BIOLOGY TEACHER 16
Tuliendekea kula chakula , Shafii alikula kidogo akaacha.
” Vipi mbona umeacha na umekula kidogo?l
” Nimeshiba
” Umekula Nini mpaka useme umeshiba?
” Si nimekupa hapa, alafu mke wangu wewe unatakiwa ule ushibe si unajua mpo wawili?
Basi usiku Ile ilipita kulikucha salama tukaanza siku mpya
Nilitoka nje nikamkuta Shafii kajiinamia nilijua lazima kunakitu atakuwa anawaza nilifika mpaka pale lakini hakushituka mpaka nilipomshika begani ndipo aliponyanyua kichwa na kuniangalia.
” Vipi mbona umekuja kukaa huku alafu umejiinamia?
” Nawaza mengi mke wangu, unajua siku zako za kujifungua zinakaribia alafu Sina ramani yoyote ya kupata pesa na kazi imekuwa mgumu kupata.
” Ni kweli tuna maisha magumu lakini Mungu hawezi kututupa atatuonyesha njia ya kutokea kwenye hili. Shafii alitoa tabasamu hafifu Kisha akasema
” Unajua kunitia moyo mke wangu.
” Sasa nisipokuwa pamoja na wewe Nani mwingine wakiwa na wewe, wenyewe tunaelewana pamoja ya kuandamwa na shida .
” Ni kweli, nimeamini wewe ndio mwanamke niliyeumbiwa na Mungu pamoja na shida nilizonazo hujawahi kujionyesha tofauti yoyote na zaidi upendo inazidi kutawala , baada ya kuhangaika na kupigwa na jua kutwa nzima najua nihaporudi kwako unaniuliza kwenye mbawa zako za upendo nakupenda Sana Alice. Nilidoges na kujikaza begani kwa Shafii Kisha nikamwambia
” Najivunia Sana kukupata baba kijacho wangu. Basi tuliongea pale na kupeana maneno ya matunaini na kufarijiana.
Usiku tukiwa tumelala nilishituka na kukosa usingizi ikanibidi nikae na kuanza kufikiria nitapata wapi pesa kwaajili ya kununua vifaa vya kujifungua. Shafii aliniambia atafanya hayo yote lakini alikosa itakuwaje na siku za kujifungua zinakaribia , nikiwa naendelea kuwaza na kuwazua nilisikia Shafii alishusha pumzi kwa nguvu . Nikamuita na kumuuliza
” Vipi mbona umepumua kwa nguvu unatatizo gani? Shafii aligeukia upande wangu Kisha akasema
” Kumbe bado haujalala, mbona imekaa kwani unajisikiaje?
” Hamna kitu…. Shafii aliwasha taa akawa ananiangalia usoni kwa wasiwasi.
” Alice niambie mama umeanza kuumwa? Nilimuangalia nikaanza kucheka.
” Khaaa Sasa unacheka Nini wakati nakuuliza Jambo la maana?
” Nalkucheka jinsi ulivyokuwa na wasiwasi , Mimi nipo sawa.
” Sasa mbona imekaa?
” Sina usingizi alafu nimechoka kulala.
” Ahaaaa nilishituka nikajua ndio tayari Mambo yameiva na hapa nilipo Nina elfu kumi tu ya akiba. Ila usijali mke wangu kukikucha nitafanya mchakato wa kupata hela ili tununue vifaa vinavyohitajika.
” Hiyo hela utaipata wapi?
” Mimi Ni mwanaume nitajua kwa kuipata
” sawa lakini nilitaka kuwasiliana na mama nijaribu kuomba msaada wa pesa kidogo.
” Hapana , usije ukafanya hivyo Hilo swala niachie Mimi.
” Lakini nataka tusaidiane…… Kabla sijamaliza kujielezea Shafii alinikayisha
” Nimesema achana na hizo habari kila kitu kinachokuhusu wewe nitakusimamia Mimi usitake kufanya watu watuongelee vibaya.
” Sawa nimekuelewa.
Kesho yake jioni shafii alirudi akiwa kanunua kila kitu kwaajili ya kujifungua pia alikuja na vinguo vya mtoto.
” Mume wangu umepata wapi pesa za kununulia hivi vitu?
“Kwani Kuna ulazima wa wewe kujua mke wangu?
” Ndio Kama mkeo ni lazima nijue . Shafii hakuwa tayari kuniambia lakini nilimkazania aniambie.
” Shafii umeanza uwizi, niambie umeiba wapi hizo pesa .
” Khaaa kwahiyo unanichukia Mimi Ni mwizi.
” Sasa umetoa wapi pesa wakati haukuwa hata na Mia mbovu mfukoni ?
” Nimepewa na Aliya .
” Aliya? Si mwanamke huyo, inakuwaje unapewa pesa na wanawake kwahiyo umepata mwanamke tajiri kakuhonga alafu unaniletea mavitu yako nimesema sitaki vitu vyako hata mtoto wangu hawezi kuvaa hizo nguo za kuhongwa , hili beseni , sabuni, mafuta na haya sijui manini nitolee hapa sikaki kuona takataka ndani kwangu. Yani shida kidogo tu umeshindwa kuvumilia unaenda kuhongwa. Niliongea Shafii akawa ananiangalia tu.
” Unaniangalia Nini si unijibu.
” Kwani umemaliza kuongea?
” Nimeweka kituo.
“Mmmh, kwahiyo povu lite Hilo linakutoka sababu ya wivu au Nini?
” Unaona na hayo majibu yako ya kifedhuri Yani unaongea ongea tu bila hata kumfikiria unaongea na mtu ambae yupo kwenye Hali gani.
” Hebu nisikilize Basi.
” Ongea nakusikiliza.
” Hivi vitu nimepewa na aliy…….
” Ina Sasa unavyolotaja jina la mwanamke wako mbele yangu.
” Nipe nafasi Basi nijiekezee.
” Sema nakusikiliza lakini halahala usianze na Hilo jina maana niliposikia najisikia kichefuchefu naweza nikatapika na wakati tumboni hakuna kitu nimeshindia mihogo vipande viwili vya mihogo.
“Hivi unafikiri naweza kukusaliti?
” Yawezekana ndio umeanza hivyo.
” Siwezi kufanya hivyo. Hizo pesa nimetumiwa na mdogo wangu wa kike anaitwa Aliya. Yalinishuka nikawa namuangalia
” Sasa Mimi nitaabini vipi?
Shafii alitoa simu yake na kupiga simu Tena video call. Si ndio akapokea huyo Aliya akaanza kuongea nae pale. Nikasikia kwani unesharudi nyumbani? Shafii akajibu.
” Ndio. Shafii alisogea nilipo akanishika mabegani
” Umeniona wifi yako? Alimwambia mdogo wake na mdogo wake aliachia tabasamu na kunisamia
“Mambo wifi?
” Safi . Niliitikia huku nikiwa natabasamu maana nilikumbuka vibaya nikimuangalia Aliya na shafii walikuwa wanaofanana flani hivi.
” Jamani wifi yangu utakuja lini kututembelea?
” Nitakuja la aunty kangu kakizaliwa .
” Jamani karibu Sana. Tulipaliza kuongea Shafii akaenda kunilaza kitandani Mimi nikaanza kuokota vile vitu maana nilikuwa nimevitupatupa pale ndani. Nilipomaliza nikaenda kukaa kitandani na kuanza kujiongeleza
” Jamani sikujua Kama Ni wifi , hukuniambia Ila Nimefurahi kumfahamu. Nilishika kinguo Cha mtoto na bebishoo nikawa nasifia Shafii alinyamaza kimnya akawa ananiangalia Kama katuni.
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU