CHAGUO LA MOYO (22)

SEHEMU YA 22

Karibu tuendelee

👇
“Nikaiweka sm pembeni kinyonge na kutafuta usingizi nilijikuta na mmiss Berat wangu maana huwa analala amenikumbatia kama katoto😔

Nilimuangalia Nicole alikuwa ameshauchapa usingizi kitambo nikawaza niende kulala kwa Berat ila nikakausha maana Nicole akiamka usiku akakuta sipo nitajibu nin kesho

Basi nikahangaika wee mwishoni usingizi ulinichukua

Asubuhi Kam kawaida nikaamka na kuanza kufanya usafi

“Hujambo”
“Sijambo shikamoo mama”
“Marahaba”

“Nilisalimiana na mama Kisha nikaendelea na kazi

Nilifanya usafi nyumba yote isipokuwa chumbani kwa Berat huko nilitaka kuwe kwa mwisho maana Nilijua nikienda hata niachia rahisi

Nilishika kitasa ili kufungua mlango lakin ulikuwa umefungwa
Nikagonga ila haukufunguliwa (atakuwa anaoga au)niliwaza na kutoka na mm nikaenda kuoga Kisha nikarudi tena kuangalia kama amemaliza ila bado mlango ulikuwa umefungwa

“Mbona unapiga kelele saizi asubuhi”
Alikuwa Lee sikumjibu nikageuza kutaka kuondoka wee alinishika mkono na kunirudisha

“Nakuuliza alafu unaondoka bila kunijibu “
“Lee naomba uniache siko sawa”
“So inanihusu nn mimi alafu una mimba eeh”
“Mfyuuu hiyo umenipa wewe au hembu niache bhn'”

“Why mwili wako ni wamoto hivi wakati sio kawaida yako”

“Ulitaka niwe wa baridi kwani nimekufa “

“Ooo siku hizi umekuwa eeh na jeuri limekujaa”

“Lee niache bhn’ Kwan una nini wewe”

“Sikuachi sasa utafanya nn'”

Alinishika mkono na kuufinya wee nilipiga kelele

“Mamaaaaa unaniumiza “

Rahul alikuwa wa kwanza kufika yaani hakuongea alimsukuma Lee chini na kunishika “uko sawa”

“Ndio ” baada ya kumjibu aliniweka pembeni kisha akamguekia Lee

“Ulikuwa unafanya upuuzi gani huu “

“Huyu kijakazi sasaiv anadharau sana mm namuuliza ananijibu jeuri”

“Kwaiyo ukaona hili ulilofanya ni sahihi Zaid”

“Sikiliza Rahul mm sio wewe wa kumbembeleza hapa alikuja kufanya kazi sio kunfnya jeuri na siku nyingine akirudia nitamuweka makofi hatoamini”.

“Ole wako unyenyue mkono wako umguse hata nyuzi kwenye nguo yake sitajali wew ni kaka yangu nitakupiga “

“Unasemaje wewe kwaiyo unataka kunipiga kisa hii takataka hapa”
“Lee chunga mdomo wako laa sivyo “
“Laa sivyo nn ee! Unataka kujifanya kidume si ndio “

Mungu wangu nini kinataka kutokea hapa
“Rahul basi inatosha mimi ndio”

“No Sonia siwez kukaa kimya huku nikiona anakufanyia kitu kibaya ‘”

“Nini kinaendelea hapa” aliongea mama na wote tukageuka kimya hakuna Alie kitu

“Jamani sinimeongea na nyie nijibuni “
.”ongea vizuri na mwanao tutakosana ohoo” Rahul aliongea na kuondoka Lee nae akaondoka nikabaki mm na mam

“Kulikuwa na nini mbona nasikia kama walitaka kugombana”

“Aaa ni Lee alikuwa nanigombeza kwakua nimegonga mlango wa chumba cha Berat kwa Mda “

“Sasa unagonganje mlango wakati mtu hayupo”

(Mmh mara hii kashaenda kazin)

” Samahani mama sikujua kuwa hayupo “

“Amesafiri leo alfajiri”

“😳Ame what “

“Amesafiri au sikuhizi husikiii” mama aliongea na kuondoka nilibakia nimekaa

Imekuwaje amesafiri bila kuniambia na wakati mm ni mpenzi wake

Yaaani niliinuka speed hadi chumbani kwa Kasi niliyo ingia nayo chumbani ilimshtua Nicole Wala sikujal
Nilichukua sm na kumpigia lakin ilikuwa inakata hata kabla haijaita nilipiga mara kibao bado Iko vile vile

“Wewe vp Kuna tatizo” Nicole aliuliza kwani hata nilimjibu niliwasha data ili nimtafute Whatsapp

Nguvu ziliniishia baada ya kuona ameni block

“Sonia unashida gani” Nicole aliongea na kunifuata Pale chini nilipokuwa nimakaa

“Kwann ameniblock ” niliongea kwa sauti ya kilio

“Nani kaku block”
Sikuweza hata kumjibu Zaid nililia tu yaani nilihisi maumivu ya sio elezeka

“Sonia ongea basi mama shid nn mbona unalia”

“Hivi mpenzi wako akikublock anakuwa ana Manisha nn” nilimuuliza huku nikifuta machozi

“Inamaana kakuchoka na hataki kuongea nawew kiufupi anakuwa hakutaki tena “

Lile jibu lilikuwa kama mkuki wa moto kwenye moyo wangu

“So amenichoka na hanipendi tena” niliongea kwa maumivu sana 😫😭

“Nani kwani ulikuwa na mpenzi
Aliponiuliza vile nilimuangalia tu bila kumjibu maana ningekwambia lazima angenilaumu n kuniambia kwann nilikubari kuwa nae

Itaendelea..

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!