
SEHEMU YA SABINI NA SABA
ILIPOISHIA SEHEMU YA SABINI NA SITA: akimwonyesha kidole mama Jackline, aliyekuwa ana muweka Jackline vizuri, wakati huo Jackline alikuwa ameshaitoboa ile drip, nakuanza kuinywa, kiukweli yalikuwa ni maji flani yaliyo andaliwa kwaajili ya kumpa nguvu, baada ya kumeza ule unga mweusi, mama Jackline alistuka kidogo baada ya kumwona yule doctor akimtazama kwa tahadhari, wakati huo Jackline aliwatazama kwa macho ya kuibia, huku akijifanya kuwa, bado amezidiwa, endelea ……….
Huku wote wawili, yani Jackline, na mama yake, lengo lao likiwa moja kwenye ile bastora, iliyokuwa chini ya kitanda, kwenye mchago, “hoooo! doctor Magreth, habari za saa hizi” alisema yule doctor, ambae alionekana kisoma jina kwenye ki name tag, alicho kivaa mama Jack shingoni, “safi doctor karibuni” aliongea mama Jackline, yani mke wamzee Nyati, huku akimwacha Jackline, na kuwatazama doctor na yule polisi, “samahani doctor, nime mruhusu huyu kamanda, aingie kwa muda huu, maana anaitaji kujuwa kinacho endela, juu ya mgonjwa wao” alisema yule doctor wa kiume alie valia koti kama yeye, “nisawa doctor, wacha mimi nirudi ward ya wazazi, maana nili wasaidia kumpokea huyu mgonjwa, ila huyu kamanda, asikae sana humu ndani, siunajuwakuwa huyu ni mginjwa wakike, japo mwalifu lakini anastahili haki zote za kijinsia” alisema mama Jack, “ndio maana nilishangaa, kukuona hapa, kumbe hupo maternity?” aliongea yule doctor wakiume, huku akimsogelea Jackline pale kitandani, “ugua pole mgonjwa, nazani hapa utapata hewa nzuri sana, maana tuna madilisha mazuri na makubwa” alisema mama Jackline, kisha akatoka nje ya chumba hicho, akimwacha doctor, yule aki mkagua Jackline kwenye macho, huku akionyesha wazi kustaajabu uzuri wa binti huyu, ambao nitofqauti na habari aliyo wai kuisikia mala kwamala, “awa madoctor wa wazazi wana uwezo mkubwa wakufikili, kutokana na kesi ya mgonjwa huyu, yani hii drip aliyo mpatia ita msaidia sana, tena kwa njia ya kunywa inaoneka inampa nguvu kwa haraka sana” alisema doctor yule, huku akimwacha Jacline na kuchukuwa sindano kwenye kabati, aka mchoma kwenye mshipa wa mkono, kisha akanyonya kihasi flani cha damu, alafu akaichomoa ile sindano, ikiwa imejaa damu kiasi flani, “kamanda, wacha kwanza tupate vipimo zaidi, alafu tuta kujulisha kinacho endelea, unaweza kusubiri hapo nje” alisema Doctor yule huku akimtazama Jackline, kwa macho ya kuto kuamini, kama kweli huyu mwanamke anemtazama, ndie yule mwanamke alie tikisa jiji na nchi kwa ujumla, tena kipindi cha nyuma, aliwai kuuwa doctor mmoja bingwa wa kina mama, hapa hapa muhimbili, ni doctor Joseph Ndilane, wakati huo aliingia yule nesi wakike, aliye tumwa drip, na Anitha, au mama Jackline, mke wa mzee Nyati, “ok! nesi wacha kwanza atumie hili drip analokunywa, mpaka majibu yake yakija, kaa hapa mtazame, mimi naenda mahabara” alisema yule doctor, na yule kamanda wa polisi, akaongeza neno, “usimwogope huyu, awezi kufungua hiyo minyololo, napia nje kuna polisi wengi sana, kama ulivyo ona” wote wakacheka, lakini yule nesi alionekana wazi kujawa na uoga, “hali yake ikibadirika nijulishe mala moja” alisema yule doctor, huku akitoka na yule kamanda wa polisi, wakimwacha nesi akiwa amesimama akitetemeka, akageuza kichwa chake na kumtazama Jackline aliekuwa ameikamatia drip, kwamikono yake, iliyo fungwa na pingu zilizo unganishwa na minyololo iliyo kuja mpaka miguuni, nesi akamwona Jackline Nyati akimaliza kuinywa ile drip, na kisha akalidondosha lile fuko la maji ya drip, kisha akamwona akijikuna kichwani, kwenye nywele zake, hapo Nesi akamwona Jackline nikama anatoa kibanio kidogo kwenye nwelezake, huku akimtazama yule nesi na usoni mwake ameachia tabasamu mwanana, kabisa ungeambiwa huyu dada ni muuwaji wakutisha, usinge kubari, “au wame msingizia dada wawawt” aliwaza yule nesi, huku anaenda kuliokota lile fuko la drip, na kwenda kuli weka kwenye chombo cha takataka, kilichopo mle ndani ya kile chumba ** “ok! kazi yako nime imaliza, sasa unawaza nini?” alisema mama Jackline baada ya kuingia ndani ya gari la mume wake na kuvua koti la kidoctor, “bado zamu yangu kuingia ndani, nataka nikaongee na Masinde” alisema mzee Nyati kwa sauti tulivu kabisa, “mh! kwanini tusi shuudie kwanza Jackline akitoka, ndiyo uanze huo mpango wako mpya” alishauri mama Jack, “tatizo wewe kuna kitu ukijuwi, muda mfupi ujao polisi wote wataamia mtaani kumsaka Jackline, wakati huo macho na hakili yote itakuwa mtaani na hapa patakuwa sehemu tulivu kabisa, ambapo mfanya usafi ataingia wardini kufanya usafi, akitumia lift na ngazi, akiwa nan doo ya kufanyia usafi, hapo vipi?” alimaliza mzee Nyati na kumfanya mke wake acheke kivivu, “we mzee balaha, yani sikuwezi kabisa” ** wakati huo Insp alikuwa ndiyo anaingia kituo kikuu cha polisi, kilicho mshangaza ni kwamba, tofauti na alivyo dhania kuwa, atakuta shamla shamla za waandishi wa habari na viongozi mbali mbali, wakija kumtazama muuwaji wakike, insp alikuta kituo kikiwa kimya kabisa kama akuna kilicho tokea, insp akakimbilia ofisini kwa mkuu wa idara ya upelelezi, ambae alimsimulia juu ya kilicho tokea kwa Jackline, kuanguka ghafla akiwa amezidwa na homa, yani kitu kinacho zaniwa kuwa ni malelia, pia alielezwa juu ya CGP alivyo chukizwa kwa kitendo cha yeye kwenda hospital, akiacha kikao pale kituo kikuu, wakati kazi yake imekwisha, mwisho akaambwa asubiri mpaka Jackline atakapo pata na fuu, ili waanze vikao mbali mbali, leo hii, hivyo insp akatoka zake na kuelekea ofisini kwake ambako, alipata nafasi ya kuandika report, ya upeleleezi mzima mpaka kumkamata Jackline, insp alianza kuifanya kazi yake, huku anawaza juu ya homa ya ghafla ya mwanamke huyu hatari, nandipo alipo kumbuka kuwa, jana usiku awakuzipata silaha, zilizo tumiwa na muuwaji huyu wakike, akarudi kwa Chief CID, nakuomba kibari cha kwenda kufanya ukaguzi kwenye nyumba ile, akaruhusiwa kufanya hivyo, kwa shariti la kurudi haraka sana pale ofisi, mala akimaliza kazi hiyo, na Johnson akaondoka na askari wapatao kumi na tano na magari mawili polisi, kuelekea huko, ** ilisha timia saa sita mchana, Denis akiwa ametulia kwenye bar moja iliyopo kona ya kwanza ya muhimbili, akinywa pombe yake taratibu huku France akipata supu ya kuku akisukumia soda, yake orange, “kwanini huyu mwanamke ananifanyia hivi jamani” aliwaza Denis, ambae aliutambua upendo wakweli wa mke wake, juu yake, “kwanini sasa alikubari kukamtwa, sasa mimi nitaishi nanani?” aliwaza Denis kiasi cha kutamani kulia kabisa, lakini akakumbuka kitu kimoja ambacho ambacho kilimfanya cheke kidogo, “nilikuwa na mwona lofa, hivi siku moja tunge gombana ingekuwaje?” aliwaza Denis akiachia kicheko kidogo, mala simu ya Jackline iliyo kuwa mfukoni mwake ikaita, akaitazama, alikuwa baba ndie mpigaji, akaipokea nakuiweka sikioni, “ndiyo mzee” alisema Denis, “sikia kijana, we! nenda nyumbani kwako, ukatulie hapo subiri simu kutoka kwangu, asijuwe mtu yoyote kama tunawasiliana” ilisikika sauti ya mzee Nyati upande wapili wasimu, hapo Denis akamalizia bia yake, akamnawisha mwanae, kisha huyooo! akaingia kwenye gari nakuondoka zake, akiwa na mwanae Fransis, ** mzee Nyati alikata simu, wakati huo huo Jackline, alikuwa akiingia kwenye gari, seat ya nyuma, akiwa amevalia mavazi ya mhuguzi wakike, “nasikia mzee Masinde bado mzima” iliuwandiyo kauri ya kwanza, ya Jackline baada ya kuingia kwenye gari, “doctor wako nimesema wewe pumzika kwanza, kazi hiyo ataifanya mganga mkuu na mimi, hapo baadae” alisema mama Jack, aliekaa seat ya dereva, huku akimwonyeshea mzee Nyati, wote wakacheka, wakati huo huo mama Jack aliwasha gari na kuliondoa taratibu sana, kuelekea geti la kutokea, *** majibu ya vipimo vya Jackline yalikuwa tayari, akakabidhiwa yule doctor wa kiume alie shughulikia swala lile, akayasoma kwa umakini sana, yakamshangaza, aka kimbilia kwenye chumba cha mgonjwa yule, ambae vipimo vilionyesha akuwa na tatizo lolote, alipo karibia mlango wa chumba alimo lazwa mgonjwa, akawaona askari wakiwa makini sana wanaendelea na ulinzi, na yule afisa kiongozi alie onekana ndie mwenye jukumu la uasimamia swala lile la usalama na ulinzi, alipo mwona doctor anakuja, nae akamfwata, “ndiyo doctor, vipimo vinasemaje?” aliuliza kwa shahuku yule, afisa wa polisi, lakini doctor alioneka kuwa katika hali ya sinto fahamu, “ebu twende ndani, hapa vipimo vinaonyesha positive positive” aliongea doctor akitembea haraka haraka, kuelekea kwenye chumba alicho lazwa Jackline, wakaingia ndani na kutazama kitandani, wote wakaduwaa, maana walimwona yule muuguzi wakike alie kuwa na Jackline mle ndani, akiwa amelala kitandani, ame valishwa nguo zile za Jackline, yani suluali nyeusi na tishet nyeusi, amefungwa ile minyororo na pingu alizokuwa amefungwa Jackline mwanzo, akionganishwa na kitanda, kiasi cha kusindwa kufurukuta, huku akifungwa kitambaa cheupe usawa wa mdomo wake, yule polisi aka msogelea haraka, na kuktoa kile kitambaa mdomoni, “imekuwaje we! mwanamke” aliuliza yule polisi, kwa hamaki ya hali ya juu, “ata mimi sielewei, nilimwona kwanza kitoa kitu kishwani mwake, nikajuwa ni kibanio, lakini baadae kiamwona akini kamata kwanguvu, huku anatoa bunduki chini ya godoro” alieleza yule mwanamke, huku anatetemeka, “baada ya hapo, alifanyaje?” aliuliza yule afisa ambae alionekana kuchanganyikiwa, “akaniambia nikipiga kelele ata nifyetua akaniambia ni vue nguo zangu na yeye akavua zakwake, alafu na mimi akaniambia nivae za kwake, alafu aka nifunga hii minyororo, hapa kitandani, alafu akaniziba mdomo, na yeye akapitia hapo dirishani” alieza yule nesi, huku akionyesha dirisha pana lililo zibwa kwa vioo pasipo nondo, ambalo kwa sasa lilikuwa wazi kabisa, hapo yule afisa wa polisi alitokambio mbio nje ya chumba kile, “Jackline ametoroka, samba nje tumasake haraka sana” alipayuka yule afisa kama alie pagawa, na askari wakaanza kusambaa ovyo, pasipo kujuwa wanae msaka kwa sasa amevaaje, na ametoka saangapi?” itaendelea………..
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU