BIOLOGY TEACHER (19)

BIOLOGY TEACHER 💖 19

Tulipofika nyumbani tuliingia ndani dada alimchukua Nurat Mimi nikamfuata Shafii chumbani.
” Mume wangu Kuna tatizo gani?
” Hujui tatizo Ni Nini?
” Ningejua nisinge uliza. Nilijifanya sielewi lakini nilikuwa najua sababu ya kununiwa Ni Nini maana namjua vizuri Sana mume wangu kwa wivu
” Hivi unajisikiaje unavyokuwa unataniana na wanaume wengine mbele yangu au unafikiri moyo wangu niwa chuma siumiii? Nilitamani kucheka Ila nilijizuia Sana maana ningecheka ningenuniwa mwezi mzima.
” Kamamaa mume wangu kwani ninkitu gani Cha ajabu nilichokuwa naongea nao so ilikuwa utani wa kawaida.
” Ghaaaa utani wa kawaida wa kumsifia mke wa mtu, eti mama Nurat inazidi kupendeza kila siku ,ona like jicho na wewe unajichekesha …
” Kwani kusifiwa Kuna shida gani….
” Ndio sitaki Sasa mke wangu usifiwe na wanaume, kwanza vijana wenyewe hivyo kabisa hawajiheshimu hata kidogo mwisho wa siku watakuja kukutongoza.

Mwanaume aliongea , alitema nyongo nikaona isiwe tabu nilimsogelea mume wangu nikakaa mapajani kwake nikamshika kidevu tukawa tunaangaliana
” Baba Nurat wangu naomba unisamehe hiki kitu hakitakuja kujitokeza tena.
“Mimi sipendi bwana, unajua kabisa nilovyokuwa na wivu na wewe.
” Najua mume wangu unanipenda na Mimi nakupenda Sana sitaki kukuuzi. Baada ya kumrembulia macho mwanaume akasema
” Nimekusamehe kuwa makini wewe Ni mke wa mtu.
” Sawa baby nimekuelewa. Tukakiss kila kitu kikaenda sawa baada ya hapo tuliingia bafuni tukaoga tulipomaliza tulienda sebleni kupata chakula Cha usiku.

Kuanzia siku hiyo nilikuwa makini Sana sikutaka kuniachia Sana hasa tulipokuwa wote dukani.

Baada ya mwaka mmoja kupita Nurat alikuwa kachangamka, shangazi yake Aliya alikuwa ksmaliza chuo alikuja tukawa tupo nae na Nurat alimzowea Sana shangazi yake. Shafii alinihangaikia nilipata chuo nikawa nasomea udaktari nilikuwa naenda chuo na Kurudi nyumbani nilisoma kwa amani nikiwa najua mwanangu yupo kwenye mikono salama. Mara nyingi Shafii alikuwa ananipeleka chuo na siku moja moja alikuwa anakuja kunichukua . Siku moja mvua ilikuwa imenyesha na hiyo siku aliniambia hataweza kuja kunichukua kunasehemu anaenda atachelewa kurudi. Basi bwana nikaamua Kurudi nyumbani kwa miguu ili niuoe mwili mazoezi. Wakati nipo njiani Kuna gari ilipita karibu yangu kwa Kasi na kunimwagia maji machafu
Ile gari ilipofika mbele ilisimama akashuka mama mmoja akanifuata
” Samahani dada, naomba unisamehe. Nilimuangalia kwa hasira maana nilikuwa nimevaa gauni ya shifoni yenye rangi ya right blue inayoonyesha madoa. Nilitoka kitambaa nikawa najifuta .
” Samahani sana….
” Usijali nilimjibu huku nikiwa naendelea kutembea yule Kaka alinifuata
” Samahani naweza kukupeleka unakoenda?
” Hapana .
” Tafadhali naomba ukubalie ombi langu. Kwakuwa nilikuwa nimechafuka Sana na ninakoenda Kuna umbali kidogo niliamua kukubali kupewa lift . Nilipanda kwenye gari nikamuelekeza ninakoelekea. Nilipofika karibu na nyumbani nikamwambia nishushe hapa. Sikutaka anifikishe nyumbani kwasababu niliogopa huenda nikamkuta baba Cha wivu. Basi alisimamisha gari nikashikwa na kumshukuru. Wakati naondoka si likanipita gari la Shafii na alikuwa akiniangalia kwa hasira. Yule Kaka alikuwa ananiaga lakini nilijifanya simsikii nikawa naenda nyumbani . Nilipofika nikamkuta Shafii kapaki gari yupo kibarazani ananisubiri . Aliponiona tu akaanza kuongea
” Kwahiyo umeamua kunidhihitishua kuwa huko mitaani sijui chuo una mabwana wenye magari nisipokuja kukuchukua utaketwa na mahawara zako.
” Shafii acha kunikosea heshima….
” Mwenyewe hujiheshimu alafu unataka watu tukuheshimu alafu mungubalivyoamua kujidhalilisha ulishukia mbali lakini nimekuona .
” Nisikilize mume wangu yule Kaka Mimi simjui amenipa lifti baada ya kunimwagia maji machafu unafikiri hivi ningekujaje huko barabarani?
” Shafii alishindwa kunielewa nikaamua kuingia ndani kuepusha kulele lakini alinifuata chumbani na kuendelea kunisema vibaya , nilishikwa na hasira nikajikuta nasema
” Sawa Ni mwanaume wangu…… Kabla sijamaliza kuongea lilipigwa vibao viwili vya haraka mpaka nikahisi masikio yameziba.
Nilikaa chini na kuanza kulia Shafii hakujali aliendelea kuongea ndipo nilipoamua kunyanyuka na kwenda kujifungia chumba Cha wageni . Aliya alikuja kunigongea ili tuongee lakini sikumfungulia .

Kesho yake baada ya Shafii kwenda kazini nilifungasha nguo zangu nikawa naondoka , Aliya aliponiona na begi aliniuliza
“Wifi unaenda wapi?
” Acha niende kwetu siwezi kukaa na mwanaume mwenye wivu kiasi hiki…
” Lakini mnatakiwa kuongea.
” Sitaki , nitaongea Nini wakati haniamini. Nipe mtoto wangu .
” Hapana huendi popote wifi. Nilipoona Aliya amemng’ang’ania Nurat niliamua kuondoka mwenyewe. Aliya alichukua simu akampigia Kaka yake na kumwambia kuwa nimeondoka nimependa nyumbani kwetu.

Jioni nilifika nyumbani nikawakuta baba na mama walishangaa kuniona maana sikutoa taarifa kuwa naenda lakini walinipokea vizuri .
” Karibu nyumbani mwanangu. Alisema baba
” Asante.
” Mjukuu wangu Yuko wapi?
” Nimemuacha..
” Kwanini umeache mtoto mdogo, umegombana na mwenzio? Niliwaekezea wazazi wangu kilichotokea mama akasema
” Mbona lilikuwa Ni Jambo la kuelewana umefanya hasira kuondoka na kumuacha mtoto.
” Unaongea Nini mama Bray Yani mtoto atukanwe , apigwe alafu useme amefanya haraka ?
Nikiwa bado naongea na wazazi wangu Shafii aliingia. Alisalimia mama akaitikia baba alimpokea kwa maneno
” Kijana umefuata Nini hapa?
” Samahani mzee wangu naomba tuongee.
” Tuongee Nini ikiwa kila siku imekuwa Ni mtu wa kunikosea tu, kwanza ulimpa mimba binti yangu, alafu ukamtorosha na Sasa umefanya ngoma ya kupiga kila unapojusikia. Baba akimfokea Sana Shafii mpaka nikaanza kunionea huruma.
” Kijana ondoka nyumbani kwangu , Kama mtoto wangu aneshindwa kuishi na wewe siwezi kulazimisha arudi kwako. Mlango uliingilia ndio huohuo utumike kutokea. Mama aliniangalia Kama vile ananaanisha niseme kitu maana anajua Shafii sio mkorofi hivyo.
” Baba Mimi nimemsanehe Shafii naomba usimfukuze.
” Haaaa wewe Tena uliekuja unajiliza Sasa unamtetea.
” Zilikuwa Ni hasira tu.

Baada ya kumtetea baba alikubali tukakaa chini tukaongea, pia Kaka Bray alifika wakamaliza tofauti na shafii na kuanza kuitana shemeji.
” Aisee wewe jamaa acha tu Yani umeulazimisha ushemeji mpaka umekolea. Bray alimwambia Shafii wakawa wanacheka.

Kesho yake jioni wazazi wa Shafii na wazazi wangu walikitana na kuuongelea swala letu pande zote mbili zilituhimiza tufunge ndoa. Kwakuwa dini zetu zilikuwa tofauti niliamua kubadili diniwazazi wangu walilidhia Hilo kwani Mungu Ni mmoja nakila mtu anamuomba kwa Imani yake. Basi siku ya tatu Mimi na shafii tulifungishwa ndoa ya haraka haraka kesho yake tukarudi nyumbani kwetu kuanza maisha mapya. Nashukuru Shafii alibadilika alipunguza wivu pia Mimi niliepuka Sana kufanya vitu vya kumuuzi.
Nurat aliondoka na shangazi yake akaenda kusalimia Bibi zake na Babu zake . Mama mkwe alimng’anga’nia Nurat akawa anaishi na Bibi yake.

Hatimae miaka ilienda nikakaribia kumaliza chuo mume wangu aliniomba nimzalie mtoto mwingine Basi tulifanya jitihada Mungu akasaidia nikabeba ujauzito nikimaliza chuo nikiwa na ujauzito wa miezi mitatu baada ya hapo nilikaa nyumbani nililea mimba yangu Shafii alinidekeza na kumuhudumia vizuri alisema
” Mimba ya Nurat ulipata shida Sana mke wangu acha hii nikutunze vyema mama watoto wangu.

Baada ya miezi 9 kutumia nilijifungua mtoto wa kiume mwenye afya Bora , Shafii alifurahi Sana, mtoto wetu tulimpa jina la Nasir. Familia yetu ilikuwa Ni familia yenye furaha na upendo mkubwa Sana .

MWISHO

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!