CHAGUO LA MOYO (08)

SEHEMU YA 08


“Kwanza haoni ajabu kukufukuza,na akisema hakutaki ujue hakuna was kukutetea hata mama hataongea …. kwaiyo muangalie hivyo hivyo kauli yake moja tu inakuondoa………..

Nicole aliposema hivyo nilimuogopa sana Berat
“Ndio yuko hivyo toka utotoni au kaanza ukubwani”nilimuuliza Nicole……..

“Toka utotoni yuko hivyo na ndio maana wanawake wanamkimbia kwa sababu ya ukauzu wake”………….

“Mmmmh haya”
“Ndio hivyo kuwa makini usiseme sijakwambia,huyo Johari anajifanya kichwa mbovu ila mbele ya Berat anakuwa sisimizi”

Basi Nicole aliondoka na mm nikapanda juu ili nikachukue nguo maana huwa anafunga chumba chake……..nilifika nikagonga lakin sikufunguliwa niligonga tena wala hakuitika …….basi nikawaza atakuwa hayumo chumbani. Kwaiyo nikafungua mlango ili nichukue hizo nguo……….😳nilitoa macho baada ya kukutana nae akiwa ametoka bafuni huku amejifunga taulo kiunoni sasa badala nirudi haraka nikabaki namshangaa alikuwa na kifua kipana huku tumboni anakama matuta hivi …………. sijui kwasababu ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kumuona mwanaume akiwa hajavaa shati ……….
“Ni Nani aliyekupa ruhusa ya kuingia chumbani kwangu bila hodi 😡”aliongea huku sura yake ikionesha kukasirika

“Na bado umesimama “
Yaani huyu kaka akikuangalia unaweza kusema anaona dhambi zako zote anamacho makali balaa ………haraka nikataka kukutetea

“Samahani ka……..”toka chumbani kwangu”……….. aliongea kwasauti ya kuamlisha Mimi ninani nibaki 🏃 nilitoka kwakukimbia………

Sasa wakati na kimbia nikapamiana na Rahul nikataka kudondoka akanidaka fasta
“Vp mbona unakimbia asubuhi yote hiii”aliniuliza huku akiniangalia usoni

“Aaaa hapana”
“Kuwa makini usjie kuumia sawae na ujiandae mapema”
“Sawa, unaweza kuniachia”nilimwambia maana alikuwa bado kanishika Sasa ile ananiachia tu mr kauzu huyu hapa…………😳mara ii kashavaa …..kila kitu hata dakika 3 hazijaisha ……🤔nawasi wasi na huyu mtu

Huyu mama atakuwa alizaa na jini inawezekanaje mtu apake mafuta na kuvaa ndani ya dkk 2 hata hizi 2 sidhani Kama zimefika……… wakati nawaza hivyo alitupita bila hata kumsalimia mdogo wake………
“Aaa mzoee ndio alivyo tena hakuna mtu mkarimu kama Berat”

“😁😁Hivi unajua mtu mkarimu yukoje au unaongea tu kwanza akikuangalia unaweza kusema anaona dhambi zako zote”

Rahul alicheka sana aliposikia hivyo
“Hamna bhn niamini mm ni mtu wa pekee sana sema hapendi kuongea “.
“Hujanishawishi Wala siwezi kumzoea mtu wa hivyo”

“Kumzoea hutoweza si wewe tu hata waliokuja kabla yako hakuna aliyewahi kumzoea kwanza ukimkosea hana nafasi ya pili anakuondoa mda huo huo, wala hakuna atakae kutetea”
“🥺Duh “
“Ila usiwe na wasi wasi nipo kwaajili yako 😊”
“Umeshasema hakuna wa kunitetea alafu unageuza tena ute upo kwaajili yangu😏”

“Yeah soni………. kabla kajamaliza aliitwa na Berat( mr kauzu ) “baadae”aliniaga na kuondoka chap niligeuka na kukutanisha macho na mr kauzu uwiiiii huyu kaka anatisha yaani akikuangalia tu unaishiwa nguvu…….nikajifanya naangalia pembeni ….wakaondoka ……Mimi huyo nikaingia chumbani kwake nikachukua nguo na kubadilisha mashuka Kisha nikatoka …….nilienda kwenye chumba chakufulia nikafua na kutoka nje nikaanika …….. nilipomaliza nikaenda kunywa chai mda huo wote walikuwa wameshaondoka tumebaki mm na Johari tu…….”unakumbuka nilichokwambia jana ee”
“Aliongea Johari baada ya mm kukaa mezani

“Ndio nakumbuka”
“Vizuri”
Nilikunywa chai Kisha nikaendelea na kazi zingine mida ya saa sita Rahul alirudi na kuniambia tuondoke Sasa nikakumbuka Johari aliniambia nikatae hivyo nikamwambia

“Rahul naona ungeenda mwenyewe tu bado Nina kazi”
“Utafanya kesho”
“Yeah hatakiwi kuondoka hajamaliza kazi kama ni nguo tutamchukulia maan ninajua saiz anayovaa”

Rahul hakuongea neno badala yake alinishika mkono na kuondoka nje

Huku Johari alivimba na kuninyoshea kidole …..😓😓

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata