BIOLOGY TEACHER 13
Shafii hakujibu swali langualiendekea kujizungusha hapo alizidi kunichanganya nikakaa chini nikaanza kulia Shafii alipoona nalia alikuja kunibembeleza
” Basi mumy usilie.
” Kwanini nisikie wakati naona kabisa unaenda kunikana huu Ni mzigo wangu najuta… Kabla sijamaliza kuongea Shafii aliniziba mdomo.
” Sitaki kusikia Hilo neno najuta hili Ni tatizo langu pia na siwezi kukutekekeza mwenyewe kwenye hili.
” Sasa tutafanyaje na vipi Kaka Bray akijua? Shafii alivuta pumzi ndefu Kisha akashusha akaniangalia Kisha akanifuata machozi
” Huna haja yakulia na Wala hatuna haja ya kuwafikiria wengine maana hili limeshatokea .
” Kwahiyo tunafanyaje, au niitoe? Nilivyosema hivyo Shafii aliniangalia huku akiwa kakunja uso.
” Kwahiyo unataka kuuwa?
” Lakini mimba bado ndogo.
” Hata Kama huwezi kufanya huo ukatili, kwanza unajua madhara ya kutoa mimba? Shafii aliongea kwa ukali mpaka nikaogopa.
” Alice usijaribu kutoa mimba yangu Ila Kuna Jambo nataka tuongee na ulifanyie kazi kwa kipindi hiki mpaka utakapo maliza mitihani yako .
” Jambo gani? Niliuliza huku nikiwa makini kusikiliza.
” Naomba usimwambie mtu kana wewe Ni mjamzito mpaka utakapomaliza mitihani yako ,baada ya hapo tutajua Nini Cha kufanya .
” Kwahiyo umekubali hii mimba? Niliuliza kana kwamba sijaelewa msimamo wa shafii
” Ndio hiyo Ni mimba yangu na wewe Ni mwanamke wangu, siwezi kukuacha kwenye hili na upendo wangu hautabadilika pia nitakabiliana kwa lolote litakalokuja mbele yangu kikubwa watu wa sijui kwaajili ya kunilinda so unajua wewe Ni mwanafunzi?
” Ndio nakuahidi kukulinda.
” Asante Sana mpenzi wangu. Sikutegemea Kama Jambo litaisha kirahisi hivyo, Basi tukapanga mipango yetu vizuri baada ya hapo Shafii aliniambia ameniletea chipsi zipo kwenye mfuko. Nilizichukua nikaiweka kwenye sahani tukala pamoja huku tukifurahia Kama zamani.
Shafii alikuwa ananijali Sana na kila siku alinisisituza kujificha japo Kuna baadhi ya vitu vilikuwa vinasnda tofauti nilikuwa mtu mwenye kisirani Sana nikigombana nae Mara kwa Mara hata Kama mtu mwingine akinikera hasira zote nilikuwa namalizia kwa Shafii nilikuwa namfokea Kama mtoto nae alikuwa ananivumilia .
Siku zilienda nikaifanya mtihani wangu wa mwisho nikawa nipo tu nyumbani , siku ambazo mama yupo nyumbani nilikuwa namkwepa ili asije kunigundua kana Nina ujauzito. Siku moja alimuuliza dada wa kazi
” Hivi Alice yupo kweli humu ndani?
” Ndio.
” Unajua Nina siku ya tatu sijakuona .
” Siku hizi muda mwingi anajifungia chumbani kwake.
” Kwahiyo kazi Ni kulala tu ndio maana ananenepa tu kwaajili ya uvivu kila muda kulala kwahiyo watu wakimaliza shule ndio wanakuwa hawana kazi za kufanya Ni kulala tu.
Mama alikuja chumbani akajikuta nimelala pembeni yangu kulikuwa na kisahani ambacho ndani yake kulikuwa na vipande viwili vya ndimu na udongo.
Mama aliniamsha kwa kunitingusha
” Wewe Alice hebu amka. Niliamka kivivu nikakaa.
” Wewe una matatizo gani mpaka una lala ovyo Kama chatu aliemeza mbuzi? Nilivuta uso wangu kwa kiganja Cha mkono alafu nikamuangalie mama ambae alikuwa anekazia macho kwenye kile kisahani Cha udongo. Mama alikinyanyua na kuushika udongo na kipande Cha ndimu alafu akauliza
” Alice hii Ni nini? Niliingiwa na hofu sikujua nimjibu Nini
” Wewe nakuuliza hiki ni Nini?
” Mmmm
” Unaitika Nini, haujasikia au haujaelewa? Nilipiga magoti na kusema
” Nisamehe mama
” Nikusamehe kwa kosa gani ulilonifanyia? Machozi yalianza kunitoka
” Alice una mimba? Mama alivyomuuliza Hilo swali alisababisha nizidishe kulia.
” Nyamaza mjinga wewe unamchulia Nani? Au unafikiri Mimi nitaogipa haya machozi yako. Niambie hiyo mimba umeiokota wapi?
” Ilikuwa bahati mbaya mama nisamehe.
Mama alikuwa Kama kachanganyikiwa
” Kwahiyo Ni kweli una mimba Alice? Mama aliuliza nikaitikia kwa kichwa.
” Alice, Alice unafikiri baba yako akijua atakufanyaje?
” Nisaidie mama.
” Nakusaidiaje Sasa? Alice mwanangu hebu niambie ukweli hiyo mimba niya Nani? Nilikaa kimnya niliogopa kumtaka Shafii niliogopa asije akapata matatizo.
” Utaniambia au nikamuite baba yako ?
” Hapana mama nitakwambia lakini naomba usimwambie baba Wala Kaka Bray.
” Sawa niambie.
” Ni…
” Ni Nini, hebu usinipotezee muda na Sasa Sina muda wa kukubembekeza . Nilisua sua kumtaja muhusika ndipo mama aliposhikwa na hasira na kunipiga vibao vya mgongoni. Nilishindwa kuvumilia nikamtaja
” Mama nakwambia.
” Sema haraka . Mama alifoka kwa sauti kubwa
” Ni shafii …. Mama alininasa kibao na kufanya nipige kelele . Kumbe baba alisikia akawa anakuja chumbani kwangu alipofika mlangoni akasikia mama anasema
” Kwahiyo kulindwa kote Kyle umeishia kubeba mimba.
” Nani ana mimba? Aliuliza baba huku akiwa anatusogelea tulipo.
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU