CHAGUO LA MOYO (15)

SEHEMU YA 15

Aliniachia tukaa na kupiga story baadae akaondoka nikaenda chumbani kwangu na kurudisha nguo kabatini Kila mda nilikuwa nakumbuka vile Berat alimstopsha mama yake nabaki na tabasamu 🥰 basi mda wakula ulifika sote tukaa mezani kula Berat alikuwa amesharudi ila ndio Kama kawaida yake haongei

Mimi nilikuwa namuangalia kwa kumuibia ibia tu huku nakula

Baada ya chakula nilienda chumbani kwake ili nikamshukuru

Niligonga na kuingia ila sikumkuta “huyu kaenda wapi sinimemuona anaingia humu jamani”niliongea mwenyewe nikachungulia bafuni hayupo nikaona nitoke asije kunikuta bure
Nikatoka ile nakaribia chumbani kwangu nikaona kile chumba ambacho kinanjia ya kushukia chini kiko wazi atakuwa kaenda chini au ngoja nikaangalie
Niliingia ila sikumuona sasa nakuja huku hata sijui nafanyaje ili kufunguke niliangaza macho ila sijaona pakubonyeza

Wakati nikiwa Bado nashangaa nilishtuka nakumbatiwa kwa nyuma Kisha mikono yake ikaniziba machoni hakuwa mwingine ni Berat mapigo ya moyo yalienda mbio hatari ghafla nikasikia tukishuka kwa chini kama lifti tulipofika akatoa kimono yake na kutembea akakaa kwenye kinanda na kuanza kupiga taratibu nikamfuata pale alipokaa nika mwambia

“Asante sana kwa kunipa nafasi nyingine”…….hakujibu alikaa kimya (hizi ni dharau 😡 yaani hata kujibu poa ni shida ) nikaona niondoke

“Kaa hapo”aliongea baada ya kuona naondoka (nani akae kwanza nakaa ili iweje😏) niliongea kimoyo moyo
“Hapana naenda kulala” nilimjibu na kutembea fasta ile nafika mahari tunaingiliaga sioni ngazi wala lifti nikamgeukia akawa yuko bz na kinanda tu nilitamani kumfyonya 😡

“Naomba unifungulie niondoke” nilimfata na kumuomba kwa sauti ya upole balaa hakunijibu Bali alinionesha kwa mkono kuwa nikae nikajifanya mbishi sikutaka kukaa nikabaki nimesimama …………..nilisimama hadi nikaisi miguu inarudi ndani mwishoni nikaona nikae
Nikasogea na kuchukua kiti kilichokuwa karibu yake nikaaa kwa mara ya kwanza nilimuona Berat alitabasamu nyie nyie huyu mtu ni mhandsome balaa unaweza kushiba ukimuangalia tu🥰 sio kushiba njaa tuelewena njaa haina masiala na mtu kabisa, yaani unasikia moyo unadunda kwa kushiba 😅 huku umetulia 😅

Kiufupi anafaa kwa matumizi 😅 matumizi yale yale unayoyajua 🙂

Aliinuka na kutoka nikajua anaondoka na mm huyo nikasimama

“Kaa hapo hapo. Nakuja'”
Aliniambia nikarudi kukaa

Akarudi ameshika mfuko uliokuwa na vitu Kisha akatoa 😶kumbe vilikuwa vifaa vya kuchorea

Akaweka mbele yangu hata bila kuongea Nilijua tu atakuwa anataka nichore hivyo nikachukua na kuweka vizuri kisha nikaa na kuanza kuchora. ……nilimchora yeye mwenyewe 😂 akiwa bz na kinanda chake. ……..basi bhn nilipomaliza aliangalia na kutabasamu (🤔Kwan huyu mtu leo vp anatabasamu tu wakati sio kawaida y usikute anataka kunila nyama au anataka kufa nn maana hata sielewi) niliwaza

Aliinuka na kuja nilipokaa akaangalia ile picha akaniangalia na kuuliza
“Kwann umenichora bila ruhusa yangu”
(😳Heee kwani nako nahitaji ruhusa ndio nikuchore )

“Aaaa a” niliishia kuongea aaa tu😅 “

“Okay mda wa kulala tuondoke” nikainuka na kutaka kuchukua ile picha akaniambia niache

“Iache hapo hapo”
Nikaacha tukaenda pakutokea tulipofika alikuja akasimama mbele yangu alanisogelea tukawa zero distance yaani akinisogelea hivi moyo huwa unatka kuchomoka maana sio kwa speed hii sasa mawazo yakanipeleka mbali nikajua anataka kuniss 😅 nikafumba macho alafu sijui ninani aliye niambia kuwa ukitaka kukissiwa unafumba macho aaa nimekumbuka nimeona kwenye tv za wazungu 🙂 basi bhn nikafunga macho mara alinishika kichwa na kukilaza kifuani mwake mkono mwingine akauzungusha mgongoni sahiyo moyo umeongeza Kasi ya kukimbia yaani Kama ningekuwa kwenye mashindano basi ningeshinda😅 basi bhn tukaanza kupanda juu( kitu ambacho sielewi huku huwa ananileta kumsikia tu akibiga kinanda tu au na mbona ananifunika macho Kila mara 🤔)

Tulipofika aliniachia nilitoka fast kama vile nilikuwa nakimbizwa na mbwa😅 huyoo nikaenda chumbani kwangu nikafika na kujitupa kitandani

Nikawa natabasamu tu mara nikaona kikaratasi kitandani kimechora emoji ya 🙂. ……….hiki kimefikaje hapa atakuwa Rahul nikakiweka pembeni na kulala

Kesho yake niliamka na kufanya usafi kama kawaida ilipofika mchana Johar aliomba nimsindikize sokon kwakuwa sikuwa na kazi nikaona niende tu

Tulifika sokon tukawa Tunanunua vitu mara nikasikia mtu ananiita
“Sonia” niligeuka na kumuangalia aliye niita

“Mungu wangu nimeisha “niliongea kwa sauti baada ya kumuona yule mtu aliye niita

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!