BINTI MDUNGUAJI (81)

SEHEMU YA THEMANINI NA MOJA

 

ILIPOISHIA SEHEMU YA THEMANINI : “ila afande kitu cha kushangaza, kumbe Marehemu Masinde, ni baba mzazi wa insp Johnson” hapo ofisi nzima ikazizima kwa ukimya wa hali ya juu, wakatazamana kwa mishangao, “jaribu kutofutisha wakati wa utani, CC, inawezekanaje hilo jambo?” aliuliza CGP, kwa sauti ya taratibu iliyo jaa mshangao mkubwa sana, endelea………
“afande imebainika, kuwa ni baba yake baada ya insp kuingia kwenye chumba ambacho mzee Masinde alikuwa amelazwa, na kumkuta mzee huyu amesha pigwa risasi, insp akaanza kulia akitaja baba! baba!, kisha insp akapoteza fahamu hapo hapo, na hivi sasa yupo hospitalini hapo anapatiwa huduma yakwanza” hapo wanadhimu wote, na CGP mwenyewe wakashusha pumzi kwanguvu, “ok! insp Johnson atolewe katika uchunguzi huo, apewe mapumziko ya msiba, na achaguliwe mwingine wakushika nafasi yake” aliagiza CGP, kisha akamalizia CGP, mwisho ichunguzwe zaidi uenda kuna mambo mengi tusyo ya fahamu juu ya mwenendeo mzima wa uchunguzi wamwanzo, sababu bado atuja juwa sababu ya mauwaji kwa awa wastafu” ** mzee Nyati na mkewake Anitha, au mama Jackline walikutana na Jackline aliekuwa na wakina Denis, kisha wakaingia kwenye gari na safari ikaendelea, “naona mkwe amepumzika” alisema mzee Nyati akitazama DENIS aliekuwa ameuchapa usingizi na kopolake la bia mkononi, France akicheza mapjani kwa baba yake, wote wakacheka kidogo, “sasa tunaenda wapi?” aluliza mzee Nyati, “nina promise ya diner kwa insp, wacha nikamsubiri, najuwa sasa hivi atakuwa anamlilia baba yake” wote wakacheka mle ndani ya gari, “babu njoo ukae na mimi” aisema mzee Nyati akimchukuwa France na kukaanae seat ya nyuma, karibu na mama Jack, ** shughuli ilikuwa kwa insp Johnson, ambae alirudiwa na fahamu, nusu saa baadae, akaganda aki wazajambo flani, “Jack umeniweza, Jack umenikomesha” alijisemea insp huku madoctor na bahadhi ya askari wenye silaha wakiwa wamezunguka kitanda alicho kuwa amelazwa, wakihisi kuwa insp amechanganyikiwa, kumbe insp aliongea kitu alicho kijuwa kabisa, insp alivuta sura ya Jackline, Japo mala ya kwanza alipo mwona alimwona kuwa ni mwanamke mrembo na mzuri sana, lakini sasa aliona kuwa ni shetani mkubwa, la mguu mmoja, insp akajilahumu kwa kuwai hospital asubuhi, kuliko kubaki kituo kikuu kuakikisha huyu mwanamke afanyi ujanja wowote, “mimi siyo muhimu, wai kamatazame baba yako, pengine analolote la kukuambia” ilijirudia kauri ya jackline, kichwani wake, “kumbe alikuwa anajuwa kunamtu akuja kumletea hiyo dawa” aliwaza insp ambae alikuwa amewekewa drip mkononi mwake, ghafla insp akaonekana kustuka, kisha waka msikia akijiuliza kwa sauti ya chini, “chakula, usiku, nyumbani kwangu, alikuwa na maana gani?” wote waliokuwa mle ndani wakatazamana, kwa mshangao, “hapana, mama Betty na Betty” alipiga kelele insp huku akiinuka pale kitandani, huku akichomoa ile sindano ya drip, akakusanya kila kilicho chakwake,koti lake (yani shati la juu la kipolisi, na buti zake, alizoenda kuvalia kwenye gari, basipo kusahau bastora yake, na kofia, huku nyuma akifwatiwa na askari wake aliokuwa nao mle ndani alikokuwa anapatiwa huduma ya kwanza, ile kutokea nje askari wengine nao waka panda kwenye magari, kisha safari ikaanza kuelekea mbezi bichi, nyumbani kwa insp, huku insp akichukuwa simu yake na kumpigia mkewake, simu iliita sana pasipo kupokelewa, mpaka ikakatika, “baba ume mponza mke wangu maskini….” alisema insp huku akishindwa kujizuwia kulia, akiamini kuwa Jackline alisha fika nyumbani kwake na kufanya yakwake, “endesha gari haraka sana” alipiga kelele Johnson, akimpiga dereva begani, kiasi cha dereva mwenyewe kushangaa, maana mwendo aliokuwa anatembea, aukuwa wanchi hii, na barabara zetu, Johnson akajaribu tena kumpigia simu mkewake, zaidi ya mala tatu, lakini aikupokelewa, mpaka hapo insp Johnson David Masinde, akajuwa amesha poteza familia, “kwanini sikukumbuka mapema jambo hili, na mtu alisha niambia kabisa” alisema insp kwa ghadhabu, akijishushia lawama kubwa sana, wakati wana pita makongo, akastuka kuona simu yake ikiita, akaichomoa mfukoni, na kuitazama akaona mpigaji kuwa ni mke wake, “haaaaa! Jackline” alijikuta Johnson amelopoka pasipo kujielewa, maana alijuwa kuwa simu ile ya mke wake, itakuwa mkononi kwa Jackline, ni baada ya kumaliza kuwa chinjilia mbali, “akaipokea kwa unyonge na kuweka sikioni pasipo kuongea neno lolote, mapigo ya moyo yakamwenda mbio, “hallow baba Bitte,” ilisikika sauti ya mkewake ikiwa na mng’amu ng’amu ya usingizi, insp akashusha pumzi kwanguvu, “mke wangu mpo salama hapo nyumbani? kwanini uliacha kupokea simu?” maswali mfululizo yalimtoka insp, “nilikuwa nimepitiwa na usingizi, vipi salama huko?” aliuliza mama Bitte, akionyesha kutia shaka juu ya Jambo flani, “salama tu nakuja huko nyumbani” alisema insp akijitaidi kuficha majonzi aliyo nayo, “saw nakusubiri, maana nimekuwekea chakula, nikajuwa utarudi mapema” aliongea mke wa insp Johnson akionekana aninuka toka kitandani, “sikia mama Bitte, usi fungue mlango mpaka nitatumia funguo yangu” alisema insp, ambae uwa nautaratibu wa kutembea na funguo yake ya ziada asa inapotokea kuwa na kazi za usiku, wali maliza maongezi na kukukata simu, kisha insp aka achia tabasamu pana sana, ** Chief Cid alipata taaliafa kuwa insp amesha zinduka na sasa anaeleka nyumbani kwake kuiwai familia yake, ambayo inaweza kuingia matatizoni, hapo Chief akampigia simu insp ilikumjulisha kuwa kuanzia muda ule alikuwa likizo fupi, na kumwuliza kama angeitaji msaada zaidi, lakini kili alipo piga simu ilikuwa inatumika, mpaka alipo amua kumpigia mtu mwingine aliekuwa karibu na insp, ilikufkisha ujumbe, na kwabahati mbaya alikuwa gari jingine, wakapanga kumjulisha watakapo fika, nyumbani kwa insp huyo, *** saa tano usiku, magari mawili ya polisi yalitililika kwa mwendo wa speed ya kuzima moto, na kujikuta wakipiga bleck za nguvu, ndani ya kiwanja cha nyumba ya insp Johnson, huku askari wakiruka na kuizunguka nyumba hiyo, insp nae Johnson akashuka faster, na kufwata mlango wa nyumba yake, huku akiutoa funguo mfukoni mwake, akafungua mlango nakuingia ndani ambako kulikuwa nagiza, nikawaida kuzima taa zandani, nyakati za usiku, insp akapilitiliza mpaka chumbani kwake anako lala na mke wake, akamwona ndio kwanza anaonekana kupitiwa na usingizi, akumstua akaelekea chumbani kwa mwanae Beatrice, nae akamwona amelala fofofo, hapo insp akatabasamu kwanguvu, nakurudi sebuleni, akatoa kavua kofia yake na kuiweka juu ya meza ndogo ya kioo, kisha akaitoa bastora yake ambayo ilikuwa na risasi zilizo jaa, maana akuwa amitumia siku hile, nay o akaiweka juu ya ile meza ndogo ya kioo, iliyo zungukwa na makochi ya kisasa, akatazama kwenye meza kubwa ya chakula, japo kulikuwa na giza, lakini akaona hot pot za vyakula, ni kawaida ya mke wake kumwekea chakula, ata akirudi usiku sana, lazima angekuta chakula mezani, insp akatoka nje na kuongea na msaidizi wake, mwenye cheo cha sajenti, “nyie nendeni, mimi siwezi kufanya lolo kwa sasa, tutakutana kesho kituo kikuu” alisema insp, na yule sajent akamwambia, “ila afande kuna ujumbe toka kwa chief, amesema umepewa likizo fupi, kwaajili ya kufanya taratibu za mazishi” maneno yale ya sajent, insp aliyapokea vyema, maana atainge kuwaje, lazima ange chukuwa likizo hiyo, kwaajili ya mazishi ya baba yake, baada ya kuagana na asakari wake, na wao kuondoka zao waka mwacha insp akizunguka nyuba yake kuikagua, na alipo ona kuwa ni salama, akaingia ndani, safari hii akawasha za sebuleni, ile mwah! macho yake yaka tuwa moja kwamoja kwenye meza kubwa ya chakula yenye viti vitano, huku kimoja kikiwa kimekaliwa na mwanamke, alie valia nguo za wauguzi, yani gauni jeupe, “mungu wangu, Jackline” alisema insp Johnson kwa mshangao na mstuko mkubwa huku akiitazama kwenye meza dogo ya kioo, lakini baastora aikuwepo, zaidi aliion kofia tu, “ndio mimi Jackline Nyati, je unaitafuta hii?” aliongea Jackline, huku akimwonyesha insp bastora yake, ambayo muda mfupi alikuwa ameiacha mezani, na sasa ikikuwa mikononi mwa Jackline, ambae alikuwa ame tulia kwenye kiti, pale kwenye meza ya chakula, insp akujibu kitu akakodoa macho kama mwizi alie kwiba sanduku la vitabu vya dini akizani fedha, “muda wa chakula cha usiku, auitaji hii” alisema Jackline kwa sauti ya taratibu kidogo, Johnson bado alikuwa ameduwaa, akimtazama Jackline kwa mshangao, nikama anajiuliza “ajafanya lolote huyu?” insp akatazama mlango wa chumba cha mkewake, ulikuwa umefungwa kama alivyo uacha wakati antoka nje, akatazama mlango wa chumba cha mwanae, nao ulikuwa umefungwa kama alivyo uacha wakati anaenda kuagana na askari wake, “husiwe na wasi wasi insp, sijaja kivita, wala kumdhuru mtu yoyote humu ndani, nimekuja kwaajili ya kile chakula ulicho niahidi” alisema Jackline kwa sauti ile ile ya taratibu, kama ujaja kuni dhuru mimi na familia yangu umefwata nini?” aliongea insp kwa sauti ya chini pia, “nimekuja kula chakula chajioni ambacho uliniahidi, au ulikuwa unanitania?” aliuliza Jackline ambae uongeaji wake, usinge zani kama ni muuwaji mkubwa, insp akujibu kitu, zaidi alijishika kiuno kwa kuchoka na mambo anayo ya shuhudia mbele yake, “ameingia saangapi?” aliwaza insp akiwa bado amesimama utazani ni mgeni pale nyumbani, “mbona ukai Johnson, au unajiuliza nimeingiaje?, niliingia ulipokuwa unazunguka kukagua nyumba, ukasahau kuwa umeacha mlango wazi” aliongea Jackline huku anatabasamu, “mimi mjinga sana” aliwaza insp, lakini Jackline nikama alikuwa anamsoma mawazo yake, “ok! ilo aliniusu sana, chamsingi ni kuwa, nimemekuja kukuambia kuwa, mambo yameisha, tena bahati nzuri ukweli wote umesha ujuwa, siyvyo insp?” aliongea Jaackline akimtazama insp, ambae alikuwa kimya kabisa, “akimsikiliza Jackline” licha ya kujuwa jinsi baba yako alivyo mfanyia baba yangu mwaka 1988, pia ume gunduwa kuwa baba yako alikuwa wewe ba baba yako mmejaribu mala nyingi kuni uwa” alisema Jackline kwakituo, ata kabla ulificha uovu wa baba yako, lakini ukashindwa kumkataza asifanye mahovu” hapo insp akashusha tena pumzi nzito, kuashilia maneno yalikuwa yana mwingia, kuona hivyo Jackline akaendelea, “japo sina uakika kama utaendelea kufwatilia kesi hii, lakini nakuomba kaambali na mimi” ssababu auna makosa yoyote” alimaliza Jackline huku anainuka toka kwenye kiti, alichokuwa amekalia, hku ameibeba ile bastora ya insp, “kwaheri Johnson, asante kwa chakula” aliongea Jackline, ambae safari hii alicheka kidogo, huku anaiweka ile bastora ya insp juu ya meza yakioo, kisha akaanza kutembea kuufwata mlango ambao bado ulikuwa auja fungwa kwa funguo, pasipo kujuwa kuwa nuyma yake, insp Johnson aalichukuwa bastora yake haraka sana, kisha akaikoki, hapo Jackline akasimama, akiwa ameutazama mlango, “simama hapo hapo Jack, ukipiga atuwa moja tu! nakufyetua” ilisikika sauti kali ya insp, ambae alikuwa ameunyoosha mkono wake wenye bastora, kumwelekezea Jackline, ambae alitulia kidogo na kushika kitasa cha mlango, na kufungua mlango, hapo ikasikika itaendelea ……..

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!