CHAGUO LA MOYO (10)

SEHEMU YA 10

Baada ya kumaliza kula nilienda chumbani kwake nilifika na kugonga……..mara kadhaa hakuitikia wala hakufungua….……”Sasa alivyo niambia nije alafu nagonga haitiki wala kufungua anamaanisha nn”niliongea mwenyewe na kugeuka ili niondoke……nilipiga hatua mbili mara nikashtuka navutwa na kuangukia kifuani mwake huku mkono wake mmoja kanishika kiunoni …… Niliinua uso nikamuangalia vizur mda huo tulikuwa zero distance na yeye aliinamisha kichwa maana nimrefu kwangu navile tulikuwa na pua ndefu😂 zikawa zimegusana Kama vile alitaka kunikiss au nina fikilia mbali………baada ya kuinua uso wangu ukakutana na wake niliona aibu hivyo nikaangalia chini……….Ila hata Kama ingekuwa wewe huyu mtu hafai hata kumuangalia machoni……. yaani anamacho makali balaa sijui huyo mwanamke wake anamuangaliaje au ndio kashamzoea………ila huyu kwa jinsi alivyo kweli anaweza kuwa na mwanamke 🤔sidhani labda maana kunawatu wanajua kujitoa muhanga Ila mm hapana”……”hiki ndicho ulichikuwa unakitaka sindio”..aliongea na kunishtua kutoka kwenye mawazo”……….”ndio”nilijibu hata bila kuelewa naongea nn…. aliniangalia kwa jicho Kali huku amenikunjia ndita balaa………..haraka alinivuta na kunipeleka kabati lilipo ….”kwani huyu kauzu ananipeleka wapi “niliwaza …………alifungua kabati kabla hata hajasema kitu nilitoa macho namna nguo zilivyokaa shagalabagala wakati nilipasi na kuziweka vizuri “huu upuuzi gani umefanya, nilikwambia nn na umefanya nn”……aliongea kwa hasira kiasi Cha kuniogopesha nikitetemeka na machozi yakaanza kunitoka. Kwajinsi nilivyokuwa muoga nilishindwa hata niongee nini said nilitikisa kichwa kuashilia hapana………”umekuwa bubu ghafula,nakuuliza nimekwambia ufanye nn na hikk nini”………”Be be berat mi mi nimefua na kupasi Kisha nikaziweka vizur “..,. kwaiyo hivi ndio umefua na ukapasi kisha ukakunja”……..aliongea huku akinionesha moja ya shati cheupe nilishangaa lilikuwa chafu na limejikunja kunja kuliko hata lilivyokuwa kabla sijafua…….”wewe”…….aliita kwa ukali mda huo nilihisi tumbo la kuhara kinaanza kumbukumbu za kipigo cha mamdogo zilinijia nikanywea kama kifaranga aliye nyeshewa na mvua…huku nikiwaza kipigo kitanihusu sekunde yoyote”nisamehe Ila sio mim”………niliongea huku machozi yakinitoka sikuwa hata na ujasiri wa kuinua sura yangu………..”moja kati ya vitu ninavyochukia kwenye hii dunia ni uongo,namchukia sana mtu muongo “………”hapana kaka mi”……”kimya”……aliongea kwa ukali kiasi walioko sebleni wakasikia………”bro kuna nini”…… ilikuwa ni sauti ya Rahul…….lakin hakuna aliyoongea kitu kumjibu…..”nataka hzi nguo zote ziwe safi ndani ya lisaa na ole wako ifike asubuhi nguo hazijakauka utajua mm ninani……… aliongea na kufungua mlango kisha akatoka …… Rahul alitaka kuingia Ila alimzuia kuwa hataki mtu chumbani kwake

Nilitoa nguo nje ili nizifue mda huo huo Rahul alikuja na kuniulza……”Sonia Nini kimetokea mbona unafua nguo ambazo ulikuwa tayari umeshazifua” ………sikumjibu niliendelea kufua alipoona simjibu aliondoka akionesha wazi kuwa amekasirika …..baada ya dakika 3 Nicole nae akaja…..”Sonia Kuna nn mbona unafua usiku alafu Rahul anagomba huko ndani “…….Sasa Nicole alivyosema hivyo nikama vile ameniambia Sonia lia weee nilianza kulia kwa kwikwi yaani nikilia kwa uchungu Sana moyoni niliwaza mda simrefu nitafukuzwa nitaenda wapi Sina mama Wala baba Wala mtu yoyote na vp mamdogo akijua niko huku akinishika sijui ataniua kwa silaha gani……”acha hizo nguo nipe nifue mimi”………….”hapana Nicole nitafua mwenyewe”
“Sonia Cha nifue hauwezi kufua katika hali hiyo”……… niliendelea kukataa lakin Nicole akachukua beseni lenye nguo kwa nguvu nikaona nimuache tu……..wakat anaendelea kufua mara akaja Mir kauzu huku kakunja uso hatari Mimi nikaisi mkojo unataka kutoka….”Nicole” aliita Nicole aligeuka kwa mshtuko “abee” ………….”ingia ndani” …… Nicole aliacha kufua fasta akaondoka bila hata kubisha……mim mda huo nilikuwa natetemeka balaa aliangalia saa yake na kusema……..”unadakika 10 tu “Kisha anaondoka ……. niliamka nakufua haraka haraka hadi nikamaliza nikaingia Ndani nikamkuta Rahul amekaa huku kainamisha kichwa alivyoniona alikuja na kunikumbatia mimi mda huo nilikuwa nimetoa 😳 tu….”I’m sorry Sonia”……sasa ile nataka kuongea nikamuona Berat aka mr kauzu yuko juu anatuangalia haraka nikajitoa mikononi mwa Rahul na kuondoka bila kusema kitu Rahul nae alitaka kumifuata naona alipomuona kaka yake akasimama …….yaani huyu kaka wana muongopa Kama vile ndio anafanya waishi😡 nilifika chumbani kwangu nikashangaa kumkuta Johari amelala kitandani kwangu …..”huyu nae vp”nilivyo sema hivyo akaamuka na kuanza kucheka “hahahahahaha unajisikiaje kijakazi mrembo”…….niliona huyu anataka kuniletea maigizo tu nikapiga hatua kuelekea bafuni Mara akanivuta kitambaa Cha kichwani kikatoka ukumbuke hapo ninakipara changu niligeuka fasta ili nimng’anye kitambaa alimuwahi na kujitupa juu ya kabati Kisha akaanza kuongea “heeee yaani mda wote umefunga kitambaa tunadhani unajistili kumbe unaficha kipara mm! Makubwa utakuwa unaukimwi wewe maana sio bure mdada Kama wewe hawezi kukaa na upala “
Nikaona huyu nikiwa hivi atanipanda kichwani”nisikilize Johari tena nisikilize kwa makini naomba unikomee tena usinizoee kwani nikiwa na ukimwi we inakuhusu nn”…….”hahahhahahaha heee kipofu kaona mwezi kwaiyo ukajitutumua kujibizana na Mimi, nilikwambia kuwa siku zako za kukaa humu ndani zinahesabika unaona nilichofanya leo Sasa huo nimwanzo”…….”hee kumbe wewe ndio umechafua nguo “….”kumbe ulijua Nani na kama hautokaa mbali na mwanaume wangu utatolewa humu ndani kama mbwa” aliongea kisha aondoka nikabaki nimesimama tu………”jamani kwani huyo mwanaume wake mimi nimemchukua? …….. nikaona nilale tu maana siku yenyewe imekuwa nzito……….
Nililala asubuhi na mapema niliamka na kuanza kazi wakati nadeki alikuja Berat………”unategemea nitaenda kazini na nguo za kulalia au nakaa nyumban”……..aliposema hivyo nikatamani kumwambia nguo zingine siziko kabatini au unataka nn Ila nikaona nikiongea nitafukuzwa bure……..haraka nikaenda nje na kuchukua shati moja na kuingia nikawa naipasi Sasa kwakuwa ilikuwa haijakauka nikaweka Moto mkali sangap nisiunguze ……….. Hapo nilitamani ardhi ipasuke niingie…. wakati nikiwa na waza nifanye nn kidume huyu hapa akiwa ametoka kuoga…….”naomba nguo”…….. nilianza kulia hata kabla sijaanza kuongea…….. alivyo hivyo akasogea na kuchukua shati Sasa siakaona ilivyoungua alinigeukia na kuniangalia kwa macho makali kama vile anataka kunimeza……”nu upuuzi gani huu”
“Samahani ni bahati mbaya”
“Hivi mama aliwezaje kuleta msichana mjinga Kama wewe ambae hujui hata kitu chochote, ili uje kufanya nn hasa…..ni mwanamke wa aina gani usiye jua kufua hata kupasi pia hujui huyo mama yako anakufundisha nn eee”aliongea mm nikainamisha kichwa chini haraka alinishika nakunivuta kuelekea sebleni ambapo alipofika aliniachia kwa kunisukuma “Berat mbona unamsukuma mtoto wawatu hivi amefanya nn”
“Sitaki kumuona huyu binti humu ndani”
Nilivyo sikia hivyo nikapiga magoti kuomba msamaha
“Boss naomba unisamehe nakuahidi sitorudia tena”
…..”we usiniguse kafungashe kila kilicho chako uondoke”
“Kwann aondoke au nikosa gani alilofanya ambalo haliwezi kusameheka”aliongea Rahul huku akinishika mkono……..”eti mwanangu umefanya nn”
“Mama nimeunguza nguo yake bahati mbaya”
“Berat mwanangu kuwa na moyo wakusamehe hilo sio kosa la kumtoa humu ndani”
“Mama Berat yuko sahihi huyu binti aondoke kwanza anaukimwi hapo alipo nywele zimenyonyoka hana hata moja”aliitikia Johari
…..na baada ya kusema hivyo Berat alisimama na kugeuka Kama vile hajasikia vizur……”ana nn”
Alipouliza hivyo Johari alinifata nilipo akanivua kitambaa nikabaki kipara nje…….wote waliniangalia kwa mshangao “ninani aliye kwambia kuwa mtu akiwa na ukimwi anakuwa na kipara”Rahul aliongea akionesha kuchukizwa ……..” kweli hakuna mahari palipo andikwa kuwa mtu akinyoa kipara basi anaukimwi na Kama akiwa nao shida iko wapi kwani niajabau au yeye ndio wakwanza kuumwa huo ugonjwa?
Aliongea Nicole

“Johari nimeshakwambia upunguze ukali wa maneno yako “aliongea mama
“Mama narudia sitaki kumuona huyu msichana humu ndani”
“Berat hii imezidi hivi unajiona Kama Mungu humu ndani kiasi Cha kuamlisha kila mtu sasa nisikilize Sonia haondoki humu ndani Kama Kuna mtu anashida juu ya hilo anaweza kuondoka yeye”
“Wow Mom kwaiyo uko tayar kufukuza watoto ulio wazaa kwasababu ya huyu kijakazi asiye na mbele wala nyuma”
Aliongea Lee
” Kama hataki kuni heshimu itakuwa hivyo haiwezekani mnipangie sheria ndani ya nyumba yangu huu upuuzi sito uvumilia tena,Sonia nenda kaendelee na kazi zako”
“Asantee mama”nilimshukuru na kuondoka Ila jicho alikokuwa akiniangalia Berat na Lee lilikuwa linatisha niliona humu ndani sio salama kwangu na sikutaka kutenganisha familia ambayo nimekuta iko vizur…………kabla sijafika mbali nilisimama baada ya kusikia Rahul akiongea
“Mama naomba utafute mtu mwingine,kwajinsi ninavyomjua Berat na Lee watamfanya Sonia aishi humu ndani kama kuzimu na siko tayari kumuona Sonia akiumia hivyo nitamtafuta kazi nyingine na nutajua mwenyewe aishi wapi”
“Hapana akae humu humu “alijibu Nicole
“Sonia atakaa hapa na sitoleta mtu mwingine “
Alijibu mama na kuondoka …… Rahul alimgeukia Johari na kusema na wewe kibonge mweusi ole wako nisikie au kuona unamsema Sonia kwa lolote baya au ahuzunike sababu yako hiyo siku ndio itakuwa mwisho wako kumbuka hili neno utajuta”
“Lakin Rahul mim” hata kabla hajamaliza kuongea Rahul aliondoka na kuja nilipo
“Sonia I’m sorry kwa kilichotokea nakuahidi kukurinda daima”
“Rahul mbona unaomba msamaha kwa kitu ambacho hujafanya wewe”
“Hapana Sonia kosa lolote litakalo fanya na familia yangu basi na mm nimo kwakua mimi pia ni mmoja wao”
“Kuwa na amani haya nimambo ya kawaida tu”
“Hakunaga Mambo ya kawaida kwenye manyanyaso”
“Haya yameisha”
“Sonia”
“Abee”
“Sorry kama nitakuwa nakosea kukuuliza hivi,kwann umenyoa nywele zako zote”…….aliponiuliza hivi niliwaza kabla ya kumjibu nikaona Bora nimdanganye maana sikuwa tayari mtu kujua historia yangu nilihisi ikijulikana inaweza kuwa fimbo nyingine ya kunichapia kwaiyo nikajibu
“Mama yangu mdogo alifariki kwaiyo nikanyoa kuashilia maombolezo”.
“Ooo pole “
“Asantee”.
“Lakin unakichwa kizuri ingekuwa mm hapa na kichwa changu kama yai sijui ningefananaje”alivyosema hivyo nilicheka sana
“Una tabasamu zuri sana natamani mda wote uwe unafurahia “aliongea kwa hisia hadi nikaogopa
“Okay nenda kanywe chai mda unaenda”nilimwambia .
“Sawa vp wew unakunywa sangp”
“Nakuja sasaiv “
“Okay “aliinuka na kuondoka baada ya kuondoka Johari akaja
“Umetangaza Vita na mm Sasa nakwambia hii nyumba utaiona chungu”.
“Hivi Johari unapepo au nini kwani nikitu gani nilichofanya Cha kutangaza vita na wew”
“Mfyuuuu”alisonya na kuondoka Ila huyu dada sio mzima Kama shida ni Rahul siukamwambie kuwa anampenda kuliko kujaziana nzi hapa mfyuu

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!