
SEHEMU YA 18
Niliingia chumbani kwangu nikalala nilikuja kushtuka ni saa mbili na nusu usiku kwakua nilikuwa mwenyewe haikuwa shida nikainuka na kwenda bafuni kuoga mda huo bado hali yangu haikuwa nzuri
Nilioga nikamaliza na kutoka nilijifuta maji vizuri Kisha nikachukua mafuta ghafla nikahisi kizunguzungu kikali nilishindwa hata kusogea kitandan nikajikuta nadondoka na kupoteza fahamu
Sikujua nn kiliendelea ila nilikuja kushtuka nikiwa nimelala huku nikiwa nimewekwa drip ya maji na pembeni yangu alikuwa Berat amelala huku amenishika mkoni
(Mungu wangu huyu si Berat au Kwan imekuwaje yuko hapa na sialienda na kina Nicole au wamerudi )niliwaza mara aliamka naisi alihisi kuwa nimeamka
Aliniangalia kwa mda bila kuongea kitu Kisha akaongea
“Unajisikiaje”
“Najisikia vizuri” nilimjibu na mara doctor akaingia aliniangalia joto nakuniuliza navyojusikia nikamwambia najisikia vizuri
“Naona hali yake kwasasa ni nzuri hivyo anaweza kupata chakula alafu apumzuke kama kutakuwa na tofauti yoyote utanijuza”
“Ok thanks ‘”
Doctor aliondoka na yeye akainuka na kutoka mda huo nilikuwa nawaza wakati nimezimia nilikuwa sijavaa na hapa naona nimevaa nani atakuwa amenivalisha 😱isije kuwa Berat Mungu wangu nisaidie asiwe yeye
Berat alirudi akiwa ameshika bakuri na kijiko alipofika aka niinua taratibu na kunikalisha nilitamani nimwambie aniache niinuke mwenyewe Kwan naumwa homa si mgogo Wala kiuno. Ila ningeanzia wap😄
“Fungua mdomo” heee anataka kunilisha no bora nile mwenyewe
“Asante naomba nile mw”
“Fungua mdomo”alinikatisha kwakuwa naipenda amani acha nikubari tu
Basi alinilisha hadi nikashiba
“Sorry naweza kukuliza”
Niliamua kujifyatua
“Uliza”
“Haijaenda Dubai?”
“Nimeenda siunaona Niko kwenye swimming pool naogelea” kwa hili jibu 😁
Niliishiwa pozi ya kuuliza tena
“Umemaliza kuuliza”
“Ndio'”
“Yes ni mimi nimekuvalisha (usikae na sawali moyoni)”
Niliangalia chini kwa aibu yaani ameona kipochi mayoa changu tena na machungwa yangu sio fea kabisa 😔
“Kwann hukusema kama unaumwa au hujui kama ni hatari vp kama ningeondoka unafikili nn kingetokea”
Nikajibu bila hata kufikilia mara mbili ” ningekufa tu kwani ku” sikumaliza sentence aliniwekea kidole akiashilia nisiendelee kuongea
“Usije ukasema hiyo kauli mbele yangu tena umesikia”
(yaani unaongea na mgonjwa kibabe hivi jaman ) nilimjibu ndio kwa kutikisa kichwa kuashilia ndio Sito Sema tena
Sasa badala atoe kidole chake kwenye lips zangu akawa anafanya kama nile ananifuta yaani anapeleka kidole kulia Kisha anakirudisha kushoto nyie nilihisi mwili pata hisia za ajabu huku kwenye kipochi mayoa changu nikahisi kama kunavuta vile
“Usirudie kufanya hiki kitu ulichofanya leo sawa” aliongea kwa sauti ya upole sana yaani kama sio yeye vile
“Sawa”nilimjibu huku nikimuangalia usoni alinisogelea na kunikiss kwe paji la uso mda huo nilifunga macho na kumshika mkono
Nilit hyfumbua macho nikakuta ananiangalia akawa anashika nywele taratibu
nyie sijui niwambie nilivyokuwa najisikia yaani kama vile homa imeisha
“Get well soon” aliongea na kuniachia akachukua kitabu na kufungua akaanza kusoma mm nilikuwa bado nimeganda kama Sanamu
Aliniangalia akaona nimekaa vile vile huku nikimtolea macho akaniambia
“Pumzika “
Nilijilaza huku nikimuangalia hivi Kwan leo kimetokea nn jamani mbona siku Iko tofauti sana au kwasababu naumwa ndio maana naona hivi yaani sikuwa nahisi kumuogopa tena moyoni nilitamani aendelee kukaa pembeni yangu 🥰 (kama nikiumwa ndio anakuwa hivi basi naomba nisipone ili Kila siku awe karibu yangu😂 ) mmeshanipoteza tayar yaani naomba nisipone 😁jinga sana mm 😄
Basi nilimuangalia hadi nikapitiwa na usingizi nilikuja kuamka nakuta nimelala juu ya kifua Cha mwamba Mr romantic sio mr kauzu tena 😂 naomba mfute hilo jina nishambadilisha 😄 nilimuangalia nikatabasamu mwenyewe 🥰
Ndio maana nimelala usingizi mzuri kumbe nilikuwa kifuani 🥰 aweee siamka 😄nikalala tena huku nasikia mapigo ya moyo yanadunda tu yaani ikawa kama beat ya kunibembeleza tu 🥰 ila ngoja nimkague kwanza nilianza kazi ya kumkagua vizuri nikawa nashika nyusi mara nywele mara nacheza pua ila kwa tahadhali😄 nilikumbuka alivyokuwa ananishika lips jana na mm nikawa nafanya vile vile siakafungua macho wee nilikurupuka ila akaniwahi na kunivuta nikarudi kifuani
“Unajisikiaje sasa”
“Najisikia vizuri “nilimjibu huku nikiangalia chini alinishika kidevu akaniinua na kusema
“Napenda jinsi ulivyo na aibu nimoja ya kitu kinachoni drive crazy lakin unatakiwa kunizoea sasa Kwan nishakuwa mwanaume wako”
“Mmmh niliguna huku nimetoa macho😳”
Mwanaume wangu tena
Kwanzia lini?
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU