BIOLOGY TEACHER 15
Shafii alifikiria kidogo alafu akamuuliza
” Mbali na hapa wapi?
” Popote pale hata Kama Ni porini ilimradi Mimi na wewe tuwe na furaha, Shafii mpenzi wangu sitaki kukupoteza, sitaki kutengana na wewe, si ulisema utanipenda siku zote za maisha yako Basi kubali kwaajili ya maoenzi yako kwangu na mtoto wetu. Shafii alizidi kuniangalia Kisha akatoa tabasamu la mbali, kabla hajanijibu simu yake iliita aliyekuwa anampigia alikuwa Ni baba yake mzazi. Kwa mbali nilisikia sauti ya baba yake Shafii kwasababu simu ya Shafii ilikuwa na sauti.
” Shikamoo baba
” Marahaba, hivi hapo nyumbani kwako Kuna binti upo nae?
” Ndio baba.
” ghaaaa hivi una akili gani kijana wangu kwaninulishindwa kuona wasichana wengine mpaka ukamchukua binti ambae Ni mwanafunzi Tena umempa ujauzito na kumchukua kwa nguvu kwa wazazi wake.
” Sio kweli baba, huyu binti sio mwanafunzi ameshamakiza shule….
” Lakini bado anatakiwa kuendelea na masomo, nisikilize Shafii Hilo limeshakuwa tatizo na Mimi Kama mzazi sitaki kuona kijana wangu unaenda jela Sasa hivi unatakiwa ujiandae uondoke kwenye huu mji kabla Mambo hayaja haribika na huyo binti muache aende kwao. Shafii alishindwa kumjibu baba yake akawa ananiangalia wakati huo Mimi machozi yalikuwa yananitoka . Baba yake Shafii akaendelea kusema
” Nitakutumia kiasi Cha pesa kwenye account yako fanya haraka uondoke.
” Sawa baba. Alijibu Shafii Kisha akakata simu alafu akanyanyuka na kuelekea chumbani. Nilijikuta naishiwa nguvu nilishindwa kuongea chochote kiufupi nilihisi Kama dunia yote umejiinamia na walimwengu wananizomea nilishindwa kukaa kwenye Kochi nikasimama, kusimama haikufaa ikanibidi nikae chini ninyooshe miguu. Wakati nahangaika pale chini Shafii alitoka chumbani akiwa kabeba begi mkononi , aliniangalia akaniuliza vipi mbona upo hivyo? Sikumjibu machozi yalikuwa yanatoka tu. Shafii alichuchumaa akaniambia
” Unahofu kuwa nitakuacha uende ukapate shida na mwanangu?
” Baba yako kasema utuache. Hapo ndipo nilizidisha kilio Kama vile nimefiwa Shafii alinikumbatia akasema
” Siwezi kuvunja ahadi yangu Kama tulikuwa wote kwenye Raha siwezi kukuacha kwenye shida Nyanyuka tuondoke. Nilinyanyuka haraka haraka Shafii akabeba begi tukatafuta usafiri wa kutupeleka kwenye hotel moja iliyopo pembeni ya mji, siku hiyo tulipumzika hapo kesho yake tulisafiri tulienda mji mwingine huko pia tulifikia hotelini . Kesho yake Shafii alitafuta nyumba tukahamia na kuanza maisha tukiwa hapo.
Nilikunampigia simu Edna ananieleza Mambo yahatoendekea nyumbani, aliniambia kila siku mama alikuwa analia na kumlaumu juu ya Mimi kuondoka na kwenda kusikojulikana. Nilimuona huruma mama yangu lakini sikuwa na jinsi nilitakiwa kumsubiri mpaka Mambo yatakapokuwa sawa maana hakuna mzazi ambae atanichukua mtoto wake siku zote.
Kwa upande wa shafii wazazi wake walipojua ameondoka na Mimi waliacha kumpa msaada , haikuwa tatizo kwa Shafii alikuwa anahangaika kutafuta kazi pia alikuwa na pesa kidogo za kutusogeza kimaisha.
Siku zilikuwa zinazidi kwenda ujauzito wangu ulikuwa vizuri lakini kwa upande wa maisha yetu Hali ilikuwa mbaya Shafii alijitahidi Sana kutafuta kazi lakini ilikuwa ngumu Sana kupata mpaka akaamua kuweka vyeti vyake pembeni na kuanza kufanyakazi yoyote itakayokuja m bele yake ilimladi tupate hela ya kula na kulipa Kodi. Kuna siku alikosa kazi na Kurudi nyumbani mikono mitupu hivyo tulipazimika kunywa maji na kulala. Hii Hali ilikuwa ilimuuniza Sana Shafii alikuwa Ananiambia
” Nisamehe Sana mke wangu kwa kukutesa , haikustahili kuishi haya maisha…..
” Shiiiii ! Usisene hivyo mume wangu najua kile unachopitia, uwepo wako kwangu Ni faraja tosha. Shafii alijilazimisha kutabasamu lakini ni wazi alikuwa anaumia Sana moyoni mwake. Kuna siku alirudi mida ya mchana akiwa kashika mua mkononi, alijikuta nimejilaza kibarazani alikuja na kukaa pembeni yangu Kisha akashusha pumzi, nilinyanyuka na kumuuliza
” Vipi mbona umechoka hivyo?
” Acha tu mke wangu Hali ni mbaya Sana Yani tangia asubuhi sijapata hata Mia zaidi ya kupata huu mua nikaamua nikuletee upunguze njaa si unajua mpo wawili.
” Usijali mume wangu ipo siku utapata. Shafii alinyanyuka akaingia ndani kwenda kuchukua kisu na sahani , alirudi akaanza kumenya ule mua na kukatakata vipande vidogo vidogo akaweka kwenye sahani alipomaliza alinisogezea.
” Kula mama.
” Tule wote. Shafii alikuwa akipata chochote kidogo alikuwa ananiletea na Mimi sikuweza kula mwenyewe hata Kama Ni matonge mawili ilikuwa lazima tule pamoja.
Tukiwa tunaendekea kula miwa yetu alikuja Kaka mmoja ambae sikuwa namfahamu Ila ilionekana wanafahamiana na shafii. yule Kaka alisalimia Kisha akasema
” Shafii Kuna kazi ya kubeba matofari. Shafii alinyanyuka haraka akanibusu kwenye paji la uso alafu akasema
” Wife acha niende nikatafute rizki tutaonana badae.
” Sawa kazi njema.
Shafii na mwenzake waliondoka haraka kuwahi hiyo kazi. Nilimkuwa namuangalia Shafii na kunionea huruma Kaka wa watu haikustahili kupitia haya, hakuzowea kuishi maisha ya shida Kama haya lakini kwa sababu yangu leo Shafii anabeba tofali ,anafanya kazi za saidia fundi na Ni mtu mwenye elimu yake. Nilimuona Sana Mungu atusanehe kwa makosa tulifanya na amfungulie rizki Shafii wangu.
Jioni shafii alirudi akiwa kabeba mfuko mdogo nilimpokea Kisha nikamuandalia maji ya kuoga. Alipotoka kuoga alivaa nguo zake Safi.
” Alice mbona haujafungua mfuko nilioleta?
” Aaaah nimejisahau. Nilitaka kunyanyuka kwenda kuangalia kilicholetwa Shafii akanizuia
” Pumzika tu mke wangu nitaandaa . Shafii alifungua ule mfuko akatoa chungwa moja, ndizi moja na mwisho alitoa mfuko mwepesi wa plastiki ambao ndani yake kulikuwa na wali maharage. Alimimina kwenye sahani na kusogeza tule. Daaah Shafii huyu aliekuwa alinipa vitu vizuri leo hii analeta wali maharage wa kwa mama ntilie Tena kwenye mfuko nilijikuta naumia nilitamani kulia lakini nikajizuia sikutaka kumvunja moyo mume wangu.
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU