BIOLOGY TEACHER 12
Nilizubaa hukuvnikiwa nimeishiwa nguvu.
” Wewe , unaweza kuniambia Mara ya mwisho kuona siku zako Ni lini?
” Mwezi uliyopita sijaona, hivi Ni kweli naweza kuwa Nina ujauzito?
” Hizo Ni dalili tu lakini unatakiwa kupima ili kuthibitisha.
” Mungu wangu naogopa Sana, hivi itakuwaje Kama nitakuwa Nina mimba ?
” Pima kwanza ndio ufikirie hayo. Jioni wakati natoka shule nilitembea barabarani nikiwa na mawazo Mara nilishituliwa na honi ya pikipiki alikuwa ni Shafii.
” Panda twende.
” Wapi?
” Kwani wewe unaenda wapi?
” Nyumbani.
” Sawa panda twende. Nilipanda kwenye pikipiki tukawa njiani nilikuwa kimnya.
” Baby vipi mbona Leo upo kimnya hivyo?
” Nimechoka sijisikii kuongea.
” Masomo ndio yamekuchosha hivyo?
” Hapana Ila mwili wangu umechokachoka tu.
” Pole. Sikumjibu pole yake nilikaa kimnya mpaka nilipofika nyumbani nilishika kwenye pikipiki na kutaka kuingia ndani.
” Alice. Shafii aliniita nikageuka
” Mbona hatuagani? Nilirudi mpaka alipo nikambia
” Samahani sipo sawa.
” Niambie mpenzi unajisikiaje?
” Ni mwili unaniuma
” Huenda utakuwa na homa, niangalie mpaka kesho Kama Hali itakuwa hivyohivyo inabidi uendo hospital .
” Sawa, lakini nilikuwa ninashida na pesa kidogo.
” Kiasi gani?
” Elfu kumi tu. Shafii alitoa wallet yake mfukoni akatoa pesa na kunipatia. Kabla sikapokea niliuliza
” Mbona unanipa pesa nyingi wakati Mimi nimeomba elfu kumi.
” Elfu Ina uwingi gani? Shika utatumia kwa Mambo yako mengine. Nilizipokea na kumshukuru.
” Asante
” Usijali Ni jukumu langu, nenda kapumzike nilifika nyumbani nitakutafuta.
Nilipofungua ndani nilibadili nguo alafu nikatoka nikaenda kwenye duka moja la dawa ambalo lipo karibu na nyumbani nikanunua vipimo viwili vya mimba nikavificha vizuri Kisha nikarudi nyumbani . Nilifika chumbani nikakaa kitandani nikawa najishauri kupima . Niliviangalia vipimo huku nikijiuliza
” Kwahiyo Kama nitakuwa mjamzito itakuwaje, nitakwambia Nini wazazi wangu na nilimwambia Shafii atalipokeaje ? Nikijiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu. Niliweka vipimo pembeni alafu nikajikaza kwanza na usingizi ukanipitia nilikuja kushitukia na mlio wa simu Shafii alikuwa ananipigia
“
Niliamka na kupokea
” Vipi mpenzi mbona nimepiga Sana simu , nimemtuma Sana messege lakini hujibu?
” Nilipitiwa na usingizi
” Pole kwa kukusumbua, bado unajisikia vibaya.
” Hapana , Nina nafuu kidogo nimetumia dawa za kutuliza maumivu.
” Sawa ngoja nikuache upumzike. Baada ya kukata simu niliiweja kitandani nikachukua vipimo vyangu vya upt nikaenda chooni nikaiweka kipimo kwenye kikopo Cha mkojo Kisha nikakaa dakika chache nikatoa. Mungu wangu nilichokiona kilizidi kuvuruga akili yangu ilitoka mistari miwili. Niliweka mikono yangu kichwani na kujisemea
” Nimekwisha Alice Mimi. Mwili wote ulikuwa wamoto Raha zote nilizokuwa nilipata kutoka kwa Shafii ziligeuka kuwa shubiri.
Nilitoka chooni nikaenda kujifungia chumbani kwangu kutokana na mawazo nilishindwa hata kula chakula Cha usiku, nilizima simu sikutaka usumbufu wa aina yoyote.
Kesho yake nilipofika shule nilimuonyesha Miriam kile kipimo. Miriam alipoona alishituka na kuniangalia usoni.
” Miriam nimekumbuka mwenzio hapa unaponiona nimechanganyikiwa .
” Kuchanganyikiwa haita saidia kitu chochote unatakiwa kujua unafanya Nini kutatua hili tatizo, Mwl Shafii umemwambia?
” Hapana naogopa hata kumwambia.
” Sasa unaogopa nini wakati ndio muhanga mwenzio?
” Nitaanzia wapi kumueleza , na akinikataa je?
” Mmmh hapo ndio mtihani inapoanzia Ila namshauri umwambie.
” Sawa lakini sio kwa Sasa natakiwa kujipanga.
Zilipiga siku tatu nikiwa Sina furaha , nilikuwa namkwepa Sana Shafii hata aliponiuliza Nina shida gani sikuwa na jibu sahihi la kumpa. Siku moja wakati tunatoka shule nilimfuata nikakwambia
” Unaenda nyumbani kwako?
” Ndio lakini Kuna sehemu napitia kwanza.
” Utakaa Sana huko?
” Hapana
” Basi naomba funguo utanikuta kwako. Shafii alitoa funguo akanipatia, tuliporuhusiwa nikaenda moja kwa moja. Nyumbani kwake. Nilijitupa kwenye Kochi nikapitiwa na usingizi. Nilikuja kushitukia na shafii alikuwa akigonga mlango.
” Ina maana nimechelewa Sana mpaka umepitiwa na usingizi.aliongea Shafii huku akinishika kiuno tukaenda kukaa kwenye Kochi.
” Niambie mumy mbona siku hizi upo hivyo?
” Nipoje?
” Sikuelewi , sijui unaninunia, huna Raha kabisa.
” Huenda Ni mabadiliko ya mwili.
” Mwili umefanyaje Tena? Shafii aliuliza sikumjibu. Akasogea karibu na kusema
” Nilimiss lips zako, nipe japo busu kidogo. Alisogea na kutaka kunibuss nikamzuia
” Sio Sasa Shafii….
” Kwanini unanizuia ?
” Kuna Jambo nataka tuongee.
” Jambo gani bwana hebu nope kidogo… Shafii alichukua Kama utani
” Acha utani Shafii hili Jambo Ni serious . Shafii alitulia akamuangalia usoni kwa muda alafu akauliza
” Ni Jambo gani hilo? Nilivuta begi langu na kutoa kile kipimo Cha mimba nikampatia , Shafii alikipokea na kumuangalia Mara mbili mbili Kisha akamuangalia usoni.
” Wewe ndio umepima ? Niliitikia kwa kichwa , alishusha pumzi na kuliweka pembeni Kisha akasimama huku akiwa anakuja kichwa kana vile kachanganyikiwa. Namimi nilisimama nikamuuliza
” Unaenda wapi Sasa?
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU