BIOLOGY TEACHER (02)

BIOLOGY TEACHER 2

Shafii aliduwaa akawa anashaa, hakutegemea Kama ningefanya vile. Niligeuka kuwaangalia watu waliokuwa wanatuangalia , Nilizuga kwa kusema
” Shafii nitakuona baada ya kumaliza kipindi Cha mazoezi, nimefurahi kukuona.
Niliondoka nikamuacha shafii akiwa bado kasimama palepale akiwa ananiangalia ninavyoondoka , Miriam alinifuata nyuma huku akisema
” Alice umefanya kitu gani Cha ajabu?
” Ajabu gani? Hata Mimi leo nimewaweza Meshack anafikiria Mimi siwezi kupata mwanaume , Sasa nimemuonyesha kuwa Nimepata mwanaume handsome kuliko yeye. Si unaemuona alivyoachwa mdomo wazi, hakutegemea Kama ningeweza kumsahau na kuanzisha mahusiano mengine.
” Unajua yule uliyemfanyia vile Ni Nani?
” Ndio niliwahi kukutana nae Yani Ni Kama rafiki yangu anaitwa shafii.
” Kwahiyo Ni Kama mpenzi wako?
” Nimekwambia rafiki wa kawaida anaitwa Shafii
” Unachojua wewe anaitwa shafii tu.
” Unauliza Maswali gani ya kijinga? Hapa nilipo moyo wangu upo kwatu hayo Mambo mengine sijali kabisa.
“Ngoja nikueleze , hiyo unaemuita shafii Ni mwalimu mpya wa biology.

Nilishituka nikashikwa na kigugumizi nikawa namuangalia Miriam usoni. Baada ya sekunde chache nikasema
” Wewe Ni mwalimu tangia lini?
” Wiki Ile uliyoumwa na kuchwa ukaomba ruhusa ndio siku tuliyotambulishwa na akaingia darasani kutufundisha.
” Mungu yangu , nimesha yavuruga kumbe ndio maana watu walikuwa wananiangalia Sana?
” Ndio.
” Sasa nitafanyaje?
” Unatakiwa kumfuata na kuomba msamaha.
” Nimeshaanza kuona aibu nitanzaje?
” Anza Kama vile ulivyoonza kumbusu… Majibu ya Miriam yalinikatisha tamaa . Siku hiyo sikuwa na hamu ya kufanya mazoezi kabisa, nilienda kukaa jukwaani nikiwa na mawazo , nilipoangalia uwanjani nilimuona shafii akicheza Mpira wa kikapu pamoja na wanafunzi wa kiume. Habari zilianza kusikika kila sehemu kuwa nilimbusu Mwl Shafii

Kesho yake asubuhi kipindi Cha kwanzakilikuwa Ni kipindi Cha biology mwl shafii aliingia darasani, nilipomuona moyo wangu ulishituka Sana hasa pale tulipo kutanisha macho niliangalia chini kwa aibu.

Mwl alianza kufundisha lakini kila muda alikuwa akiniangalia, hii Hali ilinifanya nishindwe kabisa kuelewa kile alichokufundisha. Kipindi kilipoisha alitoka, nilitoka nikamfuata
” Samahani mwalimu naomba tuongee. Shafii aliangalia saa yake ya mkononi alafu akasema
” Huu Ni muda wa vipindi , itapendeza Kama tutaongea muda wa mapumziko. Nikirudi darasani kila mtu alikuwa ananiangalia maana taarifa zilisambaa kuwa Mwalimu shafii Ni mpenzi wangu. Wengine walisema Nina bahati kupata mwanaume handsome Kama shafii, wengine walisikika wakisema vina muda Basi. Yani ilikuwa tafrani kila mtu alisema lake . Nilichokuwa naogopa ni yale maneno kufika uongozi wa juu, maana ingeweza kuniletea matatizo.
Muda wa mapumziko ilipofika nilienda kusimama karibia na ofisi ya walimu kwaajili ya kumsubiri mwl shafii, baada ya dakika Kama kumi kupita shafii alitoka akasimama mlangoni Aliponiona alianza kutembea kuelekea uwanja wa Mpira na Mimi nikaanza kumfuata Nyuma. Alisimama kwenye chuma Cha goli na Mimi nikaenda kusimama pembeni yake. Shafii alinikazia macho mpaka nikaona aibu nikaangalia chini.
” Nakusikiliza missAlice.
” Mmm samahani kwa kile kilichotokea jana… Kabla sijamaliza kuongea Shafii alicheka Alafu akasema
“Nimesha kusamehe lakini unaweza kuniambia sababu ya kufanya vile? Shafii aliuliza huku akiwa anazidisha umakini wa kuniangalia, niliendekea kujiinamia huku nikibonyeza vidole vyangu vya mikono.
” Miss Alice unaweza kuniambia?
” Mwalimu Sina sababu ya maana
” Kwahiyo ulipata mihemko baada ya kuniona?
” Hapana mwalimu naomba tu unisamehe.
” Sawa kuwa makini hapa Ni shule haipendezi tukionekana kwenye Hali Kama ile, hizi taarifa endapo zingefika kwa uongozi wa shule tungekuwa matatani, wakati mwingine Jaribu kuzuia mihemko yako.
” Sawa.
” Ok unaweza kwenda .

Niliondoka nilipofika mbele nikageuka nyuma kumuangalia , mwl shafii alikuwa kaegamia lile chuma huku akiwa ananiangalia. Nikamfuata Miriam ambae alikuwa amekaa darasani akinisubiri twende canteen kunywa chai. Nilifika na kukaa juu ya dawati.
” Vipi ,Nini kinaendelea, mwalimu kasemaje?
” Hajasema Chochote inaonekana hajali Sana kwa kile kilichotokea.
” Afadhali ,basi twende canteen.
Tulitoka darasani tukawa tunaelekea canteen Mara nikamuona mwl shafii anakuja mbele yetu.
” Miriam tugeuze sitaki kukutana na mwl shafii.
” Sasa Kama yaneisha unaogopa Nini?
” Naona aibu.
Tulibadili njia nyingine tukaenda zetu canteen.
” Sasa utamkumbua mpaka lini?
” Ni Leo tu najisikia aibu.

Kuanzia hapo nilikuwa namuogopa Sana mwl shafii hasa alipoingia darasani nilikuwa nakosa amani , Mara nyingi alikuwa ananiangalia Sana . Kutokana na Hali ya uwoga ilinipelekea kutokufanya vizuri kwenye somo lake. Kuna kipindi tulifanya test ya biology nilipata Alama mbaya. Mwalimu alipomaliza kugawa karatasi za mitihani akauliza
” Kuna mwenye tatizo?
Wapo waliotoa maoni yao na kuuliza maswali , mwalimu aliwajibu. Mimi sikuwa hata na ujasiri wa kuongea kitu. Watu walipomaliza kuuliza maswali mwalimu
alisogea mpaka kwenye dawati langu .
” Alice huna swali au maoni?
” Hapana sina. Mwalimu alichukua karatasi yangu iliyokuwa juu ya dawati akaiangalia alafu akasema
” Muda wa kutoka naomba unione.
” Sawa. Mwalimu shafii aliondoka na karatasi yangu ya mtihani.

Muda wa kutoka shule ilipofika nilibeba begi langu nikaelekea ofisini nilipofika mlangoni nilisita kidogo kuingia nikiwa nimesimama najishauri Mara Mwl shafii alisimama mlangoni akaniambia
” Ingia. Alitangulia na kwenda kukaa kwenye meza yake na Mimi niliingiwa na kusalimia baadhi ya walimu waliokuwepo ofisini alafu nikaenda kusimama pembeni ya meza yake.
” Vuta kile kiti ukae hapo. Nilivuta kiti na kuliweka vizuri Kisha nikakaa, mwl shafii alifungua karatasi za mitihani wangu akawa anaangalia jinsi nilivyojibu madudu.
” Alice Kuna tatizo linakusumbua?
” Hapana
” Hunielewi ninapokuwa nafundisha?
” Nakuelewa
” Sasa mbona umefanya madudu kwenye test? Nilikosa jibu la kumpa nilinyamaza kimnya
” Nahisi Kuna kitu kinaichanganya akili yako maana maendeleo yako ya nyuma yalikuwa mazuri na imekuwa ghafla Sana wewe kuvurunda.
” Nisamehe mwalimu nitafanya juhudi.
” Sawa shika hizi karatasi nenda kasome pia Kuna maswali nimeyaandaa unatakiwa kuyafanya.
” Sawa. Wakati nachukua zile karatasi mkono wangu na mkono wa mwl Shafii ukagusana , Kuna hisia nilihisi nikatulia kwa muda tukiwa tumegusana mikono nilipokuja kushituka nikamuangalie mwl Shafii usoni nikakuta nae ananiangalia nilitoa mkono wangu haraka Kisha nikachukua zile karatasi na mkono mwingine nikaondoka nilipokaribia mlangoni niligeuka nyuma nikakuta mwl ananiangalia. Nilitoka nje haraka nilipofika mbele nikajikuta natabasamu.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!