
SEHEMU YA HAMSINI NA TISA
ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA NANE : “sasa ugumu wake nini?, sababu huyu kama hauja mkosea, yeye akufanyi chochote” aliongea Denis kwa usibitisho kabisa, hapo Jackline nusu aangue kicheko, mala ghafla Jackline kajikuta ameuliza bila kutegemea, “hivi Denis, ukigunduwa kuwa mimi ndie huyo mwanamke uta fanyanini?” hapo Denis akageuza kichwa chake kumtazama Jackline kwa mshangao, endelea ………
Alimtazama kwa sekunde kadhaa, kisha akatazama mbele, akionekana kama mwenye kuvuta umbukumbu flani, “mbona unanitizama alafu unijibu swali langu” aliuliza Jackline, huku akiwaza kuwa pengine Denis amehisi kitu, kutokana na swali lake, “najaribu kuvuta picha harisi, lakini sipati, yani ningekuwa naanzisha ugomvi makusudi, alafu nakuita” aliongea Denis kisha wakacheka, kwapa moja, “tena ukienda kwenye pombe, tunaenda wote, wakikuchokoza tu! nawabomoa” aliongea Jackline au mama France, wakaendelea kucheka, huku safari inaendelea , nusu saa baadae waliingia MAZAO Building waka parki gari, wote wakashuka, kisha Denis akiwa ame mbeba mwanae Fransis, wakapandisha ngazi kuelekea ofisi ya kina Denis, ambako walimkuta Jeny aliendelea na shughuli zake, alipowaona alacha shuguli zake na kuwa karibisha, “hoo! Denis karibu, he! umekuja na wifi yangu, zama siku wifi” aliongea mfurulizo Jen, “safi za toka siku ile” aljibu Jackline, “jamani hongera sana umekuza” aliongea Jen, huku ana jitoa kwenye meza yake na kumfwata Denis alipo simama, “jamani we mtoto wewe, umekuwa mkubwa hivi” alisema Jen akinyoosha mikono kumchukuwa Fransis ambae alimtazama Jen kwa tahadhari ya kitoto kisha akakataa kuchukuliwa na mwanamke huyu, “Fransi mwamkie shangazi” aliongea Jackline, wakati huo Denis alikuwa ana cheka cheka huku akimtazama mwanae, aliyekuwa amefanana nae kwa kiasi kikubwa sana, Fransi alinyoosha mkono wake wakulia na kuulaza kichwani kwa Jan, kisha akautoa mala moja, “malahabaaaaa ujamboo” aliitikia Jen na hapo akukuwa na mawasiliano tena kati yao, maana Frans alitulia kijificha kifuani kwa baba yake, “niambie Jane, vipi boss yupo?” aliuliza Denis kisha, Janet aliyekuwa ame simama karibu na Denis akaguna, “mh! tena hapa alishaagiza upigiwe simu, sema sina salio” aliongea Janet huu anarudi wenye kiti chake kilichopo nyuma ya meza kubwa yenye computer, “kwani Mahadhi ajafika?” aiuliza Denis kwa sauti ya chini yenye mshangao, “amefika sana yupo ofisini, ila ana lalamika kuwa kiuno kina muuma, sijuwi jana alikutana na mwali wa kimakonde?” aliongea Janet kisha wote wakacheka, wakati huo macho ya Jackline yalikuwa kwenye screen ndogo ya TV iliypo mle ndani, ambayo ilikuwa ina onyesha, tukio la msemaji wa jeshi la polisi, ambae alikuwa anaongea na waandishi wa habari, “ngoja kwanza nimcheki” aliongea Denis huku anaelekea kwenye mlango wa ofisi yao yeye na Mahadhi, akiwa na mwanae Fransis, ambae alionekana kuwa na furaha sana akiwa mikononi mwa baba yake, Denis aliingia ofisini, akimwacha Jackline na Janet, huku bado Jacline anafwatilia maongezi ya msemaji wa polisi, na waandishi wa habari, ambapo msemaji huyo alisikika akieleza juu ya tukio la vifo vya waendesha pikipiki maalufu kama boda boda, vilivyo tokea huko nje ya jiji la dar, katika misitu ya kisopwa, “juhudi za kuwasaka hao wanawake, waliokuwa wanaendesha gari aina ya Toyota lav 4, ambayo namba zake azikuweza kupatikana mala moja, zinaendelea, pia wamesha kamatwa watu hamsini kuhusiana na tukio hilo, wapo katika vituo mbali mbalii vya jiji la Dar na vitongoji vyake” alisikika msemaji wa polisi kwenye Tv, wakati huo Denis akawa anatoka ofisini akiongozana na Mahadhi, ambae alikuwa anatembea kwa shida kidogo, akishikilia kiuno kwa nyuma, “yani hawa polisi ni washenzi sana, sasa wanazani huyo mwanamke, atakuwa mjinga kukaa kwenye guest ya karibu?” aliuliza DENIS ambae alikuwa amesimuliwa jinsi mkasa ulivyo kuwa, “tena huyo mwanamke ninge fahamu ninge mpatia zawadi kubwa sana, kisha ninge mwambia awakamue na hao polisi, yani jana wame nivamia kabisa nikiwa uchi” alilalamika Mahadhi, kisha Janet na yeye akadakia kwa utani, “mimi ningejitahidi awe rafiki yangu, alafu ninge mwambia awavizie wanaume wakwale” hapo wote mle ndani wakacheka, “sasa hao pilisi wanamtafuta wampe zawadi au wanamtafute wamfunge?” aliuliza Mahadhi na hapo wote kwakakosa jibu, ila kiukweli mwenye jibu alikuwa ni Jackline mwenyewe, ** saa nne asubuhi watu mitaani walikuwa wamekaa kwenye vikundi, wakiendelea kujadiliana juu ya tukio hilo la boda boda kukutwa wame chinjwa kama mbuzi, mijadara ilikuwa mikari sana, wapo waliosifia wapo waliokilalamikia kitendo hicho, kuwa cha kinyama, lakini wale walio kisifia kitendo kile walitoa pint zao, kuwa vijana wale na wenzao wa jamii hiyo, wana tabia ya kujichukulia hatua mikononi, maana endapo wale wanawake wangekuwa ni wakawaida wasiojuwa kupigana, lazima wangechomwa moto ndani ya gari, na wakati kosa lilikuwa ni la boda boda, wakati huo mitaa ya jiji hili, ilikuwa imetapakaliwa na mashushu wapilisi ambao walikuwa wanafanya uchunguzi, wa kubaini mtekelezaji wa tukio lile la kusisimua, mmoja wa makachelo hao, alikuwa ni Pc busungu, ambae alikuwa mitaa ya Kaliakoo, karibu kabisa na kituo kikuu cha polisi, huku insp Johnson akiwa ofisini kwake anapanga namna ya kuunda kikosi cha askari watakao ingia kwenye msako wa kumsaka Jackline Nyati, huku akifanya mkadirio wa idadi ya askari watakao unda kikosi hicho ambacho kitakuwa chini yake, Johnson aliendelea kufanya kazi hiyo huku kichwa chake kikiendelea kuchambua bahadhi ya mambo yanayo husu matukio yaliyo fanywa na Jackline, wakati anafanya hivyo kuna bahadhi ya mambo yali mfanya agundue jambo, “inawezekana anakaa karibu na maeneo ya kibamba” aliwaza insp Johnson, akwa ana vuta kumbukumbu ya matukio hayo, ambayo licha ya kufanyika sehemu tofauti za jiji, lakini mengi yalifanyika kuanzia kimara kueleka mbezi mpaka kibamba, kuanzia yule mwanamke mhudumu wa vyumba na polisi pale mbezi full dose, pia wale vijana wawili Matumaini hospital pale mbezi mwisho, ukiachilia hayo pia, kuna tukio la polisi yule alie kuwa anamfwatilia mwanamke huyo, pale kibamba njia panda, pia kuna wale matapeli ambao walikuwa wanasakwa na Jeshi la polisi walikutwa wame uwawa kwenye pori la kisopwa kama hawa boda boda, na wanawake hao walionekana wakieleka huko, kabla ya kupata hajari, “kuna umuhimu wa kuelekeza macho yetu kibamba” aliwaza insp Johnson ambae kichwa chake kilishindwa kuendelea na kazi na kuamua kuacha ile kazi, ya kufanya makadirio ya kuunda kikosi, akatoka nje ya ofisi, na kuelekea nje kabisa ya jengo hili kubwa, la polisi akitazama ueleko wa canteen ambayo utegemewa na idadi kubwa sana ya wananchi waliopo eneo hili la kaliakoo, kwa maitaji ya chakula, maana insp akuwa amekunywa chai, wala kupata chochote tumboni, “baba ina bini nimtafutie ulinzi wanguvu” alliwaza insp akiwa anelekea kwenye canteen hiyo, iliyopo mita mita chache toka kituoni hapo, ** baada ya kuingia ofisini na kumweleza boss wake, juu ya ujio wa familia yake, na kwamba anaenda nao kaliakoo kufanya manunuzi, Denis alitoka mle ofisini akiongozana na boss wake, ambae aliwasalimia Jackline na Fransis, huku akimpatia Fransisi, not ya Elfu kumi kama zawadi yake, Denis aliaga kisha yeye na mke wake na mtoto wao, wakaondoka zao kuelekea kaliakoo, mda mwingi mtoto Fransisi alionekana kuwa mchangamfu sana, akifurahia uwepo wazazi wake wote wawili, safari yao ilikuwa ni nzuri ya furaha, tofauti na wakati wanatoka nyumbani, ambapo mtoto fransis alikuwa ajamzowea baba yake, mida hii tayari alisha anza kumzowea, a kumfanyia michezo ya kumjaribu jaribu, na Denis nae akamuunga mkono mwanae wakwanza ambae alitokea kmpenda toka akiwa tumboni kwa Jackline, Jackline nae akuwa mbali alijinga katika michezo ya baba na mwana, ambayo kwa kiasi kikubwa ilikuwa ni ngumi, “huyu dogo hizi ngumi anaziona wapi?” aliuliza Denis kwa mshangao, “ameziona kwenye video ndani ya bus, wakati tunakuja,” alijibu Jackline haraka sana, maana alijuwa kuwa Fransisi, maanyingi uwa anamshuhudia akiwa katika mazoezi na yeye uigiza katika michezo yake, “basi anakichwa chepesi sana, miaka miwili tu!, chekechea” aliongea Denis wakiwa wanaingia kaliakoo, ambapo walienda karibu na kituo cha kuuzia mafuta ya gari, wakatafuta sehemu nzuri na kusimamisha gari, wakashuka na kulifunga vizuri, kisha hao wakaondoka zao, na kuanza kuzurula kwenye maduka mbali mbali, ya vifaa vya wanawake na watoto, ikwepo pia maduka yanguo na vifaa vya kuchezea watoto, kitu ambacho uwezi amini, mtoto kabla aja weza kutembea mwenywe lakini, alinunuliwa baiskeli ndogo, pamoja na vigari ambavyo angeweza kukaa ndani yake, wakati akiliendesha kwa kutumia umeme wa kuchaji, pia wakati baba huyu alie kuwa bado anamning;inio wa pombe za jana, alikuwa anaamini kuwa mke wake akuwa na nguo nzuri, baada ya kukaa sana Songea, alinunua nguo nyingi za mke wake na mwanae, pia kuna bahadhi ya nguo alinunua zilizo fanana, pengine yeye na mwanae au wote watatu, au yeye na mke wake, ikiwa pamoja na viatu, navyo walinunua kwa mtindo huo lakini idadi kubwa ikiwa ni Fransisi, na baba yake, japo kunaviatu kama rubber walinunua zilizo fanana, walijiachia pasipo kujuwa kuwa kuna mtu ametamani matumizi wanayo yafanya, akiamini kuwa wanafedha za kutosha, “njaa ina ni tafuna vibaya sana ngoja nika weke hii mizigo kwenye gari nyie ingieni kwenye jengo lile nakuja sasa hivi” aliongea Denis, akimwonyesha Jackline canteen