
SEHEMU YA SITINI NA TISA
ILIPOISHIA SEHEMU YA SITINI NA NANE : mala akaonekana mschana mmoja mrembo sana akishuka toka kwenye lile gari, akiwa amemshika mkono mtoto anea jitembeza mwenyewe, na kuingia kwenye ile bar, macho ya wote yalielekea kwa mrembo huyo, yakiwemo macho ya mzee Masinde, “yes, leo nitafaidi” aliwaza mzee Masinde, ambae alikuwa amebakiza siku moja tu! kupeleka moyo wa binadamu aliemuuwa kwamkono wake, ENDELEA ……..
Baada ya kugunduwa kuwa gari lake lime pata pancha, Denis aliegesha gari hilo karibu na bar moja, kubwa hapa kinyelezi mwisho, ambayo ilikuwa imechangamka sana, wakajadiliana na mke wake kuwa watulie mahali hapo, wakati wanafanya utaratibu wakupata mafundi wa uziba pancha, kisha waendelee na safari yao, ndipo Jackline na France wakaingia ndani ya bar hiyo, na Denis akaanza kutafuta sehmu walipo mafundi wa pancha, ** huku ndani ya bar Jackline ambae aliyavuta macho ya wanaume wengi sana mle ndani, alijiwa na mhudumu akaagiza soda mbili, moja ikiwa ni ya kwake na nyingine yam wane France, aikuchukuwa muda mrefu soda zikaletwa, Jackline na mwanae ambae sasa alikuwa na umri wa mwaka mmoja na miezi sita, wakaanza kunywa soda zao, “samaha ni dada, habari za leo” ilisikia sauti ya kiume pembeni ya Jackline, ambae kabla ya kujibu salamu hiyo, aliinua uso wake na kumtazama msalimiaji, alikuwa ni kijana mmoja aliejengeka kimisuri, na kuvalia nguo nyeusi, suluali ya jinsi na tishet, akimalizia viatu vyeusi na miwani nyeusi, “safi” aliitikia Jackline kwa kifupi, akiwa bao anamtazama yule kijana, ni kama alikuwa anamwambia sema shida yako, “samahani mrembo kuna mtu anaitaji ukaribie kwenye meza yake” alisema yule kijana kwa sauti yachini na yakunong’ona, akibonyea kidogo karibu nasikio la Jackline, hapo Jackline akaachia kicheko cha mguno, “naonekana kama kahaba?” aliuliza Jackline huku akiachia tabasamu ambalo Denis mume wake, akuwai kuliona ata sikumoja, nitabasamu ambalo watu wachache waeliona na kubakia wazima, “hapana dada yangu, ni boss wangu amevuti wa na wewe, ila kwa faidi yako, ni kwamba anafedha nyingi sana, atamaliza matatizo yako japo siyo mtu maalufu” aliongea yule kijana alie tumwa na mzee Masinde, akiagizwa kuwa lazima aakikishe anaenda na yule mwanamke, kwenye meza ya mzee Masinde, hapo Jackline alitulia kidogo akijitaidi kujizuwia hasira zake, maana akupenda kuchukuliwa kama mwanamke wa ovyo, “sidhani kama hupo sahii kaka yangu, sababu siyo matatizo yote yana malizwa kwa njia hiyo” aliongea Jackline, kwa sauti ya upole, akijitaidi kuzuwia hasira zake, “sikia dada japo ungeenda kumsikiliza pengine ungemwelewa mtu mwenyewe yupo fresh tu, anaga tatizo na mtu, si unamwona” aliongea yule kijana huku akitazma upande aliokaa mzee Masinde, Jackline nae akatazama, upande ule, macho yake yakakutana na machoya mzee Masinde ambae aliachia tabasamu na kupunga mkono, ghafla kengere ya tahadhri ikagonga kichwani kwa Jackline Nyati, ambae aliinua mkono kumpungia mzee Masinde, huku akijaribu kuvuta picha alimwona wapi, “anaitwa mzee nani?, pengine nilisha wai kumwona” aliuliza Jackline, anaitwa mzee Masinde anakaa hapo chini tu, ng’ambo ya barabara” alijibu kijana mlinzi wa mzee Masinde, Jackline akatabasamu, yule mlinzi akajuwa kuwa, Jackline amesha ingia mazima, kwa mzee Masinde, “unaweza kusogea kwenda kumsalimia” alisema yule kijana, na hapo Jackline akatazama nje ya ukumbi ule wa bar, sehemu lilipo kuwepo gari lao, akamwona Denis akiwa na mafundi wana fungua tayre la gari, lililo pata pancha, “ok! nakuja” alisema Jacklinekisha yule jamaa akaondoka zake kurudi alipokuwa mzee Masinde, mala moja Jackline akatoa simu yake na kuandika ujumbe kwa baba yake, ‘nahisi nimekutana na mzee Masinde’ baada ya kuituma akasubiri jibu, wakati huo akamwona Denis na mafundi wawili wa pancha wakimalizia kupandisha jerck na kuanza kufungua tayre, mala ukaingia ujumbe kwenye simu ya Jackline, akaufungua na kuusoma, ‘kama unauakika maliza kazi’ ilikuwa inatoka kwa baba yake, Jackline aka iweka simu yake kwenye mfuko wa suluali yake iliyo mkaa vyema kabisa, kisha akaiuka, “France nisubir nakuja” alisema Jackline, akimchezea mashavu France aliekuwa ametulia akigugumia soda, Jackline akaelekea kwenyemeza ya mzee Masinde “hoooo! karibu mrembo, karibu sana” alisema mzee Masinde huku anasimama na kumpamkono Jackline alie kuwa anatabasamu muda wote, na kufanya mzee Masinde azidi kuchanga nyikiwa, “naitwa David Masinde sijuwi mrembo unaitwa nani?” alijitmbulisha mzee Masinde kwa mbwe mbwe za hali ya juu, sana maa baada ya Jackline kukaa kwenye kiti alicho andaliwa, “niite mama Jack, inatosha” aliongea Jackline kwa sauti ya uturivu akijifanya kama anakaaibu flani kakike, “ok! Jack, agiza kinywaji, na chochote utachokiona kita kufurahisha, tuendelee na maongezi” alisema mzee Masinde, kwa sauti iliyo changamshwa na kinywaji, “samahani mzee wangu, leo nimekuja na mume wangu, kama huto jali tupange kesho muda wowote tukutane” alisema Jackline kwa sauti tulivu ya kubembeleza ambayo ilimwingia vyema mzee huyu, “kesho jioni nitakuwa na kazi muhimu sana, ila akuna ubaya, chukuwa hii namba yasimu, kesho tukutane kwenye hotel moja hivi, inaitwa paradise tower, ubungo river side” alisema mzee Masinde huku ana mkabidhi Jackline kijikaratasi kilicho andikwa kwa mashine (au computer) David Johnso Masinde, ikifwatiwa na anuani, na namba za simu, “ok! asante nitakutafuta, hiyo kesho mchana” aliongea Jackline huku anainukanakuweka kile kicard mfukoni, “usipuuze mrembo, nita yabadirisha maisha yako, jitaidi uwai mchana, maana jioni nitakuwa na kikao, na wafanya biashara wenzangu” alisisitiza mzee Masinde, huku akimtazama Jackline usoni, ambae alikuwa anatabasamu, “siwezi kukosa, maana nisiku muhimu sana kwangu, naimani ata kwako pia, itabadiri historia yako” maneno ya Jackline yali usisimua mwili wa mzee huyu, ambae alitamani iwe leo, maana alijuwa kuwa kitu anacho enda kuptakesho siyo kama anacho kipataga kwa wanawake wengine, hapo aliduwaa akimtazama Jackline akirudi kwenye meza yake, “ok, Ngwenje mpigie Ngwema muulize waakikishe kuwa wana kamilisha zoezi mapema maana ule mzigo unaitajika kesho usiku” aliongea mzee Masinde, ambae slisha watuma bahadhi ya vijana wake, wa tafute mwanamke ane jiuza, au kijana mtumiaji wa madawa ya kulevya (teja) kwa ajili ya kuchukuwa moyo wake, nakuupeleka kwa mganga, ambaapo zoezi hilo walipanga wakalifanyie hapo Paradise Tower, ambapo wange, angeingia huyo mtu anae takiwa kuuwawa, na kisha wamuuwe humo ndni baada kumkoleza kilevi, na mwisho wake, waondoke usiku kuelekea kongowe, wakiwa na moyo, hapo Kijana Ngwenye akachukuwa simu yake na kupiga kule aliko agizwa na mzee Masinde, ambae sasa alikuwa anatazama huku na huku, kukaguwa wahudumu wa kike na wanawake waliomo mle ndani, kama ange mwona atakae mfaha sikuile, alipo tazama meza ya Jackline, alimwona akiwa amekaa na mwaume mmoja ambae sura yake ilifanana na yule mtoto alekuwa na Jack toka mwanzo, “shauri zako kijana, utaibiwa na ukiwa kikwazo uta uwawa pia” aliwaaza mzee Masinde akimtazama yule kijana, ambae alihisi kuwa atakuwa ndie mume wa yule dada mrembo, “mzee mambo yanaenda vizuri, mpaka sasa wanauakika wa kumpata mwanamke, ambae wae weka miadi ya kukutana kesho jioni” alisema Ngwenje, kwa sauti ya chini, huku akiweka simu yake mfukoni, hapo nzee Masinde akatabasamu, na kutazama upande wa counter, “unamwona yule binti, anae chuwa vinywaji” mzee Masinde akamwuliza Ngwenje, “yule mweusi?” aliuliza Ngwenje huku ana tazama kule counter, “huyo huyo, nenda akaongee nae kisha lipa kwa manage, alafu mchague wakwenu tubadilishe kijiwe” alisema mzee Masinde, na Ngwenje akainuka malamoja, akiwaacha mzee Masinde na mlinzi mmoja, ** “malizeni tusepe, au tuna malizia hapa hapa” aliuliza Denis ambae akuwa na kinywaji chochote mkononi, “hapa siyo pazuri, bola twende karibu na nyumbani, ila tupitie ubungo, uwe unanielekeza mitaa” alishauri Jackline, huku wakiinuka, Jackline akiachia soda yake robo ya chupa, kwa upande wa France akuwa na uwezo wa kuimaliza soda ile, akaiacha nusu kabisa, wakaingia kwenye gari hukuwakisindikizwa na macho ya wadau wa misambwanda, kisha hao wakaondoka zao kuifwata barabara iendayo segerea, ** polisi waliopo ndani ya bar ile ambao walikuwepo pale kwa lengo la kufwatilia nyeneno zote za mzee Masinde, wakitazama mtu yoyote atakae onekana akifwatilia mzee huyu, na huo ulikuwa ni mpango wa jeshi la polisi unao simamiwa na insp Johnson, kwa leno la kukamata muuwaji, ambae walikuwa na uakika kuwa lazima muuwaji ataitaji kuchomoa roho ya mzee Masinde, polisi walishuhudia kila atuwa ya tukio la mzee Masinde kumwita Jackline na kuongea nae kwa muda mfupi, kisha wakaonekana kama wakipeana ahadi na kuachana, polisi wale awakumtilia mashaka Jackline, zaidi wali sifia ujinga, “huyu mzee anakula raha sana, ebu kama yule demu alie mwita mida ile, ni mkali kinyama” alisema polisi mmoja kati ya wawili, waliokuwa kwenye meza moja mle ndani ya bar,meza ya tatu toka kwenye meza ya mzee Masinde, “mh! mwanangu ni noma sana, yani demu yupo na mume wake hapahapa, anatongozwa na kukubari” aliongea yule polisi wapili, na wote wakacheka kidogo, “lakini yule demu ni mkali kinoma” liongea polisi wa kwanza, wakati huo polizi wote waliokuwepo eneo lile waliendelea kumtazma mzee Masinde, ambae nusu saa baadae alionekana akiondoka yeye na walinzi wake na kila mmoja wao akiwa na mwanamke, polisi nao wakaliunga, kumfwata mzee Masinde ambae aliamia bara nyingine, iliyopo mtaa wapili, ** insp Johnson jumamoss hii alikuwa nyumbani kwake pamoja na familia yake, ilishapita mezi mitatu toka tukio la kuuwawa kwa mzee Kajange na Pc Busungu, litokee, ni kama hali ilikuwa imetulia hivi, maana ata raia na vyombo vya habari, sasa awakuongelea sana matukio yanayo fanywa na muuwaji, anaesemekana kuwa ni mwanamke, hivyo insp Kajikuta akiondokewa na wasi wasi akiamini kuwa, polisi kumi wanao mfwatilia baba yake, ni ulinzi tosha kabisa kwa baba yake, japo muda wote alijitaidi kuwasiliana na wale polisi, asa mida ya jioni, ambapo wale polisi, walikuwa wanamjulisha kila kinacho endelea, kuhusu mzee Masinde, ** huku nako Denis alipita bara bara ya tabata segerea, akitokea barabara ya mandera, nakuelekea ubungo, njia nzima Denis alikuwa akimwelekeza mke wake, mitaa na majina ya sehemu walizopita, ata walipofika maeneo ya river side, Denis aliendelea kumwelekeza mke wake maeneo, “ukisikia river side ndiyo hapa, ni umbali mdogo toka makutano ya barabara ya mandera na morogoro, (ubungo mataa)” alieleza Denis na huku mke wake akiwa ana pepesa macho kutazama pande zote za barabara, kama vile alikuwa na shahuku kubwa ya kuifahamu vizuri sehemu hii, “hapa kama napakumbuka hivi” aliongea Jackline, akiendelea kupepesa macho, “au ulisha waikuingia pale Paradise Tower, aliongea Denis kwa utani, huku anaonyeesha upande wa kushoto wa barabara, wote wakacheka, “labda tulikuja wote” alisema Jackline huku ana tazama upande ule, alionyesha Denis, akaliona jengo refu lenye gholofa nane, lililo andikwa Paradise Tower, hapo Jackline akatazma upande wa pili, akaona jengo jingine kama lile lililo andikwa #MBOGO PLAZA, Hivi lile kula nalo lina bar, aliulliza Jackline huku akilitazama jengo la #MBOGO PLAZA, ambalo sasa walikuwa wameshanza kuliacha, “he! yani mtaa huu umejaa mabar na maguest, aliongea Denis na wote wakaachia kichekeo, huku wana zidi kuyoyoma kuelekea ubungo mataa, “baba France mi naona tuka dudue wine tukanywe nyumbani” alishauri Jackline na Denis akaunga mkono, itaendelea ………..
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU