BIOLOGY TEACHER 1
Alice Nelson ndio jina nililopewa na wazazi wangu japo kuwa watu wa mtaani waliizowea kuniita kamama pia ni mtoto wa mwisho kwenye familia ya watoto wawili , wakaanza Ni Kaka yangu Bray na Mimi ni mtoto wa pili na wa mwisho pia Ni mwanafunzi wa kidato Cha tano. Kaka Bray amekuwa nibmtu wa kunifuatilia Sana alikuwa hataki kuona nikiwa naongizana na mvulana , ikitokea kaniona nikiwa karibu na mvulana alimfuata na kumtishia hata ikiwezekana kumpiga hivyo wavulana wengi hawakutaka kuwa karibu na Mimi.
siku moja ilikuwa ya Jumamosi nilienda kumtembelea rafiki yangu Miriam lakini nilipofika nyumbani kwao sikumkuta ikabidi nirudi nyumbani wakati nikiwa njiani mvua kubwa ikaanza kunyesha ikabidi nisimame sehemu kwaajili ya kujikinga na mvua , nilisimama kwa muda kusuribia mvua ikatike ili niendelee na safari zangu. Nilipokuwa nimesimama Kaka Bray alikuwa ananipigia Sana simu na kunisisitiza niwahi Kurudi nyumbani
nilimueleza kuhusu mvua akaniambia
” Kwani ukinyeshewa uta yeyuka , njoo hivyo hivyo ukifika utabadilisha nguo.
” Nikiumwa je?
” Nimekwambia njoo Ni muhimu wewe kufika mapema.
Nilimkatia simu lakini bado ilikuwa kero hakuacha kunipigia . Nilipoangalia pembeni niliona mwamvuli umewekwa nalijisogeza mpaka karibu na ule mwamvuli. Jirani kulikuwa na Kaka alikuwa bize na simu. Nilihisi huenda haukuwa wake labda Kuna mtu alikuwa kausahau. Nikiwa bado najishauri kukuchukua yule Kaka alikuwa Kama vile anaondoka kwakuwa hakukuwa na mtu mwingine nikajua ule mwamvuli umesahaulika , hapo ndipo nikapata upenyo wa kuchukua mwamvuli na kupitia njia za vichochoro. Kumbe yule Kaka hakwenda mbali aliniona akawa ananifuata nilijaribu kukimbia lakini niliishia kuteleza na kuanguka kwenye tope. Nilijaribu kunyanyuka lakini nilitekeza Tena . Yule Kaka alisogea karibu na kunipa mkono, nikampa mkono wangu akanisaidia kuninyanyua
” Ona Sasa unataka kuumia bure kwaajili ya uwizi wa mwamvuli.
” Lakini sijaiba
” Ni wako? Nilishindwa kujibu nikaishi kuomba msamaha
” Samahani ….
” Unaenda wapi?
” Nyumbani Kuna matatizo natakiwa kuwahi ,sikuwa na jinsi nikaamua kuchukua huu mwamvuli nilijua mwenye nao kausahau
” Sawa lakini ingekuwa vizuri ungeuliza kwanza.
” Nimekosea nisamehe Sana. Nilijifanya mstaarabu na kuomba samahani nyingi
” Usijali ,unaitwa nani?
” Alice.
” Safi, naitwa shafii.
” Nimefurahi kukufahamu.
Nilifahamiana na shafii kwa muda mfupi lakini alikuwa mchangamfu Sana . Tulipofika sehemu akaniambia
” Safari yangu inaishia hapa , kwaheri.
” Mwamvuli wako?
” Usijali unaweza kwenda nao.
” Sasa nitakuona wapi nikurudishie?
” Haina haja unaweza kuwa nao tu, lakini utakaponiona nitakuona. Alisema Shafii huku akitabasamu. Aliondoka huku akiwa anaruka maji yaliyokuwa yanatililika barabarani.
Tuliachana na shafii na Mimi nikatembea mpaka nikafika nyumbani.
Nilipofungua ndani nilisikia kelele za watu wakisema
” Heki ya kuzaliwa Alice” niliduwaa na kuwaangalia. Marafiki zangu wote walikuwepo nyumbani ,Walinifuata na kunikumbatia na kunipongeza .
” Hongera Sana imeshakuwa msichana mkubwa Sasa uache utoto. Aliniambia Kaka Bray huku akinivuta shavu.
Boyfriend wangu Meshack alinisogelea huku akiwa anatabasamu akanipatia boksi la zawadi na kunikumbatia
” Hongera mpenzi.
” Asante.
Marafiki nao walinisogelea na kunipatia zawadi zangu. Baada ya hapo Miriam alinishika mkono na kuniburuza chumbani kwangu.
” Kaa hapo unatakiwa kubadilika hii Ni siku muhimu Sana kwako. Alitoa vipodozi pamoja na gauni jipya
” Nguo mpya imetoka wapi?
” Kila kitu unachokiona hapa kakifanya Kaka yako Bray.
” Kwahiyo ulikuwa unajua na haukuniambia?
” Sasa nawezaje kuvujisha Siri za watu.
” Hata Mimi ulishindwa kunidokeza?
” Ningekwambia isingeleta maana .
Miriam aliniandaa nikavaa nguo yangu mpya tukatoka kwenda kusheherekea. Ilikuwa ni sherehe ndogo lakini ilifana Sana. Nilikaa pembeni na Meshack tukawa tunaongea Mambo yetu wakati huo Bray alikuwa anatuangalia Sana , Kaka Bray hakuwa anataka niwe karibu na mwanaume yoyote na Mara kwa Mara alikuwa akinikanya kuhusu kuingia kwenye mahusiano.
” Meshack twende tukajuchanganye na wenzetu Kaka Bray anatuangalia Sana. Tulinyanyuka pale tulipokuwa tumekaa tukaenda kujichanganya na wenzetu.
Kuna muda nilikuwa naenda jikoni meshack alinifuata na kunikumbatia, muda huohuo Kaka Bray alifika nilimsukuma Meshack. Kaka Bray alisogea pale tulipokuwa tumesimama alafu akasema
” Nini kinaendelea hapa?
” Hakuna kitu . Nilimjibu nikiwa na wasiwasi maana namjua vizuri Kaka yangu
” Oya wewe ndio ukajifanya Khan mfalme wa mahaba au sio? Meshack alikuwa kajiinamia ikabidi Mimi nimtetee
” Kaka huyu Ni mwanafunzi mwenzangu alikuwa ananipongeza ….
” Kukupongeza Nini, nimewaona muda mrefu Sana na huo upuuzi mnaofanya , dogo kaa mbali na mdogo wangu nitakuja kukufanya vibaya. Tuliangaliana na Meshack
” Mnaangaliana Nini Kama katuni potea. Meshack aliondoka na Kaka Bray akanigeukia na kuniambia
” Wewe mpumbavu unataka niongee rugha gani ndio uelewe kuwa sitaki uwe na mahusiano?
” Lakini nimeshakuwa sipo chini ya miaka 18.
” Kwahiyo Kama imekuwa unataka kujipa Uhuru wa kuvurugwa na wanaume wasio kuwa na maana? Unatakiwa kutulia Alice, usije kutuletea aibu kwenye familia yetu. Nilinyamaza nikawa namuangalia .
akaondoka nikabaki nimesimama huku nanungunika
” Miaka 18 nimeshakuwa mkubwa lakini mtu ananibanabana , mbona yeye akiwa na wanawake zake hakuna anaemsema. Nilirudi walipo wenzangu lakini sikumuona Meshack, niliemfuata Miriam nikamuuliza
” Meshack Yuko wapi?
” Alitoka nje. Nilitoka mpaka nje kwenda kumuangalia lakini sikumuona , nilijaribu kumpigia simu lakini simu yake haikupokelewa.
Sherehe ikiisha watu wote walitawanyika. Usiku nikiwa chumbani nilimpigia simu Meshack lakini hakupokea , nilituma message hakujibu. Niliingiwa hofu nikajua lazima Meshack atakuwa kakasirika.
Kesho yake nilienda shule lakini Meshack hakuwa na mpango na Mimi, hakutaka kuongea na Mimi kabisa. Ilimbidi nimuache mpaka hasira zake zitakapoisha .
Zilipiga wiki mbili bado alikuwa kanikasirikia pia nilipata fununu kuwa ameanzisha mahusiano na msichana mmoja pale shule anaitwa zuwena, nilijaribu kumfuatilia nikaja kugundua lile lililosemwa lilikuwa kweli niliwafumania darasani wakiwa Wana kiss. Nilimuuliza Meshack sababu ya kunifanyia vile akanijubu
” Alice nimekuchoka , sitaki kutishiwa maisha na Kaka yako. Kwanza nimekuchoka hunipi ninachotaka Bora kila mtu aendelee na maisha yake
” Hiyo ndio sababu au Kuna lingine.
” Lingine Ni kuwa nilikuchoka nilikuwa nakutafutia sababu.
” Asante Sana Meshack. Niliondoka kwa hasira na kwenda kukaa nyuma ya madarasa na kuanza kulia , Miriam alinimbembeleza na kunitia moyo. Nilijikaza na kujaribu kumsahau .
Siku moja nikiwa natoka shule nilikutana na Shafii, tulisalimiana . Alinisindikiza kidogo huku tukiwa tunapiga story. Shafii alikuwa mchangamfu Sana nikajikuta navutiwa na kampani yake lakini hatukuwahi kupeana namba Wala kuekekezana tunapoishi. Tulifika sehemu akasema
” Inatosha acha nirudi.
” Asante kwa kunisindikiza
” Ok, when you see me ,I will see you. Alisema hivyo Kisha akaondoka.
Kadri siku zilivyokuwa zinaenda Meshack alikuwa alinirusha roho na penzi lake jipya, kila alipoenda alikuwa anafuatana na zuwena hata darasani walikaa pamoja mbaya zaidi kila mtu alijua nimeachika. Kusema ukweli nilikuwa naumia Sana .
Siku moja wanafunzi wote tulienda kubadili nguo kwaajili ya michezo wakati natoka chumba Cha kubadilisha nguo nilimuona Meshack akiwa kakumbatiana na mpenzi wake, niliwapita nilipofika mbele niligeuka kuwaangalia na wao wakigeuka kuniangalia nilitembea huku nawaangalia ghafla nikagongana na mtu kugeuka kumuangalia alikuwa Ni shafii.
” Wewe mbona upo hapa? Niliuliza kwa sauti Meshack alikuwa ananiangalia. Kwa akili zangu za kipumbavu nikaamua kurudisha mashambulizi nilimvaa shafii na kumtandika busu la mdomoni. Kila aliekuwepo pale alibaki mdomo wazi kwa kushangaa saiyo Mimi sikuwa na jali nilifurahi kwakuwa Meshack na baadhi ya wanafunzi walidhuhudia kile nilichokifanya
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU