BIOLOGY TEACHER 8
Mwl Shafii hakuacha kuwa ananifuatilia . Siku my ja tukiwa kantiini nilikuwa nakunywa juice Mara alikuja Jose kwenye meza niliyokuwa nimekaa na Miriam .
” Vipi warembo mko poa?
” Tuko poa.
” Naweza kuungana na nyie hapa?
” Karibu. Jose alivuta kiti akakaa na kuweka vahasha ya kaki mezani Kisha akafungua na kutoa vipande viwili vya keki aka kutugaia.
” Mmmh Leo ni kama miujiza umewaza Nini mpaka ukaamua kuja kutupa ofa? Miriam alimwambia Jose na kumfanya Jose acheke
” Kwani haiwezekani Mimi kuwapa ofa warembo Kama nyie?
” Basi tunashukuru.
” Msijali furahieni. Alisema Jose na muda huohuo alinyanyuka akawaaacha na kwenda kuungana na Mwl Shafii. Alikaa wakawa wanaongea huku wakiangalia tulipo, miriam akasema
” Kuna kitu nahisi.
” Kitu gani?
” Hizi keki haujanunua Jose kanunua Mwl Shafii.
” Umejuaje?
” Nakufahamu vizuri jose Ni bahiri sana karibia wanawake zake wote wamemuacha kwaajili ya ubahiri wake.
” Huwezi jua huenda leo imekuwa bahati yetu.
” Mmmh sizani husua zangu zinahisi kuwa Mwl Shafii ndio kanunua Jose kaagiziwa tu atuletee.
” Mimi sijui hilo ninachojua tumepewa na Jose.
” Lakini uliniambia kuwa huwa anakufuatilia.
” Ndio Mara nyingi huwa namuona ananifuatilia.
” Kwahiyo mpaka hapo huekewi Nini kinaendelea?
” Na ewe usinichanganye bwana unataka kusema nini?
” Mwl Shafii anamuonea wivu Ni wazi kuwa anakupenda.
” Mmmmh hakuna kitu Kama hicho labda awe na Jambo lake lingine.
” Kama lipi?
” Miriam tuachane na hayo sitaki kuuongelea habari za Shafii.
Likifika kipindi Cha kufanya mitihani kwaajili ya kufunga shule wanafunzi walikuwa bize na kujisomea. Siku moja nikiwa darasani najisomea alikuja mwanafunzi mmoja kuniita
” Alice unaitwa na Mwl Shafii, yupo kule uwanja wa Mpira.
” Sawa. Nilifunika vitabu vyangu Kisha nikawa natoka mlangoni nilikutana na Miriam.
” Unaitwa na Mwl Shafii.
” Ananiita Nini?
” Sijui, nenda kamsikilize. Nilitoka nikaenda kuwanjani nikamuona Shafii akiwa kakaa jukwaani. Nilienda karibu nikasimama karibu yake.
” Nimeambiwa unaniita.
” Ndio kaa hapa. Akinionyeshea sehemu ya kukaa , nilikaa pembeni yake.
” Alice yule aliekuleta na gari asubuhi alikuwa Ni Nani? Nilishangaaa maana sikutegemea Kama Kuna mtu aliniona wakati ninashuka kwenye gari ambalo nilikuwa nimepewa lift.
” Ni jirani yetu, alinipa lift baada ya kuchelewa kuja shule.
” Ni kweli?
” Huniamini? Muulize Bray atakwambia Bosco Ni Nani. Alafu nakuomba usiwe unanifuatilia mnanifanya nijusikie vibaya nimeshakuwa mkubwa nipeni Uhuru wa kujisimamia mwenyewe.
” Najua lakini Kaka yako amenipa jukumu la kujuangalia ….
” Achana na akili za Bray ananiona mtoto lakini wewe unatambua kuwa Mimi Ni mkubwa. Mwl Shafii alitulia kwa muda alafu akasema
” Najua tupo tofauti Sana na Bray , ukweli Ni kwamba sijisikii vizuri ninapokuona umesimama au ukiwa karibu na mwanaume.
” Kwahiyo unamaanisha kuwa unanionea wivu ndio maana unanifuatilia kusiri Siri?
” Aaaah hebu tuachane na hayo , Ila tambua kuwa sijisikii vizuri. Aliongea Mwl Shafii wote tukatulia kimnya kwa muda , nilitamani kuendelea kuuliza maswali lakini nilihisi kila kitu kipo wazi japokuwa hakifunguka.
” Mimi naenda.
” Sawa. Niliondoka nikamuacha akiwa amekaa. Nilifika darasani nikawa nafikiria yake maneno alivyiniambia, Miriam aliniongelesha lakini sikusikia.
” Wewe unawaza nini?
” Miriam unajua sikuelewi kabisa Mwl Shafii.
” Kafanya Nini Tena?
” Kumbe bado ananifuatilia, leo nilipewa lift na Bosco alinileta mpaka shule kumbe wakati nashuka Shafii aliniona kwahiyo ndio alikuwa ameniita ananiuliza . Miriam alitabasamu alafu akasema
” Eeeeh
” Alafu anasema aliniona na mwanaume anajusikia vibaya.
” Hahahaha Mambo yameshakuwa mambo .
” Unamaanisha Nini unaposema hivyo?
” Nini huelewi Alice,wewe si unajiita mtu mzima?
” Sitaki kujiaminisha hicho unachofikilia
” Lakini umegunfua kuwa anakupenda?
” Sitaki kufikiria hivyo, huenda Ni tamaa you zinamfanya awe vile , sitaki Tena kujisababishia maumivu.
” Sawa acha tuone itakavyo kuwa.
Tulimaluza mitihani ikafika siku ya kufunga shule , siku hiyo wanafunzi tulikuwa tumekaa vikundi vikundi tukipiga story Mara nikasikia naitwa na Mwl Shafii , nilimfuata na kumsikiliza alichoniitia.
” Alice kabla haujaenda nyumbani naomba tuonane, tafadhali usiondoke bila kufanya hivyo. Aliongea Shafii kwa upole Tena alisisitiza Sana.
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU