CHAGUO LA MOYO (07)

SEHEMU YA 07


“Nyie mtu Kama Askari wa motoni yaani akija tu kunakuwa na joto”aliongea Nicole

“Afadhali amenisaidia kuwanyoosha”…..mama mtu alijibu

“Amesaidia kutunyoosha?badala umuombee awe mtu was kwaida eti unafurahia, nakwambia usipoangalia atakufa single huyo maana hakuna mwanamke mwenye akili zake akaolewe na jitu Kama Hilo”…….. alijibu Nicole

“Nicole acha kumuita kaka yako jitu sawa”
“🙄Okay mamy sorry”
Aliinuka na kuondoka,……basi na wengine waliinuka nikabaki Mimi Rahul na johari, Sasa mda huo Johari akaanza kujichekesha pale

“So Sonia unajua kuongea kihindi”
“Hapana kaka”
“Okay nitakufundisha Kama ukipenda”

“Namm utanifundishae”aliongea Johari
“Ili uongee na Nani? Rahul aliuliza

“Jamani sininaongea na wewe “
“Tutaongea nn Mimi nawew ?”
“Kama tunavyoongea hapa “
“Sonia byee tutaonana baadae “
“Sawa kaka baadae”

Aliinuka na kuondoka basi Johari alibaki amevimba Kama andazi lililozidi amira 😏 niliamka nikaondoka akabaki amekaa pekee yake………..

Basi mida ya jioni wote walirudi kutoka kazini

Mimi mda huo nikiwa bz na kazi zangu

“Mamboo Nia”alinisalimia Lee
“Poa shikamoo kaka”
“Wewe ukijibu poa inatosha sijawa mzee kiasi hicho”
“Sawa kaka”

Akaondoka kuelekea chumbani kwake

Walipita wang, Salim. Nao wakanisalimia na kwenda chumbani kwao

Mara Rahul alirudi na kuja mahari nilipokuwa napasi

“Hi Sonia”
“Shikamoo kaka”
“Marahabaa hujambo😁”aliitkia na kucheka,

🤔Sasa kwann anacheka au nachekesha

“Aaaa nimekuletea zawadi hope utaipenda”

Nilipokea na kumshukuru
“Asante”
“Karibu”alijibu na kuondoka
Sasa nilifungua ilikuwa ni chocolate nilitabasamu na kufungua mdomo ili Nile alikuja Johari akanikwapua na kuiweka mdomoni kwake

😳😳
“Unashangaa Nini, sinilikwambia ukae mbali na mwanaume wangu”

🙄 Mwanaume wangu miguu yangu angekuwa mwanaume wako siangekuletea mwenyewe 😏(niliwaza hivyo)

“Kama hauta sikia nitakunyoo……kabla hajamaliza kuongea alipita uso wambuzi aka Berat na ukauzu wake akatupita shwaaa

Alitupita na Kama upepo bila hata salamu …………wote tukibaki 😦😦

“Yaani huyu kauzu utafikili bluce Lee sijui hata nani ataolewa na kauzu hivyo”

Aliongea Johari na kuondoka

Mda wakula ulifika wote tulikaa mezani mda huo hamna hata anae kohowa kila mtu kainama kwenye sahani yake ,……..Kama kawaida kauzu akawahi kumaliza na kuondoka yaani aliinuka tu watu wakashusha pumzi na kuonza kuongea

Mmmm🤔kwani nin huyu kaka anaogopeka hivi (nilijiuliza)

“Nicole inabidi kesho uende na Sonia kununua nguo”

“Mama nitaenda nae Mimi”alidakia Rahul
“VP hauendi kazini au”
“Nitaenda Ila nitawahi kurudi”
“Sawa”
“Mama na mm nimeishiwa nguo”aliongea Johari
“Haya na wewe utaenda”mama alimjibu
“Ataenda mwenyewe sianayajua maduka yalipo”
“Heee kwaiyo tutatoka tofaut”
“Hilo sio swali ni sentence, asanteni kwa chakula”
Alijibu na kuondoka Sasa Johari alinigeuki na kunipiga jicho hilo
Mimi nikajifanya biz kula

Tulimaliza kulamm nikaenda kuosha vyombo mda huo Johari akaja

“Kesho ukatae kuwa hautaki kwenda na Rahul”
Heee huyu dada vp

“Kwanin”
“Wee kam unataka kukaa humu ndani fanya ninachokuambia laaa sivyo utarudi polini kwenu

🥺🥺 Jamani

Nilimaliza kazi nikaenda chumbani kwangu nilifika na kujitupa kitandani Mara nikaona kikaratasi kimeandikwa (good night)sikuwa najua kusoma kilichoandikwa hivyo nikaishia kukiweka pembeni tu na kulala zangu

Asubuhi na mapema niliamka na kuanza usafi kama kawaida mara kauzu akaja nilipo na kusema……….”ufue nguo zangu na ubadilishe mashuka”

Mimi nikajifanya najua sana heshima nikamwamkia

“Shikamoo kaka” hakuitika badala yake aligeuka na kuondoka

Hivi huyu kaka anamajini au sio mtu wa kawaida ………..mara nikasikia mtu ananijibu nyuma yangu

“Hana majini ila sio mtu wa kawaida huyu”niligeuka alikuwa Nicole

“Mamboo”nilimsalimia
“Poa, yaani Kati ya mtu unaetakiwa kumuogopa na kukaa nae mbali ni Berat huyu kiumbe Hana matani wala hataki mazoea na mtu yoyote kwanza haoni ajabu kukufukuza

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!