BIOLOGY TEACHER 14
Mimi na mama tulimgeukia baba .
” Mama Bray Nani ana mimba? Kabla mama hajajibu aliona ule udongo akaniangalia usoni
” Alice umeamua kunivua nguo, umeamua kushusha heshima yangu, umeamua kunidhalilisha?
” Nisameheni baba . Baba alikasirika Sana mpaka macho yake yakawa mekundu kwa hasira, mama alivyoona vile alimuomba baba watoke wajaongee.
” Mama Alice niache nataka kuongea na alice
” Una hasira mume wangu huwezi kuongea ukiwa kwenye Hali hiyo, tafadhali naomba tutoke. Mama alimshika baba mkono wakatoka nje ya chumba changu.
Nilikuwa nalia sielewi Nini Cha kufanya nikasikia baba akisema
” Siwezi kukaa na mtoto mpumbavu Yani hafikirii nimempoteza pesa kiasi gani kwaajili ya kukusomesha leo hii anakuja kunilipa hivi.
” Sasa mtoto ataenda wapi ?
” Kesho anaenda kijijini.
Nilichukua simu nikampigia simu Shafii.
” Wameshajua Kama Nina mimba wanataka kunipelekea kijijini….. Nilishindwa kuendelea kuongea nikawa nalia.
” Alice naomba usilie …… Kabla Shafii hajamaliza kuongea Kaka Bray aliingia akachukua simu yangu na kunipiga chini ikavunjika vipande vipande Kisha akanisogelea na kunikunja
” Wewe mshenzi utaniambia huyo mshenzi mwenzio aliekupa mimba.
” Kaka Bray niache. Bray alininasa kibao nikapiga kelelempaka kila mtu alisikia Mara mama na baba walifika na kuniamulia nilipopata upenyo nilitoka mbio bila hata kuvaa viatu. Nilienda mpaka nyumbani kwa Shafii.
Nilipomuona Shafii nikaanza kulia , alinimbembeleza tukaingia ndani.
” Basi usilie.
” Shafii nitafanya Nini , sijui hatma ya maisha yangu, baba anataka kunipelekea kijijini Mimi siwezi kwenda kuishi kijijini Tena nikiwa na Hali Kama hii.
” Usijali hatma ya maisha yako Ni Mimi nitafanya kila niwezavyo kumhakikishia unaishi vizuri. Utakula na kulala vizuri pia nitahakikisha inakuwa salama wewe na mtoto wetu.
Baada ya kunibembeleza Shafii alinipeleka bafuni nikaoga Kisha nikarudi chumbani kupumzika yeye akaenda kuandaa chakula. Sikuwa na hamu hata ya kula kutokana na hekaheka nilizopitia siku nzima.
” Alice acha kunifanyia hivyo bwana hiki chakula nimeandaa kwaajili yako naomba ule hata kidogo.
” Sijisikii kabisa kula.
” Najua lakini jitahidi. Shafii alichukua chakula na kunilisha , nilikupa kidogo nikaacha. Nikasimama nikamuacha
” Naenda kulala.
” Sawa nakuja Sasa hivi. Shafii nae alishindwa kula alitoa viombo akampeleka jikoni Kisha akaja chumbani na kujikaza pembeni yangu , Shafii alikuwa ananiangalia kwa jicho la huruma alinivuta na kunilaza kifuani kwake.
” Pole kwa yote yaliyokupata Ila Nina Imani kila kitu kitakuwa sawa.
” Shafii
” Naaam
” Nashukuru Sana kwa kunijali na kujionyesha upendo wa Hali ya juu. Shafii alinibusu kwenye paji la uso Kisha akasema
” Nakupenda mke wangu.
” Nakupenda pia.
Hatimae usingizi ulitupitia nilikuja kushitukia asubuhi nikamuona Shafii akiwa anajiandaa kwaajili ya kwenda kazini
Alipoona nimeamka alinifuata pale kitandani akanibusu
” Habari za asubuhi
” Salama
” Umeamkaje?
” Salama vipi wewe.
” Niko poa.
” Ndio unataka kwenda kazini?
” Ndio Ila nitawahi kurudi, na kifungua kinywa nimeshakuandalia. Nilitabasamu alafu nikasema
“Asante.
“Ok badae kidogo.
” Uwe na kazi njema. Shafii aliondoka nikaenda kufunga mlango alafu nikarudi kulala.
Ilipofika majira ya saa tano nikaenda kuoga nilipomaliza nikawa nakula huku nikiwa naangalia tamthilia ili kupunguza mawazo. Mara nikahisi Kama Kuna watu wanagombana nje nilipunguza sauti ya TV ili nisikilize vizuri nikahisi Kama sauti ya Kaka Bray. Nilinyanyuka na kwenda kuchungulia dirishani nikamuona Bray akiwa akamsukuma Shafii nilitoka haraka na kwenda kumkinga Shafii.
” Kaka Bray muache
” Alice toka mbele yangu nimuafabishe huyu mshenzi, Yani uaminifu wangu kwako ndio ukaamua kumfanyia uhuni mdogo wangu kwani hukuona wanawake wengine mpaka mdogo wangu?
” Bray huku limeshatokea unatakiwa ukubali matokeo kuwa Mimi ni shemeji Yako.
” Wewe mpemvavu unaongea ujinga gani, Alafu unajua nitakupasua. Kaka Bray aliongea kwa hasira Sana huku akimfuata shafii ampige nilisimama mbele ya shafii
” Kaka kabla haujampasua shafii nipasue Mimi kwanza. Kaka Bray alinisukuma wakashikana na shafii na kuanza kupigana bahati watu walifika na kuamua ugomvi walinichukua Kaka Bray wakawa wanaondoka nae , Kaka Bray alijuwa anasema
” Bado hatujamalizana nitakula sahani moja na wewe nitahakikisha unalipia ulichokifanya.
Nilimsogelea shafii nikamwambia
” Achana nae twende ndani. Shafii aliokota mifuko miwili iliyokuwa imedomdoka chini tukaingia ndani nikahakikisha nimefunga mlango vizuri maana sikuwa na amani Bray angeweza Kurudi.
” Vipi hajakuumiza? Nilimuuliza Shafii huku nikiwa namuangalia usoni nikaona amevimba kwenye paji la uso.
” Sijaumia Sana .
” Mbona hapa pamevimba?
” Aliniwahi akanipiga kichwa
” Pole.
” Usijali nipo sawa.
Baada ya kutulia kidogo Shafii alinitolea nguo alizokuwa kaninunulia pamoja na simu nikamshukuru. Nilikumbuka kumpigia Edna dada wa kazi na kumuuliza kinachoendelea huko nyumbani . Edna aliniambia baba kawa mkali kama mbogo amesema atafanya awezavyo kumuadabisha Shafii ikiwezrkana atamshitaki kwa kumpa mimba mwanafunzi Alafu atanichukua na kunipelekea kijijini nikijifunze jinsi maisha yalivyo kwasababu nimekiuka maadili. Nilimshukuru Sana Edna nikamwambia aniamvie chochote kinachoendelea pale nyumbani. Baada ya kukata simu nilimwambia Shafii.
” Shafii baba anataka akufungulie kesi na Mimi anataka kunipeleka kijijini. Shafii aliniangalia bila kunijibu
” Shafii ongea chochote basi.
” Niongee Nini Sasa?
” Lakini unamjua baba vizuri atafanya kile alichokiahidi na Mimi sitaki kukuona ulipata matatizo Wala sipendi kutengana na wewe.
” Tutafanya Nini Sasa?
” Unaonaje tukaondoka tukaenda mbali na hapa?
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU