
SEHEMU YA SABINI NA MBILI
ILIPOISHIA SEHEMU YA SABINI NA MOJA : wakati huo mzee Nyati alikuwa sebuleni kwake ndipo alipo sikia habari ya hivi punde, ikionyesha tukio lililo tokea paradise tower, ya muuwaji wakike kukimbia polisi, “mh! mambo magumu” alisema mzee Nyati kwa kunong’ona, kisha akasema “mama Jack, jiandae na safari ya dar es salaam, leo hii” endelea…….
Kuli hiyo ya baba Jack, ilimstua sana mama Jack, ambae ambae alikuwa ndani kipindi hicho, “kuna nini baba Jack, au Jack amepatwa na tatizo?” aliuliza mama huyu, huku akiingia pale sebuleni, akitokea jikoni, akamwona mue wake akiwa ameelekeza macho kwenye Tv, huku pad yake ikiwa mezani, “Jack huyo?” aliuliza mke wa bwana Nyati, na yeye akitazama TV, ambayo ilionyesha tuko lililo malizika pale hotelini, na mtangazaji akielezea juwa muuwaji amefanikiwa kukimbia na gari la polisi, japo polisi walikuwa wana mkimbiza kwa magari yao, “masikini mwanangu, safari hii atafanikiwa kuwakimbia kweli?” aliuliza mama Jackline, hukusauti yake ikiingiwa na wasiwasi, mzee Nyati akujibu kitu zaidi alitazama pad na kuona kuwa ile tracking ya Jackline ikielekea tambaa na mandera load, ikielekea upande wa buguruni, hapo akachukuwa simu yake Haraka sana kumpigia Jackline, akionyesha kustuka juu ya jambo flani, “sijuwi kama atapokea..” aliwaza mzee Nyati na wakati huo huo, simu ikapokelewa, “ndio baba” ilisikika sauti ya Jackline sambamba na sauti za magari zilizo zidiwa na ving’ora vya polisi, “sikia Jackline, fwata maelekezo yangu, kama unaendelea kutumia gari basi fwata barabara mliyopita jana, ile ya kinyerezi, ukinyoosha tu umekamtwa,” alieleza mzee Nyati, ** insp Johnson akiwa nyuma kabisa yam bio hizi za magari yapolisi, huku magari ya kiraia yakiwa yame kaa pembeni, pasipo kujuwa lile lambele kabisa ni la mwalifu, insp aliyaona magari ya polisi mita mia mbili mbele yake, huku barabara ikiwa nyeupe magari yapo pembeni, insp huku anaendelea kuwasiliana na makao makuu aliomba askari zaidi, na mbwa maalumu wa polisi, wanao tumika kufwatilia waalifu, wawa fat kule watakapokuwa wanaelekea, wakati huo huo insp kwambali akashuhudia gari la polisi lililo kuwa mbele kabisa na kuyahacha mengine kwa mita kama mia tatu, likichepuka kwa ghafla njia ya tabata, pasipo kusubiri taa zimruhusu, na kusabisha magari yaliyo kuwa yanatokea buguruni, ya pate misukko suko ya kuchuna black za ghfla na yale ya nyuma yaki yagonga yambele, hapo magari ya polisi yakaonekana yaki jipenyeza na kupita sehemu ile, kisha yakaendelea kulifuuza gari analoliendesha Jackline ambalo lilizidi kuwaacha, lakini nao wakiwa wanatembea kwa ukaribu zaidi, magari kumi na saba ya polisi, yalitimua mbio kwa speed ya hajabu kulifukuzia garri hilo linaloendeshwa na Jackline Michael Nyati, huku askari wakionekana kujaa kwenye magari hayo, na silaha zao, wananchi wali shangilia kila walipokuwa wanapita, lakini mpaka wana maliza barabara ya lami, yani kinyerzi mwisho, awakuweza kumwona Jackline wala gari, walipo ulizia kwa wananchi wakaambiwa kuwa ame endelea na barabara ya malamba mawili, inayotokea mbezi, hapo mala moja wakapiga simu kituo cha polisi mbezi, wazuwie barabara hiyo, na wao wakaanza kutimua mbio kufwata barabara hiyo, lakini walipo fika malamba mawili, wakaambiwa kuwa gari lapolisi limeiacha barabara ya mbezi na kuelekea barabara ya mashambani ambayo uelekea mkoa wapwani, maeneo ya kisopwa juu, nao bila kuchelewa waka fwata njia hiyo ambayo ilikuwa baya sana, kutokana na mashimo mengi sana katika njia hiyo, bahati ikawa upande wao, ni baada yay a kutembea kidogo, walianza kuona vumbi kwa mbali, na walipo tazama vizuri waka gundua ni gari lao alilo liiba mwanamke muuwaji lilikuwa lina zidi kuchochora, Johnson akaamlisha madereva waongeze speed, na sasa walikuwa wamesha ziacha nyumba za wananchi, na kuingia kwenye mapoli na vichaka, kagiza kalikuwa kamesha anza, magari yakawasha taa, lakini gari la mbele ambalo lilkuwa na Jckline awakuliona wala wanga wake, mala ghafla wakakuta gari la polisi, lililo chukuliwa na yule mwanamke, likiwa lime simama barabara, nakuziba kabisa ile njia, hapo waka simama kwa umbari wa mita kama hamthini hivi, haraka saba askari wakashuka mala moja, wakiwa na silaha zao mikononi, wengine waka kaa kiulinzi waki tazama pande zote za barabara, huku askari kama kumi hivi wakianza kulisogelea lile gari, kwa mwendo wa taadhari, wakionyeshana ishara ya kuwa waangalifu, walitembea taratibu wakiritazama lie gari kwa umakini sana, wakiakikisha kama kunamtu ndani ya gari hili, lakini mpaka wanafika pale awakuona mtu wala kitu chochote kinachiashilia kuwepo mtu, “akuna mtu afande” alisema mmoja kati ya askari wale, walio enda kulikagua lile gari, lakini wakati anayaongea hayo waka ona kitu kama flash (mwanga mkali) ukipasua giza lililo tanda na kuishia kwenye uawa wa tank la mafuta, hapo ikafwatia mlipuko mkubwa sana, wakina Johnson wali shuhudia lile gari liki rushwa juu likiwa lina waka moto mkubwa sana, ulio sababisha kusambaa kwa vipande vya vyuma vyenye moto, vilivyo warukia wale askari kumi na kuwa potezea maisha yao, katika maumivu makubwa sana, maana ukiachilia wengine walio chomwa na vyuma na kufa mala moja, kuna wale ambao moto ulio cha nganyika na mafuta, uliwarukia na kushika kwenye miili yao, hivyo wakaanza kuungua huku waipiga kelele, wakina Johnson awakuwa na uwezo wa kuwasaidia wenzao, ambao wali poteza maisha mbele yao, zaidi Johnson ali towa amri ya askari kufwata uelekeo ulio tokea risasi, yani ule mwanga ulio toboa tank lamafuta, hapo askari wakazagaa poli lote, huku insp Johnson akipiga simu kituo cha polisi mbezi, pamoja na kikosi cha askari wa mbwa wazungukie upande wa kibamba na kuanza kusaka pori lote kuanzia ruguluni na kibamba ccm, wakija upande walipo wao, yani kisopwa, ili wakutane kati kati, wakiamini kuwa watamweka kati Jackline, na wao wakina insp waka amrisha magari ya zungukie upande wa mbezi na kutokea kibamba, iliwao wakakutane nayo kwenye barabara ya kisopwa, kwenye barabara inayo tokea kibamba, magari yakaondoka huku gari moja likiwabeba askari walio lipukiwa na gari, ambao sasa walikuwa wamesha poteza maisha, wakati huo huo, insp akapokea simu, toka kwa koplo Mashiba, simu ambayo ilimpa matumaini insp Johnson, taalifa iliyo mjulisha kuwa baba yake mzee Masinde licha ya kujeruhiwa vibaya sana, lakini bado mzima, na madoctor wanaendelea kumpatia matibabu, japo kwa sasa likuwa bado amepoteza fahamu, insp akaagiza ulinzi imara hospitalini hapo, asa chumba alicho lazwa mzee Masinde, ambae polisi bado awakufahamu kuwa ni baba mzazi wa insp Johnson, ** kibamba njia panda ya shule Denis alikuwa nyumbani kwake na mwanae France wanamsubiri mama Fance, ambae alitoka mchana akielekea saloon kusuka nywele, lakini mpaka saa mbili kasoro, akumwona mke wake, kiukweli mke wake akuwa na tabia ya kutoka nje ya penzi lao, na wala akuwai kuonyesha dariri ya kufanya hivyo, “sasa inakuwaje?” aliwaza Denis ambae aliamua kuweka filamu yakivita kwenye TV, nakuanza kutazama akisaidiana na mwanae France, huku akichukuwa pombe na kuanza kuifakamia, maana kiukweli akuelewa hii tabia ya mke wake imeanza lini, “unajuwa kama mwanake ujamlamba ata makofi machache, awezi kukuheshimu” aliwaza Denis akiendelea kugugumia pombe yake, Farance, akimshangaa baba yake,** kumbe wakati huo Jackline ndio kwanza alikuwa katikati ya msitu akitafuta njia ya kutokea kwenye barabara ambayo anaifahamu,ni barabara ya kisopwa, barabara aliyowai kufanyia mauwaji mala mbili, akiamini kuwa endapo ataipata barabara hiyo, basi atakuwa ameshafika nyumbani kwake, simu yake alikuwa ameshaizima, kutokana na kwamba akutaka polisi waone mwanga wasimu hiyo, pindi atakapo pigiwa, pia akutaka kupokea simu ya mume wake Denis, sababu akuwa na jibu la kumpa mume wake, endapo angempigia na kumwuliza yupo wapi mida hiyo, Jackline Nyati baada ya kulilipua gari kwa kutumia bunduki yake ya kudungulia, ambayo aliifungua na kuiweka kwenye begi, ikiwa vipande vipande, akaendelea na safari yake huku akikimbia kwa speed kari sana, huku smg yake aliyo ichukuwa pale hitelini, baada ya kuuwa polisi, Jackline alikimbia kwamwendo wa lisaa lizima, huku kwambali akisikia kelele za polisi, zikija nyuma yake, wakati Jackline akitokea bara bara ya kisopwa, Ghafla aka liona kundi la polisi kumi na tano wenye tochi mikononi mwao, na mbwa wakubwa wanao bweka kiukari sana, “mama yangu, kwanini sikufikilia mapema juu ya hili” alijiuliza Jackine, huku akiwasimama na kuwa tazama wale polisi wakiwaachia mbwa wao, nakuanza kumfwata kwaspeed, Jckline akapachika SMG yake begani, na kuchomoa bastola yake, aliyo ikamata mkono wa kushoto, na mkoni wa kulia akashika kisu, ** plisi wakikosi cha mbwa mbao waliokuwa na tochi mkononi mwao, wakiamini kuwa wamesha mtia nguvuni, waliwatazama mbwa wao, wakimfikia yule mwanamke, na kuanza kumshambulia, lakini kilicho tokea, awakuwai kuelezwa katika mafunzo yao, kama inaweza kutokea jambo kama hili wanalo liona kwamacho yao mida hii, kwani walimwona yule mwanamke akitummia kisu chake na bastola yake kupambana na mbwa kumi natano , na ndani ya dakika moja, mbwa wote walikuwa wame lala chini, huku wakiwa na majelaha makubwa yakisu, au matundu ya risasi, polisi wakiwa na tahamaki kwakilicho tokea, wakastuka mwanamke yule, ambae walizani kuwa ni jini au mzimu, akiingeuza SMG yake toka begani na kuanza kuwa miminia huku aki sort kurudi kichakani, mpaka anasimama yari askari kumi natano walikuwa wamepoteza maisha, “huuuu! poleni mashujaa!” alisema Jackline huku akikatiza miili ya Askari wale na kuondoka zake, atuwa chache mbele akaona taa za magari mengi sana, yakija mbele yake, akazama polini, maana muungurumo wa magari hayo ulimjulisha kuwa ni wa magari ya polisi, ni kweli, Jackline akiwa amejificha kwenye kichaka, pembeni ya barabara, dakika mbili baadae akayaona magari kumi na tani ya polisi, yaki katiza mbele yake, likiwa limepungua moja, lililo wapeleka wale marehemu hospital ya muhimbili, hapo Jackline akayatazama mpaka alipo akikisha yame potea akaanza kutimua mbio kuelekea kibamba chama, akitumia pori kwa pori, ** insp Johnson akiwa na askari wake zaidi ya mia na arobaini, walisikia sauti za mbwa wakibweka kwanguvu, wakionyesha kuona kitu na kutaka kushambulia, lakini sekunde chache, wakaanza kusikia milio ya mbwa hao ikibadirika, na kuwa ile ya maumivu na kushambbuliwa, huku kwambali wakiona tochi nyingi sana, mala sauti za mbwa zika koma, na ikafwatia milio mfululizo ya risasi, kwa sekunde chache, kisha kimya, tuukio hili waliliona na kilisikia likitokea mbleyao kwa umbari wakama kilomita moja, toka pale walipo “munguwangu, ebu tuwai jamani, anawamaliza askari huyu shetani” alipiga kelele insp Johnson, na askari wakaanza kukimbia kuelekea kule waliko iona mianga yatochi, walitumia dakika kumi kufika eneo latukio, wakakuta magari yao yameshafika kwenye eneo lile, huku taa za magari yao, zikimulika miili ya mbwa wa kipolisi na askari wao, hapo insp Johnson akachuchumaa chini, huku akionekana kuchoka, na kwa askari waliokuwa jirani yake, walimwona akifuta machozi machoni mwake, “haaaa! sijuwi kwanini wazee awa walimchokoza huyu shetani?” ilisikika sauti ya insp, iliyo ambatana na simanzi ya kilio cha uchungu, insp akiwa amechuchumaa pale chini, akitulia kwa dakika kadhaa, kichwani mwake akijaribu kuwaza namna ya kumpata Jackline Nyati, akakumbuka kuwa eneo lile mwanamke huyu, alisha wai kufanyanyia matukio kadhaa, hapo likamjia wazo, “ kibamba njia panda, kupitia luguruni” allikurupuka insp Johnson ambae alikumbuka maelezo ya marehemu Busungu, kuwa mwanamke huyu anatokea njiapanda ya shule, na pia yalisha tokea matukio jadhaa eneo hilo la kibamba njia panda, “pandeni kwenye magari haraka sana mimi nitaongoza” alisema insp huku anakimbilia kwenye gari la nyuma kabisa, akaingia kwenye gari huku askari wakigawana magari na kuingia harakasana, kisha magari yaka yakageuka alikotoka nakuanza safari, huku gari alilopanda insi Johnson likiwa mbele, ** wakati huo Jackline Nyati, aliekuwa anakimbia pembeni ya barabara, kwenye vichaka, alikuwa anapita usawa wa bwawa la kisopwa, wakati anapanda mwinuko wa eneo hilo, akaona mianga ya magari yapolisi, ikija tokea nyuma yake, hapo Jackline akajificha na kusubiri yapite, lakini akayaona yaki katisha kulia na kuelekea upande wa barabara inayo elekea luguruni, hapo Jackline akatabasamu, “wamepotea” aliwaza Jackline na kuendelea na safari yake, akijitaidi kukimbia ili kumwai mume wake akipanga endapo atawai maduka ya kibamba anunue nguo yoyote ili kumzuga mume wake, sababu wakati anaondoka pale numbani, alikuwa amevaa gauni jekundu, na viatu vyeupe vya mchuchumio, ** saa tatu usiku, kituo kikuu cha jeshi la polisi, ndani ya ofisi ya mkuu wa jeshi hilo, walionekana makanda wanadhimu wa jeshi hilo, wakiwa wame kaa wakiizunguka meza kubwa, wakiwa wametulia kwenye viti vyao, redio call ikiwa kati kati ya meza hiyo, wakiendelea kusikiliza taalifa za kimawasiliano ya kikundi kizima kilicho kwenda kumsaka muuwaji anesemekana ni wakike, Jcklne Michael Nyati, makamanda awa waliokuwa wanaongozwa na CGP, yani Chief General polisi, mwenyewe, walikuwa wamekutana toka saa kumi, baada ya kuona tukio la Pradise Tower, sasa wote walikuwa kimya wameinamisha vichwa chini, mioyo yaom ikiwa ime jawa na wasi wasi na hofu kubwa, maana walisikia jinsi vifo vingi vya askari vilivyokuwa vina endelea kutokea, wakiwemo mbwa wao waliokuwa wanategemea kwa kufwatilia nyayo za waalifu, chumba kili kuwa kimya, ni redio peke yake ndiyo iliyo sikika, na sasa waliwasikia askari wao waliokuwa wakilizunguka eneo la kibamba, na kupanga kuwa tukio la sasa liwe la kuvizia sana, ** Jackline Michael Nyati sasa alikuwa ameshafika kibamba chama, tayari alikukuwa amesha itupa hile smg, aliyoipora kwa polisi, akachukuwa mkebe mwingine wa risasi, na kuupachika kwenye bastora yake, moder 88 5.5 mm, na kuirudisha nyuma ya kiuno chake, usawa wa mfereji, ulio yagawa makalio yake, kisha akaingia ndani ya duka moja kubwa languo na viatu, na kununua gauni moja jekundu na viatu vyeupe vya mchuchumio, kwanza alitaka abadirishie hapo hapo, lakini nikama roho yake ilisita, ni baada ya kumwona kijana muuza duka, akimshangaa sana kwa jinsi alivyo kuwa amechafuka damu sehemu kubwa ya nguo zake, mpaka usoni, maana kazi ya mwisho ya mbwa ilikuwa siyo mchezo, Jackline akaondoka haraka sehemu hiyo, na kuelekea njia panda ya shule, ambako alipanga akatafute chochoro moja nakubadiri nguo zake, baada ya kuipita stendi ya daladala na pikipiki, nakutembea atuwa kama miambili, akaanza kuingia sehemu yenyenyumba chache na kufanya eneo hilo kuwa lenye giza kidogo, hapo Jackline akaanza kuangalia sehemu ambayo inge maidia kubadiri nguo zake, akaona sehemu moja iliyoonyesha kuwa inatumika kama kiwanda cha mbao, hapo akaona kuwa ndio sehemu anayoweza kubadiriisha nguo, aka piga atuwa kadhaa kuifwata ile sehemu yenye giza, iliyo tapakaa mizigo ya mbao, lakini Jackline aliyekuwa ameshika mfuko wa plastic, akasimama ghafla, na kutazama kwa umakini mahali pale, huku anapeleka mkono wake kwenye kiuno chake, usawa wa mferji uliogawa makalio yake makubwa, na kuikamata bastora yake aina ya Mic galilry moder 88, 5.5 mm, “tulia hivyo hivyo Jackline Nyati,” ilisikika sauti ya insp Johnson toka nyuma ya Jackline Nyati, hapo Jackline akatulia vile vile, akitazama kule aliko kuwa anatazama mwanzo, yani kwenye mbao, akawaona askari wawili wapolisi wakichomoka toka mafichoni, nyuma ya mbao zilizo kuwa zime pangwa mafungu mafungu, wakiwa na silaha zao mikononi, “geuka nyuma mshenzi wewe” ilikuwa ni sauti ya insp Johnson iliyo tawaliwa na ukari na hasira ya hali yajuu, Jackline akageuka, naam hapo akajikuta akitabasamu, alikuwa amesimama mbele ya kundi kubwa la askari, qaliokuwa wamemwelekezea silaha zao za kivita, huku wengine wakiongea na redio call kutoa taalifa kwa wakuu wa vituo vyao, wakidai kuwa wamesha kamata Jackline Nyati, *** mpaka hapo ndani ya chumba cha kuongea na mahabusu, Denis alimtazama mke wake, huku akishusha pumzi ndefu, ya kuchoshwa na mzigo, “kwahiyo ulifikaje nyumbani, wakati pale njiani walikuwa wamesha kuzunguka?” aliuliza Denis akimtazama mke wake alie kuwa anatazamana nae, “mh! nazani umesha sikia mengi ya kutisha, juu yangu, sina shaka kuwa auta ogopa nikikusimulia kilicho tokea, itaendelea…….
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU