
BINTI MDUNGUAJI (78)

SEHEMU YA SABINI NA NANE
ILIPOISHIA SEHEMU YA SABINI NA SABA: alafu akaniziba mdomo, na yeye akapitia hapo dirishani” alieza yule nesi, huku akionyesha dirisha pana lililo zibwa kwa vioo pasipo nondo, ambalo kwa sasa lilikuwa wazi kabisa, hapo yule afisa wa polisi alitokambio mbio nje ya chumba kile, “Jackline ametoroka, samba nje tumasake haraka sana” alipayuka yule afisa kama alie pagawa, na askari wakaanza kusambaa ovyo, pasipo kujuwa wanae msaka kwa sasa amevaaje, na ametoka saangapi?” endelea………..
Wakwanza kufika nyumbani kwa Denis, alikuwa ni insp Johnson, na askari wake, ambao waliwakuta wakina Mahadhi, boss na Janeth, wakiwa nje ya nyumba ya Denis, wameegesha gari lao, wakimsubiri mwenzao, licha yakujaribu kupiga simu yake, lakini akuwa anapokea simu yake, wakajuwa kuwa mwenzao amechanganyikiwa na tatizo ambalo lime mtokea, kiukweli walisha sikia taalifa ya kukamatwa kwa mke wake, aki tajwa kuwa Jackline Michael Nyati, ndie Jambazi la kike lililo kuwa lina uwa kila kukicha, taalifa hiyo iliwastua sana, maana ni miezi michace hiliyopita waliliona garila Denis kwenye eneo la tukio kule jengo la wajasiliamali, akini kilicho washangaza nikwamba, jinsi mama Frank alovyo mpole mzuri na mstaalabu kwao, tena mnyenyekevu, pia historia yake na Denis wana ifahamu, na ndicho kitu pekee kinachowa shangaza, maana Denis alimkuta Jackline au mama France, akiwa anauza mama ntilie, wakiwa wanaendela kujadiriana, namana ya kumsaidia mwenzao kukabiriana na swala hili, na waliamini kuwa mwenzao alikuwa anashukuru kugunduwa kuwa alikuwa anakaa na muuwaji, wakiwa wamebeba kato za bia kwaajili ya kumliwaza mwenzao, mala walistuka kidogo baada ya kuyaona magari mawili ya polisi, yakiingia pale nyumbani kwa rafiki yao, lakini awakuogopa sana wakiwa na uakika siyo wao tu, ata rafiki yao Denis, akuwa anajuwa lolote juu ya mauwaji aliyo yafanya mke wake, ambae pengine ikitokea bahati mbaya akaachiwa, basi Denis asinge weza kuishi nae, kwani ata wao wasinge subutu kumkaribia yule mwanamke, “naitwa insp Johnson, wa kituo kikuu cha polisi, mnaweza kujitambulisha nyie ninani na mnafwata nini hapa?” aliongea insp Johnson baada tu! yakushuka toka kwenye gari, huku polisi wengine wakishuka haraka, sana na kuizunguka nyumba hile, “mimi ni bwana James, ni boss wa bwana Denis, kwenye kampuni yetu ya usanifu wa majengo, huyu karani wangu anaitwa Janeth, na huyu ni Mahadhi, ambae ni sawa na bwana Denis, ni wataalamu wangu, wa michoro ya majengo” aliongea boss wao wakina Mahadhi, “na hapa mmefwata nini?” aliuliza Johnson, “tokea tulipo pata taalifa ya kulicho mtokea mwenzetu, tukajaribu kupiga simu lakini apokei, hivyo tumekuja hapa kumtazama, na tunamsubri mpaka arudi” alifafanua boss James, “ok! kwahiyo huyu bwana hayupo?” aliuliza insp, huku akisikia simu yake inaita, “hayupo tumesikia ametoka mapema” alionge boss, lakini wakati huo Johnson akumsikiliza tena, sababu tayari simu yake, ilionyesha kumstua baada ya kuliona jina la mpigaji, akaipokea ile simu haraka, nakuanza kuongea pasipo kusikika upande wa pili, “ndiyo afande ….. ndiyo nipo kibamba…. kuna lolote mkuu ……mama yangu nini?….. hapanaaaa! hapana! sitakik kuamini, hapanaaaaaaa!” alipayuka insp kwa sauti ya ukari na yajuu sana, huku ana rudi kwenye gari lake mbio mbio, “twende muhimbili haraka” aliongea insp, kwa sauti ambayo ilikuwa ikikaribia kuangua kilio, hapo askari wakarukia kwenye magari, yaliyo kuwa yanaondoka, eneo lile, na kuwaacha wakina Mahadhi, wakishangaa, kinacho tokea, wakati huo huo wakaliona Toyota Noah, linalo milikiwa na Denis, likiingia pale nyumbani, “karibuni jamani, mbona amkuni julisha ujio wenu?” aliuliza Denis, mala tu! baada ya kushuka toka kwenye gari, akimwacha France ndani yagari, “tungekujulisha endapo unge pokea simu” alisema boss James, hapo Denis akakumbuka kuwa, leo akusikia ata mala moja simu yake ikiita, aka jipapasa mifukoni lakini wapi, akuona simu yake, zaidi ni simu ya mke wake pekee, ndiyo aliyo kuwa nayo, akarudi kwenye gari ambako bado France alikuwa ndani yake, akapekuwa kwenye mikebe yote ya kwenye dash board, lakini apakuwa na simu yake, akavuta kumbukumbu, “hoooo! nitakuwa niliiacha asubuhi” aliwaza Denis huku ana mchukuwa mwanae France toka kwenye gari, na kuelekea mlangoni, akafungua na kuwakaribisha wageni wake ndani, ambao walishusha katoni za bia toka kwenye gari lao “pole sana kwa matatizo bwana Denis” alisema boss James, wakiwa wamesha tulia sebuleni na kuanza kushambulia pombe, wakidai wana mliwaza mwenzao, “kwakweli siwezi kupoa mpaka nijuwe mwisho wa mke wangu,” hapo boss James na Mhadhi wakatazama, wakati huo Janeth, alikuwa jikoni na na Fransis, akipika chakula kwaajili ya mchana na jioni, France akiendelea kuchezea vigari vyake, pembeni ya Jen, huku wakati mwingine akienda kumtazama baba yake kule sebuleni, “yani bado una mwita mke?, hivi akiachiwa utaweza kuishi nae kwa amani?” aliuliza Mahadhi kwa sauti ya mshangao, huku akimtazama Denis, “Mahadhi, Jackline akuwa mbaya kwangu, akuwa mbaya kwako wala kwa mtu mwingine, labda umesahau kuwa nyoka akuumi mpaka umkanyage mkia” alisema Denis, kwasauti tulivu na taratibu, iliyo jawa na uchungu mkubwa sana, Mahadhi na boss wakatazamana Denis, kwamacho ya mshangao, kisha wakamtazama Denis, “inamaana umeongea na Jackline baada ya kukamatwa?” aliuliza boss James, Denis akakataa kwa kutikisa kichwa, “wamenizuwia kabisa” alisema Denis, alafu nikama kunakitu Denis akakumbuka “ila kuna magari ya polisi mawili, nimepishana nayo hapo kwenye kona, walifwata nini?” aliuliza Denis, na Mahadhi akasimulia ilivyokuwa, “lakini nashangaa mkubwa wao amepikiwa simu, na aliondoka ghafla huku amechanganyikiwa, sijuwi kuna nini huko?” “tena walisema wanaelekea muhimbili” alidakia boss James, “labda yule mgonjwa alie shambuliwa jana, atakuwa amesha kufa” alisema Denis, wakatti huo vinywaji vikiendelea kunyweka, ** ndani ya ofisi ya kituo kikuu, makamanda wanadhimu wajeshi la polisi walikuwa ndani ya ofisi ya CGP, wakijadiri juu ya swala la kutoweka kwa mwanamke yule hatari, ambae nchi nzima wanajuwa kukamatwa kwake, “naagiza askari wote wa hapa dar es salaam, waingie kwenye operation hii ya kumsaka huyu, mwanamke” alisema CGP, kwasauti kari, iliyo onyesha kuwa ni amri inayo itaji ukelezaji wa haraka sana, “ndiyo afande, naomba ni nianze utekelezaji” aliongea mkuu wa idara ya Fild Force, “endelea na kazi, ila mshilikishe insp Johnson, anafahamu ujanja mwingi wa huyu mwanamke” alisema CGP, kisha Chief FF, akapiga saruti na kutoka nje ya ofisi ile, wakati huo CGP likuwa ana mgeukia msaidizi wake, “akikisha magari yote ya vituo vyote vya hapa dar, yanapata mafuta, kisha amri kwa Chief of Treaning, and Op’s, akikisha askari wote wa vituo vyote akuna ane baki nyumbani, kuanzia sasa, mpaka mwanamke huyu apatikane, isipo kuwa insp Johnson na kikundi chake, wao watafanya kazi kivyao” zilikuwa ni amri kubwasana za kuvita, toka kwa CGP, kwa ufupi mambo yalikuwa ni mtafaruku, ndani ya ofisi ile, wanadhimu walitawanyika na kwenda kutekeleza majukumu yao, ** saa nane insp Johnson alikuwa pale hospital akichukuwa maelezo toka kwa doctor na nesi walio kuwa wakimhudumia mgonjwa Jackline Nyati, kati ya maelezo yaliyo msaidia kuanza kupata mwanga wa tukio hili, ni maelezo ya nesi, alie tekwa na Jackline, ni baada ya kusema kuwa, Jackline alichukuwa bastora chini ya godoro la kitanda alilo lalia Jackline Nyati, “doctor hiyo bastora iliingiaje humu ndani ya ward?” aliuliza insp akimtazama yule doctor wa kiume, ambae alikuwa amekaa karibu kabisa na nesi, wakati huo yule afisa mwenye cheo kikubwa kuliko insp Johnson, alikuwepo tokea mwanzo, alikuwa amesimama pembeni, akitokwa jasho mpaka kwenye meno, maana kupotea kwa Jackline, ilikuwa ni janga la taifa, “kwakweli afande mimi sijuwi, sababu humu ndani niliingia na huyu afande, labda ange ulizwa doctor Magreth, ambae alimpokea mgonjwa na kuanza kumhudumia” hapo ikaagizwa, akaitwe huyo doctor Magreth wa kitengo cha wazazi, lakini ilitumia lisaa lizima kumtafuta doctor huyo, ambae licha ya kutazama kwenye orodha ya madoctor wote wa kitengo cha wazazi awa kumpata doctor mwenye jina hilo, ikaagizwa itazamwe orodha ya madoctor wote wa hospital hiyo ya rufaha, ikitumia saa lingine lizima, mpaka saa kumi jioni, awaku mpata huyo doctor Magreth, ikaagizwa waitwe madoctor na wauguzi wote wenye majina kama hayo, ilikuwa tanbua, kutokana na ukubwa wa jengo hili na uwingi wawatu humu ndani, ili waghalimu lisaa nanusu kuwakusanya wakina magreth wote waliokuwepo huku wakicuuwa na majina ya madoctor waliotoka zamu siku ile, walipatikana wauguzi na madoctor ishilini tu!, wenye majina ya Magreth, lakini kati yao akuonekana yule doctor alie mpokea mgonjwa, alieletwa na polisi, ambae ni Jackline Michael Nyati, mpaka hapo insp akajikuta anatabasamu, “Nyati yupo mzigoni” aliongea insp Johnson, huku akiinuka na kupiga saruti, kwa mkubwa wake aliekuwepo mle ndani, “afande wacha niende juu nika mtazame mgonjwa, kisha niingie mzigoni,” alisema insp na kutoka mle ndani ya ofisi aliyo itumia kufanya mahojiano, aka pandisha ngazi kwa mbio kwenda kumtazama baba yake, wenye ward ya pekee, aliyo kuwa amelazwa, akiwapita wakina koplo Mashiba na walinzi wake tisa, kwenye kolido, “mashiba kuweni makini, nazani mmesikia kilichotokea hapo chini” alisema insp akisisitiza ulinzi kwa mzee Masinde, ambae walizni wale toka jeshi la polisi awakujuwa kuwa ni baba wa insp, ** mida hiyo, Denis, na wakina Mahadhi walikuwa, wamesha pata chakula na sasa walikuwa wanaendelea kulewa, huku Janeth nae akiwa tayari amesha jiunganao, wakiendelea kunywa pombe, France yeye akiendelea kucheza, kama akuna kilicho tokea, wakati wote wa kupombeka, denis alikuwa ana lalamika juu ya mke wake, “ungekuwepo mke wangu tungekuwa tunakunywa mvinyo” alisema Denis, kwasauti iliyo kuwa imekolea kilevi, “ila unajuwa mimi nahisi nipo ndotoni, sababu siamini kama shemeji, ndie yule mwanamke tuliekuwa tuna msikia” huyo alikuwa Mahadhi ambae pia alikuwa ameanza kukolea kinywaji, ** gholofa ya tatu ya jengo kubwa la wagonjwa wa dharula, kwenye korido moja safu ya vyumba vya ward za VIP, walionekana askari kumi wakiwa wame tanda na silaha zao, huku wamevalia mavazi mahalumu ya kuzuwia risasi, mala mlango wa chuba alicho lazwa mzee Masinde ulifunguliwa, akatoka insp Johnson na doctor mmoja, ambae aliteuliwa kumtibu mzee huyu, “doctor naomba ieleweke, akuna mtu mwingine kuingia humu, zaidi ya huyo nesi na mfanya usafi, na watakaguliwa kabla ya kuingia ndani” alisema insp kwa msisitizo, huku wale askari wakisikia, “kwa upande wetu akuna tatizo, labda waambie askari wako wawe makini, maana kilichotokea hapo chini kimetushangaza sana” alisema doctor huku wakishuka chini, kwakutumia ngazi maana mala zote lifti utumiwa na wazee, au wagonjwa maututi, pia kwa wafanyakazi wenye mizigo mikubwa, insp alipofika chini aliagana na doctor, kisha akaingia kwenye gari, pamoja na askari wake kumi natano, walio ingia kwenye magari yote mawili, kisha safari ikaanza, “inamaana Jackline akuwa anaumwaa, au kunakitu aliingia nacho mahabusu?” aliwaza insp huku redio call ya insp iki sikika kiita, “hallow Siera Bravo, ujumbe toka kwa Charle charle Delta, over” hapo insp akajuwa kuwa mwito ule unamhusu, akachukuwa redio ya kwenye gari na kujibu, “Charle Charle tuma over,” hapo maongezi yaka endelea, “Siera Bravo, taja loc (location, uelekeo) yako” ilisema sauti ya kwenye redio call, “Charle, loc yangu ni mhumbili, kaliakoo dubble kilo over”(KK yani Kituo Kikuu) alisikika insp huku wakati huo magari mawili ya polisi, yalikuwa anatoka nje ya geti kubwa la hospital ya muhimbili, ‘siera bravo jitaidi kutoa taarifa kila atuwa unayo piga over” iliskka sauti toka kwenye redio, “imenakiliwa over” mita miambili toka kwenye gati la hospital ya muhimbili, ndani ya Toyota V8, lililo kuwa lime egshwa muda mrefu sana maali hapo, toka saa tano asubuhi, likuwa limepandishwa vioo mpaka juu, na kuachwa nafasi kidogo ya hewa, Familia ya mzee Nyati, ya baba mama na mtoto, wao wapekee, wakiwa ndani ya gari hilo, waliweza kushuhudia magari mengi mengi ya yapolisi yakiingia na kutoka pale hospital, na sasa walishuhudia magari mawili yaliyo sheheni polisi wenye silaha za kivit yani SMG, na mavaazi ya kuzuwia risasi, huku akionekana insp Johnson kwenye gari lililo tangulia, wote wakacheka kidogo, kisha mzee Nyati akaonekana kuwaza jambo, “hivi Jack kwa mfano wewe ungekuwa ndie insp, ungefanya nini, kumkata Jackline Nyati, baada ya kutoroka?” hapo Jackline akatumia dakika sekunde chache sana kufikili, kisha akajibu, “ninge washikilia watu muhimu wa Jackline, nazani angeitaji maongezi hapo ninge futa ushaidi, kwa risasi nyingi sana” alisema Jackline, kisha Jackline na mama yake wakaheka kidogo, kabla ya kusitisha kicheko chao kwa ghafla, alafu wakatazamana, “baba lete simu, lete simu niongee na Denis” aliongea Jackline kwa pupa, akianza kumsachi baba yake simu, “sububiri wewe, Tanzania nzima inajuwa bado hupo chini ya polisi, alafu unataka kuongea na chapombe, siatawaleta mpaka ulipo” aliongea mzee Nyati, huku anachukuwa simu yake toka mfukoni na kuipiga, akiweka loud spikeer huku anatazama pad yake, iliyo onyesha kuwa Denis yupo Nyumbani kwake kibamba, “ndiyo. ndiyo mzee… mh! ndiyo mzee, za mida hii” wote ndani yagari walisikia sauti ya Denis iliyo zidiwa na kilevi, akionyesha kutoka sehemu yenye kelele na kwenda kwenye utulivu kidogo, “umesha toka kwenye kelele?” aliuliza mzee Nyati, akijizuwia kucheka, kutokana na Denis, kuonekana kujitaidi kuongea kwa ukakamavu, ili ulevi usionekane, kwenye sauti yake, “ndiyo… mhhhh! siiii nipo nyumbani hapa” aliongea Denis akijitaidi asioekane amelewa, hapo mzee Nyati akaiziba simu kwa kiganja cha mkono, ile sehemu ya kuongelea, kisha akawmtazama mke wake, “mkwe amelewa,” alisema mzee Nyati huku akijizuwia kucheka, kiukweli Jackline alionyesha kuchanganyikiwa, lakini kabla ajaongea lolote,baba yake akaendela na maongezi, “Denis sikia kuwa karibu na simu, utapigiwa sasa hivi na mama yake Jackline, atakacho kuambia usimwambie mtu yoyote, itakutia matatizoni ikigundulika unawasiliana na sisi, sawa?” alisema mzee Nyati kwa sauti nzito na tulivu “sawa sawa, aina tatizo, mi nipo na France” alijibu Denis, kisha mzee Nyati akata simu, “amaelewa sana awezi kuendesha gari, na leo atakunywa pombe nyingi sana, maana siyo jambo dogo, unaambiwa mkeo kipenzi, tena mrembo kama mwanangu Jack, ati ni kajambaazi” aliongea mzee Nyati, na wote wakacheka, ** insp Johnson baada ya kufika kituo kikuu, akaagiza aitwe mtu wa zamu aliekuwa mapokezi toka asubuhi, akaja askari mmpja wa kike, constable, baada ya kufika pale, akamkumbuka kuwa ata yeye alipofika asubuhi alimkuta yule yule, “WP nazani unakumbukumbu nzuri ya watu walioingia humu ndani kuwaona mahabusu, ebu niambie mtu aliekuja kumwona Jackline Nyati yupoje” aliuliza insp kwa sauti ya ukari na kitisho, “ni kijana tu alikuwa na mtoto, alisema ni mume wake” alisema yule polisi wakike, huku akionyesha kutetemeka kidogo, maana ilisakata lilikuwa zito, “alitumia muda gani kuongea na mkewake?” aliuliza insp, akiwa anaandika kwenye kijitabu chake, “alitumia muda mwingi zaidi ya masaa mawili, aliondoka wakati yule mwanamke anachukuliwa kupelekwa kwenye ukumbi wamikutano” alieleza WP, nahapo Johnson akapata mwanga flani, akakurupuka haraka sana, na kukimbilia nje, “haraka sana kwenye magari, shenzi tungekuwa tumelijuwa swala hili mapema, pale pale tulipo pisha nae tunge mkamata” alisema insp huku wakiondoka kueleka Kibamba njia panda ya shule, ** jiji la dar es salaam likuwa limezizima, polisi walitapakaa kila kona ya jiji la hili, wakimsaka Jackline Nyati, alietoroka Hospital, japo ilipangwa kuwa ni kazi ya siri, lakini taalifa zilianza kusambaa taratibu, zikianzia hospital ya muhimbili, na kwa polisi wenyewe, na kuwafikia wananchi, kumbuka mdau mpaka sasa, akukuwa na chombo chochote cha habari kilicho onyesha sura ya mwanamke huyo hatari, zaidi ya watu kulijuwa jina lake, kuwa ni Jackline Michael Nyati, huku idadi kubwa ya polisi hao walimsaka mtu wasie mjuwa ata kwasura, saa kumi na mbili ikiwa inaelekea saa moja, brig gen msaafu Soud Hassan, alikuwa ameganda kwenye Tv yake toka asubuhi, akisubiri kuona binti wa mzee Nyati akionyeshwa, kukamatwa kwake, lakini mpaka inaingia saa kumi na mbili akukuwa na taalifa ya ziada, zaidi ya ile ya asubuhii, kuwa muuwaji wakike amekamatwa, lakini akukuwa na mwendelezo wahabari hiyo, kiasi mzee Soud akaingiwa na shaka, pengine kuna jambo lime tokea, kamasiyo kuuwawakwa binti huyo ilikuficha uovu wa mzee Masinde ambae mpaka sasa inasemekana yupo polisi, basi huyo binti atakuwa ameshatoroka, ** saa moja narobo kagiza ndiyo kwanza akalikuwa kana lifunika hanga la dunia, mitaa ya mbezi luis karibu na sheri ya chuo, lilionekana Toyota V8, la mzee Nyati liki yoyoma kuelekea kibamba ccm, japo lilikuwa speed kali, lakini lili pitwa na gari mbili za polisi, kama vile lilikuwa limesimama, gari hizo za polisi zilikuwa ni msafara wa Johnson ambae alisha ona kuwa Denis anausika naupotevu wa Jackline, maana ile asubuhi kuna ujanja umefanyika, hivyo moja kwa moja ilikuwa ni kwenda kumkamata Denis, kwa kumsaidia mkewake kufanya ualifu, itaendelea………

