BINTI MDUNGUAJI (51)

SEHEMU YA HAMSINI NA MOJA

ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI: insp akiwa kwenye mtaa wa Lizombe, mtaa wenye maduka makubwa sana, akapiga ile namba ya simu aliyopewa na mzee Soud, “hellow unaongea na felister, nikusaidie tafadhari” ilikuwa nisauti tamu ya kike iliyo mfanya Johnson asisimkwe kidogo, kabla ajamkumbuka yule mwanamke hatari sana, alie wi kumshuhudia akitembeza mkong’oto “na itwa Vasco, nipo mtaa wa Lizombe, naitaji kuonana na wewe” aliongea insp Johnson ambae alikuwa jirani kabisa na Pc Busungu, endelea …………..
“ok! Vasco, unainshu ya kibiashara au binafsi?” ilisikika ile sauti tamu ya mwana dada alie jitambulisha kwa jina la Felister, “mbona unawasi wasi mrembo, nielekeze ulipo, tukikutana utajuwa” aliongea insp Johnson ambae alidanganya jina, huku akiiweka sauti yake, kuwa ya ucheshi na mzaha, “mh! haya bwana subiri kidogo” aliongea Falister kisha akakata simu, “amesema tusubiri kidogo, pengine anajlemba kidogo, si unajuwa watoto wakike” aliongea Johnson akimtazama Busungu, “hiyo safi, ila mimi nina ushauri” aliongea Busungu, akitazama mazingila ya mtaa ule ulio changamka sana, na kujaza watu wengi waliokuwa katika pilika pilika, pia magari mengi yaliyoegeshwa pembeni ya barabara, na wengine yakikatiza kwa mwendo wa taratibu, “lete mchapo nakuaminia sana busungu” aliongea Jonson kwa shahuku, “ujuwe nini, huyu mtu ni mtu tunae mfwatilia ni mjana sana, lazima tutumie hakili nyingi sana, ushauri wangu ni kwamba tusiende wote kukutana na huyu mwanamke, ili iwe lahisi kuwa fawatilia endapo tutaitaji njia nyingine ya kupajuwa kwa mzee Nyati” ** kiukweli mda huo, Felister alikuwa pamoja na Jackline, na binti wa kazi alie andaliwa kwaajili ya malezi ya mtoto, wanatoka hospital ya mkoa, aliko mpeleka mtoto kwenda kumalizia bahazi ya sindano za chanjo za mtoto, “kuna mtu anasema yupo Lizombe, anataka kuonana na mimi” alisema Felister, akimtazama Jackline, aliekaa set ya nyuma ya tiyota lav 4, “basi tuelekee huko mala moja, alafu ndio twende nyumbani” alishauri Jackline, ambae alikuwa amekaa seat ya nyuma ya gari, amemshika mtoto wake, na Felister ambae aliekuwa anaendesha gari akakatakona, kuelekea mtaa wa lizombe, “amesema anataka nini?” aliuliza Jackline, “ajasema shida yake, nitaenda kujuwa huko huko” alijibu Felister ambae ni msimamizi wa miradi ya mzee Nyati, iliyopo hapa mjini Songea, “Sophi, nitolee simu yangu, kwenye huo mkoba mdogo” aliongea Jackline akimwambia binti wake wa kazi aliekuwa amekaa seat ya mbele, pembeni ya Felister, safari iliendelea kwa mda wa dakika kumi kasoro, walikuwa wanaingia kwenye mtaa wa lizombe, maa simu ya felister ikaita, lakini akuipokea kwanza akasimamisha gari mita chache toka kwenye jengo lenye ofisi yake, ambalo lime pambwa na maduka makubwa matatu nje yake, ambayo mda huu yalitapakaliwa na watu waliokuwa kwenye shuguli mbali mbali za manunuzi na au matembezi na shuguli nyingine kama hizo, alipo simamisha gari akaitazama namba yasimu, “huyoooo anapiga” alisema Felister huku akiipokea simu, “hallow” aliita Felister baada ya kupokea simu, “naona uenisahau kabisa mwenzio nime ganda hapa na kusubiri” aliongea insp kwa sauti ya kulalamika flani, “ok! hupo sehemu gani?” aliuliza Felister hku akiangaza macho huku na huku, kuangalia watu waliopo eneo lile, “nipo hapaaaa karibu naaaa….. duka la dawa” hapo Felister akatazama kwenye duka la dawa, “ok! duka la dawaaaa!” aliongea Frister, kisha wote watatu ndani ya gari wakageuza shingo zao, kutazama kwenye duka la dawa, ambalo lilikuwepo mita kama hamsini mbnyuma yao maana mtaa hule kulikuwa na duka moja tu! la dawa” licha ya uwepo wa watu wengi maali pale, lakini waliweza kuwaona vijana wawili waliosimama pamoja huku mmoja akiongea na simu, huku yule mwenzie akionekana kusogea karibu kabisa ya mwenzie ili kufwatilia mazungumzo, “yes, nipo hapa vipi umekaribia?” ilisikika ile sauti ya kijana alie jitambulisha kuwa ni Vasco, wakati huo Jackline alikuwa anajitaidi kuvuta kumbu kumbu, ya kuwa aliwai kuwaona wapi vijana wale, kabla Felister ajasema lolote, Jackline akamstua Felister na na kumwonyesha ishala ya kuto kusema lolote, kisha akamnongo’eza “mwulize yupo nani” Felister akafanya kama alivyo elekezwa, “ok! umesimama peke yako au hupo na wenzako?” aliuliza Felister huku wote watatu wakiwatazama Busungu na Johnson, wakawaona wana kunyezana kitu flani kwa ishara za mikono yao na kunong’onezana sikioni, kisha wakamwona yuke le alieshika simu akiongea, nipo mwenyewe mrembo mbona unamaswali mengi sana” kwa jubu ilo la mtu anae jiita Vasco wote wakatazamana huku wana tabasamu, huku Jackline akimwnong’oneza jambo Felister, kisha Felisteer akaongea kwenye simu, “ok baada ya dakika tano nita kuwa hapo wewe sogea mbele ya jengo kubwa la maduka matatu, nitakukuta hapo, aliongea Felister, huku bado wana wafatwatilia wale vijana wawili, ambapo waliwaona wakitazama tazama huku na huku, “ok! naliona nilile pale jengo kubwa, lenye watu wengi, poa dada yangu, usichelewe” hapo felister akakata simu, kisha wote wakabaki wana watazama wale vijana wawili ambao walijadiliana kidogo, kisha wakaanza kutembea, wakija uswa wagari lao, na kulivuka, wakaendelea kutembea wakilifwata jengo kubwa la kibiashara, linalomilikiwa na mzee Nyati, wakiwa wana watazama walw vijana wawili waliwaona wakilifikia lile jengo la maduka matatu, kisha waka onekana wakiongea jambo, alafu yule kijana mwingine ambae alikuwa akifwatilia mazungumzo ya mwenzie kwenye simu, akivuka barabara, na kuamia upande wapili, na kuelekea kwenye benchi la msafisha viatu shoe shine, kisha akaonekana akipatana bei ya kusafishiwa viatu vyake, na kisha kuvua viatu na kuvaa ndara, akiwacha mwenzie amesimama nje ya jengo la maduka matatu akitazama huku na huku, “wale ni polisi” aliongea Jackline kwa sauti ya chini, Felister aka duwaa, “tena nina wafahamu vizuri sana, ndio polisi wanao fwatilia ile inshu” aliongea Jackline akimtazama Johnson, aliekuwa amesimama mbele ya jengo kubwa, linalo milikiwa na baba yake, “ebu ngoja kwanza” alisema Jackline huku akibonyeza simu yake kumpigia baba yake, ** wakati huo mzee Michael Nyati, alikuwa pamoja na mke wake, ndani ya andaki lake kubwa sana, analo ifadhia silaha zake za kivita, pamoja na malizake zote zinazo mpatia utajiri, zikiwemo zile almas alizo tokanazo Congo, mwaka 1988, na fedha nyingi sana ambazo kikawaida asinge weza kuzimaliza kwa miaka ya hivi Karibuni, ni andaki lenye ukubwa wa mita 40, lililo jengwa kisasa mfano wa nyumba ya kisasa, yenye vyumba vinne na choo ndani yake, “hallow Jack kunatatizo?” aliuliza mzee Nyati kwa mshangao, baada ya kupokea simu toka kwa mwanae Jackline, “baba, nime waona wale polisi waliokuwa wana ni fwatilia dar” mzee Nyati alistuka sana baada ya kusikia hivyo, ume waona wapi na wanataka nini?” aliuliza mzee Nyati, na Jackline aka msimulia jinsi wale polisi walivyopiga simu na kuomba kukutana na Felister, Jackline pia akamweleza baba yake kuwa, polisi hao, wapo nje yajengo lao la kibiashara, na wame jitenga kwa mda huku mmoja akijifanya yupo peke yake, “ok! mwache Felly akamsikilize na akitaka kkupajuwa kwangu, amwelekeze nyumba ya udongo, pia akikishe ana nijulisha kila atua, awe mjanja anapjibu maswali ya hao watu, na wewe mwenyewe rudi nyumbani haraka” huo ndio ulikuwa mwanzo wa mpango wa mzee Nyati, ** baada ya kusimama kwa dakika nne pale nje ya jengo alilo elekezwa na binti alie jitambulisha kuwa ni Felister, mala aka sikia simu yake inaita toka mfukoni, akaitoa na kuitazama, akaona ni namba ya yule binti anae msubiri, Johnson akamtazama Susungu aliekuwa amekaa upande wapili wa babara, kwenye benchi la mg’alisha viatu, wakatazamana kisha Johnsonakanyesha ishara ta dole gumba, kisha akaipokea simu, “hallow .. hallow..” aliita Johnson pasipo kujibiwa, akaitazama simu yake ilikuwa ilisha katwa, wakati ashngaa kilichotokea akastuka akiguswa bega, insp Johnson alikutana na sura tulivu ya mschana mrembo, “habari yako kaka nazani wewe ndie Vasco?” ilisikika sauti ya uchangamfu iliyo ambatana na tabasamu toka kwa mrembo huyu, “hoo, naniiiii felister, ndio mimi Vasco” aliongea insp Johnson, akiusanifu uzuri wa binti huyu, “ok! bwana Vasco, sijuwi tuna weza kuongelea apa au ofisini?” aliuliza Felister huku akimtazama usoni bwana Vasco, “ata hapa hapa aina shida” aliongea Johnson au Vasco wa bandia, “ok! sawa kaka Vasco nina kusikiliza” hapo Johnson akajitambulisha kama kijana toka Mtwara alie agizwa kwa mzee Nyati, “ok! huyo mzee ni jirani ya babu yangu kule kijijini, ningekuwa na namba yake ninge kupatia, ila siyo mbali, ngoja nikuelekeze” aliongea Felister akianza kumwelekeza Vasco wa bandia, sehemu anayo patikana mzee Nyati, kisha wakaachana, na Felister akaingia ndani ya jengo kubwa la maduka matatu, akimwacha Vasco anavuka barabara na kumfwata Busungu, pale kwa mngalisha viatu, ambapo busungu alivaa viatu na kisha kuondoka zao, pasipo kujuwa kuwa, Jackline alikuwa ametulia ndani ya Toyota lav 4, akiwatazama wakiondoka zao kuufwata uchochoro wa kuelekea mtaa wa pili ambao ni mtaa wa mpambalioto, hapo Jackline akawasha gali na kuelekea mtaa wa Mpambalioto, akizungukia bara bara kuu, nikiasi cha dakika zipatazo mbili tu, tayari Jackline alikuwa amesha simamisha gari usawa wa mtaa huo tulivu sana, ambao ulikuwa na magali machache makubwa, taliyo simama kiasi cha kulizuwia gari la polisi upelelezi, aina ya land rover 110, sekunde chache baadae Jackline akiwa ndani yagari lake aliwaona wale polisi wawili wakiingia ndani ya lile gari la polisi, na kuondoka zao wakipita jirani na gari lake, “wajinga nyie subirini mnacho stahili” aliongea Jackline, akilitazama gari lile kupitia side mirror, ambapo alilitambua kuwa ni gari la polisi, akachukuwa simu yake na kumpigia baba yake, “baba, ni kweli kama nilivyo kuambia, ni polisi, ambao nili pambana nao siku ile buguruni, na kwa uakikazaidi, wameondoka na gari la polisi upelelezi lenye namba za kilahia” Jackline alimwambia baba yake baada tu ya mzee Nyati kupokea simu, “ok! umefanya vyema kuwa fwatilia, pia Felister ameniambia kuwa kijana huyo anaitaji kuongea na mimi” *** kiukweli mzee Nyati tokea alipo sikia ujio wa vijana awa waliojifanya ni vijana toka mtwara, wanataka kuonana nayeye, “kwa njia wanayo pitia, ni wazi wameelekezwa na mzee Soud, maana na yeye alifikia kwa Felister, kabla ya kuja Nyumbani kwangu, huyu mzee ameshakuwa tatizo kwangu” itaendelea ………..

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!