CHAGUO LA MOYO (01)

SEHEMU YA 1

Mpenzi msomaji Leo na kuletea kisa hiki Cha mapenz ambacho Kita kufunza mengi na kukusisimua,kukufurahisha, na kukuhuzunisha pia

Karibu tuende wote👇

Unaweza kuniita Sonia Arjun
Ni binti wa miaka 22 nilizaliwa mkoani songea,
Nikiwa na miaka 2 mama yangu alifariki hivyo nikabaki nikilelewa na Bibi yangu ambae nae alifariki nikiwa na miaka 10 baada ya bibi kufariki ndugu walikaa kikao ili kujadiliana Nani atakae nichukua na kuhusu huduma hasa shule.

Pacha wake mama (ma mdogo) alisema yeye atanichukua na atakuwa akinisomesha yeye mwenyewe ,
Kweli nilifurahi maana nilikuwa nampenda sana ma mdogo hivyo siku ya safari ilifika tukaondoka kuelekea mwanza ambako yalikuwa makazi yake,haikuwa Mara yangu ya kwanza kufika nyumban kwake kila Mara tulipokuwa tunafunga shule nilienda hivyo sikuwa mgeni kwenye familia yake,

Tulifika nyumban tukapokelewa na watoto wake pamoja namsichana wa kazi mamdogo aliniambia nikaoge Nile alafu nipumzike na mm nikatii na kufanya Kama alivyo niambia.

Kesho yake mchana alituita wote sebleni Kisha akaongea

“Nimewaita hapa ili kuwa mbia kuwa kwanzia leo Sonia atakuwa anakaa hapa na sisi”

Baada ya kusema hivyo mtoto wake wa kwanza(joy) aliongea

“Heee mama kweli ee nilikuwa nataka Nije kukuombea hilo hilo afadhali maana nampenda
Sana da Sonia”

“Aaaha! vizur sasa nataka muishi vizuri kwa upendo sawaee”alisema mamdoga

“Sawa mama”tuliitikia wote akaendelea kutuambia mambo mengine alipomaliza tulirudi kucheza,

Juma tatu walienda shule mm nikabaki nyumban na dada,jioni aliporudi kutoka kazi iliniita nakuniambia

Mwanangu naomba univumilie kidogo nikamilishe Mambo yako ili uweze kwenda shule sawaee “
Nikajibu “sawa “

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata