BIOLOGY TEACHER 18
Baada ya siku mbili kupita tuliamia kwenye nyumba mpya na shafii alianza kazi, Baada ya mshahara wake wa kwanza Maisha yalianza kubadilika angalau tulikula hata Milo mitatu kwa siku Tena unaoeleweka. Siku me ja usiku tukiwa chumbani kwetu Shafii aliniambia
” Alice mke wangu natamani Sana kusawazisha haya Mambo nikiwa na maana kwamba nataka kuweka Mambo sawa. Natamani turudi mbele ya wazazi wako tukaombe msamaha kwa kilichotokea watuondolee kinyongo ikiwezekana tufunge ndoa tukiwa na haraka za wazazi wetu.
“Ulichoongea Ni sawa lakini sishauri kwasasa,kwanza natakiwa kuongea na mama ili atengeneze mazingira ya baba kutukubali na kutupokea maana baba analaumu kwa kupoteza pesa zake nyingi kunisomesha na nimeshindwa kufika pale alipotamani nifike.
” Hiyo isiwe shida mke wangu nitapambana , nitakesha kufanya kazi Kama punda ilimradi niendeleze pale ulipoishia utaenda chuo.
” Sio Sasa hivi mtoto wangu bado mdogo.
” Sijasemea kwa Sasa hivi kwasababu nahitaji kujipanga pia Nurat anahitaji ukaribu wako kama mama.
Usiku ule tukipanga Mambo mengi kuhusu maisha yetu na shafii alikuwa na mipango mingi ya kufungua miradi kwaajili ya kuniingizia kipato na Mimi nilikuwa nakwambia nitazidisha dua aweze kufanikiwa kwani kufanikiwa kwake Ni faida yangu pia.
Maisha yalisonga na kila kukicha Mambo yalikuwa yanaenda vizuri Shafii alikuwa anatujalibsana Mimi na mwanae alibeba majukumu yake na kuwa baba Bora. Nilianza kubadilika hata ngozi yangu ilikuwa na nuru tofauti na huko nyuma nilivaa nguo nzuri na kunifanya nionekane mrembo. Pia alinitafutia dada wa kazi kwaajili ya kunisaidia kazi ndogo ndogo za hapa nyumbani.
Baada ya miezi sita kupita Shafii alifungua supermarket akaweka wafanyakazi lakini alipotoka kazini alienda kuangalia biashara unavyoenda. Siku moja aliporudi kutoka kazini aliniambia
” Mke wangu nilikuwa natamani Sana usimamie Ile supermarket maana naona Kuna vitu vinaendekea ambavyo vitaharibu biashara yetu na kutufundisha nyuma.
” Vitu gani hivyo mume wangu?
” Nimeshuhudia mfanyakazi akiiba vitu.
” Kwani hawajui Kama umefinga camera?
” Wanajua sema wanatumia ujanja ili wasionekane. Leo nimemuona mmoja kachukua vitu na kwenda kuhufadhia kwenye Dustbin.
” Kheee
” Ndio hivyo
” Sasa umemuacha?
” Nimemfukuza kazi.
” Usijali mume wangu Nurat mwanangu hata sio msumbufu nitakuwa naenda kusimamia.
Basi tulikubaliana hivyo kesho yake asubuhi niliamka nikamuandalia mume wangu chai wakati huo alikuwa bafuni anaoga na Nu wangu alikuwa bado kalala. Nilipomaliza kuandaa nilienda chumbani kumuangalia shafii
” Jamani baba Nurat bado hujamaliza kujiandaa muda unaenda utachelewa kazini.
” Si wewe Umechelewa kuniamsha.
” Pole , lakini si unajua Nurat Jana usiku alikuwa anasumbua.
Nilimfuata na kuanza kumsaidia kufunga vifungo vya shati na kunivalisha tai Kisha nikaanza kumkagua Kama yupo sawa.
” Hapo sawa Sasa twende ukanywe chai.
” Baby nitaenda bila kuvaa viatu?
” Oooh unaina Sasa mnavyonichanganya wewe na mwanao. Nilienda kuchukua viatu nikamkuta kashakaa kwenye stuli ya dressing table nikamvalisha soksi Kisha viatu baada ya hapo tukaenda dinning room nikamimina chai alikunywa kidogo .
” Asante mke wangu.
” Mbona sijaona ulipokula?
” Nimechelewa mama watoto acha niwahi nitakula jioni nikirudi , tuliachana akaondoka na Mimi nikaenda kuandaa chakula Cha mwanangu na kukihudadhi vizuri Kisha nikaenda kuoga nikamuandaa na mwanangu tukaondoka kwenda kusimamia biashara yetu.
Nilikuwa makini kwenye kusimamia biashara , kutokana na uchangamfu wangu wateja wengi walinizowea Kuna baadhi tulikuwa tunataniana na kucheka .
Shafii alikuwa akitoka kazini anakuja tunskaa pamoja mpaka muda wa kufunga tunaondoka , siku moja walikuja wateja wawili wakiume wakaanza kunitania wakati huo Shafii alikuwa anazunguka anaangalia vitu vilivyopungua huku akiwa kambeba mtoto wake, kumbe kile kitendo Cha kutanisha na wale vijana hakupenda baada ya wake vijana kuondoka akanifuata na kuniambia
” Andaa vitu vyako tuondoke.
” Mbona leo tunaondoka mapema?
” Nimesema beba kilicho chako tuondoke. Alimuita mfanyakazi mmoja akamwambia
” Imma sisi tunaondoka muda wa kufunga ukifika mtafunga .
” Sawa boss. Baada ya kumpa Ima maagizo alitoka nje na Mimi niliandaa vitu vyangu Kisha nikatoka nilimkuta kapanda kwenye gari na Mimi nilipanda nikamchukua mtoto wangu, aliwasha gari na safari ya Kurudi nyumbani ikaanza. Njia nzima tulikuwa kimnya maana nilikuwa nikimuongelesha mwenzangu alikuwa hanijibu nikajua nimeshanuniwa na baba wivu nikaanza kumuongelesha mwanangu Kama vile ananielewa ninachoongea.
” Nurat mama baba yako katununia sijui tumemkosea Nini? Shafii akinikata jicho alafu akaangalia mbele na kuendelea kuendesha gari.
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU