
BINTI MDUNGUAJI (64)

SEHEMU YA SITINI NA NNE
ILIPOISHIA SEHEMU YA SITINI TATU : mala akasikia honi kari, ikitokea kwenye gari la kina busungu, wakionyesha kuwa wanaitaji nafasi ya kupitisha gari lao, ukweli nikwamba Jackline asingeweza kusogeza gari, akiofia kubainika uongo wake kwa Denis, “nifanye je hapa?” aliwaza Jackline, huku anatazaama kwenye side mirror na kumwona Busungu anashuka toka kwenye gari lile na kulifwata gari lao, “mungu wangu nimekwisha”.endelea ……………
Aliongea Jackline kwa sauti ya kunong’ona, huku mwanae France akigeuza geuza shingo kushangaa, asijuwe anacho zungumza mama yake, hapo Jackline aka papas mle ndani kama angepata kitu chenye ncha kali, ambacho kinge faa kutumuika kutoa roho ya Busungu, akapata crew drive (bisibisi) ndefu, wakati Busungu akiwa amebakiza atuwa chache kuufikia mlango wagari la kina Jackline upande aliokaa Jackline mwenyewe, mala Jackline akamwona Denis akitokea ndani ya bar huku amebeba cartoon la bia na chupa moja ya wine, akija upande ule ule ambao busungu alikuwa anakaribia, “hallow wewe ndie mwenye hili gari?” aiuliza Busungu, huku akisimama na kumtazama Denis, ambae alisha likaribia gari, “ndio kaka samahani naona nime wagandisha kidogo” aliongea Denis huku akiungua mlango wa gari wanyuma na kuweka mizigo aliyo kuwa nayo mkononi, “mbona na unafanya mambo ya kibwege, sasa wengine wapite wapi?” aliongea Busungu kama mtu aie panic, Jackline alimwona Denis akitazama kwenye gari la kina busungu, akamwona Johnson akiwa ametulia anawatazama, kumbuka kuwa Johnson alikuwa amevalia sale za polisi, na busungu alikuwa katika mavazi ya kiraia, “maneno machafu yanatokea wapi kaka, niliweka gari hapa nikijuwa kuwa sikai muda mrefu” aliongea Denis ambae alikuwa ameonekana kukosa nguvu, baada ya kuambiwa bwege mbele ya mke wake, na mwanae jpo alikuwa anaamni kuwa France akuwa anajuwa kitu japo kwasasa alikuwa anajitaidi kutaja baadhi ya maneno, Jackline alichukuwa simu yake n kuandika namba yagari, la wakina Busungu, kisha akaisave ‘insp’ “tatizo ujitambui wewe ebu toa debe ilo sisi tuingie bwana” alikroma Busungu, kwa sauti yakibabe, Denis auwa na lakufanya akaweka funga mlango wanyuma wagari lake na kuingia ndani ya gari upande wa dereva, kisha akasogeza gari mbele kidogo, kuliacha gari lile lipite, lilipo ingia yeye akaondoa gari, mda wote busungu alikuwa amesimama akilitazama gari la Denis, “siku nyingine utajikuta hupo kituoni, mjinga wewe” alisikika Busungu akiongea maneno hayo, Denis alimtazama mke wake kwa macho ya huruma, yaliyo changanyika na aibu nyingi sana, “vipi mume wangu mbona kama umenongea?” aliuliza Jackline huku akimpapasa mgongoni Denis, “wale jamaa sijuwi wanajivunia sababu ni polisi” alilalamika Denis huku akiendelea kuendesha gari, kuelekea nyumbani, “eti ananiita bwege?” aliendelea kulalamika Denis, “sema kwasababu nipolisi tu, ila nge mtandika makofi, mpaka angesahau rangi ya gari lao” aliongea Denis kwa msisitizo, kiasi cha kumfanya Jackline acheke sana, huku akisaidiwa na France asie juwa lolote, “unacheka mama France, mpaka dakika hii ningekuwa kituoni” aliongea Denis huku nayeye akiunga kicheko, ** insp Johnson na Busungu, wakiwa pale Full Dose pub, waliendelea kupata chakula ca mchana huku waki jadilina juu ya swala la kifo cha dereva wa loli, “mpaka hapo mkuu amesha chukuwa chake, na jumatatu Kaijage ana shinda kesi kiulahini kabisa” alisema insp Johnson, akiwa na uakika wajambo analo liongea, “kwahiyo lile gari lili ibiwa week iliyo pita?” aliulliza kwamshangao bwana Busungu, “ndio maana yake, na mimi nilikua na mpango wa kumbana huyu mzee mpaka aniambie kilichotoke huko congo” waliongea mengi sana wawli awa mpaka saa nane walipo achana, na insp kuondoka zake kuelekea mjini akimwacha busungu anaendelea na kazi yake, insp alifika nyumbani kwake na kubadirsha nguo akivalia nguo za kiraia, kisha akaelekea kwa baba yake kinyelezi, huko kinyelezi insp na baba yake walikuwa katika mabishano makubwa na juu ya kitndo cha mzee Masinde kwenda ku fanya mpango wa kupindisha sheria, ili kumtoa rafiki yake, “kwataalifa yako baba ile ndio sehemu salama kwake, kumbuka kwajinsi habari zilivyo tapakaa, lazima mzee Nyati atakuwa amesha mtambua, na kupanga kummaliza” insp alijikuta akifichua siri ya kuwa mzee Nyati ni mzima, “inamaana uliidanganya serikali kuwa Nyati amekufa?” aliuliza Masinde kwa msnagao mkubwa sana, apo insp akuwa na ujanja, akamweleza jinsi mambo yalivyo kuwa na jinsi alivyo gundua kuwa mzee Nyati ni mzima, baada ya miezi tisa, lakini licha ya kusimuliwa mkasa wote huo, mzee Masinde akaamini kuwa hizi zilikuwa ni janja ya mwanae ili kumtisha yeye aachane na mipango yake, hivyo alikataa kabisa kuachana na mpango wake wa kumtoa rafiki yake mahabusu, pamoja na kumwepusha na kifungo, akiwa anaujanja insp akaondoka zake, na kurudi nyumbani akipanga kuweka ulinzi mkubwa sana wasiri kwa mzee Kaijage, akishatoka mahakamani, ** juma mosi, asubuhi baada ya Denis kuondoka kwenda kazini, Jackline alianza kazi ya kuikagua silaha yake, aina ya mugnum sniper rifle, baada ya kuakikisha hipo vizuri, aka hiifadhi vizuri na kujiandaa kutoka, pamoja na mwanae France, ** siku hiyo ya jumamosi ilimkuta Busungu akiwa kibamba ccm, ame tulia maeneo ya njia panda ya mloganzila, kalibu kabisa na waendasha pikipiki, kwenye nye kijiwe cha Masafiri cha kununua vyuma chakavu, pia jirani palikuwa na banda la chips la Majani, akiongea na marafiki zake ambao alizoweana nao siku kadhaa zilizo pita baada ya kaa mala kwa mala maali pale, story zilikuwa nyingi sana pale kijiweni, licha ya wakina msafiri na Halfani majani, kuongea na Busungu siku zote lakini awakumtambua kuwa ni polisi, wala lengo la uwepo wake maali pale, ilikuwa saa tano kasoro za asubuhi, Pc busungu akiwepo maalipale mala akasikia sauti za miguno ya watu, “ebwa heee! yani yule demu ni mkari kinyama” aliongea mjani na kuwafanya Msafiri na Busungu, wageuze shingo zao, na kutazama kule alikokuwa anatazama Majani, Busungu kaduwaa, “siamini macho yangu, yani leo kiulaini” alijisemea Busungu kimoyo moyo, huku yeye pamoja na wenzake wakiendelea kumtazama mwanamke alie kubwa amebeba mtoto, “hoya anakaa wapi yule demu” aliuliza Busungu, akiendelea kumtazama Jackline Michael Nyati, ambae alikuwa anatokea kwenye kibanda cha mchoraji, anae julikana kwa jina la #MbogoEdgar, “mh! mimi mwenyewe ndio kwanza namwona leo” alijibu Msafiri, huku wakimtazama Jackline, ambae kwa sasa alikuwa anavuka barabara na elekea upande wapili, “hoya nakuja sasa hivi” alisema Busungu huku anainuka na kuanza kumfwata Jackline kule alikoelekea, “kuwa macho kaka mali zaatu hizo” aliongea Majani akimtahadharisha Busungu, wote wakacheka, wakati huo Busungu alionekana akitembea haraka na kusimama pembeni ya barabara, akisubiri magari yapite iii na yeye aweze kuvuka, wakati huo huo Busungu alichomoa simu yake na kuipiga, ** insp Johnson mda huo alikuwa ametulia nyumbani kwake akiwaza hili na lile, huku mwanae Bite akimsumbua sumbua kwakudai safari ya beach, mala akasikia simu yake ikiita, kuitazama ilikuwa inatoka kwa Busungu, akajuwa kuna jambo jipya, akaipokea haraka na kwa shahuku ya hali ya juu, “niambiae busungu kuna lolote?” aliuliza Johnson, “kaka huku mambo mazuri, atimae nime mwona yule kahaba” alisikika Busungu akiongea kwa mbwembwe, “sikia busungu mfwatilie kwa ukaribu na umakini wa hali yajuu kabisa, mimi nipo njiani nakuja” aliongea Johnson na kukata simu, kisha akapiga kituo kikuu, akiagiza waangaliwe askari kumi haraka sana wakutane kibamba ccm, dakika chache baadae insp alikuwa njiani anaelekea kibamba ccm, ** baada ya kuvuka barabara, pc Busungu alimwona Jackline akielekea upande wa njia panda ya shule, ni kijia kilichopo pembeni kabisa ya barabara kuu iendayo morogoro, akaanza kumfwata kwa mwendo haraka sana, njia hiyo ilikuwa ni yenye ulefu wa mita mia tano, yenye watu wachache waliokuwa wanaenda na kurudi, pc busungu alimwona kwambari Jackline akiwa na mwanae mgongoni, akikaribia kumaliza eneo hili ambalo lina nyasi fupi pasipo nyumba yoyote, hapo Busungu akajuwa kuwa endapo ata mwacha amlize eneo lile atampoteza, na asingeweza kumwona tena, hivyo akuwa na jinsi zaidi ya kuamua kuanza kukimbia, wakati anakimbia macho yake yalikuwa kwa Jackline , ambae alimwona akiingia njia pnd a shule na kujichanganya kwenye kundi la watu, na kuoweka kabisa, Busungu alifika eneo lile la stend na kuanza kuangaza macho huku na huku, pengine ange bahatisha kumwona Jackline lakini wapi akumwona, akazunguka sehemu mbili tatu, lakini akumwona kabisa, kaaza kuulizia kwa watu wawili watatu waliokuwepo pale stend, lakini akuna alimweleza kumwona Jackline, ** kumbe basi wakati huo Jackline kuwa na hili wala lile baada ya kutoka kwa mchoraji, nakuona itakuwa nikupoteza mda kusubiri gari, akaamua kutembea kwa mguu, sababu nisehemu fupi sana, alivuka barabara na kuelekea njia panda huku akisikia maneno yakuchukiza ya vijana wa mtaani, wakiusifia uzuri wake, pengine walitumia lugha chafu, ambayo aikimpendeza Jackline, “cheki lile demu mwngu ukimpat yule yani unamla kama samaki” lakini akuwa na lakufanya Jackline alijitahidi kujikaza kidogo, asichukuwe atua kwa watu wale, Jackline alipo kuwa anakaribia njiapanda ya shule, akastuka na kuhisi kuwa, kama kunamtu anakuja upande wake kwa kukimbia, Jackline akutaka kugeuka nyuma, maana kama mtu huyu ana mwata yeye, angegundua uwa ameshaonekana, hivyo akajichanganya na watu wa pale njiapanda kisha akaingia kwenye duka moja la dawa, na kujifanya anaulizia dawa flani, huku akitazama yule aliekuwa anakuja kwakimbia ninani, na kweli baada ya mda mfupi akamwona mtu huyo na kumtambua kuwa ni Busungu, akiingia pale njia panda mbio mbio, nakuanza kutazama huku na huku, kama kunamtu anae mtafuta, hapo Jackline akatulia nakuendelea kumtazama Busungu huku akiendelea kuulizia dawa, alifanikiwa kumwona Busungu akianza kuulizia jambo kwa watu wawili watatu, baada ya kuka kwa dakika kadhaa mle dukani, na kumwona Busungu akikosa uelekeo Jackline akaamua kuondoka zake, akijitaidi asionekane kwa Busungu, ** baada ya kufika njia panda ya shule, insp na askari kumi waliokuja ndani ya defender, walikutana na pc Busungu, nakuambiwa kuwa Jakline ametoweka mbele ya mcho yake, wote wakabaki wameduwaa, “naona kuna dalili ya mafanikio, endelea kuchunguza” aliagiza Johnson nakuamrisha askari kuondoka zao, wakimwacha Busungu anaendelea na uchunguzi wa eneo lile, ** siku ile iliisha kiaina huku siku iliyofwata ilikuwa siku ya Jackline kufundishwa kuendesha gari, maeneo ya karibu na nyumbani kwao, kiukweli kwa Denis ilikuwa kazi ngumu sana, kumfundisha Jaackline kuendesha gari, maana alionekana kuwa mbumbu kabisa, katika zoezi hili la uendeshaji wa gari, yani toka saanne mapaka saa nane, Jackline akuweza kunyoosha tearing yagari, “yani mama France natamani nikuzabue ata vibao, yani utaazani unafanya makusudi” aliongea kwa ukari Denis, huku aki shuka kwenye gari na kuzunguka upande wa dereva na kufungua mlango, “shuka kapande kule” alionge Denis ambae licha ya kutumia mbinu zote za ufundishaji, lakini Jackline akuoonyesa dalili yoyote ya kuelewa kuendesha gari, “lakini baba France si nitaelewa taratibu?” aliongea Jackline kwa sauti ya uoga, mbele ya Denis, hapo Denis akapoa kidogo, “usijari mke wangu kilamala tukipata nafasi, nitakufundisha” wote wakacheka kidogo, “lakini baba France leo ulikasirika hen?” aliuliza Jackline kisha wote wakacheka tena, kabla Jackline aja ongea tena, “sasa tukapunguze hasira kwa mvinyo na …….” aliongea Jackline huku akizigusan asehemu zasiri za Denis, wakati huo walikuwa wanaingia nyumbani kwao, ambapo walikuta France akicheza na wenzake, wakichezea vigari na vibaiskeri, ** vyombo vyote vya habari vilikuwa vina zungumzia juu ya mahakama yatakayo fanyika kesho juu ya bwana Kaijage, ambae gari lake licha ya kukutwa na nyara nyingi za serikali, pia gari lake lilisababisiha vifo vingi sana, kwa uzembe wa dereva wa gari hilo, ambae mpaka sasa ina semekana kuwa dereva huyu amesha fariki dunia, maoni yawatu wengi walio hojiwa juu ya tkio hilo, walionekana kushauri hadhabu kari kwa mmiliki wa gari hilo, ** siku yapili ilikuwa jumatatu, siku ambayo iliannza kwa shamla shamla toka asubuhi, ukiachilia watu wengi kumiminika mahakama kuu, pia waandishi wa habari na vyombo vyao vya habari, walianza kujiandaa kuelekea mahali hapo, siku hiyo ilianza vibaya sana kwa Denis, maana baada ya kuwatayari amesha jiandaa kwenda kazini, alitoka na kuelekea kwenye gari lake, lakini kalipo jaribu kuliwasha gari alikuwaka, kila alipo jaribu kuliwasha ikashindikana, hapo akashuka na kumkabidhi mke wake funguo za gari, “vipi baba France, mbona unaacha gari?” aliuliza Jackline kwa mshangao, huku akipokea fungu za gari, “sijuwi gari lina matatizo gani, wacha niende kwa mguu, nitapata pikipiki njiani” aisema Denis huku akiondoka na kushika njia kuelekea barabarani, *** saa moja na robo za asubuhi busngu alikuwa ndio anaingia, kibamba ccm kwenye kijwe cha wakina Msafiri, japo story zilikuwa ni nyingi sana pale kijiweni, watu wakizungumzia juu ya mahakama itakayo endeshwa leo, na kila mmoja alkuwa na hamu ya kujuwa kitakacho tokea, “wewe ujuwi mambo ya polisi, mwenye fedha afungwi” aliongea Majani na Msafiri akadakia, “ila naamini kuwa huyu lazima afungwe, tena amekamatwa na ushaidi wawazi kabisa, atakwepaje,?” aliongea Msafiri, wakati huo Busungu alikuwa anakaa na kujiunga nawenzie, “wewe unakuwa mgeni na mahakama zetu bwana” aliongea Majani, wakati huo Busungu alikuwa analitazama gari ainia ya Toyota Noah, ambalo lilikuwa linatokea pale kwa mchoraji, akaona tazama ndani, akitumia dirisha la upande wadereva ambao yeye ndio alikuwa nao sambamba, akamwona dereva wa gari lile kuwa ni Jackline Michael Nyati, akiwa amejitnda nguo aina ya vitenge, nasasa alikuwa anapandisha vioo vya gari lile, hku gari hiilo likiingia barabara kuu na kushika uelekeo wa mjini, “nimekufuma mshenzi wewe” alioea Busungu na kuinuka hara sana kukimbilia sehemu zilipo egeshwa boda boda, “ingia barabara kuu elekea mjini?” alisema Busungu baada ya kukodi moja ya boda boda, bila kuzubaa yle boda boda akawasha pikipiki na kushika njia ya kuelekea mjini, wakati huo Busungu alikuwa anapiga simu kwa insp Johnson, na wakati huo hoo alikuwa anasoma namba zagari zilizo kuwa zina someka vizuri, kutokana na ung’aavu wa kibao cha namba za gari lile, itaendelea………

