
SEHEMU YA HAMSINI NA NNE
ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA TATU : sababu mtu huyo ni hatari sana, walitumia siku tatu kukamilisha mafunzo hayo, ndio siku ya ijumaa mchana safari ikaanza ya kuelekea Songea mjini, wakitangulia insp Jonson na Pc Busungu, wakipanga askari stini, waondoke saa kumi na moja jioni, ili waingie usiku, insp Johnson na Pc busungu waliwasiliana na kijana Side baada tu ya kufika mjini, na kijana Said aliwaambia kuwa mzee huyu yupo nyumbani kwake, akidai amepita sehemu hiyo mda mchache uliopita, ENDELEA ………
Wakaahidi kumpigia jioni, ila waliomba aendelee kumfwatilia kila atua mzee huyu, wakati huo maandalizi yalikuwa yana endelea, lengo likiwa ni kuakikisha mzee huyu anapoteza maisha kabisa, wakiamini kuwa itakuwa ndio mwisho wa mauwaji, mda wote Johnson alikuwa makini sana kwani alitambua kuwa hii ndio karata yake ya mwisho kumsaidia baba yake, ** taalifa zote zilikuwa zina mfikia mzee Nyati, ambae akuandaa mashambulizi yoyote zaidi, aliamua kuwa panga watu wake, kwenye njia zote za kuingilia, ikiwa ni kuchunguza kama wale polisi watakuja wangapi, na silaha gani, wakati kijana Side Tall, akiwa sehemu yake ile ile, leo akijifanya amearbikiwa a baiskeri, mschana mrembo Felister alikuwa ameegesha gari lake njia panda ya matogoro, nje ya maduka karibu na kanisa la mtakatifu Telethia, wakati huo huo binti pekee wa mzee Nyati, Jackline alikuwa ame jitega, mita mia tatu toka kwenye nyumba ya udongo, ndani yamsitu mnene, kati kati ya majabari ya mawe, akiwa ameshikilia silaha yake aina ya sniper lifle model 81, akitazama eneo lote la mbele yake kwa kutumia kilengeo cha silaha hile, chenye uwezo wa kuuwa mtu aliepo umbali wa km 3, huku bastora yake yenye kiwamba sauti, na kisu chake, vikining’inia kiunoni, ** taalifa ya uvamizi ilikuwa imesha fika makao makuu ya polisi, wakuu wa ngazi za juu wa jeshi hilo, walikuwa wametulia ofisi kwao, wakisubiri report ya tuokio hilo, na kwa jinsi walivyo kuwa wamechoshwa na matukio ya mauwaji yanayo fanana ya muuwaji ambae anaonekana kutokuwa na chembe ya huruma atakidogo, wakuu hao walitamani akamatwe mala moja na kufikishwa akiwa mzima ili auwawe kwa mateso makali, kwakuwa walimwamini mpelelezi huyu kijana, awakuwa na wasiwasi, wakati wakuu hao wakiwa wanaendelea kusubiri, ndipo mida ya saa kumi na mbili walipo pewa taalifa ya kuwa askari stini walio pewa mafunzi ya hali ya juu, wapo njiani wana elekea eneo la tukio, ** saa moja kasoro insp Johnson na Pc Busungu, walikuwa wana karibia njia panda ya mahilo, ndipo walipo mkuta Side tall akiwa anaangaika kujaza upepo kwenye tairi la baiskeri yake kwa pamp ya mkono, “tuna bahati sana na huyu dogo” aliongea insp Johnson, huku wana simamisha gari lao Toyota collora, “vipi dogo, mambo yanaendaje?” alusalimia Johnson “kumbe ni nyie blaza, mbona leo mme kuja usiku?” aliuliza Side akijifanya ajuwi lolote, “tuna mpango mzito sana na yule mzee Nyati, vipi tukupe lift?” alitania Johnson akijuwa kuwa Side asingeweza kupanda gari lao sababu anabaiskeri, wote wakacheka, “poa mtakumta sizani kama anaweza kutoka usiku huu” Said aliwaambia wakina Johnson, ambao awakupoteza mda mwingi wakaondoka zao, huku kati kati ya seat zao zikionekana silaha mbili aina ya smg (AK 47) zenye vitako vya kukunja, “huyu leo hachomoki, kama walimshindwa wao, sisi tuna mmaliza, anabakia huyo Malaya wake” aliongea Johnson kwa majigambo, huku wakiendelea na safari yao, wakitumia taa za gari kuona njia, maana giza lilisha ingia, ** wakati huo mzee Nyati alikuwa ametulia nje ya nyumba yake, amejilaza kwenye kiti chake cha uvivu pale pale chini ya mti mkubwa, akiwa ame valia Jacket na chini ame jifunga kitenge cha mke wake, mke wake akiwa amejilaza kwenye mkeka pembeni yake, wanaongea ili na lile, huku atua kumi kutoka walipo wao palionekana moto mwingi ukiwaka kwenye jiko la kuni huku sufulia ikiwa juu yake inachemka, ndio wakati mzee huyu alipo pokea simu yakwanza kutoka kwa Felister, ambae alimweleza kuwa ameona magari matatu ya polisi, yaliyo sheheni askari kibao, yakija upande wa huko kwao, kila mmoja wao akiwa na silaha, huku wachache wakiwa na silaha nzito za kulipulia majengo na maari (RPG), ile anakata tu! ikaingia simu ya Said, ikimweleza kuwa, wale polisi wawili wanakuja kwake kwenye nyumba ya udongo, tena leo wana silaha, mzee Nyati nae akamwambia Saiad kuwa ajifiche haraka, sababu una polisi weng wana kuja kisha atazame wana jipanga vipi, kisha amjulishe kwa sms, mzee Nyati baada ya kumaliza kuongea na Said akaanza kuona wanga wa taa za gari ukisogea kuja nyumbani kwake, “kazi imeanza, mke wangu kuwa mwangalifu” aliongea mzee Nyati, huku akipiga simu kwa mwanae Jackline, “kuwa makini Jack polisi wameanza kusoge eneo la tukio, tumia bunduki itakapo bidi,” baada ya kumaliza kuongea na Jackline mzee Nyati akakata simu na kuwa karibisha wageni wake, ambao ndio kwanza walikua wana simamisha gari lao, “karibuni sana vijana, naona mmenistukiza?” aliongea mzee Nyati kwa sauti ya uchangamfu, iliyoonyesha kuwa anaongea na marafiki wanao fahamiana, “samahani mzee wangu, yani ndio kwanza tunaingia, kutoka mtwara, na simu zetu zimeisha chaji” alijubu Johnson kwa sauti ya uchangamfu pia, lakini mzee Nyati alitambua kuwa uchangamfu ule ni wakulazimisha, “ok karibuni nazani leo mme kuja na mambo mapya” aliongea mzee Nyati, baada ya kusalimiana na vijana wale wawili, huku mke wake akwatolea viti wageni, “ni kweli mzee, tumekuja kwa swala la siku ile, juu ya mzee Mwijage, ni kwamba anasema kuna kitu mlizurumiana, je unaonaje kama mkikaa na kumalizana kwa njia nyingine, zaidi ya hii unayo itumia?” aliuliza bwana Johnson, huku mzee Nyati akiskiliza kwa umakini sana, “kijana unaakika kuwa mimi ndie ninae usika, na mauwaji ya wenzie Mwijage?” aliuliza mzee Nyati, wakati huo kuna ujumbe ukaingia kwenye simu ya mzee Nyati, “nina uakika asilimia kubwa sana, asa nilipo kuona pale Cosovor, siku aliyo uwawa mzee Alex mwasaga” aliongea Johnson kwasauti ya kujiamini sana, huku mzee Nyati akimsikiliza huku akisoma ujumbe toka kwa Said, ‘magari matatu ya polisi yana shusha askari wengi wenye silaha, wana tawanyika vikundi vikundi, wakuja usawa huo’ ndaivyo ilivyo sema sms toka kwa Said, mzee Nyati akampa simu mke wake ikiwa na ule ujumbe, ili ausome, akamtazama Johnson, kwa sekunde chache, “ok! uwepo wangu pale ndio uuwaji wangu?, labda unaweza kuniambia nikitu gani tulicho zurumiana?” aliuliza mzee Nyati huku akiwatazama kwa zamu vijana wale, mda wote mke wake alikuwa makini ana sikiliza maongezi yale, huku anaandika ujumbe kwenda kwa Jackline, ‘kuwa makini polisi wana tanda msituni, pia tuandalie wawili kati yao,’ akaituma, “awaja niambia ni kitu gani mezurumiana” alijibu Johnson, ambae kwa haraka alishaona bado nivigumu kwa mzee huyu kubadiri maamuzi yake, “haya basi tufanye hilo ume lifikiria hivyo, je ulisha wai kuwaza labda ni nani alie mzurumu mwenzie?” kiukweli maswali hayo yalikuwa ni magumu sana kwa Johnson, ambae atalile tabasamu la kuong lilisha pote usoni kwwake, “sikia mzee nazani huu sio wakati wa kuangalia nani ame fanya nini, swala inatakiwa uache mauwaji” aliongea Johnson kwa sauti flani ya kuamuru, hapo mzee Nyati, akamtazama mke wake, “mama Jack, nenda kaandae cha kutosha, maana leo tuna wageni” aliongea mzee Nyati na mke wake akainuka, na kuingia ndani, akimwacha mume wake na wageni wao, “kijana kazi yako ni ngumu na hatari sana, inakupasa kutumia akili nyingi sana kuifanikisha,” aliongea mzee Nyati kwa sauti tulivu, kama vile anatoa usia kwa wanadoa wanao enda kuanza maisha, hapo insp Johnson alistuka kidogo akamtazama Busungu, ambae pia alikuwa amestuka, mzee Nyati akaendelea, nazani aliekutuma kwangu, akukueleza alicho paswa kukueleza juu yangu, wewe bado kijana mdogo sana na unatamani uonekane shujaa” hapo mzee Nyati alitulia kidogo, huku wakina Johnson wakiwa wanamtazama na macho yame watoka kama wana somewa barua ya taraka, “lakini shujaa utambbuliwa akiwa ameha kufa, ila dogo, mimi nina ushauri kidogo,” aliongea mzee Nyati ambae kiulweli wakina Johnson waliona kama anawapotezea muda, “ushauri gani mzee?” aliuliza Johnson ambae alisha tambua kuwa mzee Nyati amesha watambua wao ni nani, “ongeza muda wa uchunguzi wako, ila na kutaazalisha, usijaribu jambo lote la kipuuzi, lita kughalimu” aliongea mzee Nyati safari hii ata, sura yake ilisha badirika, na kuwa ya kutisha iliyo jikunja kwa hasira, hapo insp akatazama huku na huku pasipo kuona ata kisu, au kiwembe, akajiakikishia kuwa mzee yule akuwa na silaha ata moja pale alipo, “mzee usijaribu kututisha, sisi ni polisi na tuta fanya kazi yetu kama tulivyo agizwa” alionngea kwa hasira Johnson huku akiinuka na kuelekea kwenye gar akifwatiwa na Pc Busungu, “unajifanya mtemi, sio kwetu sisi, ata tunge taka kukukamata sasa hivi tunge weza, hii yote tuna taka tumalize kwa njia ya amani” alizidi kuongea Johnso, huku akiongeza sauti, iliyo samba porini, “tumejaribu diplomasia umekataa, sasa tutajuwa lakufanya” safari hii sauti ya insp ilitokea kwenye gari, “kijana usi tegemee kufanya ivyo atasiku moja, maana aijawai kuwa lahisi kiasi hicho” alingea mzee Nyati, wakati huo mke wake alikuwa antoka nje na simu mkononi, akampatia mume wake, ambae alikuwa anawatazama wakina Johnson, ambao waliwasha gari na kutimua zao, mzee Nyati aliwatazama mpaka walipofika mwisho wa eneo la wazi, lenye vichaka vidogo vidogo, na nyasi ndefu, kisha kabla gari alijaingia kwenye eneo la msitu kuelekea mjini, mzee Nyati akaona mwanga wa taa za gari lile ukitoweka ghafla, mala akasikia mlio mkali wa honi ya gari lile la kina Johnson, iliyo pigwa mala tatu, kisha akashangaa ghafla, eneo lote la nyumba yake likitawaliwa na mwanga mkali sana, wa tochi nyingi zenye mwanga mweupe, na mkali sana, zaidi ya kumi na saba kumi na nae, na kusababisha eneo lote la kuzunguka nyumba yo pawe kama mchana, “lala chiniiiiiiiiiiii!” alipiga kelele mzee Nyati, huku akimzowa mke wake na kumlaza chini haraka sana, ni kama walikuwa wame toa amri ya kushambuliwa, maana ilisikika milio mikari ya risasi toka kwenye bunduki usawa wa zile tochi, zilizo kuwa zina wamulika, risasi nyingi sana, ziligonga kwenye ile nyumba ya udongo, wapigaji walionekana kusogelea eneo lile huku wakiendelea kushambulia, “mke vipi ulisha ndaa?” aliuliza mzee Nyati akiwa amelala chini pamoja na mke wake, risasi zikipita juu yao na kutandika ukuta wa nyumba, “tayari, tujitaidi tuingie ndani” alishauri mke wa mzee Nyati, “ok! ngoja tutafute mpenyo” aliongea mzee Nyati huku anatazama mlango, wakuingilia kwenye ile nyumba ya udongo, ambapo palionekana wazi, risasi zikigonga sana eneo lote la mlango, mzee Nyati akaitazama simu yake, ambayo ilikuwa mkononi mwake, aka mpigia Jackline, “sende chache Jackline akaipokea, “wapunguze kasi kidogo, wame tuzuwia kuingia ndani” aliongea mzee Nyati kwa sauti ya juu, akishindana na milio ya risasi, “ok! sawa, ila kuweni makini, kuna askari wengine nawaona, wanazunguka nyuma ya nyumba na wamesha karibia kabisa” aliongea Jackline na kukata simu, kisha akaiweka risasi katika chemba, aka tega jicho kwenye kilengeo, *** insp Johnson akiwa pamoja na pc Busungu, nyuma kabisa ya kundi kubwa la askari ishirini, silaha zao mkononi, aliendelea kulifwata kundi hilo kwa ukaribu na kutazama kwa umakini sana kinacho endelea kutokea, akishuhudia askari wakiendelea kumimina risasi, huku wakisogelea ile nyumba ya udongo pasipo kuacha kumimina risasi, zaidi kwa alie ishiwa risasi, alibadiri mkebe wa risasi na kuendelea kushambulia, wakati akiwa anatazama mashambulizi huku usowake ukiwa umetawaliwa na tabasamu la ushindi, mala wote wawili wakashangaa kuona askari mmoja akirushwa nyuma, huku tochi ikimponyoka na kudondokea mbali zaidi, mala mwingine tena, kabla awaja pata ufahamu zaidi, waliona askari wa tatu nae akirushwa kama wenzake, “lala chiniiiii!” alipiga kelele insp Johnson huku akilala chini pamoja na pc Busungu, hapo ashari wote wakalala chini, huku tochi zao zikimulika mbele, safari hii kwamwanga ambao aukuweza kufika mbali, kutokana na kuzuwiwa na nyasi ndefu, lakini aikusaidia walishuhudia askari mmoja akitandikwa risasi, akiwa ame lala pale pale chini, “zimeni tochiiiiii” alisema Insp kwa sauti kari, huku mapigo yakiwa yamesha simama, wakati askari wanaangaika kuzima tchi kwa uoga insp Jonson na busungu walishuhudia mzee Nyati na mke wake wakikimilia ndani ya nyumba ya udongo, huku wakikoswa koswa na risasi za askari walio zungukia upande wapili, nandio walikuwa karibu zaidi ya jengo lile, la udongo, sende chache baadae eneo lote lilikuwa giza, “shenzi kabisa, kinachofwata ni kumlipua kabisa, hapo insp sasa akachomoa redio yake ya kijeshi, “all satation, mnanipata?” aliuliza insp na viongozi wa makundi yoyte matatu yenye askari ishilini ishilini wakajibu, kuwa wana mpata, “ok! kila kikundi kiandae mambomu manne ya RPG,” amri kutoka kwa insp Johnson alie aminiwa na jeshi la polisi, hapo wakaonekana askari wawili wenye hizo silaha za RPG, vijana wanaita muanzi, wakipiga magoti na wenzao waka wawekea mabomu, kisha wakakoki na kuelekeza kwenye nyumba ya udongo, aliyoingia mzee Nyati, hiyo ilifanyika kwenye vikundi vyote vitatu, kisha ika sikasikia sauti ya Johnson, toka kwenye redio za kila kikundi, “alie ona target aipige kwa wakati wake,” baada ya maneno hayo ilisikika milindimo sita kwa mpigo, huku mabomu yakionekana hewani yakiifwata nyumba ya udongo ya mzee Nyati, na kukita kwanguvu sana, na kusababisha milipuko mikubwa sana, ikipokezana, lakini kitu cha ajabu ukaunganisha mlipuko mmoja mkubwa sana, ambao ulisababisha mpaka ardhi yote ika tetemeka, ikirusha ovyo ovyo mabati chakavu yaliyoezekwa kwenye kile kibanda, ukisambaa eneo kubwa sana, na kujeruhi bahadhi ya askari wakikundi cha pili, huku nyumba yote ya udongo ikisawajika na kuwa kama hapakuwa na nyumba, maali pale, zaidi ya moto kubwa ulio sababishwa na ule mlipuko mkubwa, hapo zikasikika shangwe za askari polisi wakishangilia ushindi, maana kwa mlipuko ule, asingeweza kutoka mtu, hapo polisi wote huku wakiendelea kushangilia ushiindi wao walizunguka eneo lote kwa tahadhari, huku wakubwa wavikundi vyao wakiwahesabu kujuwa ni wangapi wame poteza maisha, katika mahesabu yao walipungua askari sita, wanne miili yao ilionekana lakini wawili awakuonekana, wakapanga kuwa tafuta asubuhi, baada ya hapoikaanza kazi ya kukagua eneo lile ambapo waliweza kuoina miili ya watu wawili ndani ya kifusi ya udongo wa ile nyumba ya mzee Nyati, “yes nimekupata mshenzi wewe” alisema bwanz Johnson huku akichuchumaa kuutazama mwili ulio aribika vibaya, ukiwa ume ungua kiasi cha kuto tazamika mala mbili, kilicho mfanya Johnson autambue mwili ule, ni jarcket na kitenge vilivyo ungua na kugandia kwenye mwili wa mtu huyu, itaendelea……………
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU