BINTI MDUNGUAJI (79)

SEHEMU YA SABINI NA TISA

 

ILIPOISHIA SEHEMU YA SABINI NA NANE: mitaa ya mbezi luis karibu na sheri ya chuo, lilionekana Toyota V8, la mzee Nyati likiyoyoma kuelekea kibamba ccm, japo lilikuwa speed kali, lakini lili pitwa na gari mbili za polisi, kama vile lilikuwa limesimama, gari hizo za polisi zilikuwa ni msafara wa Johnson ambae alisha ona kuwa Denis anausika naupotevu wa Jackline, maana ile asubuhi kuna ujanja umefanyika, hivyo moja kwa moja ilikuwa ni kwenda kumkamata Denis, kwa kumsaidia mke wake kufanya ualifu, endelea………
Wakati huo huo Kibamba njia panda, Denis alikuwa nyumbani kwake, akiendelea kunywa pombe na rafiki zake wakina Mahadhi, lakini licha yakunywapombe nyingi sana, akusahau maneno ya mkwe wake mzee Nyati, “kuwa awe karibu na simu yake sababu mama Jackline atampigia simu muda wowote, ni kweli akiwa katika maongoezi ya kilevi na unywaji wa pombe, mala akasikia simu ile ya Jackline ikiita, akaitazama mpigaji, iliandikwa mama, hapo Denis akapokea simu mala moja huku anatoka pale sebuleni na kuingia chumbani kwake, “shikamoo!!….. Shikamoo mama! aliamkia Denis huku akijitaidi kuongea vizuri asimkosee adabu mama mkwe, lakini akasikia suti ya upande wapili ikicheka, huku inaitikia, “marahaba mwanangu, bado hupo nyumbani?” Denis alistushwa na sauti hiyo ambayo kwakiasi kikubwa sana ni kama ya mkewake mama France, “ndio ….. ndio, nipo na rafiki zangu wamekuja kunitembelea …….” alijibu Denis, kisha akaongeza “yani kama mke wangu angekuwa huru ningesema niyeye naongea nae, mmefanana sauti vibaya sana” awakina Mahadhi walimsikia DENIS akiongea na huyo mama yake huku anainuka na kuelekea chumbani kwake, ambako alitumia muda sana, wakina Mahadhi walimwona Denis akitoka chumbani na kuingia sebuleni, na kuwakuta wao wakiendelea na vinywaji, wakamwona Denis akachukuwa kopo moja jipya la bia, na lile alilokuwa analinywa mwamanzo, kisha akamyanyua mwanae France, na kuelekea upande wa jikoni, wao awakujuwa chochote, waka endelea kunywa pombe lakini azikupita dakika tano, wakasikia mungurumo wa magari yaliyo ingia kwafujo pale nyumbani kwa Denis, wote wakaenda kuchungulia madirishani, wakawaona polisi wenye silaha, wakiizunguka ile nyumba ya Denis, “mh! mwenzetu shida anayo” aliongea Boss James, huku anatazama mlangoni, ambapo walimwona insp Johns akiwa ameongozana na askari wawili wenye silaha, akaiwata redio iliyo kuwa inatoa burudani mle ndani, na kuchomoa waya wa umeme kwa kuuvuta, “watu wote mliopo humu ndani njooni hapa sebuleni,” aliongea insp Johnson, kwa kujiamini kabisa akiwa na uwakika kuwa Denis mume wa Jackline amesha mnasa, Mahadhi, Janeth na boss James, wakatazamana, kama awaja mwelewa insp, anaongea nini, “inamaana amjanielewa, nita watowa izo pombe zote mlizo kunywa sasa hivi, nasema watu wote waliomo humu ndani, mje hapa haraka sana, awezi kutoroka eneo hili nje kuna askari wengi sana” aliongea insp kwa sauti kari kuliko ile ya kwanza, “Denis! Denis!” aliita Mahadhi kwa sauti ya kilevi iliyo changanyika na uoga, wote wakatazama upande wa jikoni, wakitegemea kumwona Denis akija sebuleni kutokea jikoni, lakini awakuona mtu, “mnauakika alielekea huko jikoni?” aliuliza Johnson, huku akimkazia macho Mahadhi, ambae alionekana kuwa ni muoga kuliko wenzie, “ndiyo… ndiyo tena ameenda sasa hivi” alisema Mahadhi akitaka kuinuka kwenda kumtazama Denis, kule jikoni alikoelekea na mwanae France, “we! unaend wapi ebutulia hapo” alisema polisi mmoja huku akisukuma Mhadhi arudi kwenye kochi, kama alivyo kuwa amkaa mwanzo, Mhadhi akajibwaga pwah!, nusu amwangukie Janeth aliekuwa amekaa jirani, kisha yule askari akiwa na silaha yake, aina ya SMG, akaelekea jikoni, ambako alitumia kama nusu dakika hivi, akarudi peke yake, “akuna mtu afande” alisema yule askari, “inamaana nyie mnadanganyasiyo, Denis yupo wapi?” aliongea insp kwa sauti ya ukari sana, “mzee atuwezi kuku danganya, Denis alikuwa amekaa hapa sasa hivi” aliongea boss James, huku akionyesha kocho la pembeni yake ambalo kwa sasa lilikuwa tupu, “akapigiwa simu na mama yake, akainuka na kumchuwa mtoto akaelekea jikoni, sasa atujuwi ameelekea wapi” aliongea boss James kwa sauti tulivu lakini lionekana wazi amelewa, hapo insp akaagiza askari waongozeke toka nje na kuikagua nyumba nzima, kitendo kilicho tumia dakika kuminzima, mpaka wale askari kurudi na kusema awajaona kitu, “amesha toroka huyu mshenzi” alisema insp Johnson kwa ghadhab huku akionyesha ishara kwa askari wake waondoke zao, wakina Mahadhi wakatulia wakiwatazama walepolisi wakitoka nje, na ikifwatia miungurumo ya magari, kisha yakatokomea, “duh! jamani hapa apatufai” alisema boss James kwa sauti ya kukata tamaa, huku akijiinua kwenye kochi, “sasa nyumba tunaiachaje?” aliuliza Janeth, akiwa bado kwenye Kochi, huku Mahadhi nae akiwa tayari amesha inuka, “kama mwenyewe ameikimbia wewe utaiweza vipi?” alijibu Boss James, ambae alikuwa anachukuwa bahadhi ya bia toka mezani, “basi tuifunge alafu akirudi atatutafuta” alishauri Janeth, huku akiinuka, na kuchukuwa makopo mawili ya bia, Mahadhi nae akainua Katon moja ambalo alikufunguliwa kabisa, kisha wakatoka nje na kufunga mlango, giza lilisha kuwa jingi sana, ** baada ya kuwa wameongea na Denis na kuona kuwa asingeweza kuondoka mwenyewe pale nyumbani, kutokana na kulewa sana, ndipo mzee Nyati ambae alikuwa anajukumu lakumalizia pale Hospital, akashauri Jackline aende akawawai mwanae na mume wake, wakampatia gari, silaha na simu, wao wakibakia na bastora, kila mmoja ya kwake, na Jackline akaondoka kuwai kibamba, Jackline ambae alishuhudia polisi wengi sana, wakiwa katika mavazi ya kazi na wengine kiraia, wakiendelea kumsaka yeye alie valia vazi lake la kiuguzi, alili liiba leo mapema kwa yule nesi, ndio wakati alipo pitwa na magari mawili ya polisi yakielekea anako elekea yeye, siyo kwamba alijuwa kuwa yale magari yana elekea nyumbani kwa mume wake, ila aliingiwa na wasi wasi kwamba uenda mume wake atakuwa katika matatizo, ndipo alipo amua kumpigia kwakutumia simu aliyopewa na mama yake, na leo ndio siku pekee aliyo pokea salamu ya shikamoo, tokwa kwa mume wake na kujikuta akicheka mwenyewe, kabla ya kuitikia, akishindwa kijitambilisha, akiofia chapombe kufichua siri, akaongea kama mama yake, wakati huo na yeye alikuwa amesha fika maeneo ya shule ya msingi Kibamba, na kuliegesha gari karibu na barabara ** “ndiyo mheshimiwa, nikweli ametoroka, lakini mpaka sasa atuja watangazia wananchi, sababu tuna fanya juhudi za kumkama tena” aliongea CGP, kwa sauti ya unyenyekevu mkubwa, akionyesha aliekuwa anaongeanae kwenye simu ni kiongozi mkubwa sana wanchi, kisha akasikiliza upande wapili, ambao wenzake awakuusikia ulichoongea ila walihisi, kutokana na maongezi ya CGP, ambae aliendelea kuongea, “ndiyo mheshimiwa, tutajitahidi kwa kila njia atapatikana, kabla ya juwa kuchomoza” maongezi yalihisia hapo na simu ikakatwa, CGP najopo lake bado walikuwa ofisini kwa CGP, wakiendelea na mjadala, ambao kiukweli ulikuwa unawaumiza vichwa vyao, huku bahadhi yao wakiwa na methodopa (dawa za kushusha mapigo yamoyo) pembeni wakizi bugia kila baada ya masaa kadhaa, wakishusha pressure zao,ambazo zilikuwa zinapanda ovyo ovyo, “jamani hii simu inatoka kwa raisi, ebu nielezeni nikwanini huyu mshenzi anafanya mauwaji kwa awa wastaafu?” kiukweli wanadhimu awa walimwona mkubwa wao akiwa amekasirika kweli kweli, hapo wote wakatazamana, ikiashiria akuna mwenye jibu la swali hilo, “inamaana tokea mwaka juzi mpaka leo atukujuwa chanzo cha mauwaji?” alikoroma CGP, wote kimya, “naagiza mala moja, yuu mzee kama amepata nafuu, akahojiwe juu yahili, nazani itasaidia kupata mwafaka” japo ulikuwa ni ushauri lakini ni amri kwa mkuu wa upelelezi, “ndiyo afande itatekelezwa” alijibu Chief Cid, na kuinuka kuelekea ofisini kwake, ambako alichukuwa simu yake ya mkononi, na kumpigia insp Johnson “ndiyo afande nakusikiliza” ilisikia sauti ya insp ambae alionekana kuwa yupo njiani, maana muungurumo wa gari ulisikika kwa fujo, “unatokea wapi mida hii” aliuliza mkuu wa upepelezi, “nipo njiani natokea kibamba, tumegundua kuwa kuna mtu alikuja kumtazama Jackline Nyati mahabusu, ndie alie mpatia dawa iliyo msababishia aonekane kuwa mgonjwa” aliongea insp, akieleza mkasa mzima, kuhusu Denis na mwanamke, aliejifanya doctor Magreth, ambae inasadikiwa kuwa ndie alie msaidia kutoroka kwa Jackline Nyati, Johnson alimaliza kusimulia mkasa mzima, na Chief Cid, akapata lakusema kwa Chief General of Polisi, “imeagizwa yafanyike mahojiano na mzee Masinde, ili kupata chanzo cha yeye na mwenzie kuwindwa na muuwaji” hapo Chef Cid akasikia sauti ya kushusha pumzi nzito ya Johnson ikisikika, “afande nilienda kwaajili hiyo, lakini nilimkuta akiwa na hali mbaya kidogo, sikuweza kufanya nae mahojiano” alijitetea Johnson, sababu mimi nawewe mdau tunajuwa kuwa mzee Masinde amesha mweleza kila kitu mwanae, “ok! tembelea mala kwa mala, ilikujuwa hali yake akiweza kuongea, fanya hivyo haraka” alimaliza Chief Cid, na kukata simu, kisha akarudi kwenye ofisi ya CGP, akapiga saruti na kuanza kutoa report, “afande, insp Johnson alienda hospital leo asubuhi ma kujaribu kuhoji maka ulivyo agiza, lakini hali ya mgonjwa ilikuwa bado siyo nzuri, akashindwa kupata maelezo” aliongea Chief Cid, akiwa amesimama mbele ya kiti chake, akajikohodha kidogo, akiwapa wenzake nafasi ya kuandika anacho kiongea, Chief Cid akaendelea, “pili katika uchunguzi wa mwanzo, insp amegnduwa kuwa kuna watu wawili wameshiriki kumtorosha Jackline” Chief Cid, aliwekatena kituo akimtazama CGP, ambae alikuwa ametulia akimtazama kwa umakini, huku wengine wakendelea kuandika kwenye vijitabu vyao vidogo vya kumbukumbu, mkuu wa kitengo cha upelelezi akaendelea, “wakwanza ni wakiume ambae imefahamika ni mume wake, ambae mwanzo inasemekana akuwa anajuwa lolote juu ya mke wake, ambae amezaa nae mtoto mmoja, anaejulikana kwa jina la Denis, lakini wameenda kumkmata nyumbani kwake kibamba wamekuta ameondoka mdafupi kabla ya wao kufika” alieleza Chief Cid, na kuwaduwaza wanadhimu wote mle ndani, *** mzee Nyati na mke wake, walikuwa ndani ya viwanja vya hospital ya muhimbili, watu waikuwa niwachache sana, ni baada ya kuwa muda wakutazama wagonjwa umesha pita wana ndoa awa wali likuwa wame tulia kwenye canteen ya le ndani, ya hospital, wakitazama kwenye jengo kubwa la wagonjwa maalumu wa dharula “wacha nikamalize zoezi, wewe wasiliana na wakina Jackline” alisema mzee Nyati huku, anamakabidhi mke wake simu yake na kofia yake ya mduara, anainuka, “sawa nakutakia mafanikio, mimi utanikuta nje, alijibu mama Jackline huku na yeye akiinuka, wakaachana njia, wakati mama Jackline akielekea wenye geti la kutokea nje ya hospital, mzee Nyati yeye alielekea kwenye kibanda kidogo, kinacho tumiwa na watu wanao usika na wafanya usafi pale hospital, akaingia ndani ya kibanaa hicho na kukaa humo kwa dakika chache kisha akatoka akiwa amevaa nguo cover loly, na kofia ya mkeka kichwani nan doo maalumu ya kusafishia sakafu yenye ffagiao ya mshiuko mrefu ndani yake, akatoka na kuelekea kwenye sehemu ya maegedho ya magari, ambayo ilionekana kuwa na magari machache sana, nyingi zikiwa ni ambulance, tano, magari machache ya kawaida binafsi, na gari mbili za polisi, ambayo ayakuwa na mtu yoyote ndani, akaonekana mzee Nyati akielekea kwenye magari hayo ya polisi, alipo yafikia akachuchumaa karibu na tairi lanyuma la gari hilo. ITAENDELEA

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!