
SEHEMU YA 17
“Abee mama” niliitika baada ya kuingia chumbani kwake
Hapo natetemeka balaa
“Naomba uchukue begi langu uniwekee nguo za kutosha nimepata dharura natakiwa kusafiri sasaiv “”
Uuuuu Asante Mungu Nilijua nafukuzwa kumbe ana safari nikachukua begi na kuanza kupanga nguo mda huo mama aliingia bafuni kuoga
Dkk mbili huyu hapa nilishangaa huyu kaoga au kanawa maana sio kwa dkk hizi
“Sonia mwanangu fanya haraka “sawa mama (huyu anawenge la safari ananiambia nifanye haraka wakati hata kuvaa Bado haja Vaa ila anaweza kuvaa sekunde tu maana kama ametumia dakk mbili kuoga kuvaa si sekunde. ……….basi nikapanga chap akawa ameshamaliza kuvaa tukaongozana hadi nje akaingia kwenye gari
“Kam Kuna kitu chochote binafsi utamwambia Berat sawae” Aliniambia huku dereva akigeuza gari
“Sawa mama”
Huyo akaondoka nika Rudi ndani sasa nafika mlangoni nakutana na Johar kasimama huku ameshika kiuno
“Vp ulikuwa na presha ukidhani nitakuwa nimekusemea, hahahaha usijalia leo nimekustili ila kwa sharti moja tu ukikataa namfikishia taarifa bwana mkubwa nadhani unamjua hanaga second chance “
“Sharti gani hilo “
“Utakuwa unafanya kazi zangu zote”
“Eee ili iweje na wewe utakuwa unafanya nn “
“Nitakuwa nakaa kama hutaki sema sikulazimishi ee”
“Nilifikilia nikikataa akasema. Nitaenda wap mm😔 hivyo sikuwa na jinsi nikakubari
‘”sawa nimekubari”
“Vizuri sana haya kazi njema niko chumbani kwangu ” akaondoka nilibaki namuangalia tu
Kweli bhn nikaanza kufanya kazi zote za mule ndani
Haikuwa shida kwangu kwakua nilizoea kufanya kazi
Siku zilienda huku Rahul akiendelea kunifundisha Nicole nae alikuwa bz na chuo
Nilimzoea sana Rahul na ukalibu wetu ulizidi Sana ila sijui kwann Kila mara Berat akichelewa au akiwa hayupo nilikuwa najisika vibaya sana au kama nikipika chakula asile yaani nilikuwa nakosa amani kabisa hata sijui kwann 🤔
Siku moja nikiwa zangu bz jikon alikuja Nicole na kuniambia kuwa mama yake amesema twende Dubai ambako alikokuwa na yeye na tulitakiwa kwenda siku baada ya kesho.
‘”Dubai hii hii na yosikia kwenye radio au nyingine ” ilibidi niulize usikute mbagara Kuna Dubai mm nikachanganya mambo😂
“Ndio hiyo hiyo unayosikiaga'””
“Weee”nilitamani kuruka mm Sonia naenda Dubai ngoja nichaji sm yangu ijae ili nipige selfie za kutosha🥰
Basi siku hiyo iliisha nikiwa na furaha sana kesho yake nilifua na kupanga nguo zangu fresh tu yaani nilipakia kama nimeambiwa tunaenda kuishi huko huko
“Mhu ushamba mzigo kweli sasa umepaki vitu vyote hivyo kama vile unahama na ukoo mzima kwani umeambiwa tunahamia”.
“Alafu Johar naomba tusitowane kwenye uwepo sawa Kwan nikipaki vitu vyote vinakuhusu au umeambiwa utabeba wewe mfyuuu”
“Wewe tena kusikia Dubai masikio yamekusimama utafikili tembo mjane 😏”
“We tembo mjane ulimuona wapi au siku hizi umekuwa bi mifugo”
Basi Nicole alikuja hivyo uchizi wetu ukaishia hapo
Nyie sikieni tu Dubai yaani siku hiyo usingizi ulikata kabisa nilikuwa nawaza safari tu nikawza nikilala naweza kuchelewa ndege ikaniacha bure😅
Sijui hata usingizi ulinichukua saa ngp ila nilikuja kushtuka ni saa tatu kasoro ya asubuhi
Cha ajabu nilikuwa najisika vibaya sana yaani nilikuwa ninechemka kama vile nimewekwa kwenye moto kichwa kilikuwa kinauma balaa
“Mmm mbona imekuwa ghafla hivi jamani inakuwaje niumwe leo 😡lakin hpana nitaenda tu Kam nikupona nitaponea huko huko”
Niliinuka taratibu na kuingia bafuni nikapiga mswaki na kuenda jikon ilibidi nijikaze tu ili niandae chai mda huo watu wote Bado wako vyumban mwao
Niliandaa chai nikaweka mezan Kisha nikarudi chumbani kwangu kila dakika ilivyokuwa inaongezeka ndivyo nilivyozidi kuzidiwa
Mwishoni nikaona nibaki tu nyumbani nisije kwenda kuwapa mzigo huko wakati wanaenda kufurahi
Walipoamka Nicole alikuja chumbani kwangu na kunitaka nikanywe chai ili tujiandae kwani tunatakiwa kwenda Airport saa tano
Ilibidi nikatae japo sikumwambia kuwa naumwa sababu sikutaka wasafiri kwa wasi wasi
Nicole alinibembeleza sana ila nikakaaa akamuita Rahul ili aongee na mm lakin pia sikukubari basi wakampigia mama Yao wakamwambia akasema kama hataki basi mwacheni
Hivyo walikunywa chai wakajiandaa na kuniachia pesa ya matumizi Kisha wakaondoka
Moyoni nilibaki na huzuni nyie yaani kama Kuna mtu kaniroga alaaniwe 😓
Itaendelea………
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU