
SEHEMU YA 21
Karibuni tuendelee
👇
Nilikuwa najitoa mkono ila alinishika hakutaka kuuachia
Mda huo Rahul anatuangalia kwa jicho la kiulizo “habar ya jion mama”
“Nzuri mwanangu unaendeleaje”
“Vizuri”huyo akaondoka hata hakusalimia wengine aliwapita na kwenda chumbani mm akanicha
Sangap Rahul asije kunikumbatia yaani Hawa hawana adabu unawezaje kumkumbatia mtu mbele ya mama yako
“I miss you”alipo ongea hivyo tu nikaona mama na wengine wakainuka akabaki Johar tu
“Muwe na heshima basi Kwan hamuoni kama tupo hapa au” Johar aliongea mm mda huo nilitamani aniachie tu maana kaka yake akituona itakuwa shida
“Aaah Rahul” niliona nijitoe kwenye kumbato nisije leta shida
“Njoo” alinishika mkono na kunipeleka chumbani kwake yaani nimeshaingia chumbani kwake mara kibao ila leo nilihisi kama nafanya kosa la jinahi “aaa Rahul subiri we nenda nitakuja ngoja kwanza nimpelekee Berat mzigo wake”
“Okay nakusubiri basi”
“Poa” aliingia mwenyewe chumbani kwake mm nikaenda kwa Berat nilifika na kufungua mlango nikakuta amejifunga taulo tu aliponiona alisimama na kunifuata akanikumbatia na kusema
“Mbona umechelewa sana mke wangu ” nilikosa la kujibu maana nikimwambia nilikuwa na Rahul kitawaka so nikaamua nimuage nikalale maana kwakwel sikuwa na hisia tena kwanza niliwaza nitamwambia nn mama yake akinifukuza je “aaam naomba nikalale “
Alijifanya kama vile hajasikia nilichosema akaanza kunikiss kutokana na akili yangu kutokuwa pale sikuwa na hisia kabisa
“Vp huna hamu na mm tena”aliuliza baada ya kuona simpi ushirikiano
“Hapana ila naisi usingizi tu ‘”
“Ooo sawa twende tukaoge then ulale “
Huyu vp Kwan hajui kuwa watu wamesharudi au anaona yuko mwenyewe “hapana Berat naenda kuoga mwenyewe “
“Kwann uoge mwenyewe wakati na mm nipo”
“Aaaam “nilitamani kuongea ila nikaona atakwazika
“Okay fine kaoge alafu uje ulale”
“Mhu”
“Siumetaka kuoga mwenyewe kaoge alafu uje tulale”
Nyie sasa tutalalaje chumba kimoja wakati familia yote ipo
“Aaaa Berat naomba nikalale kwangu “
“Kwako wapi”
“Kule kwasiku zote”
“Sonia toka siku ya kwanza ulipokuwa mpenzi wangu chumba chako kilibadilika sio kile ni hiki hivyo utalala humu tena sio leo tu Bali maisha yako yote”
Mungu wangu mtu aje aongee na huyu mtu basi mbona anakuwa hivi aaa😡
“Hapana siwez kulala huku wakati familia ipo haitakuwa sawa”
“Kwaiyo unataka ukalale na familia”
“Hapana”
“So shida nn “
“Hamna ila ni”
“Rahul yes kwasababu ya Rahul ndio maana huna hamu na mimi tena Wala hata kuoga na mim hutaki nakulala kitandani na mm unaona ni kosa eeh yote hayo ni kwasababu ya Rahul si ndio “
Kumekucha 😥
“Hamna Berat ila”
“Unaweza kwenda ukipenda “alinikatisha hata kabla sijamaliza sasa nilivyokuwa mjinga badala niongee nae kwa kumpeti peti nikaondoka kweli tena sikugeuka hata nyuma
Niliwaza niingie chumbani kwangu moja kwa moja nilale zangu sasa nafika mlangoni nakutana na Rahul kabeba mifuko kama yote
“Aaa sorry nimeona nitakupa kazi ya kuja chumbani kwangu so nimeona bora nije kwako”
Shida nyingine hii sasa hapa Berat akija akakuta yuko chumbani kwangu itakuwaje. Aaaa a jamani mbona hivi lakin yaani nilitamani nimwambie aondoke ila nikashindwa
“Nilifungua mlango akaingia Kisha nikaacha wazi malengo yangu Berat asije kuja akakuta mlango umefungwa akahisi vibaya
“Mbona hufungi mlango ” aliuliza
“Aaaa Acha hivyo hivyo tu “
“Okay so nimekuletea zawadi hizi hapa”
“Alimwaga Kila kitu kitandani tukaanza kuchambua moja baada ya nyingine huku moyoni naomba tumalize aondoke nisije kukutwa
Kama kawaida yake anastory nyingi yaani anaongea balaa tukichambu zawadi zote tukamaliza ila Bado anaongea mm mda huo najibu mmm mhu alafu weee kweli hayo ndio yalikuwa majibu yangu ila hakuchoka masaa mawili yalikata anaongea tu nilianza kuona kama kero
sasa nikajifanya nasinzia
“Aaam naona umechoka ngoja nikuache basi tutaongea kesho”
“Sawa Asante”nilijibu kwa sauti ya usingizi akaondoka nikaamka na kwenda kufunga mlango
Sasa ile nataka kufunga mtu akauzuia moyo ulifanyaa pasa Nilijua Berat nikajisemea “leo ninalo “
“Silali hadi nipate jibu langu”
Uuuwiiiii afadhali kumbe alikuwa Nicole chaumbea wangu
“Jibu la gani” nilimuuliza japo nilikuwa nimeshajua anataka kujua nini
“Mlienda wapi na Berat toka saa tano tumefika hapa hadi saa mbili usiku alafu mnakuja mmeshikana mikono”
“Tulienda kanisani alafu tukaenda kukaa ufukwen basi” sikutaka kumwambia Kila kitu kwakuwa nilihisi sio wakati sahihi
“Mmmh kwanzia lini mkaenda ufukwen na Berat Kwanza huwa hatoki we sema bhn”
“Niseme mara ngapi au Kuna kingine unajojua mm sikijui”
“Haya mimi nakuonya usije ukarogwa kumpenda huyo mtu utajuta na sio kwamba simpendi kaka yangu au nakupangia no wewe ni rafiki yang natamani uwe na mwanaume wakukufanya ufurahie mapenzi na sio mtu wa kukufanya kuyachukia so kuwa makin sana”
Mhu ungejua nimeshazama na kuliwa kitambo sana hapa nimebaki mifupa tu
“Sawa” nilijibu short ili asiendelee kuongea maana na yeye yumo
“Sasa nimekumiss sana hivyo leo nitalala na wewe “
Basi alipanda kitandani akalala mimi nikachukua sm kuangalia labda atakuwa ametuma text ila hakuwa ametuma badala yake akawa ametuma . Rahul ujumbe ulisomeka hivi..
“Good night my sunshine ❣️”
Mhu haya
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU