CHAGUO LA MOYO (16)

SEHEMU YA 16

“we vp”aliuza Johar baada yakuona nimeshtuka

“Sonia kumbe litorokea huku ” nyie yule dada alikuwa ni jirani yetu kule mwanza nilitamani nikimbie au nijifanye Simjui ila kashanitaja hadi jina

“We kumbe ulitoroka “
Johar aliniuliza
“Hapana bhn huyu dada tuna matani so anatania vp Jennifer za siku”

Nilimsalimia na kumvuta pembeni ila Johar alivyo mmbea nayy akasogea

“Unajua mama yako mdogo alienda hadi kukutangaza kwenye radio free Africa tena alisema umemuibia million 3 na nguo ” nyie huyu dada yaani nimesha mkonyezasha na kumpa ishara kuwa akae kimya ila ndio kwanza anafukunyua

“Weee unataka kusema Sonia ametoroka kwao tena akaiba na pesa “

“Aaaa Jennifer Acha matani kama hayo kwenye watu wengi hivi sio vizuri’ niliamua kuongea hivyo ili Johar asijue maana akijua tu. Lazima ataenda kusema na lazim kibarua kitaota nyasi

“Matani kwanzia lini mm nawew tukawa na matani ila ulichofanya sio kizuri hata kidogo na siku mama yako mdogo akikushika utajuta kuzaliwa”

“Johar tuondoke basi tunachelewa maana tukikaa kusikiliza matani ya huyu tutachelewa Jennifer sisi tunaondoka ” niliongea na kumshika Johar mkono ili tuondoke

“Hembu subiri kwanza unataka kukatisha mada hapa…. hamna kazi ya kufanya huko nyumbani hivyo hata tukuchelewa hamna shida enhe dada ulikuwa unasema ametoroka na aliiba pesa na nguo pia”

Nyie huyu Johar kuingilia yasiyo muhusu

“Ndio hivyo dada yangu yaani alipewa hifadhi ila mwisho wa siku hilo ndio alilomlipa Dada wawatu”

Aisee nikikasirika nikataka kumchamba Jennifer ila Mungu alisaidia akawa ameitwa sijui na mwenyeji wake akawa ameondoka

“Hahahahahaha heeee Mungu kweli kuwa uyaone ndio naona sasa kumbe ulitoroka kwenu”
Johar alicheka na kuongea kwa dharau sikuwa na jibu lakumjibu Bali tulimalizia kununua vitu na kuondoka nyumbani

Sikuwa na Raha kabisa kwani Nilijua lazima tu atatumia hilo kunitoa mle ndani na kwahili nauhakika hakuna wakunitetea 😓

Tulifika mm moja kwa moja nikaenda chumban kwangu ile naingia nikakuta kitandan Kuna mfuko nilisogea na kuuchukua nikaangalia ndani kulikuwa na box la simu

“Habari ya jion”
Rahul aliingia ndani na kunisalimia
“Poa vp” niliitika kwa uso watabasamu japo sikuwa na furaha hata kidogo

“Pole na uchovu”
“Asante aam nimekuletea sm sijui kama utakuwa umeipenda”

Nyie aliposema hivyo tu nilijikuta naangua kilio kama nimefiwa vile kitu ambacho kilimshtua Rahul
Alinibembeleza na kuomba msamaha kama amenikosea

Nilimkumbatia na kuendelea kulia niliwaza nitaondoka mda mfupi na sijui nitaenda wap pia sidhan kama nitapata mtu mwenye upendo kama wake moyoni nilipata wazo kuwa niende kwa Berat nijieleze ili anisamehe na kunipa nafasi ya kuendelea kukaa ila nikikumbuka ukauzu wake nikaona hata nielewa hivyo nikaamua kukaa kimya

Baada ya kulia kwa mda nilinyamanza Rahul alinisihi nimwambie shida nn mwanzo nilikataa ila alinibembeleza niakona sio mbaya nikimwambia ukweli tu

“Rahul”
“Naam “
“Mimi ni ni”nilisita kuongea mara mlango ulifunguliwa mama akaja akionesha kukasirika balaa akasema

“Sonia njoo chumbani kwangu fasta”

Basi imeisha”😞 niliongea na kuinuka kinyonge nikatoka chumban

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!