BINTI MDUNGUAJI (73)

SEHEMU YA SABINI NA TATU

 

ILIPOISHIA SEHEMU YA SABINI NA MBILI : mpaka hapo ndani ya chumba cha kuongea na mahabusu, Denis alimtazama mke wake, huku akishusha pumzi ndefu, ya kuchoshwa na mzigo, “kwahiyo ulifikaje nyumbani, wakati pale njiani walikuwa wamesha kuzunguka?” aliuliza Denis akimtazama mke wake alie kuwa anatazamana nae, “mh! nazani umesha sikia mengi ya kutisha, juu yangu, sina shaka kuwa auta ogopa nikikusimulia kilicho tokea” endelea …………..
Denis akaitikia kwakichwa huku akiachia tabasamu lililo onyesha wazi kuwa alikuwa katika wakati mgumu, ambao Jackline akujuwa ni wanini, hapo Jackline Michael Nyati akaendelea kumsimulia mume wake, juu ya kilichotokea usiku wa jana yake, pale kwenye sehemu ya kuuzia mbao, “nilikuwa nilijuwa nimesha fiia mwisho, sababu nilihisi polisi wanapajuwa nyumbani, ndio maana waliweza kuja na kujificha maeneo yale” alisema Jackline wakati anaanza kumsimulia Denis kilicho tokea, “hivyo sikutaka kukuingiza kwenye matatizo, wewe na mtoto,” Jackline akaweka kituo kidogo, akimtazama Denis usoni, baada ya insp Johnson kuongea maneno yake, na mimi kuwa nimesha wageukia, wale polisi wengi nikiwaacha wawili nyuma yangu, nikawaona pia polisi wengine wakitokea kwenye chochoro zenye giza, hapo nikapaza sauti kumwambia insp Johnson, ** “hongera insp kwakuni kamata, lakini naombi moja, familia yangu aiusiki, wala kujuwa chochote, kama wewe usivyo usika, wala kujuwa aliyo yatenda baba yako” baadhi ya polisi walikuwa wanayasikia maneno haya kwa mala yapili, yani wakimsikia mwanamke huyu akionyesha kuwa anamfahamu mkubwa wao, washangaa sana, huku polisi wote wakigeuza shingo zao na kumtazama insp Johnson, wakitafakari maneno ya mwanamke muuwaji alie simama mbele yao, “inamaana insp anausika nahili?” ndvyo kila mmoja alivyo jiuliza, insp aliliona hilo, akakumbuka kosa alilo lifanya kule paradise Hotel wakati Jackline alipo kuwa amemshikilia Pc Ngaga, kabla ya kutokea kwenye kioo, hapo insp akainua bastora yake akimwonyeshea Jackline, ambae alihisi mda wowote atafanya ujanja, “kimya we Malaya, weka chini kla ulichonacho” aliongea kwa hasira insp, hapo Jackline akatabasamu, huku akiinuwa juu mfuko wa Rambo wenye nguo mpya na viatu, huku mkono wake wa kulia ukiwa bado umshika bastora nyuma ya kiuno chake, begi jeusi likuwa bado begani, “unamaanisha ilibomu” aliongea Jackline huku akiurusha mbele ule mfuko wa Rambo, mbele ya askari, nikama alivyo tarajia, askari walitawanyika kwa uoga, akiwepo insp mwenyewe, ambae seunde chache baadae akakumbuka kuwa alisikia akipewa report kuwa Jackline alikuwa dukani ananunua nguo, insp akagunduwa kosa, akainua uso wake na kumtazama Jackline, ambae alikuwa anageuka kwa speed ya haraka sana, huku akichomoa bastora yake, na kuji rusha pembeni upande wa sehemu ya kuuzia mbao, akijivilingisha kwa sarakasi, huku miali ya moto, pasipo sauti yoyote ikisikika, ili penya kwenye vichwa vya askari wawili walio kuwa nyuma ya mwanamke huyu harari, kisha kudondoka kama mizigo, “shambuliaaaaaa” alipiga kelele insp Johnson huku yeye akianza kupiga risasi kuelekea pale kibandani, ikifwatia milipuko mingi sana ya risasi za SMG bastora na uzi gun, huku mili mikali ya moto ikipiga kwenye ile sehemu ya kuuzia mbao, na kupasua pasua mbao za mwanachi, zinazo msaidia kama kitega uchumi, shambulizi hilo lilitumia dakika nzima, lakini akukuwa na dalili ya uwepo wa mtu eneo lile, “simamisha mapigooooo” alisema insp Johnson akirudia rudia, huku akisaidiwa na masajenti na makoplo aliokuwa nao, wakafanikiwa kusimamisha mapigo, hapo insp akajuwa akichelewa amesha mpoteza mwanamke huyu, kaamua bola askari watawanyike na kuanza kumfwata lia yule mwanamke, nikweli kwa msaada wa tochi zao, walizo zichukuwa kwa maremu askari wa mbwa, wakaanza kufwatilia nyayo za buti za mwanamke huyu, huku magari yakipita barabarani ** wanadhimu wakuu wajeshi lapolisi, waliokuwa pamoja na mkuu wajesho hilo, ndani ya ofisi yake, pale kituo kikuu cha polisi, walisismuliwa na jinsi tukio lilivyo kuwa linatokea huko kibamba njia panda ya shule, “hapana huyo awezi kuwa mwanamke, lazima apatikane akiwa mzima” aliongea CGP, hapo hapo msaidizi wake akaichukuwa ile redio call iliyo kuwa mezani wakiitumia kupata habari, akaanza kuita, huku akibonyeza kitufe flani pembeni ya simu, “hallow sierra bravo, kutoka charle Gorf kunaujumbe, over” hapo mala moja upande wapili ukajibu, “charle Gorf, tuma over” kisha maongezi yaka endelea, yakimtaka insp Johnson kuakikisha huyo mwanamke hatari anakamatwa na kufikishwa makao makuu, akiwa mzima kabisa, ni kweli kila mmoja mle ndani ya ofisi, alipata hamu ya kumwona huyo mwanamke hatari, mwenye uwezo wakimapigano, mfano wa askari commando, aliefuzu vyema mafunzo ya kijeshi, katika ngazi ya juu sana, (master level) tena kwenye chuo hatari na kikubwa cha kijeshi, chenye wakufunzi wenye uwezo mkubwa sana, maana awakuamini kuwa ni mwanamke kweli, ** insp alipo ipokea taarifa ya kuto muuwa mschana huyo hatari, aliona wanazidi kumwongezea mzigo, wakazi maana kumuuwa tu ilikuwa ni kazi ngumu, itakuwaje kumkata akiwa mzima, lakini chi ya kuwaza hayo insp aliendelea kuongoza askari wake kumkimbiza Jackline Nyati wakifwata nyayo za buti zake, ambazo kuna wakati walizi poteza na kuzipata tena, kitu kingine ambacho insp alianza kukiona kuwa ni kigumu, ni kwamba endapo Jackline Nyati atakamatwa, akiwa hai, basi kama baba yake alifanya uovu, kwa mzee Nyati wakiwa congo, unge bainika na kusababisha matatizo mengine kwa mzee huyo, ambae kupona kwake, ni kwa huruma ya mungu, kutokana na hari aliyo kuwa nayo, polisi waliendelea ufwatilia nyayo za Jackline Michael Nyati, zilizo kuwa zina zidi kuchochora kuelekea upande wajuu, wa mtaa huu wa kibamba njia panda ya shule, ikivuka shule ya msingi na kuzidi kuelekea ndani zaidi ya mtaa, ** ilikuwa saa nne kasoro, mida mbayo Jackline akiwa anasikia ving’ora vya mgari ya polisi, na michakato ya vishindo vya polisi waliokuwa wanamfwata kwa kasi, aliifikia nyumba yake hapo akaongeza speed kuufwata mlango, wa nyumba yake, akasikilizia kidogo, kama angasikia sauti yay a mtu yoyote kutoka ndani, akasikia sauti ya Tv pekee, Jackline akiwa na wasi wasi wa kuwa pengine mume wake amelewa na kuzima gari, akanyonga kitasa cha mlango, mlango aukufunguka, hapo akagonga mlango kwa tahadhari, “baba France! baba france” aliita Jackline, akijuwa fika kuwa lazima mume wake ambae alikuwa anamsubiri kwa hamu, kama ajazima gari, basi atafungua mlango haraka sana, nadivyo ilivyo kuwa, akasikia michakato ya miguu ya mume wake akikimbilia mlangoni na kufunguwa mlango, na yeye akuchelewa akazamandani haraka sana, akamwona mume wake akifunga mlango, kisha akaganda kumshangaa, yeye akumjari, kwanza kabisa akaona bola afiche ushaidi, akapitiliza mlango wa jikoni, uku anasikia ving’ora vya magari ya polisi, vikizidi kusogea karibu na nyumba hiyo, Jackline akapitiliza mpaka nje na kuingia kwenyesehemu ya kuegesha gari akainua bati moja chakavu chini kulikuwa na kama shimo flani, akaweka begi lake lenye zana zake zote za kivita, sasa sauti za ving’ora namuungurumo wa magari ya polisi vilikuwa vinasikika nje ya nyumba yao, Jackline akarudi ndani ya nyumba na kuelekea sebuleni, akamkuta mume wake Denis, na mwanae France, wakiwa wameganda kama masanamu wakimshangaa, Jackline akawatazama kwa macho ya huruma, huku ana waza mambo mawili, moja akiofia kuwaingiza katika matatizo, pili aliona uenda ukawa mwisho wa penzi lao na mwanaume anae mpenda kuliko wote, baada ya mwanamume huyu kubaini ukweli juu yake, mala wote kwa pamoja wakasikia sauti toka kwenye kipaza sauti, ikisikika toka nje ya nyumba, ni kama ile ya kuuzia sumu yapanya, “Jackline Michael Nyati, ilinijeshi la polisi, tupo nje ya yumba yako na silaha zenye risasi za moto, fungua mlango, utoke nje ukiwa mikono juu, vinginevyo tuta tumia nguvu zaidi kukutoa humo ndani” Denis na mke wake wote kwa pamoja, waliuangalia mlango, ile sauti ya kwenye kipaza sauti ikarudia tena maneno kama yale yamwanzo, Denis akiwa aelewi, kinacho endelea, au mkewake amefanya nini, Jackline yeye aliwatazama mume wake na mwanae, akamwambia mume wake “Denis kesho njoo tuonane, popote watakapo nipeleka, utafahamu kila kitu” hapo Jackline akaitoa simu yake mfukoni, na kumkabidhi mume wake, naomba piga simu kwa baba, mjulishe baba mwambie nimekamtwa, lakini kazi nimesha maliza, usi saau pia kesho kuja mahabusu yoyote nitakayo wekwa” Denis aliitikia kwa kichwa, kuonyesha aemkubariana na mke wake, huku akionyesha kujawa na wasiwasi, na pombe aliyo kuwa ameinywa ikimtoka kichwani, kiasi kwamba akaanza kumwogopa mkewe, alie tapakaa damu mwilini, hapo Denis akamwona mke wake mama France au Jackline, alie ishi nae kwa miaka miwili na miezi kadhaa, inayo karibia kufika nanusu, akifungua mlango taratibu, na kujitokeza nje, ** insp ambae alisha toa amri ya kuto kupiga risasi, akiwa na kundi kubwa la polisi wenye silaha, za kivita, walimwona Jackline akijitokeza nje ya nyumba hiyo, huku kijana mmoja akiwa nyuma yake amebeba mtoto, kijana yule alionyesha kushangaa, kwanini polisi wengi vile tena wenye silaha, wana kuja kumkamata mke wake, “simama hapo hapo ulipo, kisha piga makogoti, weka mikono nyuma yako kisogo” kile kipaza sauti kikapaza sauti yake, na Jackline akafanya kama alivyo amriwa, na hapo haraka sana, askari polisi sita, wakiwa na silaha aina ya SMG, sub machine gun kwenye mikono yao, pia wame valia mavazi maalum yakuzuwia risasi (bullet proof), walimzingira Jackline, huku wakimwelekezea mitutu ya bunduki zao, kitendo kile kilimshangaza sana Denis, mke wake amefanya kitu gani mpaka awekwe chini ya ulinzi namana ile, wakati huo Denis alishuhudia kundi kubwa la askari wengine, wakiwa wamevaa kama wenzao, pia mikononi walikuwa na siraha tofauti tofauti, kama bastora, SMG na uzi gun, walikuwa wamezunguka nyumba nzima, kiukweli ungezani wanapambana na kundi kubwa la majambazi, au magaidi waliojaribu kuiba ikulu, wakati wale askari sita wakiwa wame msogelea Jackline nakumlaza chini, kifudi fudi, wakimfunga pingu mikono kwa nyuma, (mgongoni) hapo insp Johnson akatabasamu kidogo, nakuanza kumsogelea Jackline aliekuwa amekandamizwa pale chini, alipofika pale huku bado tabasamu pana, likiwa usoni mwake, akachuchumaa chini, karibu na pale Jackline, alipo kandamizwa na askari sita, ungesema wana mdhibiti simba au #mbogo, insp Johnson akasogeza mdomo wake, sikioni kwa Jackline, kisha akamwambia, “hupo chini ya ulinzi mshenzi we! Utalipia vifo vyote” Jackline alikuwa anamtazama huyu inspector kwa hasira na ghazab, kisha kwa shida sana, kutokana na kukandamizwa na goti la askari sita, alimwambia yule insp Johnson “nitakuja kuongea na wewe, sizani kama unajuwa unachokifanya” hapo yule polisi mwenye nyota tatu, insp Johnson, akatabasamu tena tabasamu lililo chanyika na hasira kari sana, “ulishindwa kuongea na mimi kabla ujafanya upuuzi wako, utaongelea mahakamani” alisema yule inspector, huku akimtazama mama France kwa zarau kubwa sana, lakini kitu cha hajabu Jackline akatabasamu, tabasamu lililo changanyika na maumivu ya kuminywa na wale askari, “mahakamani?, sijajuwa ataenda nani, kati yako na yangu, ila ukweli nitakuja kwako kesho jioni” maneno hayo, yalionekana kumchukiza sana yule inspector, ila alijidhibiti asije kufanya makosa kama aliyo wai kuyafanya malakadhaa, nakusababisha Jackline amponyoke, “pelekeni ndani ya gari hii takataka” aliongea Johnson kwa hasira kali, Wakati huo Denis akiwa amembeba mwanae France, alikuwa amesimama mlangoni akimtazama mkewe akiwekwa chini ya ulinzi, na kundi kubwa la polisi ambalo lipo kamili na silaha za kimapambano mikononi, na sasa alishuhudia mke wake akipelekwa kwenye gari, lakini Jackline kabla ajaingizwa kwenye gari, aligeuza kichwa na kuwatazama, mume wake na mwanae France, macho yao yaka gongana, Jackline akaachia tabasamu, lililoongeza machungu moyoni kwa Denis, huku mwanae France akianza kuangua kilio, akimlilia mama yake, yule jamaa mwenye nyota tatu, inspector Johnson, alimfuata Denis pale mlangoni aliposimama namwanae, huku akiwapa ishara polisi wenzake, kuipekua ile nyumba yote, “nazani wewe ndie mume wa Jackline Michael Nyati” aliuliza insp Johnson, Dennis akaitikia kwa kichwa, akikubariana na maneno ya insp kuwa yeye ndie mume wa Jackline, “mkeo anashikiliwa na polisi, kwa kuhusishwa na mauwaji mfurulizo ya watu zaidi ya ishirini, wakiwepo viongozi wadini na wafanyabiashara wakubwa, polisi na wanchi wakawaida, maelezo zaidi utayapata kesho, fika kituo kikuu cha polisi, ambako mkeo atakuwepo pale akisubiri kushtakiwa” aliongea insp Johnson, kisha kama asiye taka swali lolote, akageuka na kuelekea kwenye moja ya gari, “tuma repot kazi imefanikiwa” aliongea insp kwa majigambo, huku akiendelea kutembea kwa madaha, akifwatiwa na askari wake, wakiwepo wale walio ingia kufwanya ukaguzi, kila mmoja, akipiga kelele, “hakuna kitu” “hakuna kitu” “hakuna kitu” wote wakaingia kwenye magari yao, magari yakaondolewa kwa kasi ya hajabu, huku gari alilopakizwa Jackline au mama France, lilikuwa katikati ya magari mengine, likilindwa na askari wenye silaha, waliokuwa wamening’nia kwenye magari ya wazi (defender), baadhi ya raia ambao walishaanza kutoka majumbani kwao, walishangazwa na tukio lile, na kuanza kuongea kila mmoja la kwake, ilimladi wanafiki awakosekani, ** ndani ya chumba cha CGP, wanadhimu wakuu wali piga kelele za shangwe, huku wakipongezana na kupeana mikono, “dah! yani kesho saa nne, tuna mtangaza mbele ya vyombo vya habari, na sasa hivi msemaji mkuu atoe taalifa kwenye TV ya taifa” aliagiza CGP, huku akiongoza wanadhimu wake kutoka nje ya ofisi, wakienda kusimama kwenye viwanja vya kituo kikuu, kumsubiri, muuwaji alie ikisa nchi kwamuda wa miaka miwili na nusu, “tena afande kitu cha kuflahisha, yule mzee Masinde bado mzima ila, ni kwamba hali yake siyo ya kilizisha japo madoctor wana sema wamejaribu kuokoa maisha ya mzee huyu, na wamesema kuwa paka kesho asubuhi, atakuwa vizuri, japo kuwa amepoteza sehemu zake zasiri” hiyo ilikuwa ni taalifa ya mnadhimu wa kitengo cha afya na tiba, akimweleza mkuu wake CGP, “huyo binti sijuwi amelele vipi, yani pamoja na ukatili nilio wai kuushuhudia katika matukio mengi sana, lakini huyu mwanamke ni kiboko yao” alisema CGP, kwasauti ya mshangao, ** wakati huo mzee Nyati, baada ya kuona mwane Jackline apatikani, kwenye simu yake, na ile alama ya tracking kwenyepad yke ikiwa imeptea, akahisi pengine mwanae amepatwa na matatizo, hivyo akaamua bola ajiandae mazima, kwa safari ya kwenda dar es salaam, kuakikisha anampata mwanae akiwa mahabusu, hospital au mutual, akiwa anapakiza mizigo kwenye Toyota V8, akisaidiana na mke wake, mala Michael France Nyati, aka sikia simu yake ikiita, akaitoa mfuko kwa pupa, na kutazama mpigaji, alikuwa ni mwane Jackline Nyati, akapokea malamoja, “ndiyo Jackline nipe report” aliongea mzee Nyati, akizani anaongea na mwanae wapekee, “hapana mzee ni mimi” hapo ndipo Michael Nyati askari wa zamani, alipo gundua kuwa kunatatizo kwa Jack, ni baada ya kupigiwa simu na Denis mume wa binti yake, lakini taalifa ya Denis ili mpa matumaini Nyati, na kuaidi kukutana na Deni siku yapili ili kushughulikia swala hili, Japo aliona wazi kabisa kuwa mkwe wake huyo alkuwa katika mshangao na kuchanganyikiwa, lakini mzee Nyati alielewa ni kwanini, sababu sikuzote Denis alikuwa anajuwa kuwa yeye mzee Nyati ni kikongwe kinacho ishi kwenye nyumba ya udongo, huko porini, ** saatano na nusu usiku, Jackline Michael Nyati alifikishwa mbele ya mkuu wa jeshi la polisi, na wanadhimu wakuu wa jeshi hilo, ambao walionyesha mshangao wa wazi kabisa, kwani walitarajia kumwona mshana mwenye umbo la hajabu mweusi, aliekomaa, kama mpika sumu, “haaaa! insp mnauakika kuwa ndiyo huyo?” aliuliza kwa mshangao mkuu wa polisi, “ndiyo afande, anaitwa Jackline Michael Nyati, mtoto wa mwanajeshi mtaafu wajeshi la ulinzi” alisema insp Johnson kwakujiamini, huku akiwa akipiga saluti, kwa mkubwa wake huyo, “ndio maana, aliweza kumnasa mzee wawatu na kumkata sehemu za siri, siyo kwa uzuri huu” alisema CGP, kwa mshangao, na wenzake wakacheka na kumuhunga mkono, wakati huo Jackline alikuwa amepigishwa magoti mbele ya wanadhimu hao, waliokuwa wakiusanifu mwili na uzuri wake, “yani ni binti mzuri sana sijuwi kwanini asinge olewa, na kutulia kwa mume wake” alisema mkuu wa upelelezi, Jackline alikuwa ametulia kimya akiwaza juu ya mskabari wa maisha yake, akiombea Deins japo awashe simu, maana alijuwa nnivigumu kupiga simu pengine angehofia kuwa stua wazazi wake ambao siku zote alikuwa anatambua kuwa, ni wazee wasio jiweza, “ona sasa ame mtia kilema cha maisha mzee wawatu” maneno hayo ya mkuuwa kitengo cha tiba, yalimstua Jackline, akizani labda aja yaelewa, “hivi akuna uwezekano wa kumrudishia u uume wake yule mzee?” aliuliza CGP, akimtazama mkuu wa kitengo cha tiba, “inawezekana ila ni operation kubwa sana, ambayo nchi yetu aiwezi kufanya, la kikubwa ni kwamba yupo hai” alijibu mkuu huyo wa tiba, hapo Jackline alipata uakika kuwa mzee Masinde bado mzima, akamtazama insp Johnson alikuwa amesimama na wale wanadhimu, akamwona kijana huyu akionyesha mstuko kidogo, akijitaidi wale makamanda wake, wasijuwe kuwa amestushwa na taarifa, ya kukatwa sehemu za siri kwa mzee wake, “haya insp, huyu aingie mahabusu kama gaidi, na adibitiwe sana, kesho saa nne tuna itaji kuongea na waandishi wa habari” hapo Jackline akainuliwa na kwa fujo na kungizwa ndani ya jengo la kituo kikuu, akipitishwa mapokezi na kuvuliwa viatu vyake, kisha akapelekwa kwenye mahabusu iliyopo chini ya jengo hilo, under ground, insp Johnson mwenyewe akiongoza, “nivyema kwakipindi hiki, unge sema nikuletee chakula gani, ambacho ujawai kula, usije ukanyongwa kabla ujakionja” alisema insp kwa dhiaka, wakati ana mfunga minyololo kwenye miguu na kuiunga nisha na mikononi, utani wa insp ukaonyesha kumpendeza Jackline, maana alitabasamu kidogo, kisha akamtazama insp aliekuwa anamalizia kunga minyololo, na kulifunga gate lenye nondo kubwa za mm 20, “asante asana, insp Johnson, kwakuni karibisha chakula, naomba kiwe cha kesho jioni, nyumbani kwako” itaendelea ………

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!