
SEHEMU YA HAMSINI NA TANO
ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA NNE : baada ya hapo ikaanza kazi ya kukagua eneo lile ambapo waliweza kuoina miili ya watu wawili ndani ya kifusi cha udongo wa ile nyumba ya mzee Nyati, “yes nimekupata mshenzi wewe” alisema bwanz Johnson huku akichuchumaa kuutazama mwili ulio aribika vibaya, ukiwa ume ungua kiasi cha kuto tazamika mala mbili, kilicho mfanya Johnson autambue mwili ule ni jarcket na kitenge vilivyo ungua na kugandia kwenye mwili wa mtu huyu, ENDELEA ………
Huku atuwa chache akiionekana maiti nyingine ikiwa ime chanwa chanwa vipande vipande, na kuungua sana huku bahadhi ya viungo vya mwili huu vikikosa kuonekana na kutambua kuwa ni nani, kilicho mfanya insp autambue ni nguo alio valiwa na marehemu yule kuwa ni gauni ambalo amda mfupi alikwa amelivaa mkewa bwa Nyati, “sasa baba yangu ataishi kwa amani, pumzikeni kwa amani bwana na bibi Nyati” alinongona insp Johnson huku tabasam moja pana sana lililo ashiria ushindi mkubwa, likitawala usoni mwake, ** siku ya pili habari kaika vyombo vyote vya hari magazeti redio na TV vilionyesha wakuu wajeshi la polisi wakiji tapa kwa kumteketeza muuwaji alie kuwa anaisumbua selikari, kwa kufanya mauwaji mfululizo, mmoja wa wasikilizaji na watazamaji, wa habari hiyo alikuwa ni mzee Masinde, ambae alikutana na rafki yake mwana Mwijage na kusherehekea, kifo cha mtu alie wanyima raha siku zote, “Denis ambae baada ya mke wake kuwepo mbali na nyumbani, alirudia tena ulevi wa kupindukia, leo hii akiwa kazini, aliipata habari ya kuuwawa kwa Jambazi kongwe, alipo yasikiamajina ya Jambazi hilo akaona yana fanana kabisa na majina ya baba mmkwe, kasoro jina moja tu! la Nyati, akizingatia uwa tukio hilo limetokea Songea, akaona bora apige simu kuulizia, lakini Jackline akamwambia yeye hajasikia tukio lolote na kama limetokea basi aliusiani na familia yao, sababu wao sio Nyati, kwa upande wa mzee Soud yeye alifwatilia kwa umakini sana habari hizi, “nilijuwa tu huyu kijana akwenda Songea kwa mazungumzo” alwaza mzee Soud huku akichukuwa simu yake na kumpigia Johnson, simu aikupatikana, alijaribu kila mala aikupatika, akawa anafanya kama mchezo, anajaribu kila baada ya nusu saa, lakini baada ya lisaa limoja na nusu, akafanikiwa kumpata “samahani nitakupigia baadae kidogo” ilisikika sauti ya Johnson, baada ya kupokelewa kwa simu, kisha ikakatwa, mzee Soud ambae alionekana kuwa na mawazo mengi sana, baada ya kuona ile taarifa kwenye vyombo vya habari, alitikisa kichwa kwa masikitiko, huku tabasamu la ouga likimponyoka usoni kwake, kukweli insp Johnson alipata sifa kubwa sana, kwa kuweza kutekeleza tukio hilo, kia kona simulizi zilikuwa ni juu yake, akimwagiwa sifa za ukamanda, kwa mda wa mwezi mzima alikuwa busy sana, kila siku akitembelea kwenye maofisi ya mawazili na wakuu mbali mbali wanchi, kuanzia raisi mwenyewe, makamo wake, waziri mkuu, waziri wa mambo ya ndani, waziri wa ulinzi na mkuu wa jeshi la ulinzi, pia aliitwa bungeni na kwenye mataasisi mbali mbali, ambako kila alikoenda alipewa zawadi za pongezi, kwa jinsi hiyo akukumbuka kutenga mda kwaajili ya kumtafuta mzee Soud japo kwa simu, ilikumjulisha kazi yake ilivyo kuwa mzee huyu alie msaidia kufanikisha zoezi hili, siyo kwmba akumkumbuka, ila aliamua kumpotezea, sababu aliamini mzee huyu akupenda yeye afanye alicho kifanya, pengine alipenda mauwaji yaendelee, nakuona baba yake akipoteza maisha, ** naam ilikuwa imekatika miezi mitatu, toka kikosi maalumu chapolisi kifanikiwe kumwangamiza mzee tishio Michael Fransis Nyati, jumamos moja, insp Johnson akiwa anatoka matembezi na familia yake huko pande za ufukwei kigamboni, akiwa ndani yagari lake kwenye foleni ya kivukoni wakati anasubiri panton MV Alena, maa akastuka mtu akigonga kioo cha gari lake upande wake, alipo mtazama, alikuwa ni mzee Soud, ghafla roho yake ilimlipuka na kumchukia mzee huyu, hapo Johnson akashusha kioo, na kumsalimia mzee Soud, “kijana naona ulishindwa kunipigia kama ulivyo aidi miezi mitatu iliyo pita” aliongea mzee Soud ambae alikuwa amesimama nje ya gari usawa wa mlango wa Johnson, “utanisamehe bule mzee wangu, nipo busy sana, ila natumaini umeisikia habari tuliyo ifanya Songea?” alijibu Johnson kwa kebei, “nimeisikia hongera sana bwana Johnson, lakini ulipaswa unitafute mala tu uliporudi” aliongea mzee Soud, na Johnson akawaza labda mzee huyu nia yake, na yeye angeonekana ni mmoja wa mashujaa, walio fanikisha zoezi la kumwangamiza mzee Nyati, “hahahaha mzee Soud bwana, nikweli nilipaswa nikuone lakini ndio kama hivyo nipo busy sana” aliongea Johnson kwa sauti ya pozi flani la dharau, huku mda wote mwanae mdogo na mke wake wakifwatilia maongezi yake, “ok! lakini ubusy huu sio ule uliopita, na uliweza kuni tafuta” aliogea mzee huyu akionyesha kuwa alianza kuingiwa na fadhaa, nazani nikwaajili ya mabadiliko ya kijana huyu, “usijari mzee wangu nitakuja na zawadi zako na zamama” aliongea Johnso akizani kuwa mzee Soud anaitaji asante baada ya kusaidia kwa kazi ya kumwangamiza mzee Nyati, hapo mzee Soud alicheka kidogo kisha akamtazama mke wa Johnson, alafu aka mtazama binti yao mdogo alie kaa set ya nyuma ya gari lao jipya aina ya Toyota wish, “asante sana, ila usijari kuhusu zawadi, jiandae kwa kazi, maana kwa sasa hupo busy na tazidi kuwa busy” aliongea mzee huyu alieonekana wazi kufadhaishwa na maneno ya Johnson, kisha akaanza kuondoka, mke wa bwana Johnson aliekuwa anafwatilia mazungumzo yale, akataka kuongea kitu lakini akasita baada ya kumwona yule mzee akirudi tena kuongea kwa sauti ya chini, “Johnson akuna mtu anaepokea zawadi pasipo kazi” aliongea mzee huyu akionekana wazi kutingwa na jambo lile, kitu ambacho Johnson alioneka kuchukizwa nacho, “sasa mzee Soud, nikueleweje, unataka nini kwangu kama autaki zawadi?” safari hii Johnson aliongea kwa uakari sana, akionyesha wazi kuchukizwa na kelo za mzee huyu, msataafu wa jeshi, hapo mzee Soud akamtaza tena mke wa bwana Johnson, “samahani mwanangu nimewaalibia siku, maana nime kuwa mjinga sana, kumwelekeza mtu kitu alicho somea” aliongea mzee Soud huku akitabasamu nakujicheka kidogo, na kumfanya mke wa Johnson nae achee kidogo, huku Johnson mwenyewe akiwa amenuna kweli kweli, “hapana baba yangu, hizi kazi zenu ni zakusaidiana” aliongea mke wa Johnson akionyesha kutambua swala flani kwenye maneno ya mzee Soud, “hapa mwanangu, labda umeiona vizuri hii bahari” aliongea mzee Soud na mke wa Johnson akaitikia kwa kichwa kukubari, unazani imesha waikuwa lahisi mtu kuogelea na kukamata samaki kwa mikono, ndani ya ile bahari?” aliuliza mzee Soud, na mke wa Johnson ambae alijuwa mzee huyu bado anaendelea kulifafanua neno lake la kumfundisha kitu, mtu alie kisomea, “aijawai kuwa lahisi, nasizani kama itakujakuwa lahisi” maneno hayo ya mke wa Johnson yaligonga kichwani kwa Johnson, akayakumbuka mala ya kwanza aliyasikia wapi, maneno hayo yalionyesha kumchanganya, akamtazama mke wake, kwa mshangao, “aswaaaa nisawa na kumkuta binadamu waleo anamiliki mamillioni, alafu analala kwenye nyumba ya udongo, kwa heri mwanangu naona magari yameanza kutembea” aliongea mzee Soud, na mke wa bwana Johnson akaachia kicheko, na kuzidi kumchanganya Johnson, kiasi cha kuto kuyaona magari yaliyo kuwa yana tembea kuingia kwenye panton, “we! baba Bite twende bwana, uoni kama magari yana tembea” hapo insp Jhnson aka stuka na kuangalia nje ya gari, akumwona mzee Soud, kabla ajakaa sawa akasikia milio mini ya honi, toka kwenye magari yaliyopo nyuma yake, hapo akawasha gari na kuanza kuondoka kuingia kwenye pantoni, “aijawai kuwa lahisi, nasizani kama itakujakuwa lahisi” kiukweli jibu la mama Bite, kwa mzee Soud, lilimchanganya sana, insp Johnson, japo mke wake huyo hakujuwa kitu chochote, kilicho mchanganya zaidi insp ambae sasa alikuwa ndani ya pantone na familia yake, ni sehemu ambayo aliwai kuisikia kauri kama hiyo, “kijana usi tegemee kufanya ivyo atasiku moja, maana aijawai kuwa lahisi kiasi hicho” Johnson aliikumbuka vyma kauri ya mzee Nyati, aliyo iongea miezi mitatu iliyopita, siku ile usiku, siku ambayo insp Johnson alianza kujizolea sifa kede kede, za kuwa kamanda shujaa, alie fanikiwa kumwangamiza mmmoja wa wauwaji wakubwa nchini, kama alie tambulika kama mpangaji wa matukio ya mauwaji mfululizo ya askari wa staafu, wa jeshi la ulinzi, na watu wengine wengi sana wakiwepo askari polisi, waliokuwa wanachunguza mauwaji hayo, kama nikeli yulemzee atakuwa ajafa nitaonekana mjinga sana, aliwaza insp Johnson akiwa amesha toka kwnye pantone, anaelekea mbezi beach numbani kwake, “baba bite vipi mbona kimya, au yule mzee amekuhudhi, ila mimi sijaona kama ameongea kit kibaya” aliuliza mke wake baada yakuona kimya kimezidi, insp akujibu kitu, zaidi aliendelea kuwaza, juu ya mzee Nyati ambae Tanzania nzima inafahamu kuwa mzee huyu amesha uwawa, “sasa ataponaje na wakati aliingia mle ndani ya kijumba chake cha udogo, na mimi nika kilipua, kabla hajatoka, na nyuma ya nyumba kulikuwa na asakari wengine wengi tu!” aliendelea kuwaza Johnson, “ila na kutaazalisha, usijaribu jambo lote la kipuuzi, lita kughalimu” kauri za mzee Nyati ziliendelea kujirudia kichwani kwa Johnson, “lakini aiwezekani akawa bado mzima, maana nime uona mwili wake, kwa macho yangu, kama atakuwa mzima basi siyo yeye, ni mzimu wake” alijipa moyo insp Johnson huku safari yao ikiendelea, kiukweli insp mpaka anafika nyumbani kwake, bado mawazo juu ya mzee Nyati yaliendelea kumsonga, huku wakati mwingine akijaribu kuya fumbua maneno ya mzee Soud, kwa mke wake pale kivukoni, “aswaaaa nisawa na kumkuta binadamu waleo anamiliki mamillioni, alafu analala kwenye nyumba ya udongo, kwa heri mwanangu naona magari yameanza kutembea” maneno haya yalikuwa na maana kubwa sana kwa kijana Johnson, akiwa pale sebuleni, alivuta picha ya mwonekano wa mke wa mzee Nyati, alionekana kuwa toofauti na mazingira aliyo wakuta, asa akikumbuka ngozi nyororo ya mama huyu mikononi na miguuni, pia akakumbuka kuwa yule mama alikuwa amepaka rangi za kucha, “inamaana le nyumba siyo anayo ishi” insp Johnson aling’amua jambo, huku akikumbuka kuwa mzee Nyati alikuwa na uwezo kifedha, maana alimshuhudia aki toa kiasi kikubwa cha fedha kwa walemavu, “uwezi kupokea zawadi kabla ujafanya kazi” bwana Johnson, alikumbuka hayo akiwa sebleni nyumbani kwake, “dah! siwe hivyooo! mzee Nyati meshakufa” asafari hii insp Johnson aliongea kwa sauti, ** siku zilienda week zikapita, miezi ikaja nayo ikapita, atimae ikatimia miezi sita jumla ya miezi tisa toka lilipo tokea tukio la kuuwawa mzee Nyati, na nimiezi tisa toka azaliwe mtoto Fransis, amani ilikuwa imetawala ndani ya jiji la dar es salaam, akukuwa na mauwaji yoyote menine yaliyotokea yanayofanana na yale, yaliyotokea mfurulizo siku za nyuma, kwa upande wa Denis, alizidi kumtamani sana mke wake na mtoto wao Fransis, mala kwa mala alikuwa anapiga simu kumsisitizia Jackline arudi dar, huku akituma fedha za matumizi kila baada ya siku tatu, ila Jackline alimwambia kuwa, wazazi wake wame zuwia asirudi mpaka mtoto aache kunyonya, maana wanaweza kum’bemenda mtoto wao, ** siku hiyo ya ijumaa, majira ya saa kumi jioni, insp Johnson alikuwa njiani ndani ya gari lake Toyota wish, akielekea nyumbani kwake mbezi, Johnson ambae alisha shau juu ya kufanikisha kummaliza mzee Nyati, maana alikuwa na uakika kuwa mzee huyo amesha poteza maisha, katika kipindi hiki bwana Johnson, alikuwa anaishi maisha mazuri yenye furaha sana, kutokana na heshima aliyopewa, kwa kufanikisha kumteketeza mzee hatari sana mwenye recordi kubwa sana jeshini, ya kuwa kijana mdogo sana na sakari mwenye cheo chachini, kufanya kazi ngumu na hatari za kivita, huku akisaidia kufanikisha mission tatu kubwa za kivita, nje ya nchi, insp Johnson akuweza kwenda kumwona mzee Soud, maana alishamwona kuwa nimmoja kati ya watu ambao walijaribu kumtisha, asipambane na mzee Nyati, hivyo akaamua kumpotezea, na akutaka kumkumbuka mzee huyu, saa kumi na nusu insp Johnson alikuwa anaingia nyumbani kwake, akaegesha gari na kuingia ndani, licha ya kukuta mlango hupo wazi, lakini pale sebuleni akumkuta mke wake, akaingia chumbani ambako nako mke wake akuwepo, akabadiri nguo toka zile za kazini, na kuvaa bukta na tishertkisha akatoka chumbani na kuingia jikoni, akumkuta mke wake, lakini akasikia sauti ya mke wake, “anaweza kuku kumbuka japo ni mda mrefu umepita,” Johnson aliisikia sauti hiyo yamke wake ikitokea nyuma ya nyumba yake, upande wa jikoni, “nilimwona jana akitokea hapa na gari lake, nikasema leo nitakuja kumsalimia” insp alisikia sauti nyinginine ya kike, na maongezi yalionyesha kuwa huyo mwanamke ni mgeni wake, na pengine ni rafiki wasiku nyingi, insp akatoka nje, na kuelekea kule ilikotokea sauti ya mke wake, na huyo mwanamke mwingine, wakwanza kumwona alikuwa alikuwa ni mke wake ambae alikuwa amekaa akitazama upande anao tokea, “hooo huyoooo! amesharudi” aliongea mama Beatrice, akimwambia yule dada aliekuwa amekaanae kwa mda wa nusu saa nzima wakiongea, yule dada pia akageuka na umtazama Johnson ambae alikuwa na shahuku ya kuiona sura ya mwanamke huyu, ambae alionekana kuwa na shepu nzuri sana, akinekana kutoka nyuma, macho ya huyo mgeni wakike na insp Johnson yakagongana, mke wa bwana Johnson, ambae alikuwa anasubiri kwa hamu, kuona wawili awa, wakikumbukana, alishuhudia vitu viwili tofauti kwa watu hawa, wakati mume wake akishikwa na mstuko mkubwa sana, lakini yule dada alioneka kutabasamu, “Jackline Nyati amepajuwaje hapa nyumbani kwangu?” aliuliza insp Jonson kwa sauti ya ya kunong’ona iliyo jaa mshangao wa wasiwasi, itaendelea…….
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU