BINTI MDUNGUAJI (80)

SEHEMU YA THEMANINI

ILIPOISHIA SEHEMU YA SABINI NA TISA: akatoka na kuelekea kwenye sehemu ya maegesho ya magari, ambayo ilionekana kuwa na magari machache sana, nyingi zikiwa ni ambulance tano, magari machache ya kawaida binafsi, na gari mbili za polisi, ambayo ayakuwa na mtu yoyote ndani, akaonekana mzee Nyati akielekea kwenye magari hayo ya polisi, alipo yafikia akachuchumaa karibu na tairi lanyuma la gari hilo. endelea…………..
La polisi, la upande wakulia, akiwa aijulkani acho kuwa anakifanya, alipomaliza akainuka na kulifwata gari lapilli, nail akafanya hivyo hivyo, ** insp Johnson baada ya kumkosa Denis nyumbani kwake na kuongea na mkubwa wake wakazi akapata wazo la kwenda hospital ya muhimbili, kuonana na baba yake, ili kumzuwia asije akaongea ukweli juu ya kile walicho mfanyia mzee Nyati, nchini congo mwaka 1988, akamweleza dereva wake, aelekee mhimbili, nae akafanya hivyo, huku gari lingine la polisi lii wafwata nyuma yao, likiwa limesheheni askali walio kuwa tayari kivita, Johnson akiwa pembeni ya dereva wake, akaanza kukumbuka bahadhi ya mambo ambayo, yalitokea katika kipindi hiki chote, akamkumbuka Jackline jinsi aliyo mtoroka pale Paradise Tower, “huyu mwanamke ni hatari sana,” alijikuta akiropoka Johnson, kabla maneno ya Jackline ayaja mjia kichwani mwake, “insp mimi siyo muhimu kwako, achana na mimi, muwai baba yako hospital, pengine akakueleza machache ambayo akuwai kukueleza, pia msaidie kuficha ushaidi wa yule mwanamke kahaba, wa hotelini, waliotaka kumchinja” ni maneno ambayo aliyaongea Jackline leo asubuhi pale mahabusu, “alijuwaje kama baba ataniambia aliyo niambia” aliwaza Johnson bila kupata jibu, ** “mama hileeee” ilikuwa ni sauti ya France aliekuwa amebebwa na baba yake begani, akitazama walikotoka, “hivi we mtoto leo umekunywa pombe kama mimi” aliuliza Denis, kwa sauti yakilevi, huku mkono mmoja akiwa ameshikilia kop la bia analoendelea kulinywa na mkono ulio mshikia France ulikuwa na kopo ambali akuwa lime funguliwa, akiendelea kutembea kwa kuyumba yumba, wakati huo walikuwa wanaingia kwenye eneo la shule, “mamaaa!” akasikika tena France ambae safari hii alianza kujipapatua toka kwa baba yake, akitaka kushuka chini, “wee acha kuhota, kabla ujalala, nitaoekana nimekunywesha pombe” aliongea Denis akianza kupepesa macho, maana akujuwa alichokifwata maali hapa, “baba France, wacha nikusaidie mtoto” ilisikika sauti toka nyuma ya Denis, nisuti ya mkewake kabisa, “mamaaaaaaa!” alistuka Denis kwa mtuko mkubwa sana, ni baada ya kugeuka na kumwona mke wake akiwa amevaa nguo nyeupe, Jackline akwai na kumziba mdomo, “nini sasa mume wangu?” aliuliza Jackline huku bado amemziba mdomo mume wake, kisha akaanza kumwachia taratibu, “huuffff! nilizania mzimu, ha! wamesha kuachia?, na hii nguo yeupe umeitoa wapi?” aliuliza kwa pupa Denis, huku akihema kwa nguvu, kama ametoka kukimbizwa, “ebu elekea kwenye lile gari jeupe, tutaongea kwenye gari” alisema Jackline akimchukuwa France toka kwa baba yake, wakaelekea kwenye gari huku Denis akionyesha wazi kufurahishwa na kitendo cha kumwona mke wake, France ndiyo usiseme, utazani alikuwa anajuwa kilicho mtokea mama yake, walitembea haraka na kuingia kwenye gari “sasa tunaenda wapi?” aliuliza Denis mala baaada ya kuona gari linaelekea upande wa barabara kuu na siyo nyumbani kwao, “nyumbani siyo salama kwako, muda wowote polisi wanakuja kukukamata, nambaya zaidi wata kupiga sana wakulazimishe useme vitu ambavyo uvijuwi” alisema Jackline, ambaae alikuwa anaendesha gari kuisogelea bara bara kuu, ya dar moro, “ninge komaa tu! kwani sikama viboko vya shule tu!” aliongea Denis kwa majigambo, wote wakacheka, mpaka France asiye juwa chochote, kiukweli walionyesha furaha, “mh! vya shuleni?, yani ungetoka huko unge sababisha nikose utamu” alisema Jackline akikamata barabara kuu ya lami, kuelekea mjini, hapo hapo wakasikia simu ya Jackline ikiita, Denis akamtazama mpigaji, alikuwa ni mzee Nyati, akaipokea, “hallow mzee nipo na komando hapa” aliongea Denis mala tu baada ya kupokea simu, “hallow mwambie Jackline awa haraka sana, tunaitaji” ilisikika sauti ya mama Jackline kwenye simu, “hoo! kumbe siyo baba” ** ndani ya jengo lefu la ghorofa saba, la emrgence, hapa muhimbili hospital, kwenye kolido la ghorofa ya tatu, walionekana polisi kumi ambao sasa walioneka kuzidiwa na uchovu wa hali ya juu, ni kutokana na kushinda mahali pale, wakimlinda mzee Masinde, maana kwa kawaida uwa kuna mapokezano ya askari, kila baada ya saa kadhaa, “unajuwa huu ni usumbufu, yani kwa gharama za vyakula hapa, ukipata milo mitatu kilasiku, kwa wiki nzima si watoto awaendi shule?” alilalamika askari mmoja, alafu usikute wenyewe wamekorofishana kwenye umabiashara yao, alilalmika mwingine, kisha maongezi yakaendelea, huku kila mmoja akilitoa lake la moyoni, wakati wanaendelea na mlalamiko yao, mala wakaona lifti ikionyesha ishara kuwa inapandisha juu, ikiwa na namba tatu, maana yake kuna mtu ana kuja kwenye flow hile, ni nadla sana lift hii kutumika, wote wakaacha maongezi na kuitazama ile lift, ilijihesabu na kusimama, kisha wakaona lango wa lift ukijifungua, alafu ikawa kimya, yani akutoka mtu, wote wakashangaa, na kuanza kuusogelea ule mlango kwa tahadhari kubwa na silaha zao wame zielekeza kwenye lift, tayari kumfyetulia mtu aliemo ndani, endapo ataoneka siyo mwema kwao, walipo ufikia wakashangaa kuona kuwa akukuwa na mtu zaidi ya ndoo ya kudekia na fagio yake, wakatazamana kwa mshangao, huku wanashusha silaha zao, kwakujuwa zilikuwa hofu zabule, lilikuwa kosa kubwa sana, kwani waliskia kishindo cha wenzao wawili wakianguka kwapamoja, ile wanageuka kushangaa, wakamwona mtu mmoja alievalia sale za wafanya usafi, nas kofia a mkeka, akiwa anajivilingisha wa srakasi ya chini, kama tairi, huku bastora yake yenye kiwamba sauti, ikiwa mkononi mwake, ikitema risasi kwa umahiri mkubwana, zilizo tuwa kwenye vichwa vyao na kuwa dondosha chini, nikta chache wote walikuwa chini akuna aliwai kufyetua ata risasi, mzee Nyati akatoa kimkebe cha risasi toka kwenye bastora yake, na kukitazama, kisha akatabasamu, “risasi kumi watu kumi, inapendeza” alisema mzee huyu huku anachukuwa kimkebe kingine na kukiweka kwenye bastora yake, akaikoki bastora yake na kuiweka mfukoni, na kuokota kofia yake iliyo mvuka, wakati ana jivilingisha, akaivaa kichwani kwake, alafu akauendea mlango wa chumba cha mgonjwa, akajariu kuufungu, nao ukakubari, ** wakati huo mzee Masinde alikuwa amelala kitandani, huku akiwaza atimayake, maana ukiachilia kunusulika kuuwawa lakini pia alikuwa amepoteza kiungo muhimu sana katika maisha, akufikilia vijana wake waliouwawa pale hotelini, yeye aliwaa juu ya dudu yake, hapo alivuta picha ya mkewake akitoka nje yandoa, kuifwata dudu, hapo mzee Masinde akamkumbika Nyati, ambae alimwona miaka mingi iliyo pita, Nyati akiwa kijana mdogo sana, ambae licha ya upole wa kijana huyo pia alikuwa mwenye mahalifa mengi katika mapigano na mipango ya kimapigano, Masinde akakumbuka moyo safi wa kijana huyo wakupatia vipande saba vya almas, kwa lengo la kukagawana, hapo Masinde akajichukia kwa roho aliyo ionyesha kwa kijana huyo, ambae mategemeo yake, ni mkumpoteza duniani kabisa, “haaaaah! sijuwi kachawi kale kakijana” aliwaza mzee Masinde, na wakahuo huo akaona mlango wa chumba kile ukifunguliwa, akaingia mtu moja alie valia sale za wafanya usafi, kichwani amevalia kofia la mkeka, “major David Johnson Masinde , pole sana” alisikia mzee Masinde, ambae bado alikuwa anamtazama mtu huyu, na sasa mzee Masinde alionyesha mshangao, maana mfanya usafi huyu alionyesha kuwa anamfahamu toka siku nyingi, “habari za siku nyingi afande” alisema yule msafishaji, huku akimsogelea pale kitandani, “kwani tulisha wai kuonana au kufahamiana?” aliuliza mzee Masinde, ambae akuweza kujiinua atakidogo, kutoka pale kitandani, “sidhani kama unaweza kunisahau katika maisha yako” alisema yule mzee mfanya usafi huku akitoa kofia la mkeka kichwani mwake, mzee Masinde akaduwaa, “mama yangu Nyati?” alisema mzee Masinde, huku ametoa macho kama aliona MV Mapinduzi (meli) inapita barabarani, “ndiyo mimi, nimuda mrefu sasa toka mwaka 1988, kule Nyilagongo” alisema mzee Nyati, huku akiwa ameachia tabasamu, “umefwata nini hapa, sema unacho taka nikupe, niafedha nyingi sana” aliongea kwapupa mzee Masinde, huku wasi waasi mwingi ukiwa ume mtawala, kabikira mbele ya wauni sita wanao taka kumbaka, mzee Nyati alitabasamia pembeni, “kamanda unakuwaje uoga hivyo, ule ujasiri wako huko wapi major?” aliuliza mzee Nyati, huku akitabasamu, “hapana Nyati, naomba unisamehe, hadhabu niliyo ipata natosha, nipo tayari kulipa chochote unacho taka” aliongea mzee huyu alie tamani kunyanyuka na kupiga magoti aombe msamaha, lakini ndiyo hivyo tena, “Masinde ulishindwa kunilipa kwa kusna asante, ukanilipa kwa risasi ya kifua, leo utanipa nini kitacho futa dhambi yako?” alisema mzee Nyatii kwa sauti tulivu kama anaongea na rafiki yake walio kwaruzana kidogo, “lakini … lakini kama hadhabu umesha nipa Nyati, kuwa na huruma” maneno hayo ya Masinde yali mfanya Nyati acheke kidogo, “unaona lahisi kumsamehe adui kuliko kumsamehe alie kutendea wema?’ aliuliza Nyati, na hapo Masinde akuweza kujibu zaidi alitoa macho ambayo yalikuwa yana ashilia kuomba msamaha kwa Nyati, “ulishindwa kuni samehe, kwakuwa uliona hasara kuniachia kipande changu kimoja cha almas kati ya saba ambavyo nilivitoa kwenu, una ahisi ni lahisi mimi kukusamehe wewe, ulie jaribu kuyachukuwa maisha yangu?” alisema mzee Nyati huku anaitoa bastora yake kutoka mfukoni, na kumlenga mzee Masinde kichwani, “tafadhari kijana…” aliongea mzee Masinde lakini kabla ajamalizia akatulizwa na risasi tatu za kimya kimya, zilizo topa kwenye paji lake la uso na kufumua kisogo chake, na kuchafua mashika meupe ya kitanda kile cha wagonjwa, “pumzika major” alisema Nyati, kisha akatoka mle chumbani na kushuka ngazi, akiziruka zile maiti za askari kumi, kuelekea chini, ile anafika ngazi ya mwsho akakutana na muhuguzi akiwa anaanza kupandisha ngazi kuelekea juu alikotoka, hapo mzee Masinde akajuwa anaiyajika kutoka haraka sana, kabla yule nesi ajapiga kelele, za kuona maiti za askari pale kwenye gholofa ya tatu, mzee Nyati ambae alitoka akiwa amevaa nguo za wafanya usafi, alienda moja kwa moja mpaka kwenye lango kuu la kutokea nje, akawapita walinzi wakampuni binafsi ya ulinzi, akaapungia mkono, na kupita zake, lakini wakati huo huo akayaona magari mawili ya polisii yakiingia pale Hospital, yakipitia kwenye lango la kuingilia, yeye akatabasamu huku ana mtazama mke wake aliekuwa amesimama mita kama mia moja kutoka pale langoni, akamfwata, “wasiliana na Jackline mwambie tukutane njiani” alisemamzee Nyati huku wakianza kutembea kuelekea Fire, mama Jackline akachukuwa simu, na kumpigia Jack, ** magari hayo Mawili ya polisi yalikuwa ni yale, ambayo yapo kwenyemsafara wa insp Johnson, yalienda moja kwamoja mpaka kwenye lile jengo la wagonjwa maalumu wa dharula, wakasimama nje ya jengo lile wakimshuhudia nesi mmoja akitoka nje ya jengo hili, mbio mbio huku akipiga kelele, utazani anakimbizwa na mzimu, “nakufaaaaa” alipiga kelele yule nesi, kiukweli muda huo eneo hili alikuwa nawatu kabisa, hapo insp Johnson akashuka haraka toka kwenye gari, wakati huo wale askari waliokuwa kwenye magari yote mawili, walikuwa wamesha ruka atakabla magari ayaja simama vizuri, na kukaa tayari kimapigano, insp akamkimbilia yule nesi, ambae nae baada ya kuona polisi wakiingia eneo lile, akawakimbilia, “tulia nieleze kunanini?” alisema insp Johnson, baada ya kumshika yule nesi wakike, “polisi.. polisi wote wamekufa” alisema yule nesi kwapua, “baba” alisema insp Johnson, huku akiwa ameganda, macho akiyaelekeza safu ya gorofa ya tatu, askari wote waka mtazama insp, wakisubiri amri, lakini insp alionekana kama sanamu lisilo na hisia yoyote, akuna aliejuwa ni kwanini, mala wakamwona ana anza kukimbia kuufwa mlango wa kuingilia wa jengo lile, *** kituo kikuu cha polisi, mambo hayakuwa mazuri, maana bado walikuwa awajapata taalifa ya kupatikana Jackline au washirika wake, ambao ni mama aliejifanya doctor, na mume wa Jackline aliekuja kumtazama mahabusu, wakati huo huo, ikaja taalifa kutoka hospital kuu ya muhimbili, taalifa amayo ili mfikia mkuu wa kitngo cha upelele, na kuzidi kuwachanganya wanadhimu awa ambao walikuwa bado wapo ofisini, nyumbani akuendeki, “jamani kuna taalifa ya kushangaza na kustusha kidogo” alisema Chief Cid, wote wakatega masiko yao, kusikiliza hizo taalifa, “kwanza kabisa mzee Masinde, yani yule mgonjwa alie nusulika jana, amesha uwawa kwa risasi ndani ya ward aliyo kuwa amelazwa” aliongea Chief Cid, na CGP kahamaki, “nini, yulemgonjwa kauwawa?” ilikuwa ni sauti iliyo jawa na mshangao mkubwa sana, “ndiyo afande, ila kingine ni kwamba ajafa peke yake, walio uwawa kwenye tukio hili ni pamoja na askari kumi waliokuwa wanamlinda” maneno hayo ya Chief Cid, nusu yachomoe roho zawatu, maana pressure zao zilipanda kwa kiwango kikubwa, hapo ungewaona wakiangaika kubugia vidonge, vya kuzuwia mapigo yao ya moyo, yasipande sana, “ila afande kitu cha kushangaza, kumbe Marehemu Masinde, ni baba mzazi wa insp Johnson” hapo ofisi nzima ikazizima kwa ukimya wa hali ya juu, wakatazamana kwa mishangao, “jaribu kutofutisha wakati wa utani, CC, inawezekanaje hilo jambo?” aliuliza CGP, kwa sauti ya taratibu iliyo jaa mshangao mkubwa sana, itaendelea………….

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!