BIOLOGY TEACHER (07)

BIOLOGY TEACHER 7


Nilikubaliana na ushauri wa Miriam kwa kumridhisha tu kwani haikuwa rahisi kusahau kilichotokea .
Siku zilienda lakini nilikuwa naona aibu Sana kumuangalia Mwl Shafii nae hakuwa abajali Yani ilikuwa Kama vile hakikutokea kitu Kati yetu. Mazowea yaliisha kabisa nikawa siendi kufundishwa nae hakuwa akiniita , watu walianza maneno ya chini chini walisema nimeachwa. Siku moja nilikuwa naenda kantini nikakutana na kikundi Cha wasichana kana wanne walipomuina wakaanza kuniongelra Tena kwa sauti ili nisikie.
” Kwisha habari yake kafunuliwa Sasa ameachwa ona anavyokonda kwa stress za kuachwa. Hilo neno liliniuma Sana ukizingatia Ni kweli nililala bae na kuachwa baada ya siku chache . Sikuwa hata na nguvu za kujibishana nao niliwapita nikaenda kantiini nikaenda kukaa sehemu aliyokaa Miriam.
” Vipi mbona hivyo , unekutana Tena na shafii?
” Hapana Ila watu wanamuongelea vibaya nashindwa hata kujitetea nabaki kuumia.
” Ni Nani huyo aliekuwa anakusema?
” Kundi la wakina Sara.
” Wajinga wale ngoja niwafuate… Miriam alitaka kunyanyuka nikamzuia
” Haina haha ya kupigisgana nao kelele. Tuliemdekea kula tulipomaliza tukawa tunaelekea darasani , tulipokuwa njiani Miriam alisimama alafu akaniambia
” Tangulia darasani nakuja.
” Unaenda wapi?
” Nimekwambia tangulia darasani nakuja. Niliekejea darasani nae akarudi nyuma Kama vile alikuwa anarudi kantiini.

Niliingiwa darasani nikawa nimejiinamia ghafla nikahisi Kama mtu Kaja kukaa pembeni yangu, nilinyanyuka kichwa nikamuangalie . Alikuwa Ni Meshack sikuamini kumuona karibu yangu maana tangu tulivyoachana sijawahi kuongea nae tukapishana tu. Meshack alinisalimia
” Mambo
” Safi
” Vipi mbona umejiinamia?
” Nimeamua…
” Mmm baada ya masomo tunaweza kukaa sehemu tuongee?
” Kuna kipi Cha kuongea Kati yetu? Nilimuuliza kwa sauti ya upole.
” Kipo, najua haupo sawa kwa kile nilichokisikia lazima utakuwa na maumivu…..
” Unaongea kuhusu Nini wewe? Hapo nilikuwa mkali kidogo maana niliona tunakoendea sio kuzuri.
” Mbona unakuwa mkali wakati Mimi sijaja hapa kwa ubaya?
” Naomba utoke naona umekuja kunidhihaki Kama hao wengine wanao jukumu bila kujua chochote? Niliongea kwa sauti darasa zima wakasikia. Muda huo huo aliingia Mwl Shafii akiwa kaongozana na Miriam. Meshack alinyanyuka akaenda kukaa sehemu yake akampaisha Miriam akae. Mwl shafii aliangalia upande nilipokuwa nimekaa Kisha akasema.
” Tafadhali naomba tusikilizane. Kila mtu alitulia na kumsikiliza alichokuwa anataka kuongea.
“Kuna habari nasikia zunaongelea chini chini kunihusu Mimi na Alice…. Niliposikia jina langu nilishituka na mapigo ya moyo yakaanza kwenda mbio.
” Sara pamoja na kundi lako mnaongoza kwa hiyo tabia, Mimi siwezi kufanya upumbavu huo mnaisema , Mimi Ni mwl na Kama mlezi wenu hapa hata Kama mnaona Kama tunalingana kwa kuniangalia .Naomba niheshimiwe kana mnavyoheshimu walimu wengine , haya maneno yakiendelea nitachukua hatua.
Baada ya kuongea hivyo aliondoka na darasa likatulia .
” Umefanya Nini? Nilimuuliza Miriam
” Nimependa kumwambia unayopitia, sipendi unavyokuwa huna Raha. Nilitabasamu Kisha Nika mshukuru
” Asante, ulianzaje kumuelezea?
” Nimemwambia kila kitu na jinsi unavyojihisi mnyonge.

Kauli ya Mwl Shafii kidogo ilimsaidia sikusikia watu wakiniongelea. Taratibu nilianza kumpotezea na kuendelea na masomo yangu na nilisema sitakiwi Tena kuingia kwenye mahusiano maana maumivu ya kuachwa yanaweza kunifanya nikawa chizi Ni Bora akili na nguvu zangu niwekeze kwenye masomo. Muda wa free nilikuwa nilienda maktaba kujisomea. Meshack akawa ananifuata fuata na kuomba tuwe tunasome pamoja, nilikuwa najaribu kumkwepa lakini kila alipomuona naelekea maktaba alinifuata na hata siku za ijumaa kwenye kipindi Cha michezo alikuwa alinifuata na kukaa na Mimi.
Siku moja tulipokuwa maktaba tunasoma akiniita jina langu nikamuangalie.
” Tunaweza tukarudisha penzi letu? Aliongea kwa sauti ya chini. Nilimuangalia kwa hasira maana sababu ya haya yote kutokea sababu alikuwa Ni yeye kuniacha .
” Shiiiii! Acha kupiga kelele. Nilimwambia na kuendelea kusoma , Meshack alishusha pumzi alafu akaendelea kufungua kitabu harakaharaka Kama mtu aliyekuwa anaangalia picha , alipofika mwisho alifunika na kukurudishia kwenye sherlf Kisha akatoka nje.

Meshack alikuwa akinusumbua Mara kwa Mara akiwa anaimba msamaha na kusema ilikuwa Ni hasira ya kudhalilishwa na Kaka Bray Ila amegundua ananipenda na hakuna mwanamke anaeweza kuwa nae zaidi yangu. Siku moja tulikuwa tumekaa chini ya mti, Kama kawaida yake akaanza kuomba msamaha.
” Alice wewe Ni mtu gani usiejua kusamehe, nionee huruma basi
” Lakini uliniambia ulikuwa unanitafutia sababu Sasa unataka Nini? Meshack Mimi sikutaki bwana
” Usinifanyie hivyo, unauumiza moyo wangu.
” Utaumia kwa muda lakini utapoa Kama ulivyokuwa kwangu. Kumbe wakati tunaongea Mwl Shafii alituona alikuja taratibu na kujibanza pembeni ya mtimwingine akawa anatuangalia, wakati huo sisi hatukumuona Meshack alikuwa ananibembekeza kuku akiwa kapiga magoti. Mara tukasikia mtu anakohowa tulishituka na kumgeukia sauti ilipotokea
” Unafanya Nini huku? Aliuliza Mwl Shafii.
” Tulikuwa tunafanya maswali. Alijibu Meshack huku akiwa anaokota daftari lililokuwa chini.
” Nendeni darasani. Tulinyanyuka tukawa tunaelekea darasani. Kabla hatujafika mbali Mwl Shafii akiniita, niligeuka na Kurudi aliposimama.
” Una tatizo gani?
” Sina tatizo lolote
” Meshack anataka Nini kwako?
” Hakuna anachokitaka
” Nimesikia mlichokuwa mnaongea , kwahiyo unataka kurudiana nae? Maswali ya Mwl Shafii yalikuwa yananishangaza
” sielewi unaongea nini maana sisi tulikuwa tunajisomea. Nilimjibu nae akashusha pumzi alafu akaniambia
” Nimesikia kila mlichokuwa mnaongea nilikuwa hapa muda mrefu.
” Kwahiyo ulikuwa unatufuatilia na kusikiliza tunachoongea?
” Nikufuatilie ili iweje, hebu nenda darasani. Nilipiga hatua chache akaniita, nilisimama nikageuka alipo
” Kuwa makini. Aliniambia hivyo nikajikuta nafyonza kimnya kimnya.
” Watu wengine bwana sijui wakoje, Sasa ananifuatilia ili iweje, wanafikiria wanaweza kunibana nisifanye ninachokitaka Mimi sio mtoto bwana.

Mwl Shafii aliendelea kunifuatilia kusiri Siri hasa aliponiona na wavulana alijitokeza mbele yangu. Siku moja nilikuwa naelekea maktaba nikakutana na Enock tukawa tumesimama tunaongea huku tunacheka ghafla tukashituka baada ya kusikia kitu kimeanguka, tulipoangalia ilinibidi nicheke kwanza maana nilishindwa kujizuia , alikuwa Mwl Shafii alijikwaa kwenye Dustbin na kutaka kuanguka ilikuwa bahati hakufika chini Ila dustbin ilianguka .
” Alice sio vizuri hutakuwi kucheka. Alisema Enock huku akimfuata Mwl Shafii na kumpa pole.
” Pole mwalimu.
” Aaaah usijal sijaumia. Alijibu Shafii huku alijiweka sawa. Alipo kuangalia alijikuta nacheka .
” Mnafanya Nini hapa, wakati huu Ni muda wa darasani?
” Darasani kwetu hatuna kipindi tulikuwa tunaelekea maktaba. Alijibu Enock
” Sasa mbona mlikuwa mmesimama hapa?
” Kuna hii karatasi ya maswali nilikuwa namuonyesha Alice. Mwl Shafii alichukua Ile karatasi akaiangalia .
” Kama hamtojali naweza kuwafundisha.
” Itakuwa vizuri Sana mwalimu.
” Enock Mimi naenda maktaba. Nilimwambia Enock
” Kwanini tusiungane pamoja maana hata wewe ulisema Kuna baadhi ya maswali huyawezi.
Nilikubaliana na Enock tukaenda kukaa sehemu na Mwl shafii akaanza kutufundisha. Kila alipomaliza kutuelekeza shwali moja aliita jina langu na kusema
” Alice umeelewa? Yani alinikazania Kama vile alikuwa akinifundisha peke yangu mpaka Kuna wakati Enock akawa ananiangalia , na Mimi nikajizima data nikawa majibundio alafu nakuuliza Enock
” Mimi nimeelewa , vipi Enock umeelewa? Enock alijibu ndio . Tuliemdekea kufundishwa safari hii Mwl Shafii hakuuliza kwa kutaka jina langu alisema mmeelewa?

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!