iliyopo karibu na kituo cha polisi, maeneo ya msimbazi, na Jackline ambae sasa likuwa amembeba mtoto mgongoni, akashauri kuwa waende pamoja, uweka mizigo alafu, ndio waende kupata chakula pamoja, “ila tufanye haraka, mkojo umenibana sana” aliongea Jackline, akiwa na uakika kuwa kwenye ile canteen lazima itakuwa na choo ndani yake, ** saa sita na nusu insp Johnson alikuwa amesha toka canteen, tanu nusu saa iliyopita, alikuwa amesimama nje ya jengo la kituo kikubwa cha polisi, akiwaza na kuwazua, mala akasikia simu yake inaita akaitazama alkuwa ni Pc Busungu, akaipokea mala moja, “niambie busungu, kunajipya lolote?” aliuliza Johnson baada ya kupokea simu, “napita hapa barabarani, naelekea canteen kupata chakula, nakuona hapo nje” aliongea Busungu, na insp Johnson akainua uso wake kutazama barabarani akamwona Pc BUSUNGU, nakuona kaka, aina noma ukitoka huku pitia ofisini, kunakitu nataka tuongee” aliongea insp Jonhson huku akipunga kono kumpungia Pc Busungu, ambae nae alijibu, kwakupunga mkono, “aina tatizo kaka, napatachakula nakuja” alijibu Busungu, huku anaelekea canteen, huku anawapita watu wengi walio zagaa, kwenye mitaa hii ya sehemu maalufu ya kaliakoo, wakiwemo mke na mume waliokuwa na mtoto wao, ambao aliwapita akiwa atuwa chake kutoka kwenye mlango wa kuingilia kwenye canteen, ** wakati huo kijana mmoja anae jiita mbwa mchafu, alikuwa atuwa chache nyuma ya wanafamilia awa, ambao alianza kuwafwatilia toka kwenye maduka ya nguo, na vifaa vya kuchezea watoto, kwa nia ya kuwaibia, maana alikuwa na uakika kuwa wanafedha za kutosha, kutokana na manunuzi waliyo kuwa wanayafanya, sasa aliwaona wanaingia canteen, akasimama nje ya cantee le kubwa macho yake yakiwa ayabanduki kwao, akiwatazama mpaka walipoenda kukaa, lakini aikupita atadakika moja akamwona yule dada akimwambia kitu ume wake, kisha yule mwanaume akatoa kiasi cha fedha na kumpatia yule dada, kisha yule mwanamke akainuka na kutoka nje kwa upande wapili, “inatosha kwa mchana” kijana huyu ambae ni mashuhuli kwa tabia ya kukaba na pola, aliongea hivyo pasipo kujuwa kuwa ni kiasi gani cha fedha alicho pewa Jackline, Mbwa mchafu alichomoka haraka akipita moja kwa moja katikati ya ile canteen iliyo jaa watu, ambao wengi wao ni wakutoka maeneo ya mbali, na pengine ni wachache sana ndio waliokuwa wanamfahamu, vyama kijana huyu ambae amesha kamatwa mala nyingi na plisi, na kuachiwa baada ya mda mfupi, Mbwa Mchafu aliongeza mwendo kumfwata Jackline, akiwa na uakika kuwa anaenda chooni, maana mlango aliopitia, ulikuwa unatokea uwani, na akukuwa na mlango mwingine wa kutokea eneo hilo la canteen, *** Jackline Michael Nyati baada ya kumkumbusha mpenzi wake Denis kuwa anaitaji kwenda chooni, Deins akampatia not ya buku kwaajili ya kulipia huduma ya choo kihasi cha shilingi za kitanzania mia mbili, akimwonyesha na uelekeo wa kilipo choo, Jackline alitembea tartibu kuelekea upande alio onyeshwa na mume wake kipenzi, lakini wakati anakatiza mbele ya watu wengi waliokuwa wanapata chakula, mala ghafla macho yake yakagongana na macho ya kijana mmoja ambae alimkumbuka mala moja, japo ni miezi tisa imepita toka alipo mwona kijana huyu, huko Songea, akiwa pamoja na Johnson pale mtaa wa lizombe, siku waliyo kuwa wanampigia simu Felister, lakini sura hii aliikumbuka mala moja, akavunga kuto kustuka kabisa, maana akuona dalili ya kijana yule ambae siku ya kwanza kukutana nae alionyesha tamaa ya ngono juu yake, kustuka wala kuogopa, Jackline akatembea na kutoka nje ya ukumbi hule mkubwa, huku akitumia ujanja mkubwa sana kumtazama yule kijana, alievalia mavazi ya kilaia, akamwona akiwa ameinamisha kichwa chini kama anawaza au kujikumbusha, jambo flani, hapo Jackline akapiga mahesabu ya kutumia mda mfupi chooni, na kutoka ikiwezekana aondoke kwa kisingizio chochote, maana maalipale hapa kumfaa tena, aliwaza hayo Jackline huku akizidi kuvuta atuwa kukifwata kibanda kimoja kilicho jitenga kikiwa na bango dogo, lililo andikwa choo cha kulipia, kubwa mia tano, ndogo mia mbili, akamwona kijana mmoja akiwa amekaa kwenye kiti, nje ya kibanda hicho na daftari mkononi, lakini kbla hajamfikia akasikia sauti ya kiume toka nyuma yake, “hoyaaa bbabu msikilize dada yangu anaitaji huduma” Jackline akageuka nyuma na kumtazama aliejiita kaka yake, akamwona kijana mmoja alie onekana kujengeka kimazoezi, huku mikono yake ikionekana kukomaa kweli kweli, lakini mavazi yake ambayo ayakuwa masafi sana wala machafu sana, akija kwa mwendo wa kasi, “ok! dada ingia pitiliiza upande wakushoto” aliongea yule kijana alie kuwa amekaa karibu na kile choo, lakini Jakline Nyati akuonyesha uharaka wowote, akamkabidhi yule jamaa msimamizi wa vyoo noti ya elfu moja, kisha akamwambia chenji achukuwe, huku Jackline ambae aliona dalili za huovu, machoni kwa yule kijana, aliye jiita kaka yake, akipitilia na kuelekea upande wa kushoto wa jengo lile dogo la choo, alifungua mlango na kuingia ndani ya choo hicho, na kitafuta cumba kiomja kati ya sita vya mle ndani akaingia na kuanza kumwaga mkojo, uko nje akasikia maongezi ya yule kijana mtunza choo, na kaka wa bandia, “niambie mchafu unasema?” aliuliza ule mtunza choo, Jacklline akusikia sauti yoyote ya mtu kujibu, zaidi akasikia mlango wa choo kile ambacho akikuwa namtu mwingine, zaidi yake ukifunguliwa, Jackline akasikilizia vishindo vya mtu alie ingia, akagundua ni vishindo vya kiume, tena sasa vilikuwa vina kuja upande wa choo alichoingia yeye, Jackline akiwa ana malizia kujisaidia, akasikia mtu ale ingia akijaribu kuufunga mlango wa choo alichoingia, ambao aliufunga kwa ndani, Jackline akatabasamu “amejileta” aliwaza Jackline wakati anajiweka safi na kuvaa nguo zake vizuri, kisha akafungua mlango kwa tahadhari, akitumia sekunde kadhaa kusimama pasipo kutoka, kama livyo tegemea, akamwona yule kaka wa bandia akijitokeza mbele yake, na kusimama akiwa na bisi bisi mkononi, “sikia we mwanamke, kimya kimya, ukipiga kelele nakutoboa, chakufanya vuanguo zako zote, mpaka hiyo bangiri, viatu na hizo hizo eleni na cheni” aliongea Mchafu, kwasauti yachini, huku akianza kulegeza mkanda wa suluali yake, kwa mkono mmoja, humu mkono mwangine bado ameshikilia ile bisi bisi, “sasa kaka mbona unavua suluali”
HUU NDIO MWISHO WA SEASON THREE
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU