
BINTI MDUNGUAJI (65)

SEHEMU YA SITINI NA TANO
ILIPOISHIA SEHEMU YA SITINI NNE : kisha ikafwatiwa kelele kutoka kwenye kundi la kina mzee Masinde na wenzake ambao walikuwa wana msadida bwana kaijage, insp akageuza shingo kumtazama baba yake, akamwona mzee Kaijage kichomoka mikononi mwa mzee Masinde, kama ambae alisukumwa na kitu kizito, na kutupwa pembeni, huku kichwa chake kikipasuliwa, na ubongo ulio changanyika na damu kutawanyika, ukiwarukia rafiki zake, na watu walio mzunguka, akiwepo mzee Masinde. endelea……..
“mungu wangu tayari” aliilopoka insp Johnson ambae bado alikuwa ameshikilia smu ambayo bado hipo hewani, ikiwa imepigwa na Polisi Consteble Busungu, insp aliwaona wakina mzee masinde na wenzake wakiangaika kutafuta sehemu ya usalama, ambayo ilikuwa ni ndani ya mahakama pekee, wakati huo wanchi nao walikuwa wakishangaa tukio walilolishuhudia, kwamacho yao, wakiona mzee Kijage akiwa amelala chini, huku kichwa chake kikiwa akieleweki, pua api sikio wapi macho yalikuwa yamesha hachia kichwa na kuzagaa kama gololi za kuchezea watoto, “vipi tena afande kuna usalama huko?” ilisikika sauti ya busungu ambae bado alikuwa ana endelea kupanda ngazi kwafujo, hapo insp akagutuka toka kwenye mawenge, na kukumbuka kuwa alikuwa naongea na simu, “Busungu, hupo nyumba moja na huyo shetani, na ameshatoa roho ya mtu mmoja” aliongea insp Johnson huku akionyesha ishara kwa askari polisi wachache, ambao walikuwa wame jificha ndani ya mahakama kuogopa risasi ya mdunguaji, akitaka wamfwate yeye ambae alianza kutembea kuelekea upande wa nyuma wa mahaka, upande ambao ni uelekeo wa jengo la wajasiliamali, ambalo inasemekana Jackline Nyati yupo huko, wale askari ambao walikuwa watano huku wenye silaha wakiwa ni wawili tu, awakushangaa walimfwata insp ambae alikuwa na bastora tu!, “insp unasema tayari amesha uwa?” ilisikika sauti ya pc Busungu akiuliza kwa mshangao mkubwa sana, “sikia busungu, mzee Kaijaje tayari yupo chini, unatakiwa uwe makini sana, si unamjuwa huyo mwanamke ni hatari sana?” aliongea insp Johnson, wakati akimaliza kutoka nje ya jengo la mahakama, nyuma yake askari watano wakimfwata, “mama yangu nimechelwa” sauti ya Pc Busungu ilipenya masikioni kwa insp Johnson, kupitia simu yake yamkononi, na kumfanya asisimkwe na nywele zake akiziona zina simama, kama zile waya za kuosafishia sufuria, “hallow busungu” kimya “busungu unanisikia busungu?” aliongea insp kwa sauti yajuu sana, lakini akujibiwa kitu zaidi akasikia ya busunu kama anaongea na mtu mwingine mbele yake, “leo Jack, naomba unieleze sababu ya kufanya mauwaji” insp aliisikia sauti ya Busungu, ambayo ilionyesha kuwa ni yaupole sana, insp akaendelea kuwa sikiliza, kwa umakini sana, huku akizidi kutimua mbio na wale askari wake kuelekea kwenye lile jengo ambali kwa njia waliyo itumia lazima wangetumia dakiika kumi adi kumi natano, maana kuna sehemu ambaz lazima zinge walazimu kuzunguka, sababu zilikuwa zimezibwa na uzio wa ukuta, huku insp akijuwa kuwa Bungu maisha yake yapo hatarini, japo alikuwa anatumia mbinu flani flani kumchelewesha Jackline iliwao wawai eneo la tukio, ** kama vile alikuwa amesaau uwezo wa mwili na hakili wa Jackline, busungu ambae baada ya kumpoteza Jackline, mbezi kwa yusuph, akaja kuliona gari la Jackline, nje ya jengo la wajasiliamari, kwa msaada waboda boda aliyekuwa wakwanza kuliona Toyota Noah lenye namba T182 C..P, hapo haraka sana busungu aka mpatia sshilingi elfu tatu boda boda, ambae alikuwa nauakika wa kupata zaidi ya elfu kumi, “lakini braza…..” alitaka kulalamka yule yule dereva wa pikipiki, lakini akashuhudia mteja wake akizi tupa elfu tatu chini “ kwani ujawai kutoa msaada wewe?” aliongea bsungu na kuondoka zake kuingia ndani ya jengo, pc Busungu akiwa anasilaha yoyote, alipandisha ngazi za gholofa hili akiwa anachomoa simu yake ili ajaribu kwa mala nyingine kumpigia insp Johnson, kwa bahati nzuri akapokea, nakuanza kumweleza juu ya uwepo wa Jackline ndani ya jengoo lile la wajasiliamari, nandipo alipoambiwa na insp kuwa tayari Kaijage amesha dunguliwa, muda wote Busungu aliongea na insp huku anaendelea kupanda ngazi mbio mbio, wakati aiingia kwenye safu ya nne na ya mwisho ya jengo ili, ambayo ikiwa tulivu ilyo kosa misongamano ya watu, huku bado akiendelea kuongea na insp Johnson, pc Busungu akastuka akikutana uso kwa uso na mschana mzuri sana mwenye umbo matata, lililoonekana vyema ndani ya gauni lililo shonwa kwa kanga, akiwa amebeba begi dogo jeusi begani kwake, licha ya kugundua kuwa yupo hatarini, lakini Busungu ambae alikuwa anafahamu kuwa insp yupo njiani, anakuja maali pale, tna alikuwa anafwatilia mazungumzo yao sababu, simu yake ilikuwa hewani, akaamua kumzuga Jackline, kwa maswali ili waweze kumtia nguvuni, ndipo alipo mwuliza swali, lile ambalo ata insp alilisikia, lakini Jackline akujibu chochote, zaidi alizidi kutembea kuelekea kule aliko simama Busungu, huku ameachoa tabasamu, kwamaana njia ndiko iliko, mpaka hapo busungu akajuwa kuwa kifo chake kime karibia, akaona bora apambane, hapo Pc Busungu akamsogelea Jackline kwa kasi sana, nakuruka juu akiachia ngumi kwanguvu zake zote, lakini akashangaa kuona mwanamke huyu akimkwepa kidogo sana, ungesema kuwa anapisha na mtu ambae alikuwa anapita njia, na busungu akapitiliza, na kwenda kutuwa nyuma ya Jackline, lakini ile Busungu ana tua chini, akastuka kumwona jackline, akimjia kwa kasi ya umeme, apo busugu ak rusha ngumi nyingime kiulenga uso wa Jackline, lakini ali sha ngaa wepesi wa dada huyu, maana alimwona akiyumba kidogo kisha kwa kasi ileile ya umeme, alizisikia ngumi nne kali zenye uzani mkubwa, zikitua kwenye mbavu zake, nakumfanya ahisi kama amepigwa na kitu kama nyundo au kipande cha nondo, simu yake ika dndoka pembeni, huku ikisikika sauti ua insp ikiita hallow! hallow! busungu“ Busungu akuwa na uwezo wa kuongea na simu yake, akajishika kwenye mbavu huku akitoa mguno wa maumivu, huku akiinama sura kaikunja kwa maumivu, macho ameyaelekeza kwa Jackline, akiitaji huruma ya Jackline, lakini ndiyo kama alikuwa anamchochea dada huyu, amtangulize kuzimu, maana alimsongelea pale alipo, na kumwongezea ngumi nzito ya kichwani, karibu na shingoni busngu akajibwaga chini huku akipiga ukelele wa maumivu, hapo Jacklne akakamata kichwa cha Busungu kwa mikono miwili na kukizungusha, na kufwatiwa na sauti ya kha! iliyo ashilia kuvunjika kwa shingo ya Busungu, ata alipo mwacha, Busungu alionekana kutulia pale chini bila uhai, hapo Jackline aka iendea simu ya busungu ambayo bado ilikuwa hewani, akaiwka sikioni huku anatembea kushuka chini, “insp kazi imeanza, najuwa unajuwakuwa bado mmoja nae ni baba yako, ukiendelea kujichanganya, na wewe utaongezeka na kuwa wasaba” alimaliza kuongea Jackline, akadakia Johnso kwa sauti ilio jaa jasira, “hallow we mwana…..” jackline akutaka kusikia Johnson anaongea nini, ndio kwanza akaitupa chini ile simu nakuzidi kushuka chini, ghorofa ya pili na jengo lachini watu walikuwa wengi sana lakini walikuwa wana tazama television kuangalia tukio la mauwaji lililo kuwa lina rushwa live toka mahakama kuu sekunde chache alikuwa amesha fika chini kabisa, lakini akamwaona insp Johnson akiingia pale mjengoni kwafujo , na kuagiza milango yakutokea ifungwe, na akuna mtu kutoka hakuna mtu kuingia huku akiacha polisi wawili wasimame kwenye ule mlango, Jackline ambae alitumia nguo yakemoja, (kanga) kujiziba nusu ya uso wake, alimwona insp Johnson akiwaacha polisi wawili pale mlangoni, mmoja akiwa na silaha aina ya smg, na mwingine akuwa na silaha, kisha insp na askari watatu wakaendelea kupandishangazi kuelekea juu, kule ambako insp aliona ishara ya kutokea risasi, huku akisikika akiongea na simu akiomba askari zaidi kutoka kituo kikuu, huku wananchi wakishikwa na taaruki, na kuanza malalamiko ya kila aina, hapo Jackline aka tazama kusho na kulia akabahatika kuona kibao kinacho elekeza vyoo vilipo, akaelekea upande huo, kisha aingia ndani ya choo kimoja wapo na kutazama kwenye dirisha, dogo lililopo juu sana, lilikuwa ni dirisha dogo la vioo lisilo na nondo, Jacklile akatabasamu, kisha aka pandisha gauni lake na kutoa kamba kwenye kapturah yake yajinsi, akaikunjuwa na kuiweka vizuri tayari kwa kazi aliyokusudia, ilikuwa ni kamba ndefu kiasi, ** wakina Denis, bado walikuwa wanatazama television ambayo ilionyesha tukio wananchi walio kuwa wanafuria kifo cha bwana Kijage alie jaribu kugeuza sheria, na kuzarau vifo vya abiria wengi walio fariki kwenye hajari, japo mtu kubwa wa serekalini aliepewa zamana ya upelelezi, ame isariti serikali iliyo mpandisha vyeo na kumpa zamana kubwa sana, ikimlipa mshahara mkubwa na malupu lupu kibao ikiwemo usafiri na nyumba nzuri ya kuishi, alisahau yote na ku geuza ushahidi, “hiyo ndyo zawadi ya mjanja” alisema Janeth, na kuungwa kono na wenzake, ** tukio hilo pia lilionyeshwa katika television nachi nzima, na mmoj wa watu waliokuwa wakitazama tukio hilo alikuwa ni mzee Michael Nyati, ambvae alikuwa ametulia sebuleni kwake mbele ya TV yake kubwa, akifwatilia tukio hilo, huku mda wote tabasamu likonekana kuchanua usoni mwake, ** nje ya jengo la wajasiliamari, watu walikuwa wamejaa wakishangaa uvamizi wa jeshi la polisi kwenye jengo lile, tayri waaandishi wa habari walikuwa wamesha fika kwenye eneo lile na kuanza kurusha matangazo, na wakati huo vilisikika ving’ola vya magari ya polisi vikija mbio eneo lile, na wakati huo lilionekana gari moja aina ya Toyota Noah likiondoka, na kupishana na magari matano yapolisi, yaliyo kuja na askari wengi sana, wenye silaha, ** “naona mambo yamekuwa mazito sasa” aliongea boss wao wakina Denis baada ya kuona taalifa imeamia kwenye jengo ambalo inasadikiwa kuna muuwaji, tena ni wakike, wakati huo kamera za wanahabari zilikuwa zinaonyesha magari ya polisi yaliyo kuwa yanaingia kwenye eneo la tukio, “Denis kumbe wewe ni muongo hen! si umesema gari lako bovu, sasa kile nini?” aliuliza Mahadhi huku akisongea kwenye TV nakuonyesha gari aina ya Toyota Noah lililo kuwa linapisha na na magari ya polisi, yaliyo kuwa yanaingia eneo la tukio, hapo wote mle ndani waka toa macho kulitazama lile gari, “kweli bwana” alisema Boss wa Denis huku wakilikazia macho gari lile, ambalo lilionekana wazi kuwa ni gari la Denis, asa kutokana na stiker moja kwenye kioo cha nyuma iliyo tangaza pombe flani, iliyotengenezwa na kiwanda kimoja cha humu nchini, itendelea……..

