BIOLOGY TEACHER 11
Nilimngangania Shafii mpaka akanuambua
” Inatosha Alice hapa sio salama
” Acha uwoga bwana hakuna atakaetoka saizi.
” Hapana tunatakiwa kuwa makini tusije tukakutwa kesho njoo nyumbani.
Nilinyanyuka nikaenda kukaa kwenye kiti huku nikiwa nimejinunisha
” Ndio umenikasirikia? Aliuliza sikumjibu , alinishika mkono akasema
” Mpenzi naomba uniangalie .nilinyanyuka macho nikamuangalie
” Unataka kila watu wajue kinachoendelea Kati yetu ikiwa wewe Ni mwanafunzi isitoshe unamfahamu vizuri Kaka yako, au unataka kunisababishia matatizo?
” Hapana mpenzi Ila najikuta natamani Sana kuwa karibu na wewe.
” Najua Ila unajua sehemu ya sisi kuwa huru tukajiachia na kufanya Mambo yetu.
” Sawa nimekuelewa.
” Alice.
” Abeee
” Nakupenda mama
” Nakupenda pia.
” Asante, Sasa muda umeenda nenda kapumzike tutaonana kesho.
“Sawa. Tuliachana Shafii akaenda chumbani kwa Bray na Mimi nilazima taa na kwenda chumbani kwangu.
Kadri siku zilivyokuwa zinazidi kwenda ndivyo penzi langu na shafii liluvyozidi kupamba Moto, alinithamini na kumuonyesha upendo wa Hali ya juu ,sikujutia kumfahamu huyu Kaka alijifanya nijione Ni msichana special Sana kwake.
Hatimae tulifungua shule masomo yakawa yanaendelea, safari hii nilikuwa makini Sana nilijitahidi kumdhibiti hisia zangu sikutaka mtu yoyote ajue mahusiano yangu na shafii zaidi ya rafiki yangu Miriam. Shafii alikuwa anawivu Sana hakutaka kuona naongizana na mwanaume Wala kuwa kawa na ukaribu nao, hivyo nilijitahidi Sana kuwaepuka ili kuepusha ugomvi Kati yetu.
Mara kwa Mara nilikuwa nilitoka shule naenda nyumbani kwake alafu ndio naenda nyumbani. Siku ya Jumamosi tulitoka na shafii akaenda kunifanyia shopping ya vitu vyangu baada ya kumaliza tulirudi nyumbani kwake nikaingia jikoni kwenda kuandaa juice nilipomaliza nilimpelekea Shafii sebleni.
” Najua una kiu Sana karibu juice.
” Asante mke wangu. Wakati narudi jikoni Shafii alinivuta mkono nikaangukia mapajani kwake.
” Nini Sasa jamani?
” Unaenda wapi unaniacha peke yangu?
” Naenda kukupikia mpenzi.
” Mmmmh hebu tutulie kwanza.
” Kwani huhisi njaa?
” Nikikuona njaa inaisha.
” Hahaha huo Sasa Ni uongo. Shafii alinivuta na kunitishia Kama anataka kuningata shingoni
” Jamani Shafii niache, niache bwana usifanye hivyo…. Tukiwa tunaendekea kugaragara pale kwenye Kochi Mara tukasikia mpango unagongwa. Tulitulia na kusikiliza
” Mmm Nani Tena huyo ananiharibia? Aliongea Shafii Kama analalamika
” Kwani ulikuwa inatetemeka kupata mgeni?
” Hapana , ninapokuwa na wewe huwa sipendi usumbufu kabisa.
” Sasa atakuwa Ni Nani? Wakati tunaendekea kuulizana maswali mlango uligongwa tena
” Sijui hebu nenda kafungue. Nilinyanyuka na kuelekea mlangoni lakini kabla aijafika Shafii aliniambia
” Hebu subiri kwanza. Alinyanyuka na kwenda kuchungulia dirishani . Baada ya kuchungulia alishituka akaja pale niliposimama
” Alice nenda haraka chumbani Ni Bray. Nilichanganyikiwa na kutaka kukimbilia jikoni Shafii alinidaka .
” Nenda chumbani. Nilikimbilia chumbani na kujifungia mlango ndipo Shafii akaenda kufungua Kaka Bray aliingia nikasikia wanaongea.
” Aisee bro ukiwa na Shem ndio huwa unajifunga hivi?
” Aaaaaa umejuaje Kuma Kuna shemeji yako humu ndani?
” Kwahiyo unataka kukataa wakati nimeona viatu pale nje. Nilishituka nikahisi nitagundulika lakini kwa bahati nzuri hajui vitu vyangu vyote. Walikaa sebleni wakawa wanaongea, Kaka Bray alikuwa amekazania anataka kumuona shemeji. Huko ndani nilikuwa nateyemeka mpaka jasho lilikuwa linatoka.
” Kwahiyo ndio hutaki nimjue Shem wangu?
” Sio hivyo hajisikii vizuri amepumzika.
” Hamna bwana uhautaki nimjue.
” Sio hivyo ndugu yangu Ila ipo siku nitakukutanisha nae.
” Poa bwana , nilikuwa napita maeneo haya nikaona sio mbaya nije kusalimia.
” Nashukuru Sana ndugu yangu na karibu Sana.
” Asante Ila nisiwe mkaaji ngoja nikuache upumzike na Shem. Shafii alikuwa anacheka tu. Muda huohuo Kaka Bray aliaga akaondoka. Alivyoondoka Shafii alifungua mlango na kuja chumbani akajikuta nimesimama aliniangalia Kisha akashusha pumzi.
” Vipi ametushitukia?
” Hapana Ila ilibakia kidogo Sana kungekutwa sijui ingekuwaje na jinsi Kaka yako alivyokuwa mtata. Nilimsogelea Shafii nikaiweka mikono yangu mabegani kwake nae aka shika kiuno changu.
” Achana nae kwani hajui Kama akiwa na dada shemeji akosekani. Shafii aliachia tabasamu akaninyanyua na kunipelekea kitandani
Siku zilizidi kusogea na ilibakia miezi 3 tufanye mtihani wa kumaliza kidato Cha sita, hivyo tulikuwa bize Sana kujisomea. Tukipanga ratiba ya Miriam kuja nyumbani kujisomea Mwl Shafii akawa anatufundisha. Kuna wakati nilienda kulala nyumbani kwakina miriam tukawa tunajisomea usiku. Nilitumiwa hiyo nafasi kwenda kulala kwa Shafii huku familia yangu ikiwa unajua nipo kwakina miriam najisomea.
Ulipita mwezi mmoja nikawa sijielewielewi nilikuwa mvivu nilipoenda Sana kulala nilishindwa hata kuamka mapema kwaajili ya kwenda shule ilikuwa mpaka niamshwe na mpaka niamke ilikuwa kwa shida Sana , kila siku nilikuwa nikigombana na mama kuhusu swala la kulala Sana.
” Yani unaamshwa kwa faida yako lakini unatuvutia mdomo, Yani wewe sijui siku hizi imekuwaje? Hayo ndio yalikuwa maneno ya mama sikumjibu nilienda kujiandaa huku nimekasirika. Siku moja nikiwa shule nilimwambia Miriam jinsi ninavyojisikia Miriam akashituka
” Wewe mwezi uliyopita umeona siku zako? Swali la Miriam lilifanya kengere ya hatari ilie kichwani kwangu maana sikuwaza kabisa Kama zinaweza kuwa dalili za ujauzito.
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU