BINTI MDUNGUAJI (71)

SEHEMU YA SABINI NA MOJA

 

ILIPOISHIA SEHEMU YA SABINI: kimara na mwenge, huku kawe wakiwa wana sikika kwambali kidogo, wakakunja kushoto na kutililikia river side, kwambali wakaanza kuona, jengo la Paradise Tower, huku wakionekana polisi wa kituo cha buguruni wakiizunguka hotel hiyo, “leo huchomoki” alisema insp Johnson, ambae alionekana kuwa na hasira zilizo changanyika na wasi wasi wa kumpoteza baba yake, endelea ………
Huku nako mzee Masinde, akaanza kujipapatua, toka kwenye kiminyo cha mwanamke mrembo, ambae sasa alimwona kama Israel mtoa roho, akiamni kuwa angeweza kujiokoa, lakini wapi, ndio kwanza akaona mwanamke huyu, akikaza mkono na kumminya zaidi, mala akahisi kitu kikali sana, misiri ya wembe, kikipita kwenye dudu yake, na kuzi pangusa, kisha zikadondoka chini kama za bandia, hapo mzee Masinde alijisikia maumivu makali sana, kwenye eneo hili la dudu, ikimkubusha miaka mingisana iliyopita, akiwa na miaka kumi na mbili, alipo tahiliwa kimila, huko musoma, tena bila ganzi, maumivu yaliuwa makali sana, mzee Masinde alitamani kupiga kelele, lakini akashindwa kutoka na mkono mgumu wa mwanamke huyu, ulio mziba mdomo wake, na kusababisha ajikute akijaza hewa domoni kwake, hapo mzee huyu akaona mwili wake unakosa nguvu, na kuanza kuregea, wakati huo kwamacho yake, yaliyo anza kulegea, na kuona giza, akamwona yule mwanamke mrembo alie mziba mdomo, anainuwa kisu na kukishusha ubavu wake, kikazama mpaka kwenye mpini, na kukichomoa, na kumsababishia maumivu makali, maana kilivyo kuwa kina toka, yale meno ya msumeno, yaliyopo nyuma ya kisu hicho, yalimsababishia maumivu makali sana, akakichomeka tena, na tena, hapo mzee Masinde akaona giza likitanda machoni mwake, na kushindwa kuelewa kinachoendelea ulimwenguni, “Jackline akiwa ame mshikilia mzee Masinde, alie kuwa amesha kata moto, akamlaza chini, kisha akajitizama, alikuwa amelowa damu, karibu gauni lake lote japo lilikuwa jekundu, lakini ungetambua kuwa limelowa damu, pamoja na viatu vyake vyeupe vye visigono virefu, hapo Jackline akaenda mlangoni, na kuufunga kwa funguo, kisha akaingia bafuni, ambako alijiweka safi na kutoka, kisha akaanza kuvaa nguo zake nyingine ikiwa ni suruali nyeusi, yenye mifuko ya pembeni kama zile za kijeshi, na tisherti nyeusi, pamoja na viatu vyenyeshingio ndefu, vyeusi vyakijeshi, awakati ana jiweka tayari kutoka, mala akasikia sauti ya ving’ora vya magari ya polisi, nje ya hotel hile, “hoya mnasikia hiyo, wanakuja hapa au..?” Jackline akasikia sauti ya wale vijana, walipo sebuleni, waki ulizana, “hooo wakubwa msala, polisi wametanda huko nje kinoma ebu mstueni mzee” ilisikika sauti ya ijana mmoja, na wakati huo huo, mlango wa chumba alichpo yeye Jackline ukagongwa, Jackline aka sogelea dirisha na kuchungulia nje, Jackline aliweza kuona chini kabisa ya jengo hilo, polisi wengi wakiwa wanalizunguka jango hilo, wakiwa na silaha za kivita, na vazi ya kuzuwea risasi, “mzee mzee kuna msala huku, chungulia dirishani” ilisikika sauti toka ebuleni, Jackline akuijari, zaidi alichukuwa bastolah yake na kutoa kimkebe cha risasi, akaitaza kuakkikisha kama ina risasi za kutosha, kisha akaipakia kwenye bastora yake, alafu akaikoki, na kuichomeka kiunoni, akachukuwa begi lake na kuitoa ile kamba aka jiligishia kiunoni mwake, akaufwata mlango wakuendea sebuleni, akaufungua kwa funguo kisha aaufungua mlango wenyewe, wale vijana wakiwa wame changanyikiwa na polisi, waka tazama mlango wa chumbani uliokuwa unafunguliwa, mala ghafla wakamwona mscha alie valia tofauti na wakati anaingia huku ndani ya chumba wakimwona mzee Masinde boss wao akiwa amelala sakafuni, katikati ya dimbwi la damu, hapo wakajuwa kuwa, yule mwanamke walie kuwa wanamsikia ndie alikuwa mbele yao, hivyo wakaanza kujihami, kwa kutafuta silaha zao, lakini aawakuwai, maana walimwona mscha yule ambae umbo la mwili wake usingeweza kuamini kitendo alicho kifanya, sababu haraka sana yule dada ali biringika sarakasi, na kuchomoa kisu kikubwa kama panga chini ya meza kisha kama alikuwa ana kata mauwa, alia wacharanga mapanga ya shingo, na vijana hao kuanguka chini, kama mizigo, huku shingo zao zikivuja damu, wamesha poteza maisha, hapo Jackline akamtazama yule mwanamke alie lala sakafuni ajitambui, kisha aka ufwata lango wa kutokea mle ndani ya chumba, huku akilitupa lile panga, juu ya kochi, kisha aka sita kidogo, Jackline akachungulia kwenye tundu la funguo la mlango ule wakutokea nje, ** insp Johnson ndio kwanza alikuwa anaingia eneo ambalo aliambiwa kuwa baba yake yupo na mwanamke ambae anaamini kuwa ndie Jackline Nyati, ile kushuka tu akaelekea moja kwa moja mapokezi, akamtaalifu manage, kuwa ile hotel imezungukwa na polisi, sababu kuna mtu hatari sana ndani ya hotel hile, chumba namba 40, gholofa ya sita, pia Johnson akaomba simu inayotumika mle ndani ya hoteli kwa mawasiliano ya mapokezi na vyumani, “piga chumba namba 40, alisema kwa sauti yenye shahuku insp huku akiamrisha bahadhi ya askari wapandishe juu, nao wakafanya hivyo, wengine wakitumia ngazi na wengine wakitumia lift, huku silaha zao zikiwa mikononi tayari kwa mapigano, ukiachilia waliobeba smg, wapo waluo beba silaha ndogo kama uzi gun, ambayo ninzuri zaidi kwa mapigano ya mjini, simu iliita kwa muda mrefu pasipo kupokelewa, “mungu wangu sijuwi kama kuna usalama” alipayuka Johnson akanza kukimbia kuzifwata ngazi, katika siu ambayo Johnson aljiona kuwa ni mwepesi na mwenye mbio, ni hiyo, sababu alitumia dakika mbili tu kupanda ngazi hizo, na kufikia ghorofa ya sita, ambapo alikuta askari wake wakiwa wame simama upande wa ndani wa kolido, la gorofa hilo, ambalo baada ya vyumba viwili kulikuwa ndio mwisho wa korido hilo, zaidi ni kioo kibwa sana, kilicho tumika kama dirisha, ambako akukuwa na sehemu ya kuendelea, huku silaha zao wame zielekeza kwenye mlango wa chumba namba 40, wakiwa kimya kabisa, hapo insp Johnso akaonyesha ishara, kwamba askari mmoja akagonge mlango, wa chumba kile, hapo wote wakatulia na kumtazama askari mmoja aliekuwa amevalia nguo za kiraia, na bstora yake mkononi huku amevalia vazi la kuzuwia risasi, ni mmoja kati ya wale askari ukumi waliokuwa na Koplo Mashiba, huyu anaitwa Pc Ngaga, akiufwata ule mlango wa tahadhari na kujaribu kunyonga kitasa cha ule mlango, na kitu cha kushangaza mlango ukafunguka mala mja tena kwanguvu hapo askari wote zaidi ya ishilini walio kuwepo upande wa ndani wa korido, wali mwona Ngaga, akishikwa ghafla na kwa haraka sana, na mtu toka ndani ya chumba hicho, huku akipokonywa bastora aliyo kuwa ameishika mikononi mwake, kisha akawekewa kichwani mwake, “msipige risasi msipige risasi” alipayuka koplo Mashiba, huku akiyoosha mkono mmoja juu, ishara ya kusuburi, hapo maho ya insp Jinson na Jackline yakakutana, “Jackline Nyati amini mwisho wako umefikia, kuna zaidi ya askari miambili nje ya hotel, uwezi kuchomoka hapa, mwachie huyo askari kisha jisalimishe” alisema Johnson kwa sauti ya kejeli, huku akiachia tabasamu la kejeri pia, lakini Jackline akuonyesha wasi wasi wowote, ndio kwanza akiwa ame mkaba na kuweka Ngaga mbele yake, na bastora ya kipolisi M12, akiwa bado amemwekea kichwani, akaanza kumkokota taratibu, kuelekea upande wa ukingo wa kioo, ambao ndio mwisho wa korido, insp akacheka kwa dharau, “una ujanja wowote Jackline, weka silaha chini usubiri kunyongwa” maneno hayo yaliwafanya atawale askari wengine wacheke kwa dharau, huku wakiwa nado wameelekeza silaha kwa Jacline alie kuwa ame mkamata kwanguvu, Pc Ngaga, na sasa Jackline alikuwa amesha kisogelea kioo kikubwa, wakamwona akitazama nje, kupitia kile kioo, wakajuwa kuwa mwanamke huyu ameishiwa ujanja, wakacheka tena, wakieendelea kumtazama, wakitegemea kumwona mwanamke huyu, akimwachia Ngaga, na kusalimu amri, lakini wakamwona Jackline akiwa tazama na kitu kilicho washangaza, ni kumwona akitabasamu, na mbaya zaidi tabasamu hilo, walishindwa kulitambua, kuwa anawasanifu, amefurahi, au amekasirika, “hoo! Johnson nazani umesahau, kuwa mimi ni mtu wa aina gani, maana unawaza kunikamata kilahisi sana” maneno ya Jackline yaliwashangaza wale askari ambao waligeuka na kumtazama insp Johnson, nikama wana mwuliza, “anakufahamu?” ililo lilkuwa kosa kubwa sana kwa askari hao, maana walisikia milipuko mitatu mfululizo ya risasi, huku kioo kikimwagika, ile wana geuka kumtazama Jackline aliekuwa ameshika Ngaga waliona ndio kwanza wana malizikia kutoka nje ya jengo hilo, wote waka kimbilia dirishani kwenye kioo kilicho pasuka, na kuchungulia, wakamwona Jackline akielekea chini kwa kasi ya hajabu huku ame mtanguliza Ngaga, wakielekea kutuwa uswa wa maegesho ya magari, na wakti huo huo polisi walio kuwa chini wakaona tukio lile hivyo kwanza kumimina risasi kumrenga Jackline alie kuwa ana shuka kwa speed, na kusababisha risasi nyingi kumpata Ngaga aliekuwa ametangulizwa, huu nyingine zikipitiliza na kuwa kosa kosa wakina Johnson, ambao wali rudi ndani, ambako sekunde chache wakasikia kishindo kikubwa sana chini, ikionyesha kuwa walituwa juu yagari, wakaende tena kuchungulia, wakamwona Jackline akijiinua toka juu ya gari lililo bondeka bondeka, akimwacha Ngaga juu ya gari hilo akiwa ametulia na vijito vya damu vikichuru zika toka kwa askari huyo, alie kuwa anaonekana wazi kuwa amesha poteza maisha, insp kwa macho yake akamwona Jackline akijificha ubavuni mwa gari lile, walilo lidondokea, huku askali watatu, wakilisogelea lile gari, na SMG zao mikononi, pia askari wengine walikuwa wanakimbia kutoka upande wa mbele wa hotel na kuzunguka huku nyuma, lakini ghafla insp Johnson akamwona Jackline akiinuka, nakuanza kumimina risasi kwa wale askari watatu, ambapo mwanzo insp alijuwa itakuwa kazi bule kwa risi zile, maana zisingepenya kwenye bullet proof, lakini alishangaa kuona Jackline akiwa tandika wale askari risasi za vichwa, na wakadondoak chini, hapo akaonekana Jackline akiokota SMG moja na mikebe mingine miwili, ya risasi, kisha akaanza kuwashambulia askari waliokuwa wana kuja mbio upande ule, hapo Insp akashuhudia askari zaidi ya sita wakidondoka mbele ya macho yake, na mbaya zaidi, akamwona Jackline akili fwata gari moja la polisi, akimiminia risasi dereva ambae mda wote alikuwa amejificha kwenye gari, akiogopa mtiti wa Jack Nyati, na kwa akaida kwenye matukio kama hayo magari ya polisi uwa hayazimwi, kwa hoyo insp akamwona Jackline akiondoka na gari hilo, aina ya one ten defender, na polisi nao wakitumia dakika kadhaa kupanda kwenye magari, na kuanza kumfukuza yeye akaagiza akari wengine wakague kile chumba alafu wa mjulishe kilicho tokea, yeye akatoka hapo na kushuka chini, akijuwa kabisa kuwa baba yake akuwa hai, “ingia kwenye gari tuwai, tumebaki peke yetu” aliongea kwa ukari sana insp, ambae aliingia kwenye gari, na kuchukuwa kisemeo cha redio call ya kwenye gari lile la polisi, “hallow station zote, target imetoka hapa ubungo inaelekea buguruni, “kama kuna plisi wazibe barabara zote, narudia kama kunapolisi wanao nisikia upande huo wazibe barabara” aliongea insp huku safari ikianza, gari alilo panda likiondoewa kwaspeed kari sana, pale paradise tower, na kushika uelekeo wa buguruni, huku mala kwa mala akitoa maelekezo ya sehemu ambazo porisi wana takiwa kukaa ili kukamata huyu mwanamke, *** wakati huo mzee Nyati alikuwa sebuleni kwake ndipo alipo sikia habari ya hivi punde, ikionyesha tukio lililo tokea paradise tower, ya muuwaji wakike kukimbia polisi, “mh! mambo magumu” alisema mzee Nyati kwa kunong’ona, kisha akasema “mama Jack, jiandae na safari ya dar es salaam, leo hii” itaendelea…..

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!