BINTI MDUNGUAJI (63)

SEHEMU YA SITINI NA TATU

 

ILIPOISHIA SEHEMU YA SITINI MBILI : “ingia barabara kuu elekea mjini?” alisema Busungu baada ya kukodi moja ya boda boda, bila kuzubaa yle boda boda akawasha pikipiki na kushika njia ya kuelekea mjini, wakati huo Busungu alikuwa anapiga simu kwa insp Johnson, na wakati huo hoo alikuwa anasoma namba zagari zilizo kuwa zina someka vizuri, kutokana na ung’aavu wa kibao cha namba za gari lile, ENDELEA ……..
Ambalo kwasasa alikuwa analitazama kwambele, simu ya insp iliita kwa mda mrefu pasipo kupokelewa kabisa, “insp unanini wewe? tutampoteza huyu, kahaba, pokea simu” aliongea Busungu kwa sauti ya chini huku, kiasi cha yule dereva wa boda boda kuto sikia vizuri, “usi jari braza si yule demu mkali alie tokea pale kwa Artist,?” aliongea dereva wa boda boda huku akijitaidi kuyakwepa magari na kuyapita, kwa fujo kulikaribia gari la Jackline Michael Nyati, lakini Busungu aka mzuwia boda boda yule asi likaribie lile gari maana ingekuwa lahisi kwa Jackline kustuka na kujuwa kuwa anafwatiliwa, licha ya boda boda ku punguza mwendo, lakini alikuwa amesha chelewa, maana walikutana na askari polisi wa usalama barabarani, waliosimama maeneo ya mbezi kwa Yusuph, “awa nao weseng… kweli, sijuwi wanataka nini?” aliongea Busungu kwa sauti ya chini, wakati piki piki inasimama na yeye akaruka haraka sana na kumfwata yule polisi alio wasimamisha, huku anatoa kitamburisho chake mfukoni na kumwonyesha yule polisi, “samahani afande, kuna dharula naomba niwai nitampoteza mtuhumiwa ninae mfwatilia” hapo yule polisi akachukuwa kile kitambulisho na kukitazama kidogo, kisha akamtazama Busungu kuakikisha kama kweli picha ya kwenye ID ni yakwake, alafu aka mruhusu aende, akiwa amesha mchelewesha, lakini baada ya hapo Busungu akiwa na dereva wa boda boda, wali chapa mwendo bila afanikio, huku busungu akijaribu kupiga simu kwa insp mala kwa mala lakini simu aikupokelewa, kwa kuwa Pc Busungu alikuwa amesha zikalili namba za gari la Jackline, akaziandika kwenye meddeji na kuzituma kwa insp, akiandika hivi ‘Jackline anakuja mjini anatumia gari aina ya Toyota Noah, lenye namba T 182C..P’ mpaka wawili awa wanafika ubungo mataa, na kuzuiliwa na taa za kuongozea magari, walikuwa awajaliona gari la Jackline, “huyu atakuwa ameenda mahakamani anataka kufanya tukio kama la sikuile kituoni” alichekecha akili, nakupata jibu hilo, “twende posta” Busungu ali mweleza yule mwendesha pikipiki, baaada ya taa kuwa ruhusu, dereva boda boda akafwata maelekezo akitarajia kutimiza hesasbu ya bisi wake mapema sana, ** huyu alikuwa Jackline Michael Nyati, ambae tokea asubuhi mumewake ajaribu kuwasha gari na kushindwa, na kuondoka kwa miguu akielekea barabarani, kutafuta usafiri mwingine, Jackline baada ya kusubiri kwa mda flani, nakuakikisha Denis amesha ondoka, yeye akaingia chumbani na kunza kujipanga, akivalia kikaptulah kifupi cha jinsi, na tishet jeusi, kisha akaelekea kwenye banda la kuifadhia gari, ambako alichukuwa begi lake jeusi na kuingia nalo ndani, ndani ya dakika kummi na tano, Jackline alikuwa amesha weka tayari silaha zake kiunoni kwenye mkanda wa kiuno wa kikaptulah chake, ikiwa ni bastorah yake yenye risasi kumi, na kiwamb sauti, kisu chake cha kijeshi, kamba yake ndefu kihasi iliyo fungwa vizuri na kuonekana ndogo, alipo maliza akavaa gauni lake kwa juu, kiasi cha mtu yoyote kuto kutambua kilicho fichwa ndani ya gauni hilo, baada ya hapo Jackline akamchukuwa mwane France ambae alisha mwanda, wakaingia kwenye gari na kuanza safari, kituo cha kwanza kibamba ccm, kwa mchoraji, akachukuwa plate namba alizoacha kwa mchoraji amchoree kibao hicho, akimkabizi namba nyingine kabisa ambazo alikuwa anazitoa kwenye simu zake, akwa msaada wa mchoraji huyo Jackline akabadirisha namba za gari, kisha safari ikaanza, wakati anatoka kibamba ccm, na kuikamata barabara kuu iendayo morogoro, na kutembea kama mita mia hivi, akaiona piki piki ikiingia barabaran, na kuja upande aliko yeye, mwanzo akujuwa kama ina mfwata, kilicho mtua ni fujo za ile pikipiki, ambayo ilipo mkaribia ilipunguza mwendo, nayeye akaiacha, na hapo ndipo Jackline alipo pata nafasi ya kumtambua abiria wa ile bodaboda, alikuwa ni Busungu, wakati anapanga kuwakimbia, bahati nzuri akaiona ile pikipiki ikisimamishwa na polisi, wa usalama barabarani, hapo alicho kifanya Jackline au mama France kuchapa mwendo wa ambulance, mpaka anafika posta akuwaona kabisa wakina Busungu, kwa kujiachia kabisa Jackline akaenda kuegesha gari lake nyuma ya mtaa wa mahakama kuu ambayo hipo jirani na kanisa kuu, yeye akaendesha gari taratibu, kisha akaliegesha pembeni ya jengo la Wajasiliamari, jengo kubwa la ghorofa nne, ambalo lipo umbali wa mita mia tano toka mahakama kuu, alicho kifanya Jackline alimwachia mwanae vifaha vya kuchezea, pipi na choclate za kutosha, “Franceeee nakuja sasa hivi naenda kuleta pipi nyingine, sawa babaaaaa” alisema Jackline huku akimchezea France shavuni, na yeye akaitiki kwa kichwa, hapo Jackline akachukuwa begi lake na kutoka nalo kwenye gari kisha akaelekea ndani ya jeng ilo la ghorofa nne, lenye ofiso kadhaa zakibiashara, huku Jackline akiwa amejitanda kanga kichwani, akapotelea ndani ya jengo lile, ambalo mda huo lilikuwa na pirika pilika za watu wengi sana, ** ndani ya ofisi ya wasanifu wa majengo, wakina Denis walikuwa wamejikusanya mapokezi, pale kwa Janeth, wakitazama kwa bashasha trevishen ambayo ilikuwa ina rusha moja kwa moja matangazo yake toka kwenye viwanja vya mahakama kuu, ambapo kwa kupitia tv wakina Denis, Mahadhi Janeth na boss wao, waliweza kuona jinsi watu wengi sana kwenye, waliojaa nje ya uzio wa mahakama hii kuu, mtangazaji wa terevision hii biafsi, alionekana akiwahoji bahadhi ya watu waliokuwepo eneo lile, ambao walikuwa wana hamu ya kusikia matokeo ya Mahakam hii, inayo muhusu mmiliki wa gari ambalo licha ya kukutwa na nyara za serekali, pia gari hilo lilisababisha hajari kubwa sana, iliyo ondoka na roho nyingi za watu, “yani huyu jamaa ataondoka na mvua zakutosha sana” aliongea Mahadhi, “wewee ujuwi kitu kabisa, yani mtu anacheza diri kama hizo alafu afungwe kilahisi” aliongea Denis akionyesha kutokuwa naimani na vyombo vya sheria, “ila Denis bwana, kumbe ni mlevi, lakini una waza mbali sana” aliongea boss wao huku wakiendelea kutazama tukio lile kwenye TV LIVE, ** Ndani ya mahakama kuu watu walikuwa wengi wakisikiliza kesi mbali mbali, huku lengo ni kusikiliza hii ya ambayo kwa sasa ndio ilikuwa inatolewa maamuzi, ni kesi ya bwana Kaijage, ambae kwa sasa alikuwa amesimama kwenye kizimba cha mahakama, huku pingu zikiwa mkononi mwake, usoni kwa mzee huyu akuonyesha wasi wasi wowote, kwa watu wanao juwa kudadisi walijuwa juwa kuwa mzee huyu Anaya fahamu maamuzi ya mahakama yanayo tarajiwa kutolewa, insp Johnson akiwa ameondoa sauti ya mlio katoka simu yake, kutokana na sheria za kimahakama, kwamba akukutakiwa kelele za aina yoyote, wakati mahakama ikiendelea, Johnson alikuwa ametulia akisikiliza maamuzi ya Mahakama, “baada ya mahakama kulizika na uchunguzi, na taalifa ya jeshi la polisi, ambao ume thibitisha kuwa gari la mtuhumiwa, nyara za serikali, bwana Charles Kijage, ambapo imegundulika kuwa gari la bwana Kaijage liliibiwa week moja iliyopita, na taalifa ya upotevu ilitolewa, AMBAYO NI PF 3 No 000…1, katika kituo kikuu, na shauri lapilli la gari kusababisha hajari hiyo imefanywa na mwizi wa gari hilo ambae alikuwa ni mwajiliwa wa bwana Kaijage, na sasa ni marehemu ambae amkutwa na umahuti uliosababishwa na majelah ya hajari hiyo, kwa hiyo mahaka aijampata bwana Charle Kijage, na hatia yoyote, hivyo basi mahaka inamwacha huru bwana Kijage kuanzia sasa,” kauri hiyo ilimaliziwa kwa chundo kugongwa mezani, na askari mmoja kusema “koooort” watu wote waka simama kisha yule Jaji akasimama na kuondoka zake, baada ya jaji kutoweka zikaripuka sauti mbali mbali za maongezi, ikiwa ni furaha na malalamiko, akaonekana bwana Kijage akichukuliwa na rafiki zake, nakuanza kutoka nje, huku wakimpongeza kwa kuchomoka kwenye ile kesi, mmoja wa rafi wa Kijage , alikuwepo mzee Masinde, hapo ndipo insp Johnson alipozinduka na kunyanyuka toka kwenye kiti alicho kalia, na kuelekea nje, ambako mpaka dakika hii, watu walikuwa wamechachamaa, wakipiga kelele, kuonyesha kuwa awakulizika na maamuzi ya mahakama, kelele zilikuwa ni nyingi sana, zikifawatiwa na wanchi kuanza kurusha mawe kuelekeza kwa bwana Kaijage, huku rafiki zake bwana Kijge wakijitaidi kumkinga na kumkimbiza kwenye gari, napolisi nao wakijaribu kuwazuwia mwanachi wasirushe mawe, ** “umeona umeona, sinilikuambia, kikowapi sasa?” aliongea Denis kwa hamaki, “kaka umeona mbali sana, du! nimekubari” alisema Mahadhi huku wiendelea kutazama TV, “cheki wananchi wanavyo chachamaa” aliongea boss, huku wakiendelea kutazama jinsi wananchi walivyokuwa wanarusha mawe, “aitasaidia chochote, yani pale kinachofwata, watapigwatu!” aliongea tena Denis, *** insp alikuwa amesimama kkwenye mlngo wa mahakama, akitazama jinsi wananchi, walivyo kuwa wana rusha mawe, huku rafiki zake Kaijage, wakijitaidi kumkinga na kumsogeza Kijage kwenye magari, pasipo kujuwa kuwa wanausogeza ugomvi kwenye vioo vya magari sababu dakika chae baadae wakaanza kuona mawe yakituwa kwenye vioo vya magari, yaliy kuwepo ndani ya eneo la mahaka, na kupasua vioo hivyo, moja ya gari lilikuwa ni gari la insp Johnson, “pumbavu gari langu” aliongea insp huku anatoa simu yake mfukoni, kwaajili ya kuomba msaada wa polisi wengine kutoka kituo kikuu, lakini ile kuitazama smu akakuta misee call zaidi ya ishilini, toka kwa Pc Busungu, na messeji kadhaa, “mh! kuna nini huko?” alijiuliza insp huku akianza ufngua zile missed call iliapige kwa Busungu, lajini kbla ajapiga akaona simu ikianza kuita tena, mpigaji alikuwa Busungu, insp akaipokea haraka, “afande naombamsaada wa askari hapa wajasiliamri, Jackline Nyati amingia hapa mfupi ulio pita nimeliona gari lake hapa nje” alisikika Busungu akiongea kwa pupa huku akionekana anapanda ngazi, hapo Johnson akajuwa tayari kuna kosa limesha tokea, akawaangalia wakina mzee Masinde wakiwa na wenzake, wanamkinga mzee Kaijage, ambapo sasa walikuwa wamegeuka, na kuanza kurudi walikotoka, yani ndani ya jengo la mahakama, baada ya mvua ya mawe kuzidi, “hallow afande unanisikia?” ilisikika sauti ya Busungu, lakini insp alikuwa amekaza macho kuwatazama wakina mzee Masinde, akamwona baba yake akiwa amemshika mkono mzee Kijage uku wenzake wakiwa wame wazunguka, insp akijaribu kutazama upande wa kushoto kwenye jengo la wajasiliamari, alikoelekezwa na busngu ambae bado alikuwa hajakata simu, naam kwenye gorofa la mwisho kabisa la jego ilo, akaona kitu kama flashi ya radi ndogo ikiambatana kunguru kuruka kwa fujo, kisha ikafwatiwa kelele kutoka kwenye kundi la kina mzee Masinde na wenzake ambao walikuwa wana msadida bwana kaijage, insp akageuza shingo kumtazama baba yake, akamwona mzee Kaijage kichomoka mikononi mwa mzee Masinde, kama ambae alisukumwa na kitu kizito, na kutupwa pembeni, huku kichwa chake kikipasuliwa, na ubongo ulio changanyika na damu kutawanyika, ukiwarukia rafiki zake, na watu walio mzunguka, akiwepo mzee Masinde, itaendelea………

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!