BIOLOGY TEACHER (17)

BIOLOGY TEACHER 17

Ilipita wiki moja tukiwa tunaendekea na maisha yetu ya kubangaiza yaliyojaa amani. Siku moja majira ya saa kumi jioni nilianza kuhisi tumbo linamkata na kuacha , kwa akili yangu finyu sikuwaza hata kumtafuta Shafii nilichofanya nilivutanguo nilizokuwa nimevaa nikajifunga kanga ya kifua na nyingine nikajifunika juu nikaenda kukaa nje. Nikiwa nimekaa pale nje nilihisi joto linazidi kiuno kinawaka Moto nikaamua kwenda kuoga nilipotoka ikawa nafuu kidogo, baada ya muda maumivu yakianzatena nikawa naenda bafuni kuoga. Nilitoka. Nakuwa na nafuu kidogo. Badae Yale maumivu hayakusikika maji Wala Nini tumbo lilikuwa kinauma mpaka nikahisi kurukwa na akili. Nikiwa nagaragara pale kibarazani alikuja mama mmoja jirani yangu akajikuta nagaragara .
” Alice vipi? Nilishindwa kumjibu niliendekea kuugulia maumivu hukuvnikiwa nimeshika tumbo. Alivyoniangalia akasema
” Mume wako Yuko wapi?
” Sijui alipo.
” Tunatakiwa kuwahi hospital, umeandaa vifaa?
” Ndio vipo pale pembeni ya kitanda. Yule mama aliingia ndani na kuchukua vifaa alipotoka akakuta imepasuka aliachia vile vitu alafu akanisogelea akaniambia nilale chini . Nilifanya Kama nilivyoambiwa alafu yeye akaanza kuita watu
” Mama neema, mama Sara njooni haraka. Wamama wslikusanyika wakawa wakajadiliana jinsi ya kunisaidia. Alikuja Bibi mmoja ambae Ni mkunga aliniangalia alafu akasema
” Mtoto anasogea, mwanangu jitahidi kumsukumaili umpate mtoto wako akiwa salama. Niliitikia kwa kichwa.
” Fuata kile ninachokwambia.
” Sawa .
” Futa pumzi ndefu alafu usukume. Yule Bibi alinipa maelekezo nikawa nafanya Kama alivyoniambia baada ya dakika 20 nilijifungua mtoto wa kike ambae alilia na alikuwa na afya nzuri tu. Baada ya hapo nilisafishwa na mtoto wangubaliwekwa vizuri baada ya hapo wamama wawili walitafuta usafiri wakanipeleka hospital kwaajili ya kuangalia Mimi na mtoto Kama tupo salama. Tulipokelewa nikaangalia Mimi na mtoto wote tulikuwa salama, muda uleule tuliruhusiwa tukarudi nyumbani. Shafii aliporudi alishituka baada ya kuona watu wapo nyumbani kwetu. Alifika karibu akasalimia kwa uwoga
” Habari za saizi!
” Salama
” Kuna usalama hapa?
” Salama.
Shafii alisimama akawa anashangaa shangaa.
” Karibu ndani.
” Asante. Aliingia ndani kwa uwoga akasogea mpaka kitandani akaona mtoto kalala pembeni yangu. Aliachana mdomo na machozi ya furaha yalimtoka.
Hakuamini kana angekuta nimejifungua alinisogelea Jaribu na kuliita jina langu.
” Alice. Nilimuangalia huku nilitabasamu.
” Umeniona mtoto wetu?
” Nimemuona , hongera.
” Asante Ni binti.
” Mbona hukunipigia simu?
” Sikuweza kabisa kwanza shukrani zote Ni kwa hao wamama wanenisaidia Sana Sina Cha kuwalipa .
” Ngoja nikawashukuru. Shafii alitoka nje na kutoa shukurani kwa majirani zangu walionisaidia Kisha akaulizia gharama za kunipeleka hospital lakini hakuna aliyekubali kulipwa.

Baada ya wageni kuondoka Shafii alikaa pembeni ya kitanda akawa anamuangalia mtoto wake.
” Siamini eti nimekuwa baba.
Baada ya siku mbili kupita niliamua kupiga simu kwa Edna na kuuliza kinachoendelea nyumbani, Edna aliniambia
” Alice unajua mama yako anawasiwasi Sana na wewe hebu mtafute umpunguzie wasiwasi maana kila siku anakutaja.
” Vipi baba na Kaka Bray?
” Sijawasikia wakiongea chochote kukuhusu Ila tambua sikubzote mama ndio anajua uchungu wa mtoto wake. Maneno ya edna yaliniingia kwani na Mimi nimeshakuwa mama na uchungu niliyoupata wakati wa kumpata hivyo nikapata moyo wa kumpigia mama. Nilipokata simu ya Edna nikiandika namba za mama ambazo nilikuwa nimezishika kichwani, nikibonyeza kitufe Cha kupiga simu iliita Kisha ikapokelewa
” Hallow. Mama alisema Mimi nikanyamaza kwanza mpaka mama alipoongea Tena ndipo na Mimi nikaongea.
” Mama…
” Alice mwanangu
” Ndio mama ni Mimi.
” Mwanangu upo wapi?
” Nipo sehemu salama mama na tayari nimejifungua nimepata mtoto wa kike. Mama alionyesha kufurahishwa Sana na hizo taarifa .
” Jamani mwanangu hongera sana, lakini Nani anakuhudumia huko?
” Usijali mama napata huduma nzuri tu Shafii ananihudumia vizuri Sana Mimi na mtoto.
” Kweli?
” Ndio mama.
” Vizuri.
” Mama naomba unisamehe kwa kilichotokea . Nimekusamehe mwanangu, hata hivyo natamani urudi nyumbani.
” Vipi baba bado Ana hasira na Mimi?
” Hajawahi kuongea chochote kukuhusu Ila Kama baba hawezi kukukataa.
” Sawa mama Ila naomba usimwambie baba chochote mpaka tutakapoweka Mambo sawa.
” Sawa mwanangu nimefurahi Sana kusikia kuwa upo sawa. Siku hiyo nilijusikia amani Sana kuongea na mama yangu.

Jioni shafii alirudi kutoka kwenye mihangaiko yake akiwa na furaha Sana alijikuta nambadilisha nguo mtoto alinishika mikono na kunitaka ninyanyuke , niliponyanyuka alinikumbatia kwa nguvu.
” Una Nini wewe, umekutwa na upepo gani leo?
” Kana Ni upepo basi nimepatwa na upepo mzuri, hivi ulisema mtoto wetu tumuite jina gani vile?
” Hatukupanga jina la kumpa ulisema tumsubiri kwanza.
” Basi jiba limepatikana huyu ni Nurat, Nuru iliyokuwa kuangaza kwenye maisha yetu baada ya kupata tabu kwa muda. Kuanzia leo wewe Ni mama Nurat.
” Sawa lakini inamaana gani kusema mtoto Ni nuru iliyokuja kuangaza maisha yetu?
” Baada ya mtoto kuzaliwa kila kitu kilikuwa chepesi kwetu na Sasa nimepata kazi nzuri yenye mshahara mzuri pia nimepostiwa nyumba nzuri kwaajili ya kwenda kuishi . Hizo taarifa zilimfurahisha Sana .
” Hongera mume wangu.
” Asante , pia nashukuru kwa kunivumilia kwenye magumu yote niliyokupitisha.
” Usijali hata hivyo nilikuwa na Imani Ni mapito ipo siku yangepita na siku zenyewe Ni hizi.
” Kweli kabisa binti yetu Kaja na baraka nimeamini ule msemo unaposema kila mtoto anakuja na sahani yake. Nurat mwanangu umekuja kufungua vifungo na kutoa kwenye shida tulizopitia

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!