BIOLOGY TEACHER 3
Kila siku ilikuwa lazima nikutane na mwl Shafii kwaajili ya kuniuliza maswali ya kile alichofundisha darasani na kunipa maswali ya kufanya nyumbani ,hivyo ilikuwa lazima niwe makini kumsikiliza. Taratibu nilianza kusahau kile nilichokifanya sikuona aibu kuniangalia Kuna wakati alikuwa akinifundisha huku akitabasamu pia alimpenda Sana kuniangalia nilipokuwa naongea .
Jamani nisiwe muongo kwenye hili kila nilipokuwa namuona Mwl Shafii nilikuwa kachanganyikiwa juu yake. Shafii alikuwa mwanaume mwenye mvuto, alikuwa serious,ilipohitajika kutabasamu alitabasamu hata ilipobidi kucheka alicheka mpaka meno yake meupe yalionekana.
Siku ya ijumaa ilifika nilienda kubadili nguo Kisha nikaenda uwanjani nikasimama pembeni ya uwanja wa basketball huko nilikutana na wasichana wengine wakiwa wanasubiri kuangalia mechi iliyokuwa inachezwa na wanafunzi wa kidato Cha tano na chacsita pia Kuna walimu wa kiume Kama watatu waliungana kucheza nao , mmoja wapo alikuwa Mwl Shafii. Wasichana walipomuina anaingia uwanjani wakaanza kusema
” Muonebi jamani huyu Kaka anakonga nyoyo za wasichana wengi Sana . Alisema msichana mmoja na mwingine akasema
” Wasichana wengi wanaokuja hapa wanakuja kumuangalia yeye.
” Ni kweli Ila inaonekana hapendi kuona wasichana wakimshobokea …
” Sio hapendi anaogopa kujichanganya si unajua anatembea na Alice
” Hivi Kuna ukweli wowote kuhusu Alice na teacher Shafii.
” Ikasemekana hivyo si unaona Alice anavyo mfuatafuata
” Mmmh inawezekana hata nae anajipendekeza tu kwani mwalimu hajaona warembo zaidi yake mpaka amfuate yeye. Aliongea Rosana msichana anaejiona Ni mrembo kuliko wenzake pale shuleni. Niliwasikia walivyokuwa wanaongea ujinga waoalafu nikaguna kwa sauti wote wakageuka kuniangalia.
” Huo ni ufisi mtaendelea kuutapani mfupa lakini hamuupati ng’oo. Endelee Ni kumaliza wino kwa kuandika barua za kumtaka wakati mwenzenu anakazi ya kuzichana na kuwachukulia Kama mahayawani. Wote walinyamaza kimnya , niliondoka na kwenda kukaa sehemu nikawa nawaangalia wachezaji wanavyoingia uwanjani
Mwl Shafii Aliniona akaachia tabasamu la mbali na kunipungia mkono. Baada ya hapo mchezo ukaanza Mimi nikawa nashangilia timu ya mwl Shafii
Baada ya muda wa mechi kuisha tukiwa chumba Cha kubadili nguo nilimkuta miriam anatoka kucheza netball, nilimfuata .
” Kama kawaida yako umetukimbia ukaenda kuangalia mechi ya basketball.
” Mbona hiyo kawaida , Miriam hivi unamuonaje mwl Shafii?
” Namuona kawaida tu, kwani vipi?
” Sasa ndio umejibuje hivyo?
” Nijibu vizuri , Yani kwa mtazamo wako unamuonaje, maana wasichana wengi wanamuongelea.
” Ndio yeye ni mzuri, pia ufundishaji wake Ni mzuri Sana kifupi namuelewa Sana.
” Najua lakini sizungumzii ufundishaji wake namzungumzia muonekano wake.
” Ana muonekano mzuri nadhani Ni ndoto ya kila mwanamke kuwa na mwanaume Kama yeye. Jibu la miriam lilinifanya niachie tabasamu. Miriam aliniangalia alafu akasema
” Wewe Kuna kapepo la umalaya kanakutembelea? Umeanza kumtamani mwalimu? Ilinibidi nicheke kwanza
” Sijui nikwambiaje Yani nimevumilia lakini nimeshindwa najikuta Nina hisia nae Sana.
” Binti Jaribu kuzuia mihemko yako usije ukafanya Mambo ya ajabu Kama uliyofanya. Siku Ile.
” Siwezi kufanya hivyo , lakini unajua wasichana wengi huwa nlwansmuandikia barua za kumtaka kimapenzi.
” Wewe, umejuaje? Na isije ikawa wewe ndio umefanya hivyo
“Siwezi kufanya hivyo.
” Kama uliweza kumbusu mbele za watu hushindwi kumuandikia barua. Miriam aliniambia ikabidi nicheke
” Hamna bwana Ile ikitokea Kama bahati mbaya.
” Tuli badili nguo Kisha tukaondoka chumba Cha kubadili nguo.
Kesho yake ilikuwa siku ya Jumamosi nilikuwa nyumbani nafuafua nguo zangu na kufanya usafi wa chumba changu. Baada ya kumaliza kazi zangu nikaelekea sebleni nilipofika nilishituka mpaka nikashindwa kupiga hatua, sikuamini Kama nimemuona Mwl Shafii akiwa nyumbani kwetu Tena anapiga story na Kaka Bray. Bray Aliponiona akaniita
” Alice hebu njoo. Shafii aligeuka kuniangalia Aliponiona ni Kama alipatwa na mshituko.
” Shafii unamuona kamamaa? Bray alimwambia Mwl Shafii
” Khaaa Alice ndio kamamaa?
” Ndio amekuwa mama mkubwa sio kamamaa Tena.
” Mungu wangu , unajua siku zote namuona lakini sikuwahi kufikiria kuwa Ni yeye amebadilika sana
” Mmmh hebu kwanza huwa unamuona wapi? Aliuliza Kaka Bray huku akiwa ananiangalia Kisha akamuangalia Shafii
” Ni mwalimu wa biology. Nilidakia nikajibu
” Kumbe unafundisha shuleni kwao?
” Ndio nimejishikiza kwa muda.
” aiseee Safi Sana , Alice ukimuona huyu mtu jua umeniona Mimi ni rafiki yangu Sana tangia tulipokuwa watoto tumekulea pamoja ,Shafii ni Kaka yako. Nilitabasamu na kuitikia kwa kichwa. Baada ya hapo wakaanza kuongea story zao ikabidi niwaachie nikaenda kukaa nje
“. Daaah hiki Nini Sasa kila siku Mambo yanazidi kuharibika. Kwanza nilimbusu kumbe alikuwa mwalimu wangu. Alafu nikaanza kuwa na hisia nae Tena Leo Lina ibuka jibya eti Kaka yangu, Ila Kaka Bray yupo kwaajili ya kuniharibia tu mipango yangu.
Jumatatu nilipoenda shule Jambo la kwanza kumueleza Miriam Ni kuwa Mwl Shafii Ni rafiki wa Bray, Miriam alicheka Sana.
” Aisee una gundu ,kwanza uliachwa
na Meshack kwaajili ya hiyohiyo Kaka yako, Sasa amekuja kuvuruga matamanio yako ya kutaka kuwa na mwl Shafii.
” Nimechoka Sasa acha niwe single tu.
” Kweli kabisa maana ikiendelea kuhangaika utakutana na zito zaidi
Kuanzia siku hiyo ilimbidi nianze kumchukulia mwl shafii kana Kaka pia nae hakuwa akiniangalia kama alivyokuwa akiniangalia zamani. Safari hii alikuwa yupo makini Sana kunifuatilia kwenye masomo yangu na kila ninachokifanya pale shuleni nikajua lazima atakuwa kaambiwa na Kaka Bray awe ananifuatilia.
Baada ya miezi kupita Kuna Kaka mmoja alikuwa akinifuatilia Sana Kuna wakati alikuja Hadi shuleni, siku moja ilikuwa muda wa kutoka shule nikiwa nimeongozana na rafiki zangu Mara nikamuona Harry akiwa kasimama mbele ya gari lake akiwa anatuangalia. Nilipomuona nikawaambia wenzangu
” Jamani tangulieni nitawakuta mbele. Wenzangu waliondoka nikamfuara Harry
” Mambo vipi?
” Safi, Harry kwanini unanifuata mpaka huku, huoni Kama utanisababishia matatizo?
” Alice Leo nimeamua kuja kwaajili ya kupata jibu langu nimesubiri kwa muda Sasa .
” Kwahiyo umeshindwa kuvumilia?
” Ndio, nahisi siwezi kuvumilia zaidi.
” Harry nilishajwambia Mimi siwezi kuwa na wewe.
” Ysinifanyie hivyo Alice mwenzio nakupenda , hebu panda kwenye gari nikupe lift.
” Hapana nitaenda na wenzangu
” Achana nao , njoo upande nahitaji kuongea na wewe
Harry alienda kunifungulia mlango lakini kabla sijafanya maamuzi ya kupanda nikasikia naitwa
” Alice. Niligeuka kumuangalia aliyeniita , alikuwa Mwl Shafii aliwa kwenye pikipiki yake Tena aliniangalia kwa jicho la ukali. Mwl Shafii alishuka kwenye pikipiki akasogea karibu yetu akauliza .
” Unaenda nae wapi? Kabla sijajibu Harry alijibu
,”Khaaa kwani huyu Ni mtoto mpaka umchunge kiasi hicho? Hata Kama wewe Ni mwalimu mipaka yako Ni huko darasani huku nje anakuwa huru kwanza unajuaje huenda nikawa ndugu yake?
Mwl Shafii alimsukuma Harry na kumgandamiza kwenye gari
” Wewe mshenzi unasema Nini? Unajua Mimi Ni Nani kwake? Shafii alikuwa mkali Sana sikuwahi kumuona akiwa hivyo.
” Nakupa onyo usije ukarudia kumfutafuta huyu msichana nitakuja kukurarua hiyo sura yako. Baada ya hapo alimuachia akanishika mkono na kunivuta ilipo pikipiki yake akapanda alafu akaniamuru nipande. Nilipanda tukaanza safari mpaka tulipofika kwenye nyumba moja alisimamisha pikipiki
” Hapa Ni wapi? Niliuliza
” Hapa ndipo ninapoishi
” Sasa kwanini nipo hapa?
” Kuna kitu nimefuata, muda sio mrefu nitakupeleka nyumbani kwenu .
Tulishuka kwenye pikipiki akanikaribisha ndani nikaingia na kwenda kukaa sebleni kwenye Kochi. Nikaanza kushangaa nyumba ilikuwa nzuri pia ndani kilikuwa kizuri vitu vyake vilipangiliwa vizuri Sana , harufu nzuri kifupi kilikuwa kunavutia Sana .
” Unatumia kinywaji gani? Aliniuliza mwl Shafii
” Hapana nipo sawa. Nilikata lakini Mwl shafii hakukubaliana na Mimi alienda kwenye Fiji akatoa box la juice na grass akaja kunitengea.
” Endelea kujihudumia.
” Asante.
Nilimshukuru alafu nikamimina juice kwenye grass nikaanza kunywa kidogo kidogo huku nikiangaza macho kuangalia kila Kona ya Ile seble. Mara simu ya mwl Shafii ilikuwa mezani ikaanza kuita. Baada ya muda mchache alitoka chumbani akiwa kajifunga taulo kiunoni kifua kikiwa wazi na mwili wake ulikuwa na majimaji ilionekana Kama alitoka kuoga. Alichukua simu yake akaipokea ,wakati huo akili yangu ilivurugika kabisa nilikuwa namuangalia jinsi alivyokuwa na kifua kizuri. Alirudi chumbani kwake akiwa anaongea na simu huku Mimi nilibaki nikijisemea
” Mungu wangu huu mbona mtego Sasa,mbona anataka kufufua hisia ambazo zilianza kupotea na kumchukulia Kama Kaka Leo hii anaanza kuzirudisha nyuma na kuamsha hisia zangu. Ilibidi nitulie na kumlaani shetani .
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU