
SEHEMU YA HAMSINI NA TATU
ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA MBILI: Ilimfanya Johnson agundue kuwa, hapa kuwa na suluhu mahali hapa, sababu mzee huyu alikwepa sana kuombwa msamaha, “kiukweli sija wai kujiuliza” alijibu insp “ok! labda ufanye kitu kimoja, nenda kaongee nae, ikiwezekana mpigie simu, akueleze vizuri, pengine ni hisia tu, maana sio kila kosa hadhabu yake ni kifo” aliongea mzee Nyati kwa sauti yenye busara na hekima, iliyo mchukiza Insp ambae alijikaza kisabuni, na kuzuga kwa tabasamu la kinafiki, ENDELEA ………..
“nikweli unachosema mzee, lakini kwanini uliwakimbia wenzak nchini congo na kuamua kuacha jeshi?” aliuliza insp Johnson, akiwa na uakika kuwa, ilo swali litamfanya mzee Nyati aleze ukweli, juu ya kisa kilichotokea huko congo, lakii alishangaa kuona mzee Nyati anatabasamu, tena tabasamu tulivu lililo onyesha kuwa mzee huyu, alikumbuka kitu kilicho mletea machungu moyoni, “labda nikuulize kijana Jaffari, unazani samaki anaweza kutoroka toka ndani ya bahari, na kukimbilia nchi kavu?” hapo Johnson na Busungu wakatazamana, kama wanaulizana kitu cha kujibu, kisha wakamtazama mzee Nyati, “nikweli aiwezekani mzee, sasa ilikuwaje ukaacha kazi jeshini?” safari hii aliuliza Busungu, hapo mzee Nyati akacheka kidogo, “sikuacha jeshi, ila jeshi liliniondoa jeshini” alijibu mzee huyu akiwa ana uakika wajibu lake, “kwa nini una sema hivyo mzee?, wakati kumbu kumbu zinaonyesha kuwa, uliacha jeshi kwa kutoroka?” aliuliza insp Johnson, akiwa na uakika kuwa lazima mzee Nyati, ata ingia mkenge na kuongea ukweli wote, “kumbu kumbu za wapi labda, alizo kuambia mwijage, au mzee Soud?” swali hili ndilo lililo mfanya insp Johnson, agunduwe kuwa maelezo yake yamevuka mpaka, kiasi cha kutaka kuweka wazi kificho chake, wakatazamana kidogo, kisha wakamtazama mzee Nyati, wakosa jibu, mzee Nyati aliligundua hilo, akatabasamu kidogo, “ok! tuyaache hayo, ila alie kusimulia ajakueleza ukweli harisi, ukweli ni kwamba jeshi lilini futa kazi, baada yakuto kuniona mda mrefu, na walichukua maamuzi hayo, pasipo kujuwa kilicho nikuta” aliongea mzee Nyati kisha akazungusha sjingo yake kutazama pande zote za eneo lile, “ona mazingira ninayo ishi, unazani ninge kimbia dar, kuja kukaa huku kwenye misitu ya matogoro (mapori)?” aliongea mzee Nyati na wakina Johnson nao waka tazama ule msitu, amba aukuwa na nyumba nyingine zaidi ya majengo ya kifahari, yaliyoonekana kwa mbali kidogo kati kati ya msitu mnene, kiukweli maswali mengiayakuwa na ajibu kwa polisi awa wawili, ambao waliaga na kuondoka zao, wakiaaidi kurudi siku yoyote kwa maongezi zaidiwakachukuwa namba ya simu, ya mzee Nyati, na kiondoka zao, pasipo kujuwa kuwa mita mia tatu ndani yamsitu ulio wazunguka, kwenye mwinuko mmoja, mkubwa wenye majabari makubwa ya mawe, alikuwepo Jackline Nyati, ame kaa mkao wa kusaka roho, huku kilengeo cha silaha kubwa aina ya sniper lifle model 81, toka marekani, akiwatazama, na kufwatilia mazungumzo yao, na kama kuna chochote kitakacho tokea, mzee Nyati na mke wake waliwasindikiza kwa macho wageni wao, mpaka walipo potea kabisa nagari lao, ndipo mama Jackline alipo simama toka pale alipo kuwa amekaa anaosha vyombo, aka funua bahadhi ya vyombo na kutoa bastora yake, kisha akatazama upande aliokaa Jackline kule porini, akanyoosha mkono juu, na kuonyesha ishara ya kuzungusha kidole kimoja hewani, “wanajifanya wajana kuliko mimi, nawasubiri mkija tena” alongea mzee Nyati huku akiachia tabasamu la muahayo wa simba, ** insp Johnson na Pc Busungu, waliendelea na safari yao wakifwata njia waliyo jia, “unajuwa Busungui kunakitu kina nishangaza sana, na akuna shaka, juu ya huyu mzee, kuwa anausika na mauwaji haya” aliongea insp wakati wana kata kona kuifwata bara bara ya jwenda mjini, wakiiacha ile ya kwenda kijiji cha Mahilo, “kiukweli ukimtazama juu juu unaweza kuzani hausiki, lakini ukimsikiliza majibu yake anausika kabisa, lakini mbona ni masikini sana?” aliongea Busungu, akionyesha wasi wasi juu ya mzee Nyati, “unajuwa nini mimi nahisi huyu mzee kunabishara haramu anaifanya, ndio maana amejificha huku porini, sababu nime mwona kwa macho yangu akitoa million moja tathlim” wwaliongea wawili hawa huku safari yao ikiendelea, “yani busungu, hapa kilicho bakia ni kummaliza tu huyu mzee, vinginevyo tutaoneka atajuwi kazi, nakulitia aibu jeshi la polisi” aliongea bwana Johnson, wakati huo walikuwa wamekaribia pale walipo mwacha Side Tall, ambae sasa alikuwa anafunga mzigo wa kuni, “ebu simama tuongee na huyu dogo” aliongea Johnson, na Busungu akasimamisha gari, “side njoo mala moja” aliongea Johnson, na kijana Saidi akalisogelea gari, “vipi mme mkuta mzee Nyati?” aliuliza Saidi, baada ya kuwafikia, “tume mkuta bwana, ila side unazani yule mzee aakuwa anafanya bishara gani kule polini” aliuliza Johnson, “kuhusu bishara sijuwi,” aliongea Saidi, akitikisa kichwa kukataa, “sikia side ebu kamata hii” aliongea insp, huku akiingiza mkono mfukoni, na kutoa noti ya shilingi elfu tano, akampatia Said, “yanini tena blaza?” aliuliza Side kwa mshangao, “usijari bwana side, yani umekuwa rafiki mzuri sana kwetu, bila wewe tusinge fika, ebu nipattie namba yako yasimu” aliongea insp Johnson, kisha haraka sana Side akataja amba zake zasimu na wote wawili wakaziandika kwenye simu zao, “sikia bwana side, kunakitu nataka utusaidie, na ukifanikiwa, nakuaidi utafurahi sana” aliongea insp pasipo kujuwa kuwa anamfundisha samaki kuogelea, “nitakuwa nakupigia simu kukuulizia kuhu huyu mzee, jitaidi simmu yako iwe hewani, “usiwe na wasi wasi blaza, we piga mda wowote nitaj]kupa habari, na sasaivi nita mfwatili kila anakokwenda, insp Johnson na Busungu, wakiwa wamelizika kwa kitu walicho kipanga na Said, waliondoka zao, kuelekea mjini, Saidi aliwatazama paka walipo potea kabisa kisha akaurushia ule mzigo wakuni porini, alafu akapekua pekua kwenye kishaka pembeni ya barabara, akaibuka na bnduki aina ya SMG, akaingia porini na kutokomea zake, ** huyu anaitwa Side, ni kijana alie ajiliwa na mzee Nyati, miaka saba iliyopita, siku ambayo Said n wenzie wanne walijaribu kuingia kwenye jumba la mzee hyu kwa lengo la kuiba, wakiwa na uakika kuwa mzee Nyati na mke wake walikuwa wamesafiri, lakini awakufahamu kuwa, kuna binti hatari sana, zaidi ya baba yake, ambae aliwapa kifinyo kilicho sababisha Said asiweze kusahau mpaka leo, maana aliwapoteza wenzake wote, na yeye kupoteza fahamu kwa mda wasiku tatu, alizinduka akijikuta ndani ya msitu mkubwa sana, na bahati yake siku hiyo ndio siku ambayo mzee Nyati alikuwa amerudi, na alienda kuifukia mizoga hiyo ambayo Jackline alishindwa kuipeleka mbali, hivyo mzee Nyati aliibeba na kuingia nayo msituni, wakati ana chimba shimo, ndio akamwona mmoja kati ya wale wavamizi akizinduka, baada ya maojiano, mzee Nyati aliamua kumwajil kama mfanyakazi wake wa shughuli za mifugo, kwa shalti la kuto eleza jambo lolote juu ya maisha ya pale nyumbani, mwisho akaanza kumwusisha kwenye shughuli zake za siri, ** baada ya kutoka kwa mzee Nyati polisi awa wawili wakarudi polis mess na kuchukuwa ramani yao ya mji wa Songea na kuanza kuikagua sehemu ile anayo ishi mzee Nyati, huku wakiangalia namna ya kupanga majeshi yao, kwaajili ya kuzingira na kumwangamiza mzee huyu hatari, ** wakati huo huo mzee Nyati nae, baada ya kupokea taalifa zote toka kwa bwana Saidi, akakaa pamoja na mke wake na mwane Jackline na kuanza kupanga namna watakavyo likabiri swala hili, “kwajinsi ninavyo juwa awa polisi, awajatumwa kuongea juu ya swala hili, awa wame kuja kufanya uchunguzi, kwaajili ya kuja kuvamia ili ani kamate, sasa basi, kuna wazo nime lipata tuwaache wafanya wanacho taka, na mimi nitawaeleza chakufanya” alielezea mzee Nyati na wote wakatulia kusikiliza mpango wa mzee huyu mwenye hakili nyingi, *** siku yapili Insp Johnson na Pc Busungu, wakitumia land rover 110, walielekea kwenye kambi ya wapigania uhuru, kwenye pori la selous, na kukutana na askari waliokuwa wanaendelea na mzoezi makali sana, wakajiunga nao na kuanza kuwaelekza namna ya kuzingila na kuangamiza, wakieleza kuwa umakini mkubwa sana unaitajika, sababu mtu huyo ni hatari sana, walitumia siku tatu kukamilisha mafinzo hayo, ndio siku ya ijumaa mchana safari ikaanza ya kuelekea Songea mjini, wakitangulia insp Jonson na Pc Busungu, wakipanga askari stini, waondoke saa kumi na moja jioni, ili waingie usiku, insp Johnson na Pc busungu waliwasiliana na kijana Side baada tu ya kufika mjini, na kijana Said aliwaambia kuwa mzee huyu yupo nyumbani kwake, akidai amepita sehemu hiyo mda mchache uliopita, itaendelea ………..
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU