CHAGUO LA MOYO (04)

SEHEMU YA 04

Nilifikilia nikikamatwa wataninywa supu😔 Ila siko tayari kuendelea kukaa humu ndani……….nilizama kwenye dimbwi la mawazo mwisho nilistuka baada ya mama Anethi kunivutia ndani …..”hembu vaa hiyo nguo haraka bila hata kuongea niliingia nilikokuwa na lala nikavaa na kuchukua picha ya mama na ya bibi Kisha tukatika nduki mda wote mlinzi alikuwa nyuma ya nyumba akifua nguo zake hivyo alikuwa hajui kinachoendela ……. masikini sijui wakija na kukuta sipo atakuwa kwenye Hali gani Ila Sina jinsi😓……..niliacha baadhi ya vyakula jikon watajiju 😏…….. tuliingia kwenye gari na kuondoka Hadi stendi kuu ya mabasi …….tulifika akasimama na kuniambia…..”Sasa sikia unaenda dar es salaam huko utakuwa mfanya kazi wa ndani kuhusu mshahara ntaelewana wenyew, hakikisha unafanya kazi yako vizur na uwe na malengo najua maisha yako unayajua hivyo ukiharibu huko sitakuwa na msaada tena”…… “Asante sana mama kwa msaada wako” ……… usijali Mimi ni mama nimeshindwa kuona ukiumia kila siku……..hakikisha hauvui hicho kitambaa usoni wasije kukuona sawa…….sawa……alishtuka akanikatia ticket na Kisha akaongea na kinda ili alifika ampigie mwenyeji wangu…..niagana nae kwa machozi Kisha nikapanda na safari ikaanza …….na baada gari kutembea kwa mda mrefu hatimae tulifika dar watu walishuka na Mimi nikawa wamwisho nilisubiri mwenyeji wangu nilimkumbusha konda akasema kuwa bado hajafika nilikaa pale Hadi konda akaanza kufoka kuwa anachelewa sana hivyo ataondoka……..niliogopa na nikawaza vipi Kama hatokuja😓

Baada ya kusubiri lisaa hatimae alifika alikuwa ni mdada mmoja hivi mrefu mwembamba kiasi mweupe na alikuwa na nywele ndefu Hadi mgongoni ….niliwaza huyu ni mzungu au Ila hapana Hana sura ya kizungu labda kachanganya. ….hello dear sorry nimechelewa kulikuwa na na foleni Sana….. aliongea Yule dada……..haina shida shikamoo…nilijibu na kumuamkia……..acha zako Mimi sio mkubwa hivyo vo uko wap mzigo wako……. hapana Sina mzingo (sikuwa nimebeba nguo kutokana na nguo nilizokuwa nazo zilikuwa zimechakaa Sana hivyo nilichukua picha tu) nilivyomjibu hivyo hakutaka kuuliza maswali mengi zaidi tuliongozana Hadi kwenye gari safari ikaanza mada wote huo nilikuwa bado nimevaa nikabu ……
Inaitwa Nani(aliuliza)
“Naitwa Sonia”
“Oo! hongera unajina zuri mimi naitwa Nicole”
“Asante”
“Wewe ni mwarabu au mpemba au mhundi, usishangae nimeona rangi yako pamoja na macho yako walivyo ndio maana nimeuliza”……
“Ni mchanganyiko wa muhindi na mtanzania”……wow hatimae Rahul kapata mwenzake”…..
(😳 Rahul kapata mwenzake 🤔 Mungu wangu usikute naenda kuuzwa🥺)…….”Rahul nikaka yangu yeye baba yake ni muhindi ndio maana nasema kapata mwenzake so usihisi vibaya😊”……. (afadhali maana nilikuwa nimeanza kuwaza)
“So una miaka mingap”
“Nina 22”
“Wow mwezi wangap”.
“Wapili”
“Tarehe ngap”
(Huyu dada vp mbona maswali mengi)”tarehe 14″
😲😲 What so tunalingana namm nimezaliwa mwezi wapili tarehe hiyo hiyo wow nimeipenda hii🥰”
Nilitabasamu maan sikujua nijibu nn

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!