna askari polisi wata ingia mkoani kwake kwa kazi maalumu, na kwamba wasi buguziwe,wakwanza kufika Songea alikuwa ni insp Johnson na PC Busungu, ambao walitangulia kwaajili ya kwenda ufanya uchunguzi, baada ya kufika Songea moja kwa moja insp Johnson alienda kwenye mtaa ulio andikwa kwenye namba ya simu aliyopewa na mzee Soud, insp akiwa kwenye mtaa wa Lizombe, mtaa wenye maduka makubwa sana, akapiga ile namba ya simu aliyopewa na mzee Soud, “hellow unaongea na felister, nikusaidie tafadhari” ilikuwa nisauti tamu ya kike iliyo mfanya Johnson asisimkwe kidogo, kabla ajamkumbuka yule mwanamke hatari sana, alie wi kumshuhudia akitembeza mkong’oto “na itwa Vasco, nipo mtaa wa Lizombe, naitaji kukuonana na wewe” aliongea insp Johnson ambae alikuwa jirani kabisa na Pc Busungu, itaendelea …..

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!