BINTI MDUNGUAJI (62)

SEHEMU YA SITINI NA MBILI

ILIPOISHIA SEHEMU YA SITINI MOJA : wakati huo huo simu ya Jackline ikaita Jackline akaitazama simu yake, akaona jina lime andikwa baba, akaipokea na kuweka sikioni, hapo Denis akusikia kitu chochote zaidi ya shikamoo, kisha ikafwata ndiyo ndiyo ndiyo, mwishoni kabisa ikawa sawa, alafu simu ikakatwa, alafu Jackline akasema “kazi imeanza” maneno hayo yali mstua Denis akamtazama mkewake kwa mshangao, ENDELEA ………..
“Kuna nini tena kimetokea?” aliuliza Denis kwa mshangao mkubwa, akijuwa kuwa kuna tatizo nyumbani, maana Jackline au mama France uwa anapigiwa simu kutoka nyumbani kwao Songea tu, kwa baba yake, “baba anasema, mama anaumwa” alijibu Jackline kwa sauti ya chini, kama vile amenyongea flani hivi, “kwa hiyo unafanyaje, tutaenda au inabidi utatuma fedha?” hapo Jackline akamtazama mume wake kwa macho yakipekee, yaliyo jaa upendo na shukurani, huku anasogeza mkno wake wakushoto na kuushika mkoni wakushoto wa Denis, “nashukuru sana mume wangu, kwa kuwajali wazazi wangu, nazani tuwatumie fedha tu!, iwapo atazidiwa sana tutaenda kuwaona” hapo Denis alijikuta akitaasamu “usijali mke wangu, ilo nijukumu langu kuakikisha wazazi wetu wana pata tiba na maitaji mmuhimu, kwani wazazi wako ni wazazi wangu, ila sijuwi nikiasi gani kitaitajika kwenda kutuma?” aliuliza Denis, “nazani nifedha kidogo tu za dawa” alisema Jackline huku wanaendelea kula, “hapana Jack, nazani wanaitaji fedha za kutosha, sababu atuja watumia fedha toka ulipo kuja kutoka Songea” aliongea Denis na Jackline akuwa na kipingamizi, ila wakakubariana kuwa kesho waende pamoja mjini kisha Jackline aende kutuma fedha hizo, ambazo nikiasi cha shilingi laki tatu za kitanzania, ** taalifa ya kukamatwa kwa KAIJAGE, ilitapakaa sana nchini, ukiachilia mzee Nati na insp Johnson pia ilimfikia rafiki yake mzee David Masinde, baada yakuipata taalifa hii bwana masinde akamkubuka mkuu wakitengo cha upelelezi wakosa ya jinai alie msaidia kumtoa bwana Mathayo sikule aliyo uwawa, hivyo akampigia simu kuitaji msaada wake, baada yakupokea simu mkuu wakitengo cha upelelezi , mzee Masinde alimweleza shida yake, na wakakubariana kusaidiana kwa kuficha ushaidi, huku wakitumia unja kama ule wa mwanzo, wa kutengeneza nyaraka fake ya kuibiwa kwa gari, huku wakipanga kutoa uhai wa dereva, ambae mpaka sasa alikuwa yupo hospital akitibiwa majalaha aliyo yapata kwenye hajari, natukio hilo lilipngwa lifanyike usiku ule, “andaa millon ishilini kwangu, na kumi kwa mtu atakae fanya kazi hiyo, njoo nayo kesho asubuhi , ofisini kwangu” alimaliza mkuu wa upelelezi, na mzee Masinde akaubaliana nae, * ijumaa saa mbili asubuhi, insp Johnson alikuwa ndani ya ofisi yake katika jengo kubwa la kituo kikuu, akimalizia kukagua report ya siku iliyotoka, kisha akainuka na kuelekea ofisini kwa mkuu wakitengo cha upelelezi, akatoe report ya sikuile, kisha aende kumwona mzee Kaijage kule mahabusu, laikini wakati anatakakuingia ofisini kwa mkuu wake, akazuiliwa, akiambiwa kuwa kuna mgeni ndani ya ofisi hiyo, hivyo alitakiwa asubiri kidogo, mgeni huyo atoke, insp alikaa kwenye kiti kimoja kati ya vitatu vilivyo kuwepo maalipale, huku akiwaza juu ya mzee Kaijage, ambae ni rafiki mkubwa wa baba yake, na apakuwa na shaka kuwa, mzee huyu ni mmoja kati ya wale waliotakiwa kuuwawa, “lazima nimshawishi ani eleze kitu ambacho walikifanya huko congo” aliwaza insp Johnson ambae alikuwa ana amini kuwa endapo atajuwa siri hiyo, itakuwa lahisi kwake kumaliza swala hili, wakati Johnson anaendelea kuwaza mahari pale mala akaona mlango wa ofisi ya mkuu wa upelelezi, unafunguliwa, na akamwona baba yake mzee Masinde, akitoka ndani ya ofisi hiyo Johnson akaduwaa, “ba….. ha! mzee umefwata nini hapa” aliongea kwa sauti ya chini insp Johnson, huku anainuka toka kwenye kiti alicho kuwa amekalia, na kumwafwata baba yake, “usijari Johnson, nilikuwa na maongezi kidogo, na mkubwa hapa” aliongea mzee Masinde, kisha akaanza kutembea kuelekea nje ya jengo lile, insp alimtazama baba yake mpaka alipopotea nje yajengo, insp akaingia ndani ya ofisi ya mkuu wa upelelezi, akamkuta boss wake akiwa anaifadhi fedha kwenye begi lake dogo la mkononi, “hooo! insp karibu, tena nilikuwa nataka niagize uitwe haraka, maana kunajambo lakushngaza limetokea huko hospital” alisema mkuu wa kitengo cha upelelezi, ambae akuwa anafahamu kuwa mzee Masinde ni baba wa Johnson, Johnson nae akasalimia kwa kupiga salut, kisha akiwa bado amesimama mbele ya meza kubwa mle ofisini, akauliza, “samahani afande, huyu mzee alietok mna fahamiana,?” hapo Johnson akamwona afande wake akibabaika kujibu “haaaaa! mh!!!! huyu bwana ni mwana siasa, ni rafiki yangu wamda refu sana, toka tupo chuo cha magogoni, wakati huo tuna somea siasa, alikuja kunisalimia tu!” aliongea mkuu hyu akimdanganya Johnson, huku akiwa na uakika Johnso atokuwa na uwezo wakufahamu uongo huo, wakati Johnson akiwa anashangaa jibu la afande wake, mzee huyu aka muwai, “insp kunatukio lilitokea jana, kuna hajari ilitokea huko kibaha” alianza kuongea mkuu waupelelezi wa makosa ya jinai, akimweleza Johnson kuhu kifo cha dereva wa gari lililo sababisha hajari na kukutwa na nyara za serikali, huku akiwa anasikitika sana juu ya kifo cha dereva, mkuu wakitengo cha upelelezi alisema kuwa derva huyo alikuwa mtu muhimu sana kwa upelelezi wa tukio hilo, sababu gari hilo lilikuwa limerepotiwa kuibiwa siku chache zilizo pita, taalifa hiyo ilimstua sana insp ambae kengere ya tahadhari iligonga kichwani mwake, huku likimjia tukio lililo tokea mwaka mmoja uliopita, kwa mzee Mathayo, “kwahiyo afande, huyu alie kamatwa inabidi aachiwe?” aliuliza Johnson kwa mshangao, “hapana insp, huyu bwana ataachiwa jumatatu mahakamani, baada ya kuwakirisha report ya upotevu” aliongea mkuu wakitengo cha upelelezi, huku akimruhusu insp kuwakilisha report yake, ** baada ya kufika ofisini, na kuomba luksa Denis na mke wake wakiwa na mtoto wao France wakaondka na kuelekea mjini kutuma fedha, “unajuwa baba France mimi sizijuwi sehemu nyingi hapa mjini?” aliongea Jackline huku, wakati wakiwa wana katiza maeneo ya fire, “kama wapi mke wangu?” aliuliza Johnson huku akipunguza mwendo, “huko wanakosemaga poster, bandalini ata maakama siijuwi yani nakujuwa hospital tu!?” aliongea kwa mtindo wa kulalamika Jackline, “ok! inabidi twende kwanza tukatumefedha, kisha nikuzungushe mpaka ikulu, ukakuone” alisema Denis huku akikata kna kuingia kaliakoo, “alafu inabidi week end hii nikufundishe kuendesha gari, ikiwezekana tutafute gari jingine liwe linakusaidia katika miznguko midogo midogo” aliongea Denis huku akiendelea kuendesha gari kuelekea ofisi za zamani za kamata (kampuni ya mabasi Tanzania) , ambapo sasa zilikuwa zina milikiwa na kampuni moja ya mabasi ya mtu binafsi, “mh! nitaweza kweli baba France?” aliongea Jackline nakumfanya Denis acheke kidogo, “kwanini usiweze mama France, nikitu lahisi tu, nitakufundisha kuanzia kesho” aliongea Denis akimwondoa wasi wasi, mke wake, “mh! sizani kama nitaweza” aliongea Jackline wakati huo waikuwa wameshafika, na kusimama nje ya ofisi za kamata yazamani, “utaweza tu! wala usiwe na wasiwasi” Jackline akashuka kwenda kutuma fedha, huku Denis akibakia ndani yagari na France, ** baada yakutoka ofisini kwa mkuu wakitengo cha upelelezi, insp Johnson akiwa na mawazo tele, akaondoka peke yake, akielekea kibaha hospital ya Tumbi, akitumia gari lake binafsi aina ya Toyota wish, insp Johnson akiwa anahisi hatari ikikaribia siku za karibuni, maana alionganisha matukio ya vifo hivi, vyote vilitanguliwa na flani linalomweka muusika adharani, ilionyesha kuwa muuwaji alisha wasahau mawind yake, hivyo alitumia nafasi kama hizi kuwa ng’amua, na kuwamaliza, insp alipofika maeneo ya mbezi maeneo ya magari saba, akamchukuwa Busungu, kisha wakaenda pamoja Tumbi kufwatilia kilicho msibu dereva, mpaka kupelekea kifo chake, dakika kumi natano insp alikuwa ndani ya Hosptali teule ya tumbi waki jaribu kuulizia kilicho sabisha kifo cha dereva huyu, ambapo waliamabiwa kuwa dereva huyu amepoteeza maisha isha baada ya kuvuja damu nyingi, lakini walipoomba taalifazake za mwanzo, waligunduwa kuwepo na utata, maana zilionyesha kuwa marehemu ni mmoja kati ya watu wachace walio umia kidogo katika hiyo hajari, hapo Johnson na busungu wakatazamana, “kuna mchezo mchafu unachezwa” alisema Johnson huku wanaelekea kwenye gari lao na kundoka zao, kurudi mjini, ** ilikuwa ni safari fupi sana yenye mzunguko mfupi, wa njia moja, maana baada ya kumaliza kutuma fedha kwenye kampuni ya bus, Denis akiwa anamtembeza mke wake, waliingia mnazi mmoja, wakaelekea pster na kunyoosha ocean road akiiita hospital na kutokea ikulu, kisha kwa maombi ya Jackline, wakasimama maeneo ya bandarini, kwenye kituo cha poster ya zamani, mita mia nne kutoka mahakama kuu, hapo wakashuka na nakuanza kutazama mandhari ya bahari, ambapo walitumia kama nusu saaa hivi kutazama eneo hilo, pasipo Denis kujuwa Jackline alikuwa analengo lake jingine kabisa, baada yakulizika wamesha tazama vyakutosha wanafamilia hao, waliingia ndani yagari, nakuondoka zao, safari yao ilitumia nusu saa nyine mpaka Denis aiposimamisha gari mbezi akienda kununua cartoon la bia na mvinyo mwekundu kwaajili ya mke wake, Denis aishuka kwenye gari na kuelekea ndani ya full dose, akiliacha gari karibu na sehemu ya kuingilia na kutokea, akiamini atatoka mda siyo mrefu, ** “ebwanae nasikia njaa kari sana” aliongea insp Johnson wakati wanapita mbezi kwa Yusuph, “kuna pub moja hapo, wanachakula kizuri sana, kwasikuzote nilizo shinda huku ndio na kula ga hapo” aliongea Busungu, na kumwelekeza Johnson, sehemu aliyo itaja, dakika tano baadae walikuwa wanaingia sehemu hiyo, lakini wakakuta kuna gari aina ya Toyota noah, ikiwa imeegeshwa kwenye sehemu ya kuingilia, “watuwengine bwana sasa ndio kupakigani huku” aliongea kwa Johnson huku anapiga honi kwanguvu, akilipigia lile gari mbele yake, lakini akuna alie stuka zaidi waliona kama kuna mtu ndani yagari, tena mwanamke, ambae alikaa upande wa abiria, na akuonyesha kujari honi ile, “ngoja kwanza” aliongea Busungu huku akishuka toka kwenye gari na kulifwata gari lile, *** Jackline aliliona gari la insp Johnson likiingia pale Full dose pub, kwanza alilifananisha, maana aliliona siku moja tu! tena nyumbani kwa insp Johnson, siku ile alipoenda, hivyo akatulia na kulitazama kwa kutumia back vew, na bahati mbaya gari hilo likaja na kusimsms nyuma ya gari lao, ambalo liliziba njia, Jackline akatazama vizuri, akawaona watu waliokuwa ndani ya gari hilo, akawatambua mala moja, ni insp Johnson a busungu, akimtambua kuwa nikijana ae mwona miezi sita iliyopita pale kweny canteen kaliakoo, Jackline akaumiza kichwa afanye nini, ili wakina busungu wasimwone, mala akasikia honi kaari ikitokea kwenye gari la kina busungu, wakionyesha kuwa wanaitaji nafasi ya kupitisha gari lao, ukweli nikwamba Jackline asingeweza kusogeza gari, akiofia kubainika uongo wake kwa Denis, “nifanye je hapa?” aliwaza Jackline, huku anatazaama kwenye side mirror na kumwona Busungu anashuka toka kwenye gari lile na kulifwata gari lao, “mungu wangu nimekwisha” itaendelea………

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